Uonavyo: Kati ya prof LIPUMBA na Dr SLAA ni nani zaidi?

Na walikuwa wanayatafuta haya.Mie simo wakati mwingine mjifikirie vizuri kabla ya kuleta mada za kizandiki.

Hapo kwenye mada nimeomba pia CV zao mkuu. Haya tuseme Slaa ni zaidi kwa mengine. Vipi kuhusu CV zao? Mbona hapa unaruka kiunzi? Tuendako watanzania tutaanza kudai kuchagua ma rais kutokana na CV zao. Hapo itakuwaje? Kupiga kelele za kupambana na mafisadi na kutaja majina yao hadharani si kigezo cha ubora katika utawala mkuu.
 
nchi kama US zina mambo fulani ambayo hupelekea kuwa mtu anayegombea uraisi ni lazima awe tajiri lakini kiukweli sio kuwa tajiri bali ni kuwa umefanikiwa kufutana na kazi ambayo mgombea (mtu) amekuwa akijishugulisha nayo kabla ya kutaka kuwania kuingia ofisi hiyo kubwa.

Ninachotaka kusema hapa ni mafanikio yanayoonekana kwa Dr. Slaa pamoja na mambo mengine ni katika uendeshaji (umiliki!??) wa hospitali/kituo ya CCBRT. Huyu mwenzake Prof. Lipumba nimjua siku zote kama mchumi aliyetukuka lakini sifahamu hasa kielelezo (visible/tangible) cha mafanikio yake kinachoweza kuonekana. Labda mwenye kujua atujuze hapa

kiongozi mkuu wa CUF!
 
Kwa vile wanaJF wameshaelewa lengo lako mada imefungwa ndio maana tunachangia vitu nje ya mada.

Umejitahidi sana kunitoa kwenye mada kwa muda mrefu sababu ya ushabiki wako wa kitaarabu taarabu. Haya sasa, kama unakubari tusitoke kwenye mada. Sasa turudi kwenye mstari.
 
Umejitahidi sana kunitoa kwenye mada kwa muda mrefu sababu ya ushabiki wako wa kitaarabu taarabu. Haya sasa, kama unakubari tusitoke kwenye mada. Sasa turudi kwenye mstari.

Ili turudi kwenye mada wacha tabia ya kureach conclusion unayoitaka wakati umeuliza swali wewe.Lengo lako unataka Lipumba aonekane yuko juu ya Rais ajaye Dr Slaa.Kitu ambacho ni kama mbingu na ardhi
 
Ili turudi kwenye mada wacha tabia ya kureach conclusion unayoitaka wakati umeuliza swali wewe.Lengo lako unataka Lipumba aonekane yuko juu ya Rais ajaye Dr Slaa.Kitu ambacho ni kama mbingu na ardhi

Tume ya uchaguzi si ndiyo huandaa uchaguzi. Je, wanatume hawana haki ya kupiga kura? Ok, acha nikukubalie mkuu. Ngoja nikae kimyaaa!! Kazi kwenu.
 
Huwa na jiuliza ingekuwa je kama lipumba angekuwa hana elimu ya kiwango hicho alicho nacho,maana japo ana elimu yake nzuri tu ni mtu hasiyeweza hata kujenga hoja nyepesi tu.

Juzi alikuwa anazungumzia juu ya cuf kikimbiwa na wanachama wake kwa kile wanachodai uongozi wanacha hichi ni mbovo,akaulizwa analijulichukulia je swala hilo


Majibu aliyo yatoa ndiyo yalinifanya nijiulize tena juu ya usomi wa huyu jamaa na endapo watanzania wange jisahau na kumpa uongozi wa nchi hii tunge ikimbia hii nchi na kuhakikishieni maana ni kheri ya JK mara 100

Lipumba sijapata kumjua kiundani nje ya siasa,na sijawapata kujua mafanikio yake kwa upande wataaluma yake toka akiwa mshauri wa mambo ya kiuchumi wa mzee Ruksa ambapo hakuna kipindi ambacho hii nchi imewahi kuyumba kiuchumi kama kipindi cha uongozi wa mzee Ruksa na mshauri wake wa maswala ya uchumi akiwa yeye pro Lipumba.


Sina sababu ya kumzungumzia Dr.Slaa, kwani kila mtu anajua mafanikio yake kisiasa n nje ya siasa.
 
Slaa anamvuto sana kisiasa, anajua kujenga hoja sana na ikakubalika, Lipumba tatizo chama chake kimepoteza uelekeo. But, Slaa yuko juu sana si tu kwa Lipumba, hata kwa J.K. isipokuwa Tume ya uchaguzi ndio iligeuza matokeo na kumpa J.K. ushindi.
 
Dr Slaa yupo Juu automatically ila Lipumba mpaka wampigie promo kwamba ni mwanauchumi bora dunia hadi UN wakamchukua.
 
mmeanzisha thread wenyewe mnachangia wenyewe.Tatizo imewauma sana mapokezi makubwa aliyoyapata mtaalamu wa uchumi duniani profesa lipumba.Si vibaya mkaendele kujifariji na 'msomi' wenu wa sheria za kanisani,


Mkuu mi sidhani kama kuna mtu anasema Lipumba sio msomi, ki taaluma yupo juu lakini anatumiaje/ametumiaje Elimu yake kuleta maendeleo katika nchi yake au hata chama chake? ukiwa linganisha watu hawa kwa fikra za kidini, waislam mtasema Lipumba yupo juu but kwa wakristo wasomi wa aina ya hao 2 wako wengi and this is why katika CUF Lipumba anaonekana kama Mungu while Maalim Seif anaonekana kama Mtume (Rejea tamko alilolitoa Prof Safari wakati ameshindwa uchaguzi wao)

Kuwa mkweli, Lipumba amewahi kufanya nini ambacho ni remarkable kwenye jamii yeyote hata kwenye Uislam wenyewe, Dr Slaa kwanza aliye tusibitishia kwa ushahidi juu ya wizi uliofanywa na serikali, serikali ya ccm inanyimwa sana usingizi na huyu kuliko Prof Lipumba, huyu Padree pia ndiye aliyewezesha kujengwa shule nyingi sana za sekondary akiwa katibu mkuu wa dini yao, shule hizo hata watoto wa kislam wanasoma hadi leo, ndiye kiongozi wa hospitali za CCBRT ambazo nina hakika hata Waislam wana/wametibiwa n. k
Kwenye uchaguzi toka Lipumba amewahi kugombea, kuna siku amewahi hata kupata Kura milioni 2? angalia Dr. tume ilitangaza amepata kura 2.6M baada ya kuchakachua, ki ukweli Lipumba anapendwa zaidi kidini na sio performnce ya chochote.
 
Dr Slaa amekuwa msaada mkubwa sana kwa maendeleo ya demokrasia Tanzania,hayumbishwi na progranda za CCM,anasimamia haki,ukweli na maendeleo ya watanzania waliosahaulika katika kipindi chote cha miaka hamsini,
 
Dr slaa yupo juu hakuna wa kumfananisha naye hapa Tanzania,DR ni mkombozi wa vijana na watanzania wote
 
Mkuu nimeweka hii baada ya kuona hawa watu wanasifiwa sana kila mtu kwa upande wake. Kutaka kujua nani zaidi kati ya hawa jamaa si kufikiri kwa ufinyu ila ni kwa mapana na marefu. Wote wawili wana umuhimu katika jamii yetu kutokana na michango yao. Sana nataka tupate nani zaidi ya mwenzake.

DR. SLAA PRO. LIPUMBA
1. Dr. Slaa ni Mkristo wakati Pro. Lipumba ni Muislam
2.Slaa amejenga chama kwa misingi ya kitaifa wakati Lipumba Amejenga chama kwa misingi ya
Uislam
3.CDM kinazidi kuimarika CUF kinazidi kusambaratika
4.SLAA Aligombea Urais kwa mara ya kwanza na kufaulu kupata kura nyingi Lipumba Aligombea Urais kwa mara ya tatu na kura zikazidi kushuka

5. SLAA Anautumishi uliotukuka toka akiwa PAdre Lipumba Ndiye alikuwa mshauri wa uchumi wa Ali Hassan Mwinyi
(wote mnajua uchumi ulikuwa hovyo kiasi gani!)
6. Maisha yao wote ya mahusiano yana utata! (Uchumba wa uzeeni wa Dr, Slaa haueleweki na wala sijawahi kusikia kama Proff. Lipumba ana mke na watoto!
7. CDM kina mizizi nchi nzima CUF kina mizizi zanzibar na hasa pemba tu!

kwa leo naomba kuwakilisha
 
Tunafanya makosa makubwa kuwalinganisha watu hawa,tukisema ukweli watu watachukia.hivi unaweza kumlinganisha Prof Lipumba na Dr Slaa? Ktk eneo lipi hasa? Kielimu lipumba yupo juu,uwezo wa kujenga hoja lipumba yupo juu; hatuwezi kufananisha mchanga na jiwe.lipumba ni jiwe walilolikataa waashi na limekuwa jiwe kuu na hakuna wa kufanana nae kielimu,kisiasa.
 
Nadhani tumlinganishe Lipumba na Mkullo! to me lipumba Is more technical.. hafai kua rais ila mtendaji mkuu kwenye wizara ya fedha! Mkullo anatucost sana pale wizara ya noti
 
Wote ni wanasiasa wazuri,
Tafauti yao ni ndogo tu,Dr Slaa amekuwa pamoja na watanzania mara kwa mara hata baada ya uchaguzi wakati Prosesa Lipumba anawajali na kuwapenda watanzania kipindi cha uchaguzi tu
 
Jamani naomba sasa turudini kwenye mada kuu ya msingi. Huko tunakoelekea hakuwezi kutujenga kwa lolote.
 
Dr Slaa anafaa kuwa rais wa Tanzania, Lipumba hafai kuwa rais wa Tanzania wala uenyekiti wa uchumi wa dunia. Kwanza Lipumba hana kauli ya uweledi ya kusisimua vichwa vya watu hata alivyokuwa cass miaka ya 90's ilikuwa ni vichekesho kumsikiliza. Aliua uchumi wa Tanzania na hatuta fanya makosa tena ya kumkabìdhi mamlaka.
 
Back
Top Bottom