Unakumbuka mapenzi ya sekondari? ...kipindi hamna simu za mkononi?

Wakati nkiwa sekondari simu za mkononi zilikuwa bado hazijaenea sana,ndo kwanza zilikuwa zinaingia nchini!Njia kuu ya kukutana na msichana wako ilikuwa kwa kuandikiana barua,au mnaambiana mkutane wapi.
Basi,nlikuwaga na msichana wangu wa form3 mtaani, Siku moja nkiwa likizo kitaa tukaaidiana tukutane,akanambia nimpitie kwao sababu baba na mama yake na mdogo wake watakuwa wamesafiri.
siku iyo nlikuwa naenda ku*** naye,si unajua.nkafika nkagonga geti....lahaulaaa!kumbe mzee wake aliairisha safari.na hakuweza kunambia mana kulikuwa hamna simu kama sasa ivi.nkamsalimia,mdingi akaniuliza unasemaje?nkapiga akili nkamwambia mama kanituma kuulizia kuku(alikuwa anafuga kuku wa kisasa).akasema zipo chache,kakutuma ngapi?alivosema chache,mi nkasema nkitaja nyingi atasema hana.nkasema anataka kuku 20.akasema anabahati kweli wapo 20net.nkamwambia ngoja nkwambie mama basi.akasema mamako hanaga shida mpelekee ataniletea hela.
Wadau.nlibebeshwa kuku 20,nkaziuza kwa bei ya hasara kwa wakaanga chips.
...unakumbuka kisa gani kilichokutokea katika mapenzi ya sekondari?

dah,kaka hii kali sana!!uliwabebaje sasa?
 
hahaha nimekumbuka jamaa alikutwa na baba mdogo anarusha vijiwe aliingizwa ndani kakunjwa shati nikaitwa kuulizwa ni nani nikamkana, nilivoona wanataka kumpa kipondo nikajikuta nasema namjua namjua msimpige, akaachiwa kile kikao nilichokalishwaaa??? sitasahau
 
kuna binti tukitaka kumeet inabidi niende kwao na kurusha jiwe kwenye uzio wa mabanzi,akisikia mlio anatoka nje.siku moja nilirusha jiwe likapitiliza kwenye tundu na kumgonga dingi yake,alikuwa kasimama nje.yule dada alinimaind sana kisa kwa nn ckuangalia kwanza!
 
ha ha ha ha tihi tihi umefurahisha sana jamani!! ila mapenzi yale yalikuwa matamu sana mana yalikuwa ya kuviziana jamaa akusubirie kwenye geti la shule na atoe mimacho la sivyo ukijichanganya na wenzio hawezi kukuona itakuwa ndio bye!!

umeona eh?mlisumbuaga sana watu kabla ya simu.sa ivi mambo yamekuwa simpooooo kwa wanafunzi sasa ivi.
 
dah,kaka hii kali sana!!uliwabebaje sasa?

jinsi nlipata shida na wale kuku.wala usinikumbushe nlivowabeba yani.mana kwanza nawaza ntawapeleka wapi,na nawaza ntamuuzia nani kuku wote!!alinisaidia sana jamaa yangu mmoja.bila yeye hata wale wauza chipsi singewajua,japo waliwanunua kwa hasara
 
Kaka mimi ni muathirika wa issue hii,mimi nilikuwa na toka na msichana niliyyekuwa nimemtangulia kidato,nilipomaliza form 4 nilirudi nyumbani lakini baada ya kukaa kwa mda niliambiwa niende kwa kaka kumsaidia kufanya shughuli fulani,ile shuleilikuwa ya binafsi hivyo mtu ukituma barua posta ni lazima uongozi wa shule uisome so sikuweza kumtumia barua posta kumtaarifu sipo nyumbani,kwa hiyo yeye akajua bado niko home.kulikuwa na magari ya abiria kipindi hicho mtu akiandika barua na kuomba waidondoshe mahali fulani inafika.dada kaandika barua ya kwanza kaweka kwenye basi ikafika mzee akasema ngojqa niisome ikiwa kunaujumbe wa haraka niwasiliane na kijana wee alipochana bahasha kwanza kakutana na kiss be4 read ndani yake kakuta fulani yahani sitokusahu dea nakumbuka pindi tuko wote kamasiku ile yaani niliridhika dia husinisaliti na mwisho na omba uninunulie vyupi na taiti za kufanana na vyupi hivyo!kilichoendelea impact yake ipo hadi leo
 
Hivi karatasi za kuandikia barua zile za maua zinazonukia bado zinauzwa stationery? Aliyevumbua mobile na internet amewakosesha vijana uhondo.

Yaani mtu unakuwa na file la barua; unafanya kurudia rudia kusoma. Afu uwe boarding jamaa asiandike mbona anapewa talaka; maana mabwenini ni kutambiana nani kapokea barua.
 
Kama mjuavyo shule za sekondari miaka ya 1998 zilikuwa bado ni chache hivyo ulikuwa unalazimika kwenda kusomea ugenini.Nilipofika huko nilianzisha uhusiano na kakiburudisho tulikokuwa tunasoma nako.Hako kakiburudisho kalikuwa kanaishi kwa babu yake sasa tulikuwa tuna tabia ya kutumia ishara ya kiburudisho kujifunga uzi mguuni halafu anapitisha huo uzi dirishani tukifika tunavuta uzi kiburudisho kikisikia kinavutwa kinakuja kufungua.La haula kumbe babu alikuwa amekwishatushtukia na ishara tunayoitumia siku hiyo akamwambia kiburudisho walikuwa wanalala na mdogo wake waende kulala chumbani kwake tulipofika kama kawaida tuko na mshkaji wangu alikuwa anam.....mdogo mtu ili asivujishe siri.Tukavuta kamba babu alivyosikia anavutwa akajua tayariiiii akafungua mlango ndani giza tukazama ndani fasta weee tuliaanza kupokea kichapo huku mselaangu anajitetea sio mimi babu huwa namsindikiza huyu tulivyofunguliwa kila mmoja alipita njia yake tulikuja kukutana geto kila mmoja akijikuna.Kesho yake shuleni mstaarini babu akaja amemshkilia kiburudisho mwalimu nae akatuzungushia laundi zake za kutosha huku babu akisimulia mstaarini alivyotukamata ilikuwa aibu.Mselaangu sasa hivi anafanya kazi wizara ya aridhi huwa tukikumbushana tunacheka sana.

Kiburudisho umenikumbusha mabli sana na nimecheka kweli hapa nilipo,da cha kwangu ndio balaa maana hua sitaki kumbuka
 
ROFLMAO...u made my day...pole sana bandugu lakini umenifurahisha sanaaa

Serves you right though tryna mess with his daughter....

Thank God for technology:A S 100:
 
Hahahahahahaa
dah,mimi kwakweli nilikua narusha mawe juu ya Paa la nyumba yao,then anatoka!
 
Huu mchezo nimekuja kuucheza nikiwa Advance, O level nilikua boya boya dizain enzi hizo Tanga tech pale kuna watoto wa kifungilo wakajipendekeza eti wanataka penpals wakaandika majina yao kama kumi hivi na location pia ili tuwasiliane kisha kama vip likizo tuweze kuonana coz wote walikua wanatoka dar...basi bana barua ikafika bwenini (chui domitory) wazee tukajinyakulia majina kila mtu lake kuna jina moja lilikua limekaa kishari shari 'ASHA' kila mtu akawa analikwepa akihisi atakua asha ngedere mcharuko kumbe ndo mzuri kuliko wote, ofcoz me nilichukua hilo jina coz nilichelewa nikakuta majina mazuri mazuri yote wameshayawahi wadau...tukaanza kutumiana na kupokea barua...nakumbuka ule upuuzi eti unaandika kwanza barua kwenye rafu afu ndo unakuja kuiandika vizuri kwenye karatasi zetu zile za kimahaba maua maua nini dizain fresh...basi bana twende na kwenda school kwao kuaanza unoko barua ikifika na kuhisiwa ya malavi davi inasomwa assembly wazee tusiokubali kushindwa tukabuni mbinu ya ki scolfied kila herufi tukaipa symbol kwa mfano A=x, B=j, C=u nk so kama nimeandika 'sdaenfdhbgn' unakuta inamaanisha 'hello baby i missed u' nk, so unakuta barua nzima imeandikwa katika mfumo wa 'djfhsbshwhfhbf' huku kila herufi ikiwa na maana yake na kuiandika ilikua inagharimu almost hata siku mbili...unautuma mzigo hata akiikamata huyo mwalimu wao bado haelewi umeandika nini na dem nae anatumia kama siku mbili hivi kuisoma hadi kuimaliza...ujio wa facebook simu za mkononi kwa wingi umerahisisha sana maisha...nakumbuka unasimama assembly barua zainaitwa yako isipoitwa unahisi ka umepata supplementary core subject...kweli maisha yanachange fasta
 
Kwa kweli tumetoka mbali, sa ivi ni mwendo wa teknolojia.
Kabla ya simu hata msiba mtu ilikuwa inabidi mtu asafiri hadi kwa ndugu, ndio ampe taarifa.
 
Back
Top Bottom