UpWork Freelancing: Kama wewe ni kijana ambae huna kazi pita hapa

Kainetics

Senior Member
Jun 20, 2022
131
259
Habari wana JamiiForums, kwa bahati mbaya au nzuri, mambo mengi ambayo naandika au natamani kushare humu yashaongelewa tayari , na hata hii kitu ambayo naandika saa hivi. Freelancing.

Though, approach nlioona inatumika na wengi ni tofauti kabisa na ile ambayo nimekuwa nikitumia hivyo naona ni vyema kushare.

Title ya thread nimeandika 'Kama wewe ni kijana ambae huna kazi pita hapa' maana nahisi wengi ambao wanapitia hio kitu wanaweza pata unafuu wakiamua kuipa Freelancing nafasi, kwa kuwa swala la ukosefu wa ajira ni shida ambayo inataka kuzoeleka. Ila hii ni kitu inayoweza fanywa na mtu yeyote yule, as long as uko serious.

Huitaji mtaji wowote isipokuwa skillsets zako, bando, simu na laptop. (Kama ni University underGraduate una advantage kubwa, ila hata kama hujafanikiwa kufika chuo lakini unajikubali kwenye kile unachofanya hii inakuhusu).

Hivyo basi, ndani ya hizi dakika ngapi ntajaribu kuonesha namna sahihi unavyoweza ingiza pesa 'kama mtanzania' kwa kufanya hii freelancing. Walau kuingiza kati ya laki mbili hadi nne kwa mwezi.

Utangulizi
Kainetics Screenshot ya UpWork.jpg


Hio ni screenshot yangu ya Freelancer Profile ya Upwork. Nime censor picha yangu pamoja na Bio, kwa sababu ambazo ntaelezea sio muda. Kwa haraka haraka ukiiangalia utaweza kuona yafuatayo;

🤓 Japokuwa picha nime censor, iko potrait,hd na sura inaonekana vizuri.

🤓 Pembeni ya Jina langu kuna 'Verified Blue Tick' hii ikimaanisha nimepass mtihani wao.

🤓 Inaonesha location yangu ni Dar es Salaam, Tanzania na Muda.

🤓 Job Success Rate ni 78%.

🤓 Nina $1,000+ in Earnings ( Roughly Million mbili kwa Tsh zetu).

🤓 Nimefanya kazi 18 zenye total ya masaa 318.

🤓 Kuna hio One liner yangu iayoonesha nadeal na kutengeneza websites na applications, Chini naonekana na charge $7 kwa saa then inafuata description.

Kila kitu nlichoandika hapo juu (mbali na hela niliokwisha ingiza,) kina umuhimu wake kwenye kudetermine success rate yako kwenye kupata kazi na wateja wa kurudi na ntajaribu kuelezea namna utakavyo setup profile yako iwe presentable.

Mambo mengi ambayo ntaongelea kama ushawahi pitia hizi thread nlizoona za freelancing, hayatakuwa sio mageni isipokuwa kitu kimoja ; Badala ya kuchukua tender za wazungu, chukua kazi za makampuni ya kiafrika, yaani East na Southern Africa. Simple.

Kama umesoma kufikia hapa huelewi hata freelancing au hio UpWork ni nini, ngoja niielezee kiufupi;

Freelancing ni nini?

Freelancing ni aina ya biashara ambapo makampuni yanakuajiri kwa masaa kadhaa kuyafanyia kazi fulani. Kazi inaweza kuwa yeyote ile na malipo utalipwa kwa saa.

Hivyo basi, kama umesomea lugha advance na chuo, na uko vizuri kwenye kiswahili na kingereza unaweza kuwa mtafsiri, au kama uko creative kwenye kufanya graphics za aina yoyote ile, au unapenda kuandika kama mimi na unaweza fanya creatve writing, copywriting, proofreading na editing, au uko mtaalamu kwenye web design, au programming, au unajua video editing, kutunga nyimbo, motion graphics , nk unaweza fanya freelancing.

Freelancing unaweza fanya kwa kujiunga kwenye tovuti au apps zinazojishughulisha na hio kitu, kama Freelancer.com, Fiverr na UpWork. Ila hii guide ni kwa UpWork.

Unahitaji Nini Kuwa Freelancer?

🏷 Kama utataka kuwa freelancer, kitu cha kwanza utahitaji uwe na uelewa kuhusu kile unachotaka kufanya, yaani uwe Intermidiate au Pro.

🏷 Mbili, uwe umekisomea kitu husika na walau uwe una Undergraduate Degree. Kama huna lakini una uhakika uko vizuri kwenye skillset husika, unaweza chukua course inayohusiana na skillset husika mf. Web Design kutoka Udemy yenye cheti na kutumia hicho ili kuchukua test na kuwa verified.

🏷 Utabidi uwe na mambo ya msingi kama Picha yako inayoonesha sura vizuri, namba ya simu, anwani na namna ya kupokea malipo(Kama PayPal).

🏷 Itabidi uwe na simu, laptop(kama kazi yako ni ya kwenye computer) na bando.

🏷 (Sio lazima ila ni mhimu) Ujaribu kutengeneza kijiwebsite cha portfolio kinachoonekana vizuri. Lipa hata Web Designer akutengezee, hii ni sawa na resume au CV yako. Kama hujui Portfolio ni nini, ni tovuti inayoonesha kazi zako bora. Kama unasema wewe ni Video editor, edit video kadhaa uweke kwenye website yako iliyokaa ki video editor kuonesha uko pro na unajua unachokifanya.

🏷 Lastly na mhimu kuliko hayo yote; Itabidi ufahamu kujibrand.

Kufanya Freelancing Kwa Akili Kama Mtanzania

Changamoto ambayo wengi wanakutana nayo ni kupata kazi kwenye hizi sites maana wanaofanya hizi mambo ni wengi mno, na wewe ulie anza leo huwezi pewa kazi kirahisi kama kuna mimi ambae nlikutangulia kujiunga.

Pia watu wa ughaibuni huko wanapenda kupewa kipaumbele kwa kuwa grading system za haya makampuni ya Upwork , Freelancer, Fiverr na kadhalia yanapenda kuamini kuwa waliochukia elimu kwao huko wan tendency ya kuwa bora kuliko watu wa huku. Kitu ambacho kina ukweli kwa asilimia kadhaa. Na kama unaenda fanya kazi ambazo ni IT au Programming related, waTanzania hatuna reputation nzuri.

Hivyo, usishindane na wazungu bali exploit marketplace ya waafrika. Baada ya wiki kadhaa au miezi fulani utajishukuru.

Fanya Hivi;

Jiunge kwenye hio Upwork, kwa majina halisi na verify email yako na unga namna yako ya kupokea malipo.

Ukishajiunga Upwork, na ukasetup profile yako, chagua skills zinazoendana na kile unachojua ila ziwe kama 15 tu. Mfano mimi ni Web Designer. Ila naweza Design Apps za Android pia, hivyo nayo ntaichagua pamoja na programming languages ninazofahamu, PhP, Javascript, HTML5 na CSS3. Pia mambo kama UI Design, Debugging na Optimisation yako related na nnayafamu hivyo ntayalist.

Baada ya hapo , kinachofuata ni kuandika Bio yako; ambapo kuna kichwa na maelezo(niliyoficha). Hivi vina play part yake kwenye kudetermine kama watakupa kazi au kukuacha. Ndo maana nikasema kuji brand ni muhimu.

Kujibrand Kwenyewe

🏷 Heading

Heading yangu ni simple, ila creative: "I turn crazy ideas into websites, even apps | 5 years experience."

Hio inatosha kumpa idea anaetoa gig mimi ni mtu wa aina gani. Moja, kuweka neno 'crazy' ni kwamba naweza kabiri concept ngumu likija swala la kutengeneza dynamic websites na apps. Na sentence ya pili inasema nina experience ya miaka 5. Hivyo sijaanza jana.

Lastly, ni title yenyewe haiko formal hivyo kuonesha nina personality sio kujaribu ku impress kwa kuweka uongo (Haha, wakati experience yenyewe ni miaka tatu ya kujifundisha mwenyewe lakini hayupo atakae niuliza 😂😂).

Hivyo kama labda utakuwa unataka kuwa mtafsiri, au video editor. Weka title ambayo sio rahisi kusomeka formally na pie ikutofautishe na wenzio kwa kukupa ka personality.

Tuseme uko fluent kwenye Kiswahili, Kingereza na Kifaransa na unataka fanya kazi za Translation, tumia title ilotulia kama;

"I can change the voice in my head into three different languages (English, Swahili and Français) | Since I was little :)"

Title ya hivyo inaonesha ujuzi wako, experience na personality yako.

🏷 Description

Hii ni mhimu kuiandika kwa kuelezea ni nini unachojua, unakijua toka lini, na ndani ya huo muda umeweza kufanya project zipi na zipi na unalenga wateja wa aina gani.

Link porfolio yako pia. Unaweza pitia bio za wenzio kuona zimeandikwaje, nawe unadike ya kwako ila usi copy na kupaste.

🏷 Accolades

Je kitu unachosema unakifanya umekisomea? Kama ndio kwenye ku edit profile yako, chagua chuo uliko graduate na course uliyosomea. Iwe inaendana na kile unachoenda kuwa unafanya. Kwa Web Design, kama umesoma Computer Science inatosha.

Kama hujasomea bali umejifundisha kienyeji, Jichange uchukue course Udemy hata ya $10 yenye cheti, na uifanye. Then tumia hicho cha Udemy.

Lastly, ni kuverify account. Sio lazima, ila ni mhimu. Baadhi ya Freelancing platforms kuchukua mtihani kwenye kile unachosema unakijua watacharge $5 hadi $15, na kwendana na portfolio yako unaweza usiwe charged.

Kwenye kufanya haya yote, jitahidi kutumia laptop.

Sio mpaka ufaulu maswali yote, ila uki weza 65% kupanda utakuwa verified.

Fungua account ya Linked pia, for clarity.

🏷 Pricing

Kabla huja decide utakuwa unalipwa dollar ngapi kwa saa, angalia freelancer wengine wanatoa kwa bei gani. Ili usi overcharge.

Kwenye web design nacharge $7/hour. Na sio shida. Kumbuka una lenga ku deal na waAfrika sio wazungu.

Baada ya kumaliza hayo yote, twende kwenye kutafuta hizo kazi.

Kazi Zenyewe

Fact ambazo wengi wanazisahau ni kuwa kwenye Africa yetu hii hii, zipo nchi zinaendelea na zina presence online kama Misri, South , Kenya na Nigeria na baadhi ya makampuni na mashirika huweka kazi zao mtandaoni zifanywe na freelancers.

Freelancer wenye akili, ni wakenya maana wao wanajishulisha na hizi, huku wengi ambao nimekutana nao kwa Tanzania yetu wanajaribu bahati yao kwa project za wazungu. Nlikuwa nafanya hivyo, na probabilty yakupata kazi, ukiwa mtanzania na account mpya ni karibia na 2%.

Hivyo filter project unazosearch ziwe zinalipa below average na zina toka Africa. Chance yako ya kupata kazi utakuwa umeiboost kwa hadi 75% maana bei za wazungu kwa waafrika zinakuwa kubwa hivyo kama unaonekana uko vizuri kwanini wasikupe kazi wewe?

Changamoto na Ya Kuzingatia

Changamoto kubwa utakayokutana nayo ni namna ya kupokea malipo. Jitahidi kupata account ya PayPal unayoweza tumia kupokea hela. Unaweza tafuta line za Safaricom Kenya, etc na kuitumia kuactivate then ukailink na kadi yako ya tz. Au unaweza nicheck kutengenezewa account iliyo complete.

Nyingine ni namna ya kuprove umefanya kazi kwa masaa husika. Jitahidi kazi zako za kwanza uzifanya kwa wepesi ili uwe na Success score kubwa. Ila ukiziwaisha saana utalipwa kidogo, maana point ya kufanya kazi kwa masaa ni unalipwa kwendana na idadi ya masaa ulofanya kazi.

Kama ni kazi kama Transcription, Web Design, ku edit, copywriting au kutranslate maneno na utafanya kwa computer, tumia Screen recorder ku record session zako.

Au piga Screenshot kila baada ya lisaa. Maana waafrika kwenye mambo ya hela mambo mengi.


Mwisho ni jaribu jenga mazingira mazuri ya kupewa kazi za kurudi, ukijenga unaweza ombwa namba na kuanza hata kupewa kazi nje ya UpWork.

Mwisho

Nimefanya kazi 18 kwenye hio UpWork, lakini hizo ni kampuni nne tu. Inamaanisha wananipa kazi za kujirudia. Kampuni mbili za WaKenya (Ipo shule private, na Kampuni ya Insurance) na Moja ya wa South na nyingine ya Nigeria. Mambo kama SEO, Kuwatengenezea apps, directories, learning portals, ad campaigns, etc. So nawe waeza fanya kazi diverse pia.

Wa South na hao waNigeria zipo kazi, wameweza nipa nje ya UpWork. In short nipo kama Tech Support wa tovuti zao endapo kitu kikitokea. Point ni kuwa communicative na ongea vizuri, wata kuconsider, sio kama ilivyo kwa wazungu.

$1k sio nyingi, ningekuwa serious na hizo mambo na kutaka kuifanya fulltime nadhani potential ya kuearn zaidi ipo, sema mambo mengi 🙂.

Changamoto ya kupata gig ya kwanza ukiivuka, kupata kazi nyingine itakuwa sio ngumu kivile tena, pambana, give it your whole, na kwa hako ka muda ambako utakuwa ukisubiri kazi, waweza jiajiri nyumbani kwa style hio maana hizi namna nyingine za kuingiza pesa online nazoshare ( humu na huko kwenye blog) wengine wananambia hawana hela ya kuanzia, so kama unahisi unayo masaa matano per day ya kupoteza , fanya freelancing huku unasubiria ajira au kujiajiri.

Nawasilisha.
 
Mkuu, mimi nina ujuzi aina nne..
3D modelling, video editing, song writing na beat making...
Je nawezaje kuandika profile yangu ili vyote hivyo vionekane?
Inawezekana japo itapunguza credibility score yako. Ila haimaanishi kuwa huwezi exploit hizo skill zako zote nne.

Kwenye hii thread nimejaribu ongelea UpWork lakini UI yake na hizo mambo zote zina apply hata huko Freelancer na Fiverr pia.

Unachoweza kufanya, ni kufungua account inayodeal na skill set moja au kadhaa zinazoelekeana. Kipindi hicho naongeza maarifa nlikua najifunza majitu mengi mengi 😄😄 ko na hio nimefanya pia. Yaani kila skillset unaitengenezea account kwenye site yake.

3D Modelling wafaransa ndo wanaongoza, hata hizi kampuni za Africa zina tend kuhire nje kwa ajili ya hilo. Ila kama uko vizuri kwenye Autodesk Maya na Max, unaweza pata gigs za matangazo ya TV(kama unaweza animate pia). Ila kama umeweza hio 3d Modelling basi nakushauri kujaribu kujifunza Motion Graphics. Hela za wanaigeria nyingi utatoa huko. So hii inaweza kuwa UpWork skill.nyingine ukaweka Fiverr na Freelancer.
 
Mkuu, mimi nina ujuzi aina nne..
3D modelling, video editing, song writing na beat making...
Je nawezaje kuandika profile yangu ili vyote hivyo vionekane?
Skill nyingine ambayo tunashare ni hio Beat making na video editing. Kwa beat making kama uko vizuri, usichukue gigs za ku compose izo beats maana artists wengi wana ma producer wao. Shida ipo kwenye kumix na kumaster.

Kama uko vizuri, unaeza sema uko specilized in Sound Engineering na kwa kuwa ni Creative work, huitaji kuwa unesomea. Mimi nimemaster FL Studio, but DAW unazotumia zikiwa nyingi ndo unprofessional wako utaonekana mkubwa.
So kama uko vizuri kwenye Ableton , CuBase na Pro Tools pia utakula hela za wanaigeria maana wanajua kucompose beat ila kumix na kumaster shida, so gigs za hivyo ni nyingi. Japo utakuta uko limited kwenye masaa utayo spend kwenye project. So hii skillset waweza iweka Fiverr.
 
Skill nyingine ambayo tunashare ni hio Beat making na video editing. Kwa beat making kama uko vizuri, usichukue gigs za ku compose izo beats maana artists wengi wana ma producer wao. Shida ipo kwenye kumix na kumaster.

Kama uko vizuri, unaeza sema uko specilized in Sound Engineering na kwa kuwa ni Creative work, huitaji kuwa unesomea. Mimi nimemaster FL Studio, but DAW unazotumia zikiwa nyingi ndo unprofessional wako utaonekana mkubwa.
So kama uko vizuri kwenye Ableton , CuBase na Pro Tools pia utakula hela za wanaigeria maana wanajua kucompose beat ila kumix na kumaster shida, so gigs za hivyo ni nyingi. Japo utakuta uko limited kwenye masaa utayo spend kwenye project. So hii skillset waweza iweka Fiverr.
Ok, nimekupata mkuu, ngoja nile msuli wa mixing. Kuhusu 3D, naweza kufanya animation pia ali shida ni software ambayo naijua (blender) inaonekana haitambukiwi kama pro 3D software, inachukuliwa poa. Ngoja nile msuli wa motion graphics pia.

Shukran kwa hints mkuu
 
Ok, nimekupata mkuu, ngoja nile msuli wa mixing. Kuhusu 3D, naweza kufanya animation pia ali shida ni software ambayo naijua (blender) inaonekana haitambukiwi kama pro 3D software, inachukuliwa poa. Ngoja nile msuli wa motion graphics pia.

Shukran kwa hints mkuu
Sawa sawa.
 
Skill nyingine ambayo tunashare ni hio Beat making na video editing. Kwa beat making kama uko vizuri, usichukue gigs za ku compose izo beats maana artists wengi wana ma producer wao. Shida ipo kwenye kumix na kumaster.

Kama uko vizuri, unaeza sema uko specilized in Sound Engineering na kwa kuwa ni Creative work, huitaji kuwa unesomea. Mimi nimemaster FL Studio, but DAW unazotumia zikiwa nyingi ndo unprofessional wako utaonekana mkubwa.
So kama uko vizuri kwenye Ableton , CuBase na Pro Tools pia utakula hela za wanaigeria maana wanajua kucompose beat ila kumix na kumaster shida, so gigs za hivyo ni nyingi. Japo utakuta uko limited kwenye masaa utayo spend kwenye project. So hii skillset waweza iweka Fiverr.
Sawa mkuu.

Nadhani ipo haja ya mimi kujifunza softwares ambazo zinatambulika kama professional softwares. Maana kwenye beat making mi natumia Cakewalk anmbayo ni open source na kwenye 3D natumia blender ambayo ni open source pia.
 
Sawa mkuu.

Nadhani ipo haja ya mimi kujifunza softwares ambazo zinatambulika kama professional softwares. Maana kwenye beat making mi natumia Cakewalk anmbayo ni open source na kwenye 3D natumia blender ambayo ni open source pia.
Anha sawa, Open Source hao jamaa hawazutambui maana hazifundishwi vyuoni.

Kungekua hakuna haja ya kuscreen record kazi kudetermine utalipwa sh ngapi, ungelist kule hizo pro soft kakin ukabaki tumia hizo open source jufanya kazi
 
Anha sawa, Open Source hao jamaa hawazutambui maana hazifundishwi vyuoni.

Kungekua hakuna haja ya kuscreen record kazi kudetermine utalipwa sh ngapi, ungelist kule hizo pro soft kakin ukabaki tumia hizo open source jufanya kazi
Shukran mkuu, hapo lazima cracks zihusike, au pia ukitumia cracked software inapunguza credibility?
 
Back
Top Bottom