Uongo unaoongelewa saluni

Yaani saluni za wanawake zina vibweka, majungu, umbea, magigambo na uwongo wa kila namna.
Leo nikiwa saluni kujiweka safi, mara akaingia dada mmoja na mizigo yake, anaonekana ametoka shopping.
Kaja, hata bila kuulizwa kaanza kusimulia jinsi ndege za vita zilivyopita chinichini akiwa Karikoo. Eti rubani mmoja akamuona msichana wake, akaigandisha ndege hewani na wakaanza kupiga soga, baada ya muda kidogo akaipaisha tena.
Yaani saluni ndio makao makuu ya uwongo.
Naomba na nyie muongeze na nyie uwongo mliousikia huko.

Hiyo ni "joke".
 
Tangu lini umbea ukawa umejaa ukweli?
Siku zote umbea lazima uwe umeongezwa chumvi ama sukari, zaidi ya hapa yanakua maongezi na sio umbea.

mi nadhani chumvi si muhimu sana hapa, kimsingi umbea unakuwa zaidi ya maongezi kwa kuwa habari zake zinakuwa hazina uhakika sana, tena neno 'naskia' ndio hutawala mazungumzo.
Kingine, umbea shurti uhusu maisha ya individual au familia ama kikundi cha watu, kifupi 'people'.
Sawasawa?
 
raha ya saluni umbea babu we!
Ndo nini kutengenezana kimya kimya?

Ukitaka kazi yako iheshimike iheshimu,kufanya eneo la kazi kijiwe cha umbea na wewe utaonekana huna maana pamoja na kazi unayoifanya.
 
Hivi watu hua mnaenda saluni kupiga na kutafuta umbea au kujitengeneza?

Ukifika weka mziki wako uwe unatoa pale unapohitaji kutoa maagizo tu. . . maana hata kusikiliza na kwenda kuhadhithia kwingine ni umbea tosha.

Mimi huwa nashangaa mtu anatoka nyumbani kwake anaenda kukaa saluni kupiga soga,inafika lunch time na yeye anaagiza chakula kama wafanyakazi wa salon utadhani na yeye alikuwa anafanya kazi,unashangaa kwa nini asikae nyumbani kwake akapika?

Alafu ukimuangalia ni mtu mzima sio teenager,inashangaza sana.
 
Ukitaka ku-enjoy umbea wa salun, nenda zile za wadada walio-high class utacheka hadi uzimie.

Kila mmoja anataka kuonekana Beyonce, Oprah au michele Obama, yani huwa full burudani kama uko kwenye movie vile.
 
Utasikia wanasema "Ile range rover juzi nilimpelekea fundi aniweke subwoofer nyuma mwee hela aliyochaji ni ndogo sana maana nilitegemea anichaji laki 8 hivi"

Au mwingine ataongezea " Mwanangu hahahaaaa juzi kanichekesha, eti alimwona babu yake huko Uk akimpungia wakati ndege inajaribu kutua kwenye runway!"

Funga kazi ni hii, "Unajua msusi, sipendi nywele za uswazi nataka hii ya 70,000 unisuke sawa?"
 
kweli ukiwa mbeya ukitaka habari nenda saloon ,lakini kama umefata kilichokupeleka haitakusumbua
 
yaani saluni za wanawake zina vibweka, majungu, umbea, magigambo na uwongo wa kila namna.
Leo nikiwa saluni kujiweka safi, mara akaingia dada mmoja na mizigo yake, anaonekana ametoka shopping.
Kaja, hata bila kuulizwa kaanza kusimulia jinsi ndege za vita zilivyopita chinichini akiwa karikoo. Eti rubani mmoja akamuona msichana wake, akaigandisha ndege hewani na wakaanza kupiga soga, baada ya muda kidogo akaipaisha tena.
Yaani saluni ndio makao makuu ya uwongo.
Naomba na nyie muongeze na nyie uwongo mliousikia huko.

hivi mara hii uko bongo? Na yule jamaa anayekubaka kumbe uko naye bongo ndugu yangu? Mie nilitegemea uko naye mamtoni; kwani ulisema mambo ya shule n.k.;
 
au utawaskia, beyonce mshamba kweli kachana nywele ka wa manzese

au yan siku opra ananunua hilo gauni yalikuwa yamebaki mawili moja akachukua yeye jingine mie

Utasikia wanasema "Ile range rover juzi nilimpelekea fundi aniweke subwoofer nyuma mwee hela aliyochaji ni ndogo sana maana nilitegemea anichaji laki 8 hivi"

Au mwingine ataongezea " Mwanangu hahahaaaa juzi kanichekesha, eti alimwona babu yake huko Uk akimpungia wakati ndege inajaribu kutua kwenye runway!"

Funga kazi ni hii, "Unajua msusi, sipendi nywele za uswazi nataka hii ya 70,000 unisuke sawa?"
 
Saluni za kike = vituo vya majungu/umbea/magigambo/uwongo
Saluni za kiume = Vituo vya poda/bwimbwi/unga/madawa ya kulevya
 
usiniambie ulikuwa Lisa Magic Hands?
Saluni(za kike na za kiume) umbea ndo mahala pake. Ukitaka kujua nani kaachika, nani muathïrika, yupi amefumaniwa juzi, nani anatembea na nani, vyote utavipata huko.
Watu huwa wanashambulia za kike peke yake, lakini hata za kiume nazo ni b'laa, hasa zile zenye vinyozi wakazi!
Na zile nyumba mnazoendas kufanya massage nazo pia hazijambo kwa kuuza maneno.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom