Uongozi wa hospitali ya rufaa Mbeya waomba msaada

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
[h=6]UONGOZI wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, imeomba serikali kuwapatia haraka iwezekanavyo madaktari wengine kuja kuziba nafasi zilizoachwa na madaktari 72 waliotimuliwa hivi karibuni.

Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk. Eliuter Samky alitoa ombi hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro aliyefika hospitalini hapo kuangalia hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa.

Dk. Samky alisema kuondoka kwa madaktari hao kumesababisha huduma katika kitengo cha upasuaji kubakiwa na madaktari bingwa wanne akiwemo na yeye wakati kitengo cha macho hakina daktari kabisa.

“Kwa kweli hali ya utoaji huduma imekuwa ngumu sana kwani tuna madaktari 39 tu hospitali nzima na Hospitali ya Wazazi ya Meta ina madaktari wawili tu waliobaki. Kwa kweli tunahitaji nguvu ya madaktari wengine kuja kutusaidia,” alisema Dk. Samky.

Akijibu maombi hayo Kandoro alisema kuwa wanafanya utararibu wa kupata madaktari wa upasuaji kutoka katika hospitali za wilaya za Kyela, Mbozi na Rungwe ili kuwapeleka Rufaa kusaidia kukidhi mahitaji ya wagonjwa.

Pia aliwaomba wakazi wa Mkoa wa Mbeya kufuata utaratibu wa kitabibu wa rufani ili kupungunza msongamano mkubwa unaoweza kujitokeza katika hospitali za Rufaa na Mkoa kwa kutibiwa katika Vituo vya Afya badala ya kukimbilia hospitali kubwa.-


Tanzania Daima
[/h]
 
Wasubiri wataletewa tu.. serikali dhaifu iko kwenye mchakato wa kutafuta madaktari toka nje
 
Akijibu maombi hayo Kandoro alisema kuwa wanafanya utararibu wa kupata madaktari wa upasuaji kutoka katika hospitali za wilaya za Kyela, Mbozi na Rungwe ili kuwapeleka Rufaa kusaidia kukidhi mahitaji ya wagonjwa.
sijui kandoro anamdanganya nani.sasa huko wilayani itakuaje?
 
Kweli kabisa, halafu bado anasisitiza wafuate utaratibu wa rufaa (rufani), yaani waanzie dispensary, health centre, DISTRICT HOSP, then mbeya rufaa..... ok ameshawatoa Drs wilayani.... nini kitafanyika huko?
 
wengine wanafikiri kabla ya kusema na wasiwasi Rais husema ndiyo huanza kufikiri kwa kina
 
Hawa 39 walio baki ni wasaliti wakubwa pumbavu zao wana lialia nini sasa wao si wamejifanya nio marobot wanapiga kazi!
Wapige kazi sasa wasaliti wakubwa nyie kwani madaktari
walio fukuzwa si walikua wana dai maslahi ya wote sasa iweje nyie mnajifanya hayawahusu???
Nyambav!!!!!!!
 
Back
Top Bottom