sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,034
Kuna anko anaenda miaka kama 43 hivi ana familia yake yenye watoto wawili wa kiume.
Mke wake yuko fresh sijawai sikia malalamiko, ni mtiifu, anawajali ndugu wa mme wake, anafua nguo za mmewe japo kuna housegirl, kanisani anaenda, n.k.
Kila mwaka unapoisha siku 2 baada ya krismas kwenye tarehe 27 hivi, mke wake huwa anarudi kwao kwa kuomba ruhusa ya kwenda kusalimia kwao, ni mtu kwa mikoa ya nyanda za juu kusini.
Sasa kuna kipindi mwaka 2020 mke wake alienda na watoto huko kwao waende kuwaona wajomba, bibi, kina mama mkubwa, n.k. Mme hakuafiki akampa ruhusa kwa roho nyeupe kabisa.
Mwaka juzi alienda peke yake.
Mwaka jana tena aliomba aende na watoto, Anko ni kama machale yalimcheza, waliporudi akaanza kuchukua hatua za kuhakikisha kama anachokihisi ni kweli,
Siku 1 tu baada ya mke na watoto kurudi, akasubiria mke wake atoke nyumbani, aliwachunguza kwa umakini watoto, La Haula!! aliwezza kuziona chale kadhaa japo zilikuwa ni ndogo sana, alipowauliza watoto mwanzoni walisita ila aliwazidi akili kirahisi wakafunguka kwamba usiku wa manane waliamshwa wakaambiwa wavae boksa tu, walipelekwa jikoni chumba cha nje, walikuta taa zimezimwa ila kuna chungu maji yanachemshwa halafu kuna mtu akawa kashika tawi dogo la mti lenye majani analichovya kwenye chungu kisha anachapa mgongoni na tumboni mara mbili, wakaambiwa warudi chumbani ila waliona wengine wanaendelea, asubuhi walichanjwa, mama yao aliwaasa sana wasiseme chochote akawanunulia mpira na vitu vizuri vizuri.
Yule mkubwa anasema mara ya kwanza kuna supu ilichemshwa ila ni kama zimechanganywa na mchanga, kula ilikuwa taabu sana maana ina mchanga, baada ya kula kuna mchanga walilazimishwa kuuvuta kwa pua wakawa wanapiga sana chafya, hawakuwa peke yao, hata mama yao nae alikuwa anapiga sana chafya.
Anko ameunganisha doti kaona kwamba zile tripu za kila mwisho wa mwaka huwa ni za kwenda kutambika.
Ajabu ni kwamba mama yao ni muhudhuriaji mzuri sana wa kanisani, kila siku hio nyumba ni lazima wasali, kuna utaratibu wa kupokezana kusali, leo house girl, kesho baba, kesho mama, kesho mtoto wa kwanza, kesho mtoto wa pili, kesho mgeni, n.k. na tena inabidi uwe na fungu kabisa, ulielezee kisha ndio usali.