Uongo unaoongelewa saluni

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,684
8,833
Yaani saluni za wanawake zina vibweka, majungu, umbea, magigambo na uwongo wa kila namna.
Leo nikiwa saluni kujiweka safi, mara akaingia dada mmoja na mizigo yake, anaonekana ametoka shopping.
Kaja, hata bila kuulizwa kaanza kusimulia jinsi ndege za vita zilivyopita chinichini akiwa Karikoo. Eti rubani mmoja akamuona msichana wake, akaigandisha ndege hewani na wakaanza kupiga soga, baada ya muda kidogo akaipaisha tena.
Yaani saluni ndio makao makuu ya uwongo.
Naomba na nyie muongeze na nyie uwongo mliousikia huko.
 
usiniambie ulikuwa Lisa Magic Hands?
Saluni(za kike na za kiume) umbea ndo mahala pake. Ukitaka kujua nani kaachika, nani muathïrika, yupi amefumaniwa juzi, nani anatembea na nani, vyote utavipata huko.
Watu huwa wanashambulia za kike peke yake, lakini hata za kiume nazo ni b'laa, hasa zile zenye vinyozi wakazi!
 
ila ukweli ni kwamba za kike ni balaaa
 
Uwongo upo kila kona mpaka Ikulu, Bungeni, Maofisini...lol

wanasiasa wanayakataa hata majina yao.
Nape alitangaza ushindi wa Igunga, baadae akakataa.
Alipokuwa usa na malecela akakiri kuwa ni yeye ndo aliyetangaza ushindi wa ccm
 
Hivi watu hua mnaenda saluni kupiga na kutafuta umbea au kujitengeneza?

Ukifika weka mziki wako uwe unatoa pale unapohitaji kutoa maagizo tu. . . maana hata kusikiliza na kwenda kuhadhithia kwingine ni umbea tosha.
 
Mtu hana shule, hana assignment, hana majukumu, either anaishi kwa dada, shemeji, mjomba, binamu, kulakulala, au golikipa,
unatarajia atapiga stori gani? wakati anapokuwa anapitisha muda kusubiria kengele ili akale? lazima apige umbea
Ndo maana mtu akiniambia yupo busy bongo, me namwona mwongo tuu!
Tumezoea bla bla ambazo hazima manufaa yoyote
 
Hivi watu hua mnaenda saluni kupiga na kutafuta umbea au kujitengeneza?

Ukifika weka mziki wako uwe unatoa pale unapohitaji kutoa maagizo tu. . . maana hata kusikiliza na kwenda kuhadhithia kwingine ni umbea tosha.

raha ya saluni umbea babu we!
Ndo nini kutengenezana kimya kimya?
 
Sasa kama ndio kazi yake malalamiko ya nini?
Endeleeni kusambaza.

msome vema mdada mleta uzi. Hana tatizo na umbea, ila ana tatizo na urongo wa huko saluni, as u know umbea ukiwa ukweli raha sana.
Sawasawa?
 
Tangu lini umbea ukawa umejaa ukweli?
Siku zote umbea lazima uwe umeongezwa chumvi ama sukari, zaidi ya hapa yanakua maongezi na sio umbea.
 
Yaani saluni za wanawake zina vibweka, majungu, umbea, magigambo na uwongo wa kila namna.
Leo nikiwa saluni kujiweka safi, mara akaingia dada mmoja na mizigo yake, anaonekana ametoka shopping.
Kaja, hata bila kuulizwa kaanza kusimulia jinsi ndege za vita zilivyopita chinichini akiwa Karikoo. Eti rubani mmoja akamuona msichana wake, akaigandisha ndege hewani na wakaanza kupiga soga, baada ya muda kidogo akaipaisha tena.
Yaani saluni ndio makao makuu ya uwongo.
Naomba na nyie muongeze na nyie uwongo mliousikia huko.
kama ni uongo huyo kapitiliza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom