Hivi hii ni HABARI LEO au habari jana.........??MALALAMIKO ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya kampeni za mgombea urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa kuwa zimejaa matusi, yalidhihiri jana pale kampeni za mgombea huyo zilipotumika kumtukana Rais Jakaya Kikwete na mama yake mzazi.
Kabla ya kuanza kumtukana Rais wa nchi ambaye pia ni mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Slaa mwenyewe alitamba kuwa katika viwanja hivyo vya Mwembeyanga, Temeke ndipo alipotoa tuhuma dhidi ya viongozi wengine bila kushitakiwa wala kukamatwa.
Dk. Slaa ambaye alianza hotuba yake kwa kutoa maneno machafu dhidi ya CCM na viongozi wake na kutumia muda kidogo kuelezea hoja za Ilani ya uchaguzi ya chama chake na kujibu hoja za wapinzani wake, kabla ya kumaliza alitoa nafasi kwa mgombea ubunge wa Temeke kuonesha umahiri wa kujenga hoja.
Mbali na kumpa nafasi mgombea huyo aoneshe umahiri huo kwa dakika mbili ili apimwe kama anaweza kutumia dakika tatu wanazopewa wabunge kujenga hoja bungeni, Dk. Slaa aliwaomba wananchi wampigie kura mgombea huyo, kwa kuwa kupitia wagombea wa ubunge wa Chadema akiwemo huyo, ndipo anapotarajiwa kumpata Waziri Mkuu na mawaziri wengine wasiozidi 20.
Hata hivyo mgombea huyo, Dickson Amos, alitumia nafasi hiyo kumtukana matusi ya kumdhalilisha Rais Kikwete na mama yake mzazi na kusababisha matangazo ya moja kwa moja ya TBC1 kutoka katika viwanja hivyo, kukatishwa ghafla ili kustahi ustaarabu wa jamii ya kitanzania.
Matusi hayo ambayo ni aibu kuyaandika, yalitolewa katika mkutano wa hadhara na uliokuwa ukisikilizwa na wasikilizaji mbalimbali wa TBC 1 nchi nzima.
Katika muda mfupi alioutumia kujibu hoja zilizoelekezwa kwake na wapinzani wake kisiasa, Dk. Slaa alisema hahitaji shahada ya uzamivu kwa ajili ya kusimamia masuala ya uchumi wa nchi.
Alikiri kweli yeye ni mbumbumbu wa uchumi kwa sababu amesomea sheria, lakini uchumi aliosoma mwaka 1972 unatosha kujua hali ya Mtanzania na jinsi ya kumsaidia.
Alikuwa akimjibu Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala aliyesema mgombea huyo hajui mambo ya uchumi na kumtaka aache kuyajadili.
Aliwataka Watanzania kumpatia wabunge wengi wa Chadema ambao watafuta sheria iliyopandisha bei ya bati na ya saruji na kudai kuwa Watanzania wanalipa kodi nyingi katika bidhaa zao kuliko hata ilivyo kwa nchi za Afrika Mashariki.
"Kama Dk. Kamala haelewi ninachosema akasome gazeti la East Afrika ukurasa wa tatu, ila nina mashaka kama anajua Kiingereza vizuri… na afahamu kuwa Dk. Slaa ni rais wa Watanzania na sio wa Afrika Mashariki," alisema na kuongeza kuwa yuko tayari kufuta mikataba yote inayowaumiza wananchi.
Source: Habari leo 27/10/2010
Kuna watu wanavihere here sana hapa!
Leo katika taarifa ya habari channel ten nimemwona kikwete akisema kwamba ametukanwa na wapinzani wana midomo michafu iliyojaa matusi. baadae wakaonesha kinana akisema kwamba watashtaki tume kuwa wametukanwa.
Nonsese kabisa!!!! Acheni hizo Habari Leo -- tunawafahamu nyie ni mawakala wa CCM pamoja na kwamba mnalipwa kutokana na kodi zetu. Hamujwezi kuongeza mauzo ya gazeti lenu kwa crap ya namna hii Niliiangalia hotuba yote live -- hakuna matusi -- ni shutuma juu ya shutuma ya utawala mbovu wa JK, binafsi kupenda anasa badala ya kushughulikia umasikini wa Wananchi, kuwalea mafisadi na kuwapigia debe pamoja na kwamba wana kesi mahakamani.
Dr Slaa alisema pamoja na JK kuwa mbunge wa Bagamoyo karibu 20 yrs, hakufanya lolote, watu wengi wa kwake huko ni masikini sana, atafanyaje kwa Tanzania nzima?
Aliloambiwa JK ni hali halisi ya utawala wake, na si matusi, labda tu hayo yalitamkwa kwa njia ya ukali, kwani afanyayo rais huyu yanaudhi kwelikweli!!!
Sasaungefafanua tusi liko wapi? Hivi wewe unaridhika na CCM inavyoendeshwa kifamilia?Rais kuwasafisha mafisadi ni sawa? Ina maana hana washauri au hasikii la Mtu? Sasaasiyefunzwa na Mamaye ni yupe kama si huyo anayekiuka katiba aliyoapa kuilinda.Fafanua au na wewe tukuone ni haohao."..........Matusi hayo ambayo ni aibu kuyaandika, yalitolewa katika mkutano wa hadhara na uliokuwa ukisikilizwa na wasikilizaji mbalimbali wa TBC 1 nchi nzima........"
Mhhh sidhani kama alivyosema mwandishi wa habari leo kuwa ni sahihi yaani matusi hayo ni mazito hayafai kutajwa. Bahati nzuri mwenyewe nimeyasikia LIVE, alichosema yule mgombea ubunge wa Chadema (jimbo la temeke) japo siafikiani naye kwa maana kumuhusisha mzazi wa mtu ktk issues ambazo yeye hahusiki ni makosa kimsingi. Kama huyo jamaa anasema JK hakufundishwa na mama yake ndio maana anafanya kama anavyofanya, kwa mtazamo wangu NAFIKIRI HATA HUYU MGOMBEA UBUNGE WA CHADEMA NAYE PIA HAJAFUNDISHWA NA MAMA YAKE, MAANA KWA MWENYE AKILI YEYOTE ASINGESEMA KAMA ALIVYOSEMA. JAMII YETU INATUFUNDISHA KUHESHIMU WATU WAZIMA, HATA KAMA SI MZAZI WAKO. UNAPOMTUSI MZAZI WA MWENZIO NI SAWA NA KUMTUSI MZAZI WAKO.
BAADA YA KUMSIKILIZA HUYU MGOMBEA UBUNGE WA CHADEMA NAPATA WASIWASI KAMA KWELI HUYU JAMAA NI MWANACHADEMA DAMU DAMU NA SIO MTU ALOPANDIKIZWA ILI CHADEMA WALIKOSE JIMBO HILO. KABLA YA MATUSI YA HUYO JAMAA NILIAMINI KUWA MWAKA HUU CHADEMA ITAPATA MAJIMBO YOTE YA DAR, LAKINI BAADA YA MATUSI YA HUYO JAMAA NIKASIKITIKA SAANA NA KUSEMA BASI CHADEMA WESHAPOTEZA HILO JIMBO. NAWAOMBA SAANA VIONGOZI WA JUU WA CHADEMA KUWA KWA MUDA ULIOBAKI WAJIEPUSHE NA BLANDA KAMA ALIZOFANYA HUYU JAMAA HIYO JANA
Kama ninavyosema humu wengi ni CHADEMA. Kwangu mkishinda itakuwa heri kwa kuwa yale mnayodhani sio matusi ndiyo tutakayomtamkia DR Slaa atakapokuwa Raisi, tuone kama mtastahimili. Hatahivyo nina uhakika hamtashinda kwa kura kiduchu za humu. TCHAOOOOOO!Habari Leo!!! Duh!! Kwanza hata hawajui kwa nini watu wana chuki dhidi ya CCM na JK wao!!! Wapinzani wanahangaika viwanja vya kufanyia mikutano kutokana na roho mbaya ya CCM -- wanawakatalia viwanja walivyopora!!! Hii ni roho mbaya sana -- inaudhi na inapandisha hasira.
Nalichukia hili gazeti kwa moyo wangu wote, nawe mhariri mkuu ukae mkao wa kufunga virago nchi itakaporudishwa kwa watanzania wenyewe hapo october 31.MALALAMIKO ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya kampeni za mgombea urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa kuwa zimejaa matusi, yalidhihiri jana pale kampeni za mgombea huyo zilipotumika kumtukana Rais Jakaya Kikwete na mama yake mzazi.
Kabla ya kuanza kumtukana Rais wa nchi ambaye pia ni mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Slaa mwenyewe alitamba kuwa katika viwanja hivyo vya Mwembeyanga, Temeke ndipo alipotoa tuhuma dhidi ya viongozi wengine bila kushitakiwa wala kukamatwa.
Dk. Slaa ambaye alianza hotuba yake kwa kutoa maneno machafu dhidi ya CCM na viongozi wake na kutumia muda kidogo kuelezea hoja za Ilani ya uchaguzi ya chama chake na kujibu hoja za wapinzani wake, kabla ya kumaliza alitoa nafasi kwa mgombea ubunge wa Temeke kuonesha umahiri wa kujenga hoja.
Mbali na kumpa nafasi mgombea huyo aoneshe umahiri huo kwa dakika mbili ili apimwe kama anaweza kutumia dakika tatu wanazopewa wabunge kujenga hoja bungeni, Dk. Slaa aliwaomba wananchi wampigie kura mgombea huyo, kwa kuwa kupitia wagombea wa ubunge wa Chadema akiwemo huyo, ndipo anapotarajiwa kumpata Waziri Mkuu na mawaziri wengine wasiozidi 20.
Hata hivyo mgombea huyo, Dickson Amos, alitumia nafasi hiyo kumtukana matusi ya kumdhalilisha Rais Kikwete na mama yake mzazi na kusababisha matangazo ya moja kwa moja ya TBC1 kutoka katika viwanja hivyo, kukatishwa ghafla ili kustahi ustaarabu wa jamii ya kitanzania.
Matusi hayo ambayo ni aibu kuyaandika, yalitolewa katika mkutano wa hadhara na uliokuwa ukisikilizwa na wasikilizaji mbalimbali wa TBC 1 nchi nzima.
Katika muda mfupi alioutumia kujibu hoja zilizoelekezwa kwake na wapinzani wake kisiasa, Dk. Slaa alisema hahitaji shahada ya uzamivu kwa ajili ya kusimamia masuala ya uchumi wa nchi.
Alikiri kweli yeye ni mbumbumbu wa uchumi kwa sababu amesomea sheria, lakini uchumi aliosoma mwaka 1972 unatosha kujua hali ya Mtanzania na jinsi ya kumsaidia.
Alikuwa akimjibu Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala aliyesema mgombea huyo hajui mambo ya uchumi na kumtaka aache kuyajadili.
Aliwataka Watanzania kumpatia wabunge wengi wa Chadema ambao watafuta sheria iliyopandisha bei ya bati na ya saruji na kudai kuwa Watanzania wanalipa kodi nyingi katika bidhaa zao kuliko hata ilivyo kwa nchi za Afrika Mashariki.
Kama Dk. Kamala haelewi ninachosema akasome gazeti la East Afrika ukurasa wa tatu, ila nina mashaka kama anajua Kiingereza vizuri na afahamu kuwa Dk. Slaa ni rais wa Watanzania na sio wa Afrika Mashariki, alisema na kuongeza kuwa yuko tayari kufuta mikataba yote inayowaumiza wananchi.
Source: Habari leo 27/10/2010
Dream!Nalichukia hili gazeti kwa moyo wangu wote, nawe mhariri mkuu ukae mkao wa kufunga virago nchi itakaporudishwa kwa watanzania wenyewe hapo october 31.