Unakumbuka mapenzi ya sekondari? ...kipindi hamna simu za mkononi?

Nakumbuka nikiwa mazengo msingi kuna dem alimtolea nje kaka angu, basi me nikamuandika barua ya kumtukana alaf nikamchora picha wana mdu. Basi yule dada akaipeleka kesi kwa walimu. Nikaitwa ofisini kwanza wakanionyesha barua nikakili kuwa ni mimi, kilichofuata ni nilitandikwa fimbo na walimu wote ofisini. Nilirudi nyumani ****** meusi yamevia damu na sikumwambia mtu na bro aliporudi nikampa stori yaliyonipata! huwa sisahau tukio hili ilikuwa 1996 nipo la sita.
 
Jamaa yangu mmoja alikuwa akimfuatilia dem wamtaani kwetu pale kilimani dom, siku moja tulikwenda nyumbani kwao na dem bahati akatoka mama yake alikuwa ni jaji pale dodoma kwa kuzuga ilibidi tununue spinachi na mchicha wa mia mbili tukaondoka. Tulilaani kweli maana haikuwa kwenye bajeti na zile mboga tuliwapa bata mzinga ! hii yote ilitokana na kukosa mawasiliano ya sim.
 
haa haa hah...izo mboga si mngepeleka kwa bi mkubwa mdau?
 
Me nlikuaga nashobokewa na vitoto vya kike enzi hzo bt mwenyewe nlikuaga domo zege..
 
Kama mjuavyo shule za sekondari miaka ya 1998 zilikuwa bado ni chache hivyo ulikuwa unalazimika kwenda kusomea ugenini.Nilipofika huko nilianzisha uhusiano na kakiburudisho tulikokuwa tunasoma nako.Hako kakiburudisho kalikuwa kanaishi kwa babu yake sasa tulikuwa tuna tabia ya kutumia ishara ya kiburudisho kujifunga uzi mguuni halafu anapitisha huo uzi dirishani tukifika tunavuta uzi kiburudisho kikisikia kinavutwa kinakuja kufungua.La haula kumbe babu alikuwa amekwishatushtukia na ishara tunayoitumia siku hiyo akamwambia kiburudisho walikuwa wanalala na mdogo wake waende kulala chumbani kwake tulipofika kama kawaida tuko na mshkaji wangu alikuwa anam.....mdogo mtu ili asivujishe siri.Tukavuta kamba babu alivyosikia anavutwa akajua tayariiiii akafungua mlango ndani giza tukazama ndani fasta weee tuliaanza kupokea kichapo huku mselaangu anajitetea sio mimi babu huwa namsindikiza huyu tulivyofunguliwa kila mmoja alipita njia yake tulikuja kukutana geto kila mmoja akijikuna.Kesho yake shuleni mstaarini babu akaja amemshkilia kiburudisho mwalimu nae akatuzungushia laundi zake za kutosha huku babu akisimulia mstaarini alivyotukamata ilikuwa aibu.Mselaangu sasa hivi anafanya kazi wizara ya aridhi huwa tukikumbushana tunacheka sana.
 
Mimi nilipobale* nilikuwa form two(1993). Nilikuwa nasoma boarding basi nilimpenda mtoto wa pekee wa teacher wangu aliyekuwa akiishi karibu na skuli basi nikapanga na binti kwenda kumaliza ** jumamosi jioni kwani wazazi wake wanaenda kwenye harusi. Basi nilitia timu nikaingia chumbani nikaanza majukumu si nikajisahau saa nne tukasikia geti linagongwa kwanini nisiingie mvunguni. ! Ilinibidi nikae pale usiku binti alipokuja tuliendelea na majukumu. Jumapili asubuhi nikarudi uvunguni kwani hawakuenda church nikakaa kutwa nzima demu aliniletea ka wali na maji. Usiku binti akaja tukalala ila sikuweza tena kwa ajili ya njaa asubuhi ya jumatatu baba na mama wa binti waliondoka na binti alienda shule nyumba ikafungwa. Binti alirudi mchana chapu akanifungulia nikatoka sasa noma kurudi shule kwani kuna sheria za kufa mtu. Ila nilifanikiwa kurudi tangia siku hiyo nilijuta
 
mkuu, umenikumbusha kuna siku nilipanga nae kuwa nikikaribia kwao nimtumi mtoto fulani..yule mtoto si akaenda akamuita mbele ya wazazi wake, basi wale wazi wakamtuma yule mtoto aje aniambie niende maana wazazi wake hapo, nikaenda kwa shauku kuingia ndani mlango ukafungwa na kaka mtu na pembeni kuna dingi na mama yake huku wakinikaribisha na kunitaka niseme shida yangu..nikasema nina shida na mtoto wao akaitwa alikuwa jikoni, alipofika tukawa tunatazamana tu..fasta nikawaza niombe daftari lake nikaandike n
 
Mimi nilipobale* nilikuwa form two(1993). Nilikuwa nasoma boarding basi nilimpenda mtoto wa pekee wa teacher wangu aliyekuwa akiishi karibu na skuli basi nikapanga na binti kwenda kumaliza ** jumamosi jioni kwani wazazi wake wanaenda kwenye harusi. Basi nilitia timu nikaingia chumbani nikaanza majukumu si nikajisahau saa nne tukasikia geti linagongwa kwanini nisiingie mvunguni. ! Ilinibidi nikae pale usiku binti alipokuja tuliendelea na majukumu. Jumapili asubuhi nikarudi uvunguni kwani hawakuenda church nikakaa kutwa nzima demu aliniletea ka wali na maji. Usiku binti akaja tukalala ila sikuweza tena kwa ajili ya njaa asubuhi ya jumatatu baba na mama wa binti waliondoka na binti alienda shule nyumba ikafungwa. Binti alirudi mchana chapu akanifungulia nikatoka sasa noma kurudi shule kwani kuna sheria za kufa mtu. Ila nilifanikiwa kurudi tangia siku hiyo nilijuta

mkuu umenivunja mbavu hapa...vip suala la kwenda kujisaidia?sipati picha kama choo likuwa ni choo cha nje...
 
Mimi nilipobale* nilikuwa form two(1993). Nilikuwa nasoma boarding basi nilimpenda mtoto wa pekee wa teacher wangu aliyekuwa akiishi karibu na skuli basi nikapanga na binti kwenda kumaliza ** jumamosi jioni kwani wazazi wake wanaenda kwenye harusi. Basi nilitia timu nikaingia chumbani nikaanza majukumu si nikajisahau saa nne tukasikia geti linagongwa kwanini nisiingie mvunguni. ! Ilinibidi nikae pale usiku binti alipokuja tuliendelea na majukumu. Jumapili asubuhi nikarudi uvunguni kwani hawakuenda church nikakaa kutwa nzima demu aliniletea ka wali na maji. Usiku binti akaja tukalala ila sikuweza tena kwa ajili ya njaa asubuhi ya jumatatu baba na mama wa binti waliondoka na binti alienda shule nyumba ikafungwa. Binti alirudi mchana chapu akanifungulia nikatoka sasa noma kurudi shule kwani kuna sheria za kufa mtu. Ila nilifanikiwa kurudi tangia siku hiyo nilijuta

mkuu,ulitakiwa umuoe huyo binti kabisa.
 
ha ha ha ha tihi tihi umefurahisha sana jamani!! ila mapenzi yale yalikuwa matamu sana mana yalikuwa ya kuviziana jamaa akusubirie kwenye geti la shule na atoe mimacho la sivyo ukijichanganya na wenzio hawezi kukuona itakuwa ndio bye!!
 
Back
Top Bottom