UONGOZI wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, imeomba serikali kuwapatia haraka iwezekanavyo madaktari wengine kuja kuziba nafasi zilizoachwa na madaktari 72 waliotimuliwa hivi karibuni.
Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk. Eliuter Samky alitoa ombi hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro aliyefika hospitalini hapo kuangalia hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa.
Dk. Samky alisema kuondoka kwa madaktari hao kumesababisha huduma katika kitengo cha upasuaji kubakiwa na madaktari bingwa wanne akiwemo na yeye wakati kitengo cha macho hakina daktari kabisa.
Kwa kweli hali ya utoaji huduma imekuwa ngumu sana kwani tuna madaktari 39 tu hospitali nzima na Hospitali ya Wazazi ya Meta ina madaktari wawili tu waliobaki. Kwa kweli tunahitaji nguvu ya madaktari wengine kuja kutusaidia, alisema Dk. Samky.
Akijibu maombi hayo Kandoro alisema kuwa wanafanya utararibu wa kupata madaktari wa upasuaji kutoka katika hospitali za wilaya za Kyela, Mbozi na Rungwe ili kuwapeleka Rufaa kusaidia kukidhi mahitaji ya wagonjwa.
Pia aliwaomba wakazi wa Mkoa wa Mbeya kufuata utaratibu wa kitabibu wa rufani ili kupungunza msongamano mkubwa unaoweza kujitokeza katika hospitali za Rufaa na Mkoa kwa kutibiwa katika Vituo vya Afya badala ya kukimbilia hospitali kubwa.-
Tanzania Daima
Hawa 39 walio baki ni wasaliti wakubwa pumbavu zao wana lialia nini sasa wao si wamejifanya nio marobot wanapiga kazi!
Wapige kazi sasa wasaliti wakubwa nyie kwani madaktari
walio fukuzwa si walikua wana dai maslahi ya wote sasa iweje nyie mnajifanya hayawahusu???
Nyambav!!!!!!!
Kandolo ni mjinga hasitaili kabisa kuwa kiongozi. Sasa anapowatoa huko Kyela na Tukuyu it means hakuna wangonja? Huyu kila sehemu anaharibu, shame on you KandoloHuo ndio ujinga serikali ilivyotimua ilitegemea nini?Hapa liwalo na liwe tu.
Ni kweli kabisa hata mimi sikupenda uwepo kabisa tangu mwanza, lakini suluhisho hapa tulipo ni nini? Je ni kufukuza waliogoma? Nadhani kuna suluhisho bora zaidi kuliko hili, hapa kila upane serikali na madaktari unapaswa kushuka ili kukutana katikati kumnusuru mwananchi anayeumiamgomo wa madaktari hauna tija kwa taifa hasa kwa wananchi maskini.
nawashangaa sana watanzania wanaoshabikia mgomo.
sijui kandoro anamdanganya nani.sasa huko wilayani itakuaje?