Uongozi wa hospitali ya rufaa Mbeya waomba msaada

Nadhani wakati wanawatimua walitumia masaburi kufikiria.
 
UONGOZI wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, imeomba serikali kuwapatia haraka iwezekanavyo madaktari wengine kuja kuziba nafasi zilizoachwa na madaktari 72 waliotimuliwa hivi karibuni.

Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk. Eliuter Samky alitoa ombi hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro aliyefika hospitalini hapo kuangalia hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa.

Dk. Samky alisema kuondoka kwa madaktari hao kumesababisha huduma katika kitengo cha upasuaji kubakiwa na madaktari bingwa wanne akiwemo na yeye wakati kitengo cha macho hakina daktari kabisa.

“Kwa kweli hali ya utoaji huduma imekuwa ngumu sana kwani tuna madaktari 39 tu hospitali nzima na Hospitali ya Wazazi ya Meta ina madaktari wawili tu waliobaki. Kwa kweli tunahitaji nguvu ya madaktari wengine kuja kutusaidia,” alisema Dk. Samky.

Akijibu maombi hayo Kandoro alisema kuwa wanafanya utararibu wa kupata madaktari wa upasuaji kutoka katika hospitali za wilaya za Kyela, Mbozi na Rungwe ili kuwapeleka Rufaa kusaidia kukidhi mahitaji ya wagonjwa.

Pia aliwaomba wakazi wa Mkoa wa Mbeya kufuata utaratibu wa kitabibu wa rufani ili kupungunza msongamano mkubwa unaoweza kujitokeza katika hospitali za Rufaa na Mkoa kwa kutibiwa katika Vituo vya Afya badala ya kukimbilia hospitali kubwa.-


Tanzania Daima

Abbas Kandoro sijakuelewa vizuri. Unamaanisha hao Madaktari utakaowaleta kutoka Wilaya za Mbozi, Rungwe na Ileje watalijaza pengo la hao Madaktari 72 waliofukuzwa? Na huko walikotoka wagonjwa watatibiwa na akina nani? Au wao hawahitaji kutibiwa na madaktari bingwa? Sijaelewa hawa viongozi wetu wanataka kutupeleka wapi mwaka huu.
 
Hawa 39 walio baki ni wasaliti wakubwa pumbavu zao wana lialia nini sasa wao si wamejifanya nio marobot wanapiga kazi!
Wapige kazi sasa wasaliti wakubwa nyie kwani madaktari
walio fukuzwa si walikua wana dai maslahi ya wote sasa iweje nyie mnajifanya hayawahusu???
Nyambav!!!!!!!

Dah inasikitisha sana nawewe ni Mtanzania? Au nyie ndio wale mnaruka India kwa hii kitu haiwaathiri? Si ndio wewe GAMBAGWANDA mkubwa weee aghhhhhhh
 
Asubiri madoc toka Irani wanakuja. Pia wastaafu wanankuja. Huyo ni the Great JK anasuluhusha mgogoro wa madoc Tz
 
hii ndo nchi iliyobalikiwa kuwa na rasiliimali nchi waniita nchi ya maziwa na asali na sio shida na machungu,yaap kweli tuna uongozi uliokamilika rais DHAIFU,waziri mkuu LIWALO NA LIWE hapo patamu yetu macho sisi tuliobebeshwa gunia la misumari halafu wanatuita wapenda aman
 
Huo ndio ujinga serikali ilivyotimua ilitegemea nini?Hapa liwalo na liwe tu.
Kandolo ni mjinga hasitaili kabisa kuwa kiongozi. Sasa anapowatoa huko Kyela na Tukuyu it means hakuna wangonja? Huyu kila sehemu anaharibu, shame on you Kandolo
 
mgomo wa madaktari hauna tija kwa taifa hasa kwa wananchi maskini.
Ni kweli kabisa hata mimi sikupenda uwepo kabisa tangu mwanza, lakini suluhisho hapa tulipo ni nini? Je ni kufukuza waliogoma? Nadhani kuna suluhisho bora zaidi kuliko hili, hapa kila upane serikali na madaktari unapaswa kushuka ili kukutana katikati kumnusuru mwananchi anayeumia
 
...duh!...hapo sasa ndo kisu kimegonga mfupa...wakati wanawatimua hao ma-dr 72 huko Mbeya walitutangazia kwa mbwembwe kuwa watawaita ma-dr wastahafu watano kuziba hilo pengo la ma-dr 72,sasa imekuaje tena?!,hesabu zimegoma ku-balansi?!,mimi nilikuwa nangoja kwa hamu sana kuona jinsi watu watano wanavyoziba pengo la watu 72...
 
kandoro anatoa matumaini hewa,AMO sio madaktari tusijidanganye.hivi kuna kiongozi yoyote anayependa kutibiwa na AMO?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Hivi kyela na rungwe hakuna wagonjwa mpaka madaktari watoke hukoo?? Na kama huko hakuna wagonjwa kwanini madaktari hao waliajiriwa huko?
 
aliwatoa huko wilayani nani atafanya kazi pande hizo............. kweli wameishiwa hata uwezo wa kufikiri
 
sijui kandoro anamdanganya nani.sasa huko wilayani itakuaje?

Huko Kyela, Mbozi na Rungwe ni watajaza, wahamie katika jiji la Mbeya. Hii ndiyo hali inayoitwa Management by Crisis!!!

Management by Crisis: describes the common problem of allowing unexpected events, interruptions, problems, or emergencies to dictate your priorities and actions. Managing by crisis is not all good. The idea of management by crisis is best if the organizations have time and resources to complete a crisis management plan before they experience another crisis.
 
Back
Top Bottom