Undani wa Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa

Wakuu, vp mgombea binafsi?wengine hatuna imani na vyama vya siasa. Woote wezi tu. Zito ana hammer original ya kimarekani. Mshahara gani kama sio dili za humo bungeni ndio zimemuwezesha kusukuma gari ya mmarekani.hatudanganyiki na vyama vyenu. Woote lenu moja tu. Tuliiona nec ya odinga na kibaki then baada ya kuiangusha kanu,si waligeukana?wadanganyeni wengine ila sio mimi. Sina chama na sihitaji chama.
 
Ni kweli mkuu hawa jamaa wawili wanahitaji uangalizi wa hali ya juu tena si kwa nguvu za kibinadamu bali kwa uwezo wa mwenyeenzi mungu ili waweze kutufikisha NCHI YA KUSADIKIKA. tupo nyuma yao mungu awabariki.

pili nasi kundi la vijana tuache ushabiki, tuwe watekelezaji. tuamioni kuwa sasa ni wakati wa mabadiliko.
 
Wakuu, vp mgombea binafsi?wengine hatuna imani na vyama vya siasa. Woote wezi tu. Zito ana hammer original ya kimarekani. Mshahara gani kama sio dili za humo bungeni ndio zimemuwezesha kusukuma gari ya mmarekani.hatudanganyiki na vyama vyenu. Woote lenu moja tu. Tuliiona nec ya odinga na kibaki then baada ya kuiangusha kanu,si waligeukana?wadanganyeni wengine ila sio mimi. Sina chama na sihitaji chama.

Wewe ni sawa na kipofu utamshauri nani?
 
WanaJF,
Nawashukuru sana nyote kwa jinsi mlivyoipokea na kuijadili hii mada.Idadi ya watu walioipitia hoja hii na waliochangia mpaka sasa ukilinganisha na threads nyingine za leo imeonyesha wazi kwamba viongozi hawa wawili Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa ni majabali wa siasa za upinzani na Tanzania kwa ujumla.

Kwa kupitia maoni yenu nyote mpaka sasa imeonekana dhahiri wale Pro-CDM walioko hapa jamvini na waliojitambulisha rasmi wanawaunga mkono majabali hawa kuendelea kuongoza chama hiki na upinzani kwa ujumla.Nimegundua kitu kimoja cha ziada wafuasi wa Chadema wana imani kubwa na viongozi hawa wawili na wasingependa viongozi hawa kutenganishwa kwa njia yoyote walau kwa sasa.Nimefurahishwa na comment moja hapa kwamba baada ya viongozi hawa wawili kuiingiza Chadema Ikulu 2015 basi Freeman Mbowe ataweza kuruhusiwa kukaa pembeni.Lakini sharti akiingize kwanza chama Ikulu.Nimeipenda hii!!
Wapo rafiki zangu kina Rejao,Faiza Foxy,Ritz,Kim Kardash,Barubaru na wengineo wachache ambao wanajulikana hapa jamvini kama wapinzani wakuu wa Chadema.Pamoja na kwamba hoja mlizoleta ni za mzaha zaidi dhidi ya majabali hawa wa kisiasa,lakini nimezipenda kwa sababu mbali na kujadili kwa mizaha mmeshindwa kupinga kwa hoja chochote kile nilichoeleza katika mada yangu juu.Lakini niwashukuru kwani michango na mizaha yenu inazidisha utamu wa mjadala

Wito kwa Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa
Ningependa viongozi hawa wote wawili wasome yote yaliyoandikwa kwenye hii mada.Najua Dr Wilbroad Slaa yuko huku jamvini,sina uhakika sana kama Freeman Mbowe naye yupo.Lakini naomba walau wasaidizi wao wawatonye viongozi wao kuhusu hii mada ya leo.Pia naomba viongozi hawa wawili wasome kwa makini madai yote yaliyojadiliwa na wanaJF mpaka sasa na michango itakayoendelea kutolewa kwa sababu mjadala haujafungwa.Kama kuna mapungufu yoyote watakayoelezwa kulingana na mada hii wajirekebishe ili azma yao ya kukamata dola 2015 itimie.Wanapaswa kufahamu kitu kimoja tu-wanachama wana imani kubwa nao!!

WanaJF nafurahi kuwa member wa hili jukwaa.Thank you all.Tuendelee na mada yetu.
 
kila nikisoma post zenu nazidi kuichukia saccoss ya wachaga
Laiti kama baba yako angelikuwa Daktari au Mwalimu nafikiri ungeipenda zaidi CCM kuliko uipendavyo sasa achilia mbali kama angelikuwa mkulima tena wa jembe la mkono kijijini kwenu..
 
WanaJF,
Kwa kupitia maoni yenu nyote mpaka sasa imeonekana dhahiri wale Pro-CDM walioko hapa jamvini na waliojitambulisha rasmi wanawaunga mkono majabali hawa kuendelea kuongoza chama hiki na upinzani kwa ujumla.Nimegundua kitu kimoja cha ziada wafuasi wa Chadema wana imani kubwa na viongozi hawa wawili na wasingependa viongozi hawa kutenganishwa kwa njia yoyote walau kwa sasa.Nimefurahishwa na comment moja hapa kwamba baada ya viongozi hawa wawili kuiingiza Chadema Ikulu 2015 basi Freeman Mbowe ataweza kuruhusiwa kukaa pembeni.Lakini sharti akiingize kwanza chama Ikulu.Nimeipenda hii!!
Nimejiunga na CDM ikiwa chini ya uenyekiti wa Makani, na hakika kabla ya kuchukua uenyekiti, sikujua kama Freeman angeweza kuwa kiongozi mahiri kama alivyodhihirisha kwenye uenyekiti wake. Kuheshimu umahiri wake, nimewahi kuandika humu kuwa, tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, hakuna kiongozi wa chama chochote cha siasa Tanzania, (CCM inclusive) aliyeongoza kwa ufanisi kama Mbowe.
Hata hivyo, suala la ugombea wa uenyekiti inabidi mlichukulie kwa umakini sana. Ukisema tu kuwa lazima Mbowe aongoze hadi CDM iingie Ikulu, inaweza kuwa ndio mwanzo wa kuiingiza CDM kwenye shimo ambamo haitatoka tena au itachukua miaka mingi sana kuja kutoka. Adui zenu wanawafuatilia kwa umakini sana, na hili la kusema lazima Mbowe, lazima Slaa ni magoli mnayojifunga wenyewe. Ni vema mkawaachia wanaotaka kugombea wakajitokeza ili wapimwe na wanachama wenyewe kuamua.

Nilipinga sana kauli ya Mchange kuwa ameijenga CDM huko Kibaha, kwa hiyo wanachama wengine hawana haki ya kugombea huko, na kwa nguvu hiyohiyo, nitapingana na mpango wowote kuwa Mbowe aachiwe hadi CDM iingie Ikulu. Hata hivyo, yeyote anayetaka kugombea shurti awe critically scrutinized. Hizi harakati za kina Kafulila kutumwa huko NCCR na watu kama Mchange kulia kuwa hawana hela ya kufungua kesi wakati wanapata hela ya kuhonga wajumbe wa vikao ni za kumulikwa ili tujue nani yuko nyuma ya hizi harakati, na madhumuni yake ni nini. Vinginevyo, nikichukua fomu kutaka kumng'oa Mbowe msijeanza kupiga mayowe kwani sijatumwa na wala simtumikii fisadi yeyote.
 
Hawa jamaa ni changamoto kwetu sisi pia kujiuliza tunaweza kuwasaidia na kuchangia vipi maendeleo ya chama mbadala. Saa nyingine kazi yao na mikiki mikiki wanayokutana nayo pamoja na watanzania wengi kuwa usingizini kunawakatisha tamaa. Naomba mtujuze wakija huku Marekani na pia ile website ya chama iwe na watu wanafuatilia huko mara kwa mara kwa ajili ya kujenga chama imara cha kisasa na chenye kuwajali watu wa rika zote.
 
Nikiangalia jinsi CDM ilivyo machachari nchi nzima hivi sasa ndio ninaona umakini wa hawa majabali wawili
 
Mbowe amewashika pabaya chadema; ni taasisi ya kuuza na kununua bidhaa zake..market..sijui akikosa chairman atafanya kazi gani given "elimu yake mgogoro"

Slaa huyu babu anatumika tu na wenye chama chao; akishasafisha njia watamflush sasa hivi bado anatumika..muda muafaka haujafika..

Anyway siasa inalipa..na chadema ni easy place kuchuma; tumia ndege yako ulipwe na pesa chama (by the way ndege ingekodishwa na nani?? easy money au siyo??

Mbowe all the best wewe ni enterprnuer aisee..
 
Vipi CUF itasimamisha mgombea Arumeru?
 
Back
Top Bottom