Arsene Wenger,
Mkuu katika kujadiliana mara zote ni hoja kama zako ndizo huongeza kima cha kufikiria, wala usijisikie vibaya kuandika fikra zako. Binafsi toka siku ya kwanza nilipozungumzia swala hili nilipima mengi sana na hasa hali halisi ya nchi za kiafrika..Kama ingekuwa Ulaya ama nchi zenye demokrasia ya kweli basiUbunge ungekuwa na nguvu zaidi lakini sivyo hapa kwetu.
Majuzi tu huko Holland na Uingereza tumeona jinsi bunge lilivyokuwa na nguvu hata kuvunja serikali iliyopo na kuitisha uchaguzi mpya.. hii haiwezekani nchi zetu, mbunge anachukua majukumu yasiyokuwa ya mbunge na kwa bahati mbaya Ubunge nje ya CCM wewe ni ADUI.. Wenzetu Zanzibar walikuwa hivyo hivyo, wakipingana kwa jina la vyama wakasahau kwamba wao ni Wazanzibar kwanza. Sasa hivi taratibu wanajitambua na wanaelewa kwamba kutengana kwao kisiasa kulizidi kuwatenganisha hadi Upemba na Ungazija ukarudi kama wakati wa Sultan.
Bara nako tunatakiwa kujipanga upya, swala sii kumwondoa JK madarakani isipokuwa kuwaondoa CCM na hakuna dawa ya kuua nyoka isipokuwa kumkata kichwa. Huko Zimbabwe kusimama kwa Morgan kugombea urais against Mugabe ndiko kulikobadilisha historia ya nchi ile baada ya vyama vikuu ZANU na ZAPU kuungana na kuondoa ushindani kwa muda mrefu sana. South Afrika tumeona mabadiliko yakianzia kiti cha Ikulu,Kenya, Zambia, Malawi you name it..ni kiti cha Ikulu ambacho kinaweza piganiwa zaidi ktk kuleta mabadiliko na Bunge limefuata mabadiliko ya kiti hicho..
Kumbuka tu kwamba mfumo mzima wa Popular vote unalenga zaidi ushindi wa Ikulu na sii Ubunge.. Kama tungekuwa tukitumia mfumo wa electral vote ambapo chama chenye wabunge wengi ndicho kinachukua Ikulu basi bila shaka tungeweka nguvu zetu zaidi ktk Ubunge zaidi. Hii ndio hali halisi ya nchi zetu mkuu wangu. Hata Nyerere aliyajua hayo na ndio maana aliweka picha ya mgombea yeye mwenyewe akipingana na Ukuta, hali ndani ya chama walikuwepo watu waliopingana naye. Hivyo miaka 23 ya Utawala wa Nyerere ulitokea tu kwa sababu ya mfumo uliokuwepo hivyo tusiendekeze sana akili ya kwamba mgombea wa CCM ni lazima akubalike..Mara zote ushindani unapotokea ndipo watu huamka, mkumbuke Augustine Mrema kama sii wao kuvugana na kufuatiwa kwa vyama CUF na Chadema ktk uchaguzi mwaka 2000 ingekuwa ngumu sana kwa Mkapa.
Makosa ya kutoungana vyama vya Upinzani yameisha fanyika lakini bado hatujachelewa ikiwa bado watakubaliana kumsimamisha mgombea mmoja ktk kiti hiki.. Pia swala la muda mfupi sii hoja kabisa...CCJ imevuma toka mwisho wa Desemba kufikia mwezi wa March tayari Tanzania nzima imeshikwa na homa. Hii ina maana wananchi wamechoka! wanasubiri nabii atakaye warudisha ktk ibada ya kweli. Watu walijiuliza CCJ ni kina nani hao! je, tumaini jipya limepatikana na mengi yalizungumzwa ingawa mimi binafsii naamini ilikuwa changa la macho kupunguza nguvu ya hoja za Ufisadi. Hata hivyo bungeni hapakukalika, Ikulu hadi mitaani hadithi ilikuwa CCJ tena basi habari zilisambaa kwa uharaka zaidi ilipofahamika kwamba ni Waasisi wa chama CCM..Kwa muda mfupi sana CCJ ilitingisha Taifa zima kisiasa, lakini kwa kuwa CCJ imekosa nguvu kwa sababu hadi sasa hivi hakuna jina maarufu ambalo wananchi walitegemea..
Dr.Slaa can, he is the right candidate isipokuwa anahitaji WATU na mkakati bomba nyuma yake..Ni rahisi sana kumshinda CCM kwa hoja. Ni rahisi sana kumshinda CCM tofauti na wengi wanavyofikiria na naposema dr.Slaa anahitaji watu inabeba uzito mkubwa wa hoja nzima ya mgombea. What he need ni support ya baadhi ya watu haswa toka ktk taasisi muhimu sana. Kifupi Dr.Slaa akitumia mbinu alizotumia mwalimu kutuletea Uhuru wetu. Akikaa na wazee waasisi wa Uhuru na Muungano wa jamii hizi mbili na kusikiliza ushauri wao..Ushindi unaweza patikana na kama hautapatikana basi Upinzani wa kweli utakuwa umezaliwa UPYA.