Upotoshaji huu wa Gazeti la Jambo Leo ni mpaka lini?

Leo ktk gazeti la Jambo Leo,ukurasa wa kwanza kuna kichwa cha habari kinachosema Chadema Inahusishwa na mashetani,na eti Dr.Slaa ana jini lake linalomsaidia mambo yake ya kisiasa,pia ktk dini hiyo kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Pope naye yumo. Mwandishi amekwenda mbali zaidi kwa kumuhusisha Marehemu Kanumba na hiyo dini ya mashetani.Katika kujenga hoja amewaonyesha viongozi mbalimbali wa Dunia kuwa ni waumini wa dini hyo ya kishetani...
Kwa hili wakubali hata zile alama za V jeshini wanapewa mafree mason
 
ndo tatizo la kuwa na waandishi either mambumbumbu au njaa kali, akiwa mbumbumbu atatenda anachoaminishwa bila kukifikiria yeye binafsi au kuacha anachokiamini, na kama ni njaa kali atatumiwa na wenye pesa kama mtaji tu then baadae atatupwa kapuni. mara nyingi viandishi uchwara vya namna hii ndo vinachelewesha mapinduzi kutoka ktk serikali za kizurumati/kibabe
 
mbaya zaidi katuchonoa hata sisi wakrsto tafadhali mambo ya siasa yaishie kwenye siasa ulikofika kaka damu inanukia DINI NI MAISHA YANGU plz ewe mwandishi wa hilo gazeti tafakari kabla
 
[h=2]Gazeti la Jambo Leo [/h]Mkuu, gazeti la Jambo Leo uandishi wao wakati mwingine unashangaza sana; yaani wananikumbusha hulka za baadhi ya JF members kutoka Kenya ambao wana usongo usio wa kawaida kuhusu TANZANIA, yaani wana mawazo kupofu kupindukia wemeghubikwa na ndoto za kudhani wanaweza ku-control Taifa letu remotely kwa ku-incite wasomaji wa makala zao hili kulifanya TAIFA letu tufalakane kama walivyo KWAO, unaweza kufikili labda nchi yetu ni koloni la Kenya.
 
nafikili ata yeye mwandishi baada ya kusoma makala yake alijiona anaupungufu wa kinga kwenye ubongo wake
 
Kuna waliopeleka sanda lindi wamekufa......leo mhariri...........aliwasema vibaya CDM eti ni mashetani.....wa gazeti hilihili kwa vile aliruhusu tuhuma..........hatunaye tena mhhhhhhhhhh
 
Mimi nashsngaa sana, kwahiyo wanataka kutuambia kuwa jini la Dr. Slaa ndo lilitunga slogan ya CCM ya maisha bora kwa kila m-tz,ambayo sasa kila wakiiona wanakwepa kuiangalia,wanataka kutwambia kuwa hilo jini ndo limepandisha bei ya unga,mchele, sukari, na kila bidhaa kiasi cha wananchi kushindwa kumudu gharama za maisha.

Kwamba hilo jini ndo linaongoza safari za jk na kwamba huwa anasafiri bila kujitambua na hivyo kuwa mzigo kwa taifa, kwamba hilo jini ndo linaleta mgawanyiko ndani ya CCM hadi kufikia viongozi waandamizi wa chama na serikali kusemana majukwaani, hilo jini ndo lilimwekea lusinde matusi mdomoni, hilo jini ndo lilimfanya Mkama kuzungumza kauli za ajabu msibani, hilo jini ndo lilimfanya Wassira asinzie bungeni na hadi kuzomewa jimboni kwake,

Hilo jini ndo linawafanya wananchi wasihudhurie mikutano ya chama hadi wabebwe na mafuso na ahadi za ubwabwa,na kwamba hilo jini ndo linaleta ndege kutoka qatar bila serikali kuwa na habari kisha jini hilo linapakia twiga bila kuonekana,na mengine mengi.Basi hilo jini la Dr.Slaa ni kiboko,na CCM kwani msitafute jini lenu mbona viongozi wa juu kabisa wana uwezo huo. Nawasilisha
 
Wakuu

Sitaenda kwa undani sana juu ya stori hiyo kwa sasa (kwa sababu kadhaa kutopreempty masuala mengine). Lakini natumaini wahusika watakuwa wanafutailia mjadala huu katika forums mbalimbali ambako stori yao inajadiliwa.

Just simple thinking, kwa hiyo wale wapiganaji wote kwenye majeshi yetu wenye alama ya V katika mabega yao kama utambulisho wa vyeo vyao ni wanachama wa kundi lolote la Masonics? Au wakubwa wao wanaowavalisha ndiyo mabosi wao katika Masonics?

Kwa hiyo huwa wanawavalisha utambulisho wa ufuasi wa Papa na makundi ya Masonics? So wanaowavalisha c wanakuwa ndiyo wafuasi wakubwa zaidi maana wanatoa mpaka vyeo kwa hao wenzao wa chini, si ndiyo, kwa logic ya stori hiyo...Haya...

Alisema Shafi Adam Shafi kwenye Kitabu chake cha Kuli, "YANA MWISHO HAYA".

Waambieni tatizo kubwa litakalowaondoa madarakani ni kutojua wajibu wao kwa wananchi na kushindwa kabisa kuwatumikia. Kuiandama taasisi ya CHADEMA na viongozi wake kwa sasa haiwezi kabisa kusaidia badala yake inazidi kuongeza chuki ya wananchi dhidi ya hiyo serikali. Maana CHADEMA si chanzo cha matatizo yanayoisumbua nchi kutokana na uongozi mbovu.

Kuiandama CHADEMA kwa kuizulia masuala ya uongo, uzushi, umbea, propaganda zingine za hatari kabisa hata kuhatarisha msatakabali wa wananchi, hakuisafishi CCM, wala hakutaiponya serikali hii dhaifu.

Tumikieni wananchi, piganieni na wapeni haki zao na matumaini yao. Watawapenda. Lakini kinyume chake ni kwamba wataendelea kuwapenda CHADEMA na viongozi wake maana wamejitoa kuwapigania na kuwatumikia.

Hizi ni dalili nzuri. Ni ishara nzuri sana za watu wanaolalama, wanaoanguka. Ni vyema watetezi wao wakawa makini katika kutafuta hoja na namna ya kuwatetea na kuwabeba. Maana si kila mzigo unabebeka na si kila mtuhumiwa anaweza kutetewa.

kweli kabisa kamanda
 
Vipi kuhusu gazeti la Mbowe, kanisa mkiambiwa ukweli mnatoa mapovu.
 
Huo ni mpango mfu wa kushawishi watu waichukie CDM kwa mambo ya kusadikika, vijigazeti vyenywe hivi vya mfukoni vinaandaliwa sebuleni kwa watu na kutumiwa na vitoto vya watawala kuzima Nguvu ya umma. HATUDANGANYIKI Kamwe?
 
Back
Top Bottom