DOKEZO Hospitali ya Rufaa ya Mbeya haina Incinerator

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya inachafua hali ya hewa na kuhatarisha afya za Wananchi hospitalini na wanaoizunguka kwa kukosekana Incinerator (mashine maalum ya kuchomea taka).

Incinerator ya mwanzo iliharibika lakini kwa sasa wamefunga jiko lenye chimney ndefu tu ambalo linatoa moshi wenye uchafu directly hewani bila kusafishwa kama incinerator inavyotakiwa kufanya kazi.

Hii inakuwa kero muda wowote wanapochoma taka hatari za hospitali na mbaya zaidi huwa zinachomwa mchana wakati kuna upepo hivyo moshi unasambaa kila mahali.

Majibu ya Hospitali ya Rufaa: Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya yatoa ufafanuzi madai ya kukosekana kwa Mashine ya Kuchomea Taka
 
Back
Top Bottom