Ungependa kukutana na hawa JF members?

Sina haja ya kukutana nao hao baadhi yao wana tabia mbaya sana ya kuingilia PM za watu. Ushauri kwa Maxence Melo na JamiiForums waboreshe eneo la PM hawa Mods wasiwe na access ya kuingia kabisa
Hakuna mwenye uwezo wa kuingilia PM ya mtu yeyote. Unapokuwa PM angalia idadi ya watu waliopo (kwa kubonyeza nukta tatu upande wa kulia, chaguo la kwanza lilioandikwa "Participants") na kama mtu sio sehemu ya mjadala bofya Kick-out kumtoa.
 
Kuna muda ukiwa pm hata kama conversation inawatu wawili, pale juu utaona inaandika 3 online. Mtu wa tatu anayeongezeka ni huyo YinYang. Yeye ndio Head of Content Management, huwa anatabia ya kusoma pm
Mkuu Analyse ,

Sina uwezo wa kuingia PM yako, na hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kuingilia PM yako. Kwenye uwanja wa PM kuna sehemu ya Participants ambapo inakuruhusu kuangalia watu mliokwenye maongezi. Hizo tuhuma unazoleta hazina ukweli wowote.
 
Hakuna mwenye uwezo wa kuingilia PM ya mtu yeyote. Unapokuwa PM anaglia idadi ya watu waliopo na kama mtu sio sehemu ya mjadala bofya Kick-out kumtoa
Mkuu sasa huyo watatu anakuwa ametokea wapi?

Mi imeshanitokea tena sio mara moja lakini ghafla unashangaa imerudi tunabakia wawili bila hata kubofya hiyo Kick-out.

Inakuwaje kuwaje hapo Mkuu.
 
Mkuu Analyse ,

Sina uwezo wa kuingia PM yako, na hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kuingilia PM yako. Kwenye uwanja wa PM kuna sehemu ya Participants ambapo inakuruhusu kuangalia watu mliokwenye maongezi. Hizo tuhuma unazoleta hazina ukweli wowote.
Kwahiyo unaangalia tu ephen anachat na nani? Bila kusoma tunachoandika?
 
Hakuna mwenye uwezo wa kuingilia PM ya mtu yeyote. Unapokuwa PM angalia idadi ya watu waliopo (kwa kubonyeza nukta tatu upande wa kulia, chaguo la kwanza lilioandikwa "Participants") na kama mtu sio sehemu ya mjadala bofya Kick-out kumtoa.
Kwanini huwa naona 3 Participants? ni bora basi na huyu mshiriki mwingine nimtambue sio anakuja kuingilia falagha za watu bila ruhusa kwa kifupi ule ni utovu wa nidhamu na huyo Mshiriki wa tatu jitahidini kumdhibiti. Na Mimi nimeshatafuta namna ya kumuumbua wakati wowote.
Angalizo msinipige BAN tu.
 
Waonyeshe picha mtandao umeshindwa hata picha hazionekani wautendee aki kwanza huu uliopo ndio waongeze binafsi nawapa 4/10 bado jf hawaeleweki na customer care ambao ndio hao mods wako active kwenye vitu viso na maana Sana kama ban lakin wakiambiwa vitu kama picha ovyooo
 
Back
Top Bottom