Upuuzi wa TBC1: Rais Kikwete atukanwa 'live'

MALALAMIKO ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya kampeni za mgombea urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa kuwa zimejaa matusi, yalidhihiri jana pale kampeni za mgombea huyo zilipotumika kumtukana Rais Jakaya Kikwete na mama yake mzazi.

Kabla ya kuanza kumtukana Rais wa nchi ambaye pia ni mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Slaa mwenyewe alitamba kuwa katika viwanja hivyo vya Mwembeyanga, Temeke ndipo alipotoa tuhuma dhidi ya viongozi wengine bila kushitakiwa wala kukamatwa.

Dk. Slaa ambaye alianza hotuba yake kwa kutoa maneno machafu dhidi ya CCM na viongozi wake na kutumia muda kidogo kuelezea hoja za Ilani ya uchaguzi ya chama chake na kujibu hoja za wapinzani wake, kabla ya kumaliza alitoa nafasi kwa mgombea ubunge wa Temeke kuonesha umahiri wa kujenga hoja.

Mbali na kumpa nafasi mgombea huyo aoneshe umahiri huo kwa dakika mbili ili apimwe kama anaweza kutumia dakika tatu wanazopewa wabunge kujenga hoja bungeni, Dk. Slaa aliwaomba wananchi wampigie kura mgombea huyo, kwa kuwa kupitia wagombea wa ubunge wa Chadema akiwemo huyo, ndipo anapotarajiwa kumpata Waziri Mkuu na mawaziri wengine wasiozidi 20.

Hata hivyo mgombea huyo, Dickson Amos, alitumia nafasi hiyo kumtukana matusi ya kumdhalilisha Rais Kikwete na mama yake mzazi na kusababisha matangazo ya moja kwa moja ya TBC1 kutoka katika viwanja hivyo, kukatishwa ghafla ili kustahi ustaarabu wa jamii ya kitanzania.

Matusi hayo ambayo ni aibu kuyaandika, yalitolewa katika mkutano wa hadhara na uliokuwa ukisikilizwa na wasikilizaji mbalimbali wa TBC 1 nchi nzima.

Katika muda mfupi alioutumia kujibu hoja zilizoelekezwa kwake na wapinzani wake kisiasa, Dk. Slaa alisema hahitaji shahada ya uzamivu kwa ajili ya kusimamia masuala ya uchumi wa nchi.

Alikiri kweli yeye ni mbumbumbu wa uchumi kwa sababu amesomea sheria, lakini uchumi aliosoma mwaka 1972 unatosha kujua hali ya Mtanzania na jinsi ya kumsaidia.

Alikuwa akimjibu Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala aliyesema mgombea huyo hajui mambo ya uchumi na kumtaka aache kuyajadili.

Aliwataka Watanzania kumpatia wabunge wengi wa Chadema ambao watafuta sheria iliyopandisha bei ya bati na ya saruji na kudai kuwa Watanzania wanalipa kodi nyingi katika bidhaa zao kuliko hata ilivyo kwa nchi za Afrika Mashariki.

"Kama Dk. Kamala haelewi ninachosema akasome gazeti la East Afrika ukurasa wa tatu, ila nina mashaka kama anajua Kiingereza vizuri… na afahamu kuwa Dk. Slaa ni rais wa Watanzania na sio wa Afrika Mashariki," alisema na kuongeza kuwa yuko tayari kufuta mikataba yote inayowaumiza wananchi.

Source: Habari leo 27/10/2010
Hivi hii ni HABARI LEO au habari jana.........??
 
Kwa nini munashambulia gazeti badala ya kujibu hoja kama aliyoyasema huyo mgombea ubunge ni sahihi au siyo katika mila za hapa kwetu Tanzania?

Nadhani haifai kwenda kwenye extreme na kuanza kumsema mama yake fulani hana adabu. Jee ingekuwa ni wewe ungefurahi kutukanwa mama yako kwa kuambiwa hakukufunza?

Wazee wetu lazima tuwaheshimu na inatia uchungu kama mtu atakutukania au kumkejeli mzazi wako.
 
wapinzani ni fotokopi sawsawa? kikwete hajafunzwa na mamaye sawasawa? anayeona katukanwa aende mahakamani.binafsi sipendi matusi awe mdogo au mkubwa ila nasisitiza asiye na adabu afunzwe adabu j"pili.
 
sidhani kama ni matusi ambayo hayawezi kuandikwa ila si kwamba ninasupport maneno hayo laikini nionavyo huyu mwandishi naye ameyakuza sana:bowl:
 
Angalizo:
Dickson Amos Ng'hily alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha CCJ (Bara) kilichokufa na baadaye kuhamia CHADEMA July 2010, Hivyo bado hajakomaa sana ndani ya CHADEMA inabidi tumpige semina na msasa wa namna gani ya kuongea ukiwa mwanasiasa. Maana unaweza kutumia methali nzuri lakini isipostahili na wapinzani wako(CCM) wakaigeuza wanavyotaka wao ieleweke na kuishia kukaangwa na jamii kisiasa.
 
Kuwa mjinga ni kufanywa mjinga, usikubali kuwa mjinga kwa kufanywa mjinga. Haa haaaa mkuu bado unasoma magazeti ya udaku ya ccm pole sana. Ila usiwe unatuletea sisi hapa.
 
Leo katika taarifa ya habari channel ten nimemwona kikwete akisema kwamba ametukanwa na wapinzani wana midomo michafu iliyojaa matusi. baadae wakaonesha kinana akisema kwamba watashtaki tume kuwa wametukanwa.

Halafu sijaona channel ten wakitoa habari za mgombea hata wa cuf au yeyote wa uchaguzi zaidi ya wa ccm. halafu kwenye matangazo ya mapumziko ya habari wanatangaza ccm. sasa najiuliza hawa kweli ndo wale ambao walishikia kidedea kuhusu north mara? mbona wapo sooo pro kikwete badala pro tanzanians?

Kuna haja ya hizi taasisi kushtakiwa baada ya uchaguzi ili wawajibishwe kwa sheria zilizopo kwani mkiwapeleka tume ya mawasiliano wataishia kupewa barua ya onyo tu wala hawatajifunza
 
Nakubaliana asilimia mia moja na wanaopinga alichokifanya huyu Dickson Amos Ng'hily, kwa kweli si uungwana kabisa sababu chama chetu ni cha kiungwana. Huyu jamaa amekosa umakini na hajui matumizi mazuri ya muda. Nafkiri hata kwa waliofuatilia wanaweza kusema kwamba hicho kitendo chake hakikupokelewa vizuri hata na waliokua wakimsikiliza. Kwa nini wameamua kumsimamisha mtu ambaye hajakomaa CHADEMA?

Dkt ni mtu makini sana na naamini wengi wenu mlimuelewa alichokisema mwisho kuhusu nini kifanyike kama ukifanyiwa kitu cha kuudhiwa (Lugha mbaya) na watu wanaoamini chama kingine. Unawedha kufahamu (Kwa mtazamo wangu) Alikua akimfunza Bw. Ng'hily jinsi ya kupambana na wenzetu maana wao wamezoea kufanya hivyo.

Leo katika taarifa ya habari channel ten nimemwona kikwete akisema kwamba ametukanwa na wapinzani wana midomo michafu iliyojaa matusi. baadae wakaonesha kinana akisema kwamba watashtaki tume kuwa wametukanwa.

TBC mkuu wetu kasema wenzie MAJUHA yaani wale waliokutana jana Mwembe Yanga! Pia ametumia matusi, lakini hii inaonesha ni kwa kiasi gani huyu jamaa hastahili kuongezewa miaka mitano ijayo maana anamkimbiza kichaa aliechukua nguo zake wakati yeye anaoga mtoni.
 
:nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono: sijaona tusi,dk slaa yupo sahihi na huyo mbunge yupo sahihi
 
Mbunge yuko sahihi kabisa. Kwani Kikwete alivyosema watu wenye ukimwi wameupata kwa sababu ya kiherehere chako hakua amewakosea adabu hao watu? Kwani Kikwete alivyosema wanafunzi wanaopata mimba wamepata hizo mimba kwa sababu ya kiherehere chako hakua amewakose adabu hao wanafunzi? Kikwete hana adabu tena hana adabu sana tu. Na kama mama yake alimfundisha adabu, sasa mbona hatuoni kama anayo. Kwa baadhi yetu, tunaona kuwa mama yake ka alimfunza adabu hakuielewa au hakumfunza kabisa. Ni wajibu wetu sisi sasa tumfunze hio adabu.
 
Nonsese kabisa!!!! Acheni hizo Habari Leo -- tunawafahamu nyie ni mawakala wa CCM pamoja na kwamba mnalipwa kutokana na kodi zetu. Hamujwezi kuongeza mauzo ya gazeti lenu kwa crap ya namna hii Niliiangalia hotuba yote live -- hakuna matusi -- ni shutuma juu ya shutuma ya utawala mbovu wa JK, binafsi kupenda anasa badala ya kushughulikia umasikini wa Wananchi, kuwalea mafisadi na kuwapigia debe pamoja na kwamba wana kesi mahakamani.

Dr Slaa alisema pamoja na JK kuwa mbunge wa Bagamoyo karibu 20 yrs, hakufanya lolote, watu wengi wa kwake huko ni masikini sana, atafanyaje kwa Tanzania nzima?

Aliloambiwa JK ni hali halisi ya utawala wake, na si matusi, labda tu hayo yalitamkwa kwa njia ya ukali, kwani afanyayo rais huyu yanaudhi kwelikweli!!!

Mkuu labda matusi ni kusoma report ya kawambwa ya utekelezaji wa ilani ya CCM bagamoyo ambayo matundu manne ya choo yamejengwa kwa mil 700
 
"..........Matusi hayo ambayo ni aibu kuyaandika, yalitolewa katika mkutano wa hadhara na uliokuwa ukisikilizwa na wasikilizaji mbalimbali wa TBC 1 nchi nzima........"

Mhhh sidhani kama alivyosema mwandishi wa habari leo kuwa ni sahihi yaani matusi hayo ni mazito hayafai kutajwa. Bahati nzuri mwenyewe nimeyasikia LIVE, alichosema yule mgombea ubunge wa Chadema (jimbo la temeke) japo siafikiani naye kwa maana kumuhusisha mzazi wa mtu ktk issues ambazo yeye hahusiki ni makosa kimsingi. Kama huyo jamaa anasema JK hakufundishwa na mama yake ndio maana anafanya kama anavyofanya, kwa mtazamo wangu NAFIKIRI HATA HUYU MGOMBEA UBUNGE WA CHADEMA NAYE PIA HAJAFUNDISHWA NA MAMA YAKE, MAANA KWA MWENYE AKILI YEYOTE ASINGESEMA KAMA ALIVYOSEMA. JAMII YETU INATUFUNDISHA KUHESHIMU WATU WAZIMA, HATA KAMA SI MZAZI WAKO. UNAPOMTUSI MZAZI WA MWENZIO NI SAWA NA KUMTUSI MZAZI WAKO.
BAADA YA KUMSIKILIZA HUYU MGOMBEA UBUNGE WA CHADEMA NAPATA WASIWASI KAMA KWELI HUYU JAMAA NI MWANACHADEMA DAMU DAMU NA SIO MTU ALOPANDIKIZWA ILI CHADEMA WALIKOSE JIMBO HILO. KABLA YA MATUSI YA HUYO JAMAA NILIAMINI KUWA MWAKA HUU CHADEMA ITAPATA MAJIMBO YOTE YA DAR, LAKINI BAADA YA MATUSI YA HUYO JAMAA NIKASIKITIKA SAANA NA KUSEMA BASI CHADEMA WESHAPOTEZA HILO JIMBO. NAWAOMBA SAANA VIONGOZI WA JUU WA CHADEMA KUWA KWA MUDA ULIOBAKI WAJIEPUSHE NA BLANDA KAMA ALIZOFANYA HUYU JAMAA HIYO JANA
Sasaungefafanua tusi liko wapi? Hivi wewe unaridhika na CCM inavyoendeshwa kifamilia?Rais kuwasafisha mafisadi ni sawa? Ina maana hana washauri au hasikii la Mtu? Sasaasiyefunzwa na Mamaye ni yupe kama si huyo anayekiuka katiba aliyoapa kuilinda.Fafanua au na wewe tukuone ni haohao.
 
Kwa jinsi JK anavyoendesha CCM ni matusi kwani amewatenga waasisi na kukumbatia mafisadi na wanafamilia/marafiki.
 
Mara nyingi inategemea mlengwa atalichukuliaje neno analoambiwa na mwenzake. Kwa hali hiyo neno lolote ukimwambia mtu mwingine lakini yeye akalitafsiri kimatusi linaweza kuwa ni tusi kwake. Lakini katika hili hakuna tusi, hapa ni kuonyesha umahiri katika lugha yetu ya kiswahili ambayo bahati mbaya sana kwasasa Watanzania wengi inatupiga chenga. Mgombea ubunge jimbo la Temeke kupitia CHADEMA, katika kusisitiza hoja yake alimalizia na methali -"asiyefunzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu". Hii ni methali nzuri tuu ya kiswahili na wala katika matusi yaliyomo kwenye kamusi haipo. Kama CCM wameshitaki ilhali wao ndio waoongoza kwa kutukana washindani, basi swali kwao ni hili: mkuki kwa nguruwe kwa binaadamu mchungu? au chongo kwa mnyamwezi kwa mzaramo ni kengeza?

"Moringe wote ni wamasai lakini sio kila mmasai ni Moringe"
 
Habari Leo!!! Duh!! Kwanza hata hawajui kwa nini watu wana chuki dhidi ya CCM na JK wao!!! Wapinzani wanahangaika viwanja vya kufanyia mikutano kutokana na roho mbaya ya CCM -- wanawakatalia viwanja walivyopora!!! Hii ni roho mbaya sana -- inaudhi na inapandisha hasira.
Kama ninavyosema humu wengi ni CHADEMA. Kwangu mkishinda itakuwa heri kwa kuwa yale mnayodhani sio matusi ndiyo tutakayomtamkia DR Slaa atakapokuwa Raisi, tuone kama mtastahimili. Hatahivyo nina uhakika hamtashinda kwa kura kiduchu za humu. TCHAOOOOOO!
 
MALALAMIKO ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya kampeni za mgombea urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa kuwa zimejaa matusi, yalidhihiri jana pale kampeni za mgombea huyo zilipotumika kumtukana Rais Jakaya Kikwete na mama yake mzazi.

Kabla ya kuanza kumtukana Rais wa nchi ambaye pia ni mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Slaa mwenyewe alitamba kuwa katika viwanja hivyo vya Mwembeyanga, Temeke ndipo alipotoa tuhuma dhidi ya viongozi wengine bila kushitakiwa wala kukamatwa.

Dk. Slaa ambaye alianza hotuba yake kwa kutoa maneno machafu dhidi ya CCM na viongozi wake na kutumia muda kidogo kuelezea hoja za Ilani ya uchaguzi ya chama chake na kujibu hoja za wapinzani wake, kabla ya kumaliza alitoa nafasi kwa mgombea ubunge wa Temeke kuonesha umahiri wa kujenga hoja.

Mbali na kumpa nafasi mgombea huyo aoneshe umahiri huo kwa dakika mbili ili apimwe kama anaweza kutumia dakika tatu wanazopewa wabunge kujenga hoja bungeni, Dk. Slaa aliwaomba wananchi wampigie kura mgombea huyo, kwa kuwa kupitia wagombea wa ubunge wa Chadema akiwemo huyo, ndipo anapotarajiwa kumpata Waziri Mkuu na mawaziri wengine wasiozidi 20.

Hata hivyo mgombea huyo, Dickson Amos, alitumia nafasi hiyo kumtukana matusi ya kumdhalilisha Rais Kikwete na mama yake mzazi na kusababisha matangazo ya moja kwa moja ya TBC1 kutoka katika viwanja hivyo, kukatishwa ghafla ili kustahi ustaarabu wa jamii ya kitanzania.

Matusi hayo ambayo ni aibu kuyaandika, yalitolewa katika mkutano wa hadhara na uliokuwa ukisikilizwa na wasikilizaji mbalimbali wa TBC 1 nchi nzima.

Katika muda mfupi alioutumia kujibu hoja zilizoelekezwa kwake na wapinzani wake kisiasa, Dk. Slaa alisema hahitaji shahada ya uzamivu kwa ajili ya kusimamia masuala ya uchumi wa nchi.

Alikiri kweli yeye ni mbumbumbu wa uchumi kwa sababu amesomea sheria, lakini uchumi aliosoma mwaka 1972 unatosha kujua hali ya Mtanzania na jinsi ya kumsaidia.

Alikuwa akimjibu Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala aliyesema mgombea huyo hajui mambo ya uchumi na kumtaka aache kuyajadili.

Aliwataka Watanzania kumpatia wabunge wengi wa Chadema ambao watafuta sheria iliyopandisha bei ya bati na ya saruji na kudai kuwa Watanzania wanalipa kodi nyingi katika bidhaa zao kuliko hata ilivyo kwa nchi za Afrika Mashariki.

“Kama Dk. Kamala haelewi ninachosema akasome gazeti la East Afrika ukurasa wa tatu, ila nina mashaka kama anajua Kiingereza vizuri… na afahamu kuwa Dk. Slaa ni rais wa Watanzania na sio wa Afrika Mashariki,” alisema na kuongeza kuwa yuko tayari kufuta mikataba yote inayowaumiza wananchi.

Source: Habari leo 27/10/2010
Nalichukia hili gazeti kwa moyo wangu wote, nawe mhariri mkuu ukae mkao wa kufunga virago nchi itakaporudishwa kwa watanzania wenyewe hapo october 31.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom