Kibunango
Platinum Member
- Aug 29, 2006
- 8,423
- 2,272
CUF na CCM... ipi hasa ina asili ya Usultani?Sultani CCM
CUF na CCM... ipi hasa ina asili ya Usultani?Sultani CCM
Wacha ubarakala huo , ila kwa kukusaidia hakuna hata mmoja mwenye asili ya Usulutani ,halafu haiwezekani kuwepo na Masultani wawili au watatu katika Nchi moja ila anakuwepo mmoja na wengine kama wapo inakuwa sio masulutani bali Machifu ambao hawa hupatikana kama wapinzani.CUF na CCM... ipi hasa ina asili ya Usultani?
Tatizo la mwiba ndio walewale anaowazungumza Prof Safari mgando mtupu.Kwenu usultani ni wa asili Maalim sefu miaka nenda rudi badilisheni viongoizi utaona maendeleo ya CUF yanavyobadilika kuelekea kuwa na mafanikio.Kuna jamaa yangu mmoja husema kama mtume Muhammad asingeelezwa kwenye Qur'an ni wa mwisho basi maalim Seif angekuwa ni mtume sasa mawazo kama haya ni mgando mtupu na ndiyo majority ya wana CUF wanayo bila maalim SEif au Prof Lipumba hakuna CUF.Kwa mtaji huo ushindi dhiidi ya SISIM wasahau.CHADEMA itajipatia ushindi2010 kilaini.Mfano mzuri uchaguzi uliopita Hivi karibuni mbeya pamoja na kupiga nyimbo za kwaya CUF na kumuweka menja wa kampeni askofu CUF ilishindwa kwa mbali sana.Nilazima ujute maana itakuwa hakuna tena chauchau ,na kila kitu kitafuata mkondo wa sheria ,rushwa za mabilioni zitakuwa na grade ya uhaini ,polisi atakaejulikana kabambikiza kesi ataenda jela ,yaani kutakuwa na sheria uchwara kibao ambazo zitakufanya uogope hata kutupa karatasi,hapo ndipo utakapoona kuwa bora utawala wa Sultani CCM ukiweza kufungua dirisha kumwaga machicha.
Mwenye asili ni CUF manake wao wanauhusudu kweli kweli Hebu tazama kalenda za CUF ya mwaka 2000 jinsi Siff alivyoonekana sura yake na ndevu alvyozichonga hakuna tofauti na mfalme wa oman ili hali picha iko juu ya wananchi wa zanzibar kichekesho kingine huko zenji kila mwana CUF wakipeleka matangazo ya kifo humtaja maalim Seif apate taarifa swali linakuja hivi maalim Seif anawafahamu wanachama wake wote kwa majinaCUF na CCM... ipi hasa ina asili ya Usultani?
Tatizo CUF wamekariri hoja zao...na sasa zinakera masikioni mwa watu! Kwani hakuna jipya tokea walipomfukuza James Mapalala na hawato kuwa na jipya mpaka Maalim Seif aka Madevu(Sultan wa Ndotoni) atakapo ondolewa katika chama.Najua nimewachoma ila ndio hivyo Sultani CCM lazima aondoke hakuna lugha mbadala hapa,nyie mvisheni vilemba vya ukoka Sultani CCM lakini ajue siku zake zinahesabika ,hilo sio la kulifanyia mzaha.
Na lazima mumtetee Sultani CCM maana siku akiangushwa ndio mwisho wenu wa kuonekana hapa JF
Ama kudai huu ndio mwisho wa CCM ni sawa na kuota mchana kweupe. Endelea na ndoto zako za Alinacha..
Na kufikiri Sultani CCM hawezi kuondoka utawalani ni mazoea ya kutawaliwa na kufanywa mtumwa ndani ya nchi yako.
Najua nimewachoma ila ndio hivyo Sultani CCM lazima aondoke hakuna lugha mbadala hapa,nyie mvisheni vilemba vya ukoka Sultani CCM lakini ajue siku zake zinahesabika ,hilo sio la kulifanyia mzaha.
Na lazima mumtetee Sultani CCM maana siku akiangushwa ndio mwisho wenu wa kuonekana hapa JF
Anyways,huu ni mtizamo wangu tu mkuu,sorry kama nimekukwaza...Be blessed
Unanichekesha, mtumwa unamjua wewe?
Mtumwa ni huyo hapo kati mwenye madevu, yeye na jamaa zake wa kisiwa cha pili ndio watumwa... Na wataendelea kuwa watumwa mpaka pale watakapotia akili vichwani mwao.
...Otherwise nawashauri ninyi CUF mjipange upya kukifufua chama(nilitegemea mngeanza mkakati huu kwa kuwabadilisha viongozi wenu wa kitaifa lakini hola,kwangu mimi mtu kama Lipumba na Seif walitakiwa kupumzika wawapishe wengine nao wajaribu,wao wabaki kuwa wazee washauri tu wa chama),pia kukifanya kiwe cha kitaifa zaidi badala ya cha Kipemba zaidi...
Bw. Balantanda- hapo ndipo lilipo tatizo la CUF. Hawana dira ya kupanua chama chao nje ya Pemba wanaridhika na support kubwa waliyonayo Pemba. Wanasahau kuwa hawana nguvu tena hata kidogo popote pale nje ya Pemba. Hivi Chama kama hicho vipi kitaweza kuongoza Dola (Zanzibar) na Tanzania kwa jumla kwa kutegemea nguvu yake iliyopo Pemba tu. CUF imeshindwa kusambaa Unguja sikwambii Bara. Eti halafu wanakaa na kupiga mayowe tu. sasa sijui wanataka tuvunje sheria zetu za Demokrasia na kukiruhusu hicho Chama ambacho siku zote kitakuwa hakipati ridhaa ya wananchi walio wengi- kiunde Serikali (Kiongoze Dola?)pia kukifanya kiwe cha kitaifa zaidi badala ya cha Kipemba zaidi...
Tatizo kauli yako hii ya kuwaita Masultani ndiyo inachanganya(labda utafute kauli mbiu nyingine) maana katika hali ya kawaida mimi CUF ndio daima mnaonesha chembe za usultani(mabandiko yako hapa yananifanya nikuhusishe moja kwa moja na CUF) tofauti na ilivyo kwa CCM,kwa mfano tangu mfumo wa vyama vingi umeanza mwaka 1992 naona hakuna mabadiliko sana ya kiuongozi katika CUF na wagombea wa urais katika uchaguzi mkuu ni walewale(S.S.Hamad na Prof.Lipumba),ina maana hakuna wana CUF wengine wenye sifa ya kugombea Urais(ama hawa ndo wameandikwa kwamba ni lazima wawe marais),je?,kuna demokrasia ndani ya CUF????(Hapa ndipo chembe mojawapo ya usultani inapojionesha ndani ya CUF)...Vilevile ile hali ya CUF kuweka base yake Pemba zaidi(ambako watu wengi wana asili ya Arabuni walikotokea Masultani) nayo inaonesha 'usultani' wa CUF...Jiulize kwa nini CUF ina wabunge na Wawakilishi wengi toka Pemba tofauti na ilivyo kwa Unguja na Tz Bara(Kumbukumbu zangu zanionesha hawana Mbunge wa kuchaguliwa Bara zaidi ya wale wawili wa kuteuliwa,kama nimekosea hapa nisahihishwe)...CCM yenyewe ina Wabunge toka Bara na Visiwani(japo haijaambulia kitu Pemba) kuwaita ni Masultani unakuwa hauwatendei haki,labda utupe sababu(zinazojitosheleza) za kuwaita wao Masultani...Otherwise nawashauri ninyi CUF mjipange upya kukifufua chama(nilitegemea mngeanza mkakati huu kwa kuwabadilisha viongozi wenu wa kitaifa lakini hola,kwangu mimi mtu kama Lipumba na Seif walitakiwa kupumzika wawapishe wengine nao wajaribu,wao wabaki kuwa wazee washauri tu wa chama),pia kukifanya kiwe cha kitaifa zaidi badala ya cha Kipemba zaidi...Aidha ifikie kipindi wewe Mwiba na wengine muache haya mambo ya kulialia na kushutumu kila wakati(siasa za jazba hazijengi zinabomoa) maana hili ndo linawafanya CHADEMA wawapige bao na kuwa chama kikuu cha upinzani(wamedhihirisha kuwa wana mikakati tofauti na ninyi CUF)...Inafikia kipindi kila nikiiona post ama thread yako mkuu Mwiba najihakikishia kuwa lazima nikutane na malalamiko ya kumwaga bila kusahau neno (ma)sultani CCM(na kweli nakutana nayo)...Anyways,huu ni mtizamo wangu tu mkuu,sorry kama nimekukwaza...Be blessed[/QUOTE
Pengine neno usultani linakukera na hivyo unalihusanisha na UARABU. Kwako usultani maana yake mtawala wa Kiarabu. Usultani ni mamlaka yasiyo na mpinzani juu yake yaani kuendelea kutawala na kutawala kama sio wewe basi mwanao au mpwao au wa ukoo wako. Sasa chukulia utawala wa Zanzibar kwa vitendo na maneno umeshasema kuwa CCM ndiyo yenye haki ya kutawal maisha visiwa vya Zanzibar. Tafadhali nipe jina la utawala wa namna hiyo. Kwa Zanzibar ndugu yangu utapaa shida kuwabaguwa Waarabu na weusi. Naomba fanya utafiti au uulize kwani mfano mmoja tu Amani ni Mwarabu kuliko Seif Sharifu ikiwa rangi ndio kabila.
Kuhusu kuendelea kwa wale wale ndani ya chama cha CUF kipi cha kushangaza? Nakupa mifano na baadae utafakari kwanini hili linatokea. Mkumbuke Odinga Odinga wa Kenya. Jiulize Samuel Malecela alishakuwa Waziri Mkuu kwa nini alitaka Urais hata baada ya kupigwa muhuri na Nyerere? Fanya tafakuri na ujiulize huko CCM zaidi ya Mwenyekiti (anaebanwa na kofia ya Urais kuna mabadiliko gani? Mabadiliko ni wale wachache Rais(anapokuwa Mwenyekiti) anaopenda kuwa nao. Zaidi ya hapo lbda baada ya vifo wabunge wa CCM ni wale wale waliokuwa wakati wa Nyerere.
Lengo langu ni kukuonyesha kuwa siasa zetu WAAFRIKA/Watanzania ni biashara yenye tija na nani yuko tayari kuacha biashara yenye tija.Tusiongozwe na Chuki binafsi za ukabila au dini katika kuchanganua mambo.
Hebu nieleze kipi kinachokushangaza kuona chama fulani kina ngome pahala fulani na kwa upande wa CCM na CUF kule Zanzibar siri ni hii. Kule Unguja Tabaka la waliokuwa nacho walipinduliwa na walio wengi masikini na Mapinduzi hayo yaliwaletea mambo mengi mazuri kwa wakati ule. Elimu bure,ardhi,Matibabu bure na madaraka ambayo waliyakosa wakati wa usultani na kwa hivyo MAPINDUZI ni kila kitu kwao. Waroho wa madaraka kwa kupitia CCM wanalijuwa hilo na hivyo wanatumia propaganda(inayowafika hata nyinyi msiojua hali halisi ya visiwa vile) kuwa upinzani unahujumu Mapinduzi ingawa zile faida zote za Mapinduzi hayo hazipo sasa. Kwa Upande wa Pemba Watawala wa Zanzibar wanaizarau Pemba na watu wake wote na Hivyo mtu yeyote anaewatetea wanamuona kama nusu Mungu. Hapo ndipo CUF wanachukua advantage kwa kupiga kelele za uongo kuitetea Pemba na hivyo Wapemba wataendelea kuwapa sapoti.
Tabia ya kuwadharau wapemba imo ndani ya damu ya Waunguja hivyo inakuwa vigumu kubadilisha tabia yao na kuwaweka daraja sawa. Sasa niambie nini unachotegemea?
Bw. Balantanda- hapo ndipo lilipo tatizo la CUF. Hawana dira ya kupanua chama chao nje ya Pemba wanaridhika na support kubwa waliyonayo Pemba. Wanasahau kuwa hawana nguvu tena hata kidogo popote pale nje ya Pemba. Hivi Chama kama hicho vipi kitaweza kuongoza Dola (Zanzibar) na Tanzania kwa jumla kwa kutegemea nguvu yake iliyopo Pemba tu. CUF imeshindwa kusambaa Unguja sikwambii Bara. Eti halafu wanakaa na kupiga mayowe tu. sasa sijui wanataka tuvunje sheria zetu za Demokrasia na kukiruhusu hicho Chama ambacho siku zote kitakuwa hakipati ridhaa ya wananchi walio wengi- kiunde Serikali (Kiongoze Dola?)
Tabia ya kuwadharau wapemba imo ndani ya damu ya Waunguja hivyo inakuwa vigumu kubadilisha tabia yao na kuwaweka daraja sawa. Sasa niambie nini unachotegemea?
Ndugu yangu Ngekewa Acha hiyo. Haifai staghafiru kidogo. Acha kuwadanganya wale wasioijua au wasiofika Zanzibar. Hivi Wapemba gani wanaodharauliwa? Ni pamoja na wale waishio maisha ya raha kabisa na kutembea na magari ya kifakhari, na kuendesha biashara kubwa kubwa, na kuwa na majumba mazuri mazuri ndani ya Mjini Zanzibar. Unajua adhabu ya watu wanaoshadidia ethnicity. Aste aste-Ndugu yangu.