Elections 2010 Unamuunga mkono Dr. Slaa kugombea URAIS mwaka 2010? Jiandikishe hapa

Ningefurahi sana kama angegombea na kushinda ila kuchukua uongozi wa nchi(Urais) si kazi ndogo hasa kwa mtu kutoka upinzani, Mkakati ingebidi ufanywe mapema kidogo, pengine sasa tuanze kampeni kwa ajili ya 2015. Ila vilevile Kikwete hastahili kurudi..! na dawa ni kumpa upinzani ndani ya CCM na kumng'oa.
 
Luteni, tukubali kutokukubaliana. Unaona Thomas Sankara (Mawazomatatu) anasema tumechelewa na wewe unasema tunatangaza mapema, jamani huu ni mwezi wa tano. Kweli tumechelewa ila kwa kuangalia hotuba ya jana ni kama vile kwa Tanzania wote wamechelewa. Kama Tanzania imeongozwa na watu wasio hata na degree, itakuwaje mtu Dr. Mzima aseme hawezi? Kashajionyesha kuwa anafaa na kazi yetu sasa ni KUMBEBA na kumuweka Magogoni ili ASAFISHE huo UOZO uliojilundika hapo kwa miaka mingi. Kwa kuanzia nina uhakika kabisa mishahara na marupurupu makubwa ya Wabunge, Mawaziri na safari za Rais zitapungua. Manunuzi ya kifahari yatapunguzwa na ufuatiliaji wa karibu wa pesa zetu kwenye matumizi utakuwa wa hali ya juu. Sasa hapo Mungu akupe nini?

Mawazomatatu, kumpata mpinzani ndani ya kile chama cha CCM ni sawa na haiwezekani. Kumbuka kwamba yeye ndiye mwenyekiti wa CCM na hivyo hukumu za nani agombee ni yeye anafanya. Mie bado naona dawa ni Dr. Slaa na kufanya kampeni za Kizazi kipya na very agresive in short time. Na uzuri na ubaya wa Tanzania ni kuwa watu wanasahau haraka. Unaweza ukaanza hata miezi 3 kabla na ukashinda na uanze mwaka mzima nyuma na ukashindwa.
 
Mkuu Sikonge nimekupata vizuri sana..!, mi nimesema hayo kwa kuangalia siasa za Tanzania, Watanzania wanaangalia nini kwenye kuchagua viongozi wao?? na ninaposema watanzania naomba uliangalie hili kwa picha kubwa kabisa (mpaka vijijini huko ambako bado wanajua rais ni Nyerere). Kwa mchanganuo wangu naona makundi matatu makubwa kwenye siasa za Tanzania:

Kundi la kwanza:
Watanzania wasiojua nini kinaendelea kwenye nchi yao kutokana na ukame (kutofikiwa) wa habari, hawa hawajui gazeti wala internet na pengine hata kusoma hawajui.

Watu kama hao inabidi uwafikie uwaambie Dr.Slaa ni nani? amefanya nini? na kwanini anafaa kuwa Rais?? Lazima wajue nini kinaendelea ndani ya CCM na kwanini tunahitaji kuondokana nayo? Masuala haya mimi na wewe ni rahisi sana kuyajua na ni rahisi kushangaa kwanini watu kama hawa hawayajui haya, lakini hiyo ndio hali halisi..!

Kundi la Pili:
Hawa ni watu wanaojua ukweli wote na uoza wa CCM ila kutokana na kwamba wanafaidika na uongozi wa ccm au wanajikomba (rejea wazee wa mkutano wa rais pale Diamond juzi kama mfano) kwa uongozi ili kupewa zawadi ndogondogo(fedha,nguo, baiskeli n.k) au matarajio ya kuja kufaidika mbeleni.

Hawa nao inabidi waelimishwe na waambiwe athali za matendo yao kwamba nchi itafika mahali tutakua tunaishi kama wanyama (survival of the closest to ccm) na mwenye uwezo wa kuiba zaidi ndie ataefaidika zaidi. Mwishowe tutafika mahali hakuna cha kuiba.

Kundi la Tatu:
Ndilo lenye watu wachache lakini wenye uwezo wa kuleta mabadiliko wakiamua. Wengi wetu (humu JF na kwingine) tunaangukia kwenye kundi hili, tunaujua uoza wa CCM na hatma ya nchi yetu kama tutaendelea kuwa ktk hali hii. Kundi hili linahitaji kuamka na kujitoa kwa ajili ya nchi, kuwaelimisha wasioelewa na kujitokeza kuchukua Uongozi wa nchi. Kwa bahati mbaya sana kundi hili lenye ufahamu mkubwa limekua likiona siasa kama mchezo mchafu huku wakisahau kuwa kila idara ya maisha yao inaguswa kwa namna moja au nyingine na maamuzi ya wanasiasa.
 
Labda huyu Dr. Slaa anatakiwa KUAMSHWA. Nimeona tufanye SENSA ya haraka haraka humu ndani ya JF. Kwa wale wote wanaoona DR SLAA agombee mwaka huu basi hebu jiandikishie jina lako tuone mwisho wa wiki tutakuwa wangapi. Tujitokeze kwa wingi ili kumuonyesha Dr. Slaa anavyohitajika.

Dr. Slaa, samahani nimeamua kuanzia jina lako kwa makusudi kabisa maana JEMADARI lazima awe mbele na wengine watafuata.

1. Dr. Slaa 2. MKANDARA 3. King of kings 4. Masanilo kugema 5. Fidel80

6. Bht 7. Tanzania 8. Ndege ya Uchumi 9. Jiwe 10. Jakathesi

11. Technician 12. Kilembwe 13. Ndjabu Da Dude 14. Bollo Yeng 15. Selous

16. Nyamizi 17. Mfwatiliaji 18. Sikonge 19. Ben 20.Lorah

21. Chief 22. Alpha 23. Malunde-Malundi 24. Muhindi 25. Nanu

26. Betina 27. Baija Bolobi 28. Epigenetics 29. Member 911 30. Mlalahoi

31. Mag3 32. Nndondo 33. Tai Ngwilizi 34. Sn2139 35. Shalom

36. Mc 37. Firstlady1 38. Henge 39. Nemesis 40. Mchili

41. Ngambo Ngali 42. Positive Thinker 43. Advocate Jasha 44. Zhule 45. Araway

46. Pasco 47. Mbu 48. The Invincible 49. Vivian 50.

51. Holowane
 
Najiandikisha ila utaratibu nadhani haujakaa vizuri kivile. Kingi nimejiandikisha, ila sijajua ni namba ngapi nipo
 
Mkuu Sikonge nimekupata vizuri sana..!, mi nimesema hayo kwa kuangalia siasa za Tanzania, Watanzania wanaangalia nini kwenye kuchagua viongozi wao?? na ninaposema watanzania naomba uliangalie hili kwa picha kubwa kabisa (mpaka vijijini huko ambako bado wanajua rais ni Nyerere). Kwa mchanganuo wangu naona makundi matatu makubwa kwenye siasa za Tanzania:

Kundi la kwanza:
Watanzania wasiojua nini kinaendelea kwenye nchi yao kutokana na ukame (kutofikiwa) wa habari, hawa hawajui gazeti wala internet na pengine hata kusoma hawajui.

Watu kama hao inabidi uwafikie uwaambie Dr.Slaa ni nani? amefanya nini? na kwanini anafaa kuwa Rais?? Lazima wajue nini kinaendelea ndani ya CCM na kwanini tunahitaji kuondokana nayo? Masuala haya mimi na wewe ni rahisi sana kuyajua na ni rahisi kushangaa kwanini watu kama hawa hawayajui haya, lakini hiyo ndio hali halisi..!

Kundi la Pili:
Hawa ni watu wanaojua ukweli wote na uoza wa CCM ila kutokana na kwamba wanafaidika na uongozi wa ccm au wanajikomba (rejea wazee wa mkutano wa rais pale Diamond juzi kama mfano) kwa uongozi ili kupewa zawadi ndogondogo(fedha,nguo, baiskeli n.k) au matarajio ya kuja kufaidika mbeleni.

Hawa nao inabidi waelimishwe na waambiwe athali za matendo yao kwamba nchi itafika mahali tutakua tunaishi kama wanyama (survival of the closest to ccm) na mwenye uwezo wa kuiba zaidi ndie ataefaidika zaidi. Mwishowe tutafika mahali hakuna cha kuiba.

Kundi la Tatu:
Ndilo lenye watu wachache lakini wenye uwezo wa kuleta mabadiliko wakiamua. Wengi wetu (humu JF na kwingine) tunaangukia kwenye kundi hili, tunaujua uoza wa CCM na hatma ya nchi yetu kama tutaendelea kuwa ktk hali hii. Kundi hili linahitaji kuamka na kujitoa kwa ajili ya nchi, kuwaelimisha wasioelewa na kujitokeza kuchukua Uongozi wa nchi. Kwa bahati mbaya sana kundi hili lenye ufahamu mkubwa limekua likiona siasa kama mchezo mchafu huku wakisahau kuwa kila idara ya maisha yao inaguswa kwa namna moja au nyingine na maamuzi ya wanasiasa.
MawazoMatatu

Nashukuru kwa ufafanuzi wako kwa nini tusikimbilie kumlazimisha Slaa agombee urais, nikitolea mfano wako wa makundi kundi la pili (the puppets) ndilo lenye matatizo makubwa na linajua athari za uongozi uliopo lakini kwa maslahi yao halitaki kukubali ukweli, kwa hiyo kuli convince kundi kama hili kuwa kuna shujaa kama Slaa ni kazi kubwa.

Makundi yaliyobaki la kwanza (vijijini) na la tatu (know how) ni rahisi kidogo ukilinganisha na la pili, kumuuza Slaa kwa kundi la kwanza inawezekana lakini inahitaji nyenzo kubwa na muda, Dr. Slaa anajulikana sana na kundi la tatu hata la pili (the puppets), sasa watu wa kumuuza watoke wapi au kundi lipi, tukisema watoke kundi la tatu ambalo ndilo walimo wanaJF kwa hali halisi itakuwa kazi na kusema kundi la pili walimo ma puppet wa chama tawala vile vile ni kazi kweli kweli.

Sasa kifanyike nini, tusijidanganye kuwa Slaa ameshakuwa maarufu kuliko Mrema, umaarufu wa Slaa ni wa utendaji kazi tofauti na umaarufu wa Mrema ambao ni wa propaganda(mdomo sana/na uongo ndani) ambao kwa siasa za Tanzania bado una play part kubwa hasa vijijini, ukiwaambia watu wa vijijini kuwa tumewaletea Slaa kwa vile alifichua wizi wa EPA sijui kama watakuelewa usikute wengine hata EPA hawajui ni nini, kwa hesabu ya haraka haraka ndiyo maana sisiem wanaomba usiku na mchana Slaa agombee, kwa hiyo mimi bado nasema tumsubiri mwenyewe aamue kwa vile nafikiri anajua uzito wa kazi ulio mbele yake.
 
Mawazomatatu na Luteni,
Ninashukuru sana kwa mawazo yenu. Ila mie na hawa wangine ngoja tuwe ma Thomas wa kwenye Biblia. My last ujumbe kwenu ni :
english1.jpg
 
mie napinga asigombee sasa hivi na apeleke nguvu zaidi kuongeza wabunge wapinzani bungeni.tukishaliteka bunge hapo itakuwa rahisi sana kushinda uraisi.lakini kwa sasa jinsi mchezo mchafu unavyofanyika kwenye uchaguzi kumueka dr slaa october kugombea kiti cha uraisi ni sawa sawa na kupoteza wabunge 10 wa upinzani bungeni.

Dr. Slaa please usigombee uraisi nakuomba uongeze bidii katika kuongeza wabunge wa upinzani zaidi bungeni.
 
Arsene Wenger, hata uandike vipi na upinge vipi hilo sisi hatuangalii. Binadamu anayesikiliza maneno ya kuvunja moyo, huwa hafiki mbali. Hakuna aliyejua kuwa Inter Millan itashinda mechi (ifungwe goli moja tu) huku ikiwa na wachezaji 10 na inacheza na Barcelona yenye wachezaji 11. Lakini iliwezekana.
Hata mfanyeje, bado CCM itakuwa na wabunge zaidi ya NUSU. Sasa kwa nini kupoteza muda na UBUNGE wakati ukipeleka mtu Magogoni, atakuwa zaidi ya hao wabunge wote wa upinzani? Kwa nini unaomba kisu kukata mti wakati unaweza kutumia shoka/msumeno ? Kama kucheza faulo, una uhakika gani mwaka huu CCM hawatamchezea Faulo? Tumewazoesha vibaya sana CCM na pia mwaka huu CCM wenyewe wamegawanyika sana na ni kipindi pekee cha kumtandika konde la knock out huyu Tyson muuma watu.
 
Mkuu Sikonge nimekupata vizuri sana..!, mi nimesema hayo kwa kuangalia siasa za Tanzania, Watanzania wanaangalia nini kwenye kuchagua viongozi wao?? na ninaposema watanzania naomba uliangalie hili kwa picha kubwa kabisa (mpaka vijijini huko ambako bado wanajua rais ni Nyerere). Kwa mchanganuo wangu naona makundi matatu makubwa kwenye siasa za Tanzania:

Kundi la kwanza:
Watanzania wasiojua nini kinaendelea kwenye nchi yao kutokana na ukame (kutofikiwa) wa habari, hawa hawajui gazeti wala internet na pengine hata kusoma hawajui.

Watu kama hao inabidi uwafikie uwaambie Dr.Slaa ni nani? amefanya nini? na kwanini anafaa kuwa Rais?? Lazima wajue nini kinaendelea ndani ya CCM na kwanini tunahitaji kuondokana nayo? Masuala haya mimi na wewe ni rahisi sana kuyajua na ni rahisi kushangaa kwanini watu kama hawa hawayajui haya, lakini hiyo ndio hali halisi..!

Kundi la Pili:
Hawa ni watu wanaojua ukweli wote na uoza wa CCM ila kutokana na kwamba wanafaidika na uongozi wa ccm au wanajikomba (rejea wazee wa mkutano wa rais pale Diamond juzi kama mfano) kwa uongozi ili kupewa zawadi ndogondogo(fedha,nguo, baiskeli n.k) au matarajio ya kuja kufaidika mbeleni.

Hawa nao inabidi waelimishwe na waambiwe athali za matendo yao kwamba nchi itafika mahali tutakua tunaishi kama wanyama (survival of the closest to ccm) na mwenye uwezo wa kuiba zaidi ndie ataefaidika zaidi. Mwishowe tutafika mahali hakuna cha kuiba.

Kundi la Tatu:
Ndilo lenye watu wachache lakini wenye uwezo wa kuleta mabadiliko wakiamua. Wengi wetu (humu JF na kwingine) tunaangukia kwenye kundi hili, tunaujua uoza wa CCM na hatma ya nchi yetu kama tutaendelea kuwa ktk hali hii. Kundi hili linahitaji kuamka na kujitoa kwa ajili ya nchi, kuwaelimisha wasioelewa na kujitokeza kuchukua Uongozi wa nchi. Kwa bahati mbaya sana kundi hili lenye ufahamu mkubwa limekua likiona siasa kama mchezo mchafu huku wakisahau kuwa kila idara ya maisha yao inaguswa kwa namna moja au nyingine na maamuzi ya wanasiasa.

Wasomi wenyewe wanapotosha jamii na tafiti za kuwafurahisha watawala (REDET) huku wanajua unataraji nini ? Ni pale tu walalahoi watakapochoka na kusema sasa na si kwa porojo za ukumbini
 
Arsene Wenger, hata uandike vipi na upinge vipi hilo sisi hatuangalii. Binadamu anayesikiliza maneno ya kuvunja moyo, huwa hafiki mbali. Hakuna aliyejua kuwa Inter Millan itashinda mechi (ifungwe goli moja tu) huku ikiwa na wachezaji 10 na inacheza na Barcelona yenye wachezaji 11. Lakini iliwezekana.
Hata mfanyeje, bado CCM itakuwa na wabunge zaidi ya NUSU. Sasa kwa nini kupoteza muda na UBUNGE wakati ukipeleka mtu Magogoni, atakuwa zaidi ya hao wabunge wote wa upinzani? Kwa nini unaomba kisu kukata mti wakati unaweza kutumia shoka/msumeno ? Kama kucheza faulo, una uhakika gani mwaka huu CCM hawatamchezea Faulo? Tumewazoesha vibaya sana CCM na pia mwaka huu CCM wenyewe wamegawanyika sana na ni kipindi pekee cha kumtandika konde la knock out huyu Tyson muuma watu.
haya mkuu,yale yalikuwa maoni yangu tu kutokana na ukweli halisi.naunga mkono yeye kugombea uraisi siku ambayo uchaguzi wa haki utakapo fanyika lakini uchaguzi huu wa sasa hivi bado kabisa na nirahisi kuongeza wabunge wa upinzani sasa hivi kuliko kumpata raisi mpinzani.

naheshimu maoni yako.
 
Back
Top Bottom