Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,744
Bw. Balantanda- hapo ndipo lilipo tatizo la CUF. Hawana dira ya kupanua chama chao nje ya Pemba wanaridhika na support kubwa waliyonayo Pemba. Wanasahau kuwa hawana nguvu tena hata kidogo popote pale nje ya Pemba. Hivi Chama kama hicho vipi kitaweza kuongoza Dola (Zanzibar) na Tanzania kwa jumla kwa kutegemea nguvu yake iliyopo Pemba tu. CUF imeshindwa kusambaa Unguja sikwambii Bara. Eti halafu wanakaa na kupiga mayowe tu. sasa sijui wanataka tuvunje sheria zetu za Demokrasia na kukiruhusu hicho Chama ambacho siku zote kitakuwa hakipati ridhaa ya wananchi walio wengi- kiunde Serikali (Kiongoze Dola?)
Wewe Pakacha wacha kuvuja ,nani kakwambia kama CUf ipo Pemba tu au sapoti yake ni Pemba tu, hata Kikwete Mkubwa wa Chama Sultani CCM anafahamu fika kuwa sio Pemba tu bali Zanzibar nzima hakuna hata wacha mtu hata mdudu anampa sapoti sultani CCM vilevile mikoa ya Pwani yote halikadhalika mikoa ya Magharibi yote Sultani CCM hapendwi maana kama kupendwa wale waliosema watajitenga si Wapemba peke yao hata huko Kigoma Kagera walisema hivyohivyo. Watu wamechoka na utawala wa Sultani CCM.
Mnajua wazi leo hii WaZanzibari ukiwaamsha usiku wa manane au wacha hilo wawe wamekunywa ulevi wa tende ,muwaambie wapige kura basi hawamchagui Sultani CCM ni juzi tu mmerusha mapanga pale Magogoni yaani kama mnapendwa na mnajua mnawapenzi yanini kupiga watu mapanga na minyororo huoni kama Sultani CCM ameishiwa na hana wananchi wanaompa sapoti ,ndio maana yake na hapo sio Pemba ni Unguja ,nyie mnasema Unguja ni wafuasi wa Sultani CCM watupu sasa mapanga ya nini ,Kiteto ni wafuasi wa Sultani CCM watupu sasa sime za nini ?
Nyinyi dawa yenu ipo jikoni ,hao mnaowatumia kwenda kupiga watu minyororo na mapanga watakuja kupewa kibano cha mbwa koko mpite mkilia midomo juu.