Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,897
- 941
Mbunge Martha Mariki Atoa Mashuka 100 Katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Katavi, Mhe. Martha Mariki kupitia Chama cha Mapinduzi [CCM] Mkoa wa Katavi ametoa Shuka 100 kwaajili ya kuwasidia wagojwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi na Vituo vya afya vilivyopo wilaya ya Tanganyika na Wilaya ya Mlele Katika mkoa wa Katavi.
Akizungumnza baada ya kukabidhi Shuka hizo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi Mbunge huyo wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi amesema kuwa Msaada huo ni sehemu ya kuelekea kilele cha Siku ya Mwanamke duniani.
"Nimefika katika hospitali yetu hii ya Rufaa Mkoa wa Katavi nimekuja kukabidhi shuka 40 tunaamini yatakwenda kutatua changamoto Kidogo lakini Shuka hizi zipo 100 tutazigawa katika maeneo mbalimbali shuka 20 tutapeleka Kituo cha afya Ilembo" - Mhe. Martha Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi
"Tumeangalia changamoto katika Wilaya ya Tanganyika hususani eneo la Karema katika kituo cha Afya Karema tutapeleka Shuka 20 lakini bila kusahau Wilaya ya Mlele kituo cha afya Inyonga tutapeleka Shuka 20" - Mhe. Martha Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi
"Kipekee zaidi nimpongeze Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa sisi wananchi wa Mkoa wa Katavi tumeona na tumeshuhudia ilani ya chama cha Mapinduzi ikitekelezwa zaidi ya Asilimia 90 kwa kuboresha sekta ya Afya mfano mzuri ni kujegwa kwa hospitali hii ya rufaa mkoa wa Katavi" - Mhe. Martha Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi, Dkt. Serafini Patrice amemshukuru Mbunge Martha Mariki kwa kuona umuhimu wa kutoa Shuka 40 katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi pamoja na maeneo mengine ili kusaidia wagonjwa katika hospitali na vituo vya afya.
Attachments
-
6klpo.JPG81.5 KB · Views: 1
-
WhatsApp Image 2024-03-06 at 19.44.10.jpeg162.3 KB · Views: 1
-
WhatsApp Image 2024-03-06 at 19.44.10(1).jpeg160.6 KB · Views: 1
-
WhatsApp Image 2024-03-06 at 19.44.11.jpeg170.1 KB · Views: 1
-
WhatsApp Image 2024-03-06 at 19.44.11(1).jpeg134.1 KB · Views: 1
-
WhatsApp Image 2024-03-06 at 19.44.11(3).jpeg163 KB · Views: 1
-
WhatsApp Image 2024-03-06 at 19.45.01.jpeg152 KB · Views: 1
-
1NBVC.JPG85.4 KB · Views: 1
-
2XZAS.JPG84.9 KB · Views: 1
-
7JIUYT.JPG64.9 KB · Views: 1
-
3nbvhy.JPG87.7 KB · Views: 1
-
5mlkpo.JPG92.8 KB · Views: 1