Mke wangu anatazama Cartoon kuliko Watoto wetu

Nyafwili

JF-Expert Member
Nov 27, 2023
2,774
6,885
Habari wana JF, poleni na majukumu ya hapa na Pale 🤝.

• Kuhusu hili suala, naona kama ni uraibu wa mke wangu kutazama katuni na watoto kila dakika. "[uende - urudi ni katuni kwenda mbele na michezo ya hapa na pale.] "

• Mke wangu huwa anafurahia sana kutazama na kuimba pamoja na watoto wetu pindi wanapongalia katuni hiyo, na endapo watoto wetu kama watakua hawajaangalia hiyo katuni huwa akiwasimulia hadithi hizo baada ya watoto kuludi kutoka shule au kutoka maeneo yao ya kucheza. Kila nikiangalia hili suala la katuni, naona kabisa kuna kitu hakipo sawa kabisa.

• Kuhusu katika majukumu yake kama mke na mama wa watoto wetu, kwa kweli yupo vizuri sana analea watoto safi kabisa, ila kinachonipa wasiwasi mkubwa ni kuhusu hili suala la kuangalia katuni bila kupumzika. Yani wamegeuza nyumba kuwa nyumba ya katuni. [ uende - urudi ni katuni kwenda mbele ] na michezo ya hapa na pale.

• Kama kutakuwa na njia au namna yeyote ile naomba msaada wa kurekebisha hili tatizo la katuni.

"Nahisi kuna kitu kibaya, maana simuelewi kabisa kuhusu mke wangu, wakati mwingine hata haangalii sinema ninazotaka tuangalie pamoja, isipokuwa tu atajilazimisha kishikaji lakini moyo wake unakua unawaza katuni tu. Hata tukiwa tumekaa kama familia yeye na watoto wetu huendelea kupiga stori za katuni.

• "Mke wangu, mwenye umri wa miaka 33 sasa, anafurahia sana kutazama katuni zaidi kuliko hata watoto wetu. Mvulana wetu wa kwanza ana umri wa miaka 11 hadi wa mwisho ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 4.

• Naona kama mke wangu amepatwa na uraibu wa katuni hivi , wao ni kuimba nyimbo za katuni , kupiga ngoma zao na kujadili mambo ya katuni kila wakati.

• Nimejaribu kumweleza kuwa sipendi kabisa tabia ya kuangalia katuni kila sekunde lakini wapi!!! , silalamiki kwa sababu wanafurahi lakini sielewi uraibu wa mke wangu ni nini hasa?. Hata wakati watoto wakiwa hawapo karibu, yeye ataendelea kutizama filamu za katuni peke yake. Watoto Watakapofika nyumbani , atawasimulia yote aliyoyatazama na hata kuwaonyesha kwa vitendo matukio ya kuchekesha/yenye hisia.

• Tafadhali kumbuka kuwa, ameajiriwa kikamilifu na bado anafanya kazi zake kama mke na mama. Sina tatizo lolote kwa upande huo, je amezoea filamu za katuni au kuna kitu kimejificha? Au nimuache akikua ataacha mwenyewe, Maana sielewi kabisa."

• Je, kitu gani ninaweza kufanya ili kumsaidia mke wangu ? Inanisumbua sana akili yangu kwa namna fulani.

😎Hii ni story ya kijana Mwenye familia ya watoto wa tatu ✍️✍️✍️✍️.

download (3).jpeg
download (2).jpeg
download (1).png
 
Tuko wengi mkuu sio huyo tu.

Ni kawaida as long as anatimiza majukumu yake mpotezee
Wengi ni wale tuliolelewa mazingira ya kukaa ndani
Upweke wetu wa kutokaa sana na kucheza na watoto wengine faraja tulipata kwenye katuni
Tumelelewa na kampani ya katuni.

Na midori
Binafsi huniambii lolote Kuhusu katuni.
 
Mimi nafikiri wewe ndio una tatizo maana kwenye maelezo yako hakuna tatizo lolote kwa mkeo! Mke wako anafanya wanachofanya Walimu wakiwa na watoto wetu mashuleni hucheza nao,huimba nao na kama siku ukibahatika kwenda ukakuta wanafundishwa na Walimu unaweza ukafikiri wote ni watoto…
Kama hii ni habari ya kweli basi mkeo ni mmoja ya wanawake bora kabisa ambao kila mwanaume angependa kuwa nae!
Mke wako anafanya kitu ambacho hata wewe ulipaswa kukifanya kwa watoto wako…kuwa mzazi hakuishii kwenye kutoa hela tuu…Ungepata wasaha ungewauliza wanao wanajisikiaje wakicheza au kuangalia katuni na Mama yao..? Majibu yao yanaweza kukufanya ukaanza na wewe kuangalia nao katuni au kucheza nao ukipata muda!

NB:Maoni yangu yabaki kama yalivyo kama hii story ni ya kweli….
 
Habari wana JF, poleni na majukumu ya hapa na Pale 🤝.
• Kuhusu hili suala, naona kama ni uraibu wa mke wangu kutazama katuni na watoto kila dakika. "[uende - urudi ni katuni kwenda mbele na michezo ya hapa na pale.] "

• Mke wangu huwa anafurahia sana kutazama na kuimba pamoja na watoto wetu pindi wanapongalia katuni hiyo, na endapo watoto wetu kama watakua hawajaangalia hiyo katuni huwa akiwasimulia hadithi hizo baada ya watoto kuludi kutoka shule au kutoka maeneo yao ya kucheza. Kila nikiangalia hili suala la katuni, naona kabisa kuna kitu hakipo sawa kabisa.

• Kuhusu katika majukumu yake kama mke na mama wa watoto wetu, kwa kweli yupo vizuri sana analea watoto safi kabisa, ila kinachonipa wasiwasi mkubwa ni kuhusu hili suala la kuangalia katuni bila kupumzika. Yani wamegeuza nyumba kuwa nyumba ya katuni. [ uende - urudi ni katuni kwenda mbele ] na michezo ya hapa na pale.

• Kama kutakuwa na njia au namna yeyote ile naomba msaada wa kurekebisha hili tatizo la katuni.
"Nahisi kuna kitu kibaya, maana simuelewi kabisa kuhusu mke wangu, wakati mwingine hata haangalii sinema ninazotaka tuangalie pamoja, isipokuwa tu atajilazimisha kishikaji lakini moyo wake unakua unawaza katuni tu. Hata tukiwa tumekaa kama familia yeye na watoto wetu huendelea kupiga stori za katuni.

• "Mke wangu, mwenye umri wa miaka 33 sasa, anafurahia sana kutazama katuni zaidi kuliko hata watoto wetu. Mvulana wetu wa kwanza ana umri wa miaka 11 hadi wa mwisho ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 4.

• Naona kama mke wangu amepatwa na uraibu wa katuni hivi , wao ni kuimba nyimbo za katuni , kupiga ngoma zao na kujadili mambo ya katuni kila wakati.

• Nimejaribu kumweleza kuwa sipendi kabisa tabia ya kuangalia katuni kila sekunde lakini wapi!!! , silalamiki kwa sababu wanafurahi lakini sielewi uraibu wa mke wangu ni nini hasa?. Hata wakati watoto wakiwa hawapo karibu, yeye ataendelea kutizama filamu za katuni peke yake. Watoto Watakapofika nyumbani , atawasimulia yote aliyoyatazama na hata kuwaonyesha kwa vitendo matukio ya kuchekesha/yenye hisia.

• Tafadhali kumbuka kuwa, ameajiriwa kikamilifu na bado anafanya kazi zake kama mke na mama. Sina tatizo lolote kwa upande huo, je amezoea filamu za katuni au kuna kitu kimejificha? Au nimuache akikua ataacha mwenyewe, Maana sielewi kabisa."

• Je, kitu gani ninaweza kufanya ili kumsaidia mke wangu ? Inanisumbua sana akili yangu kwa namna fulani.

😎Hii ni story ya kijana Mwenye familia ya watoto wa tatu ✍️✍️✍️✍️.

View attachment 2856301View attachment 2856302View attachment 2856303
Mchunguze vizuri nayeye sio katuni kweli!? Maana usije ikawa unamzuia mwenzio kuwapenda ndugu zake .
 
Mimi hakuna character maarufu wa kwenye cartoon simjui, nazijua na kuzipenda sana.
Na niko mbele kufuatilia, ikitoka tu mpya naruka nayo napeleka home tunaangalia.

Tofauti na mpira na drama za kikorea, napenda sana animation.
Hizo Cinderela, Barbie Mariposa, Little Mermaid n.k ndio kama sala ninavyozijua 😂😂
 
Kawaida tu hiyo, ngoja nikutajie ninazo zipenda mimi...

-Tom and Jerry (normal).
-Bellerin.
-Pikapau (Portuguese)
-Makarao.(Kenya)
-Ed,Edd and Eddy.
-Masha and the bear.
-Katoto (Ug).
-Shrek.
-The croods.
-The lion king (Hakuna matata).
-Small foot.
-Big foot.
-Luka.
-The lorax.
-Hotel translavia.
-Rango.
-Peter rabbit.
-Dr seuss, the rolax maker
 
Back
Top Bottom