Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,814
- 11,991
Mnamo Agosti 13, 2023, Waziri Ummy Mwalimu alitoa taarifa kwa Umma ya kueleza kuwa ameunda Kamati ya uchunguzi wa malalamiko ya mitihani ya Watarajali.
Kamati hiyo iliwasilisha ombi kwa Waziri Ummy la kuongezewa muda wa ziada kuendelea kufanya uchunguzi wa kina wa malalamiko ya Watarajali hao na Waziri Ummy alikubali ombi hilo.
Aidha, ikumbukwe kwenye tamko la Waziri Ummy Mwalimu alielekeza Baraza la Madaktari Tanganyika kuendelea kutekeleza majukumu na taratibu nyingine za mafunzo ya Watarajali kama ilivyoainishwa kwenye Sheria mpaka hapo itakavyoelekezwa vinginevyo.
Baraza la Madaktari la Tanganyika (MCT) limeundwa chini ya Kifungu cha 4 cha Sheria ya Udaktari, Udaktari wa Meno na Afya Shirikishi Sura Na. 152 na linatekeleza majukumu yake kuhakikisha jamii inapata huduma nzuri na salama kutoka kwa Wanataaluma wenye sifa. Kwa msingi huo Baraza lina wajibu wa kuhakikisha Wanataaluma wanakuwa na sifa za utendaji kazi unaotakiwa kwa kuzingatia mwenendo na maadili ya kitaaluma.
Tunaomba Watarajali wote wawe na subira na waendelee kufuata maelekezo ya Baraza la Madaktari Tanganyika.