Unaishi vipi na mwanaume asiyepokea ushauri wa mwenza/ watu wengine?

Fanya kinachowezekana maana madhara yake yanagharimu adi ustawi wa familia. Nakwambia haya kwa sababu nimekulia familia ya aina hii mpaka kesho mzee wangu hashauriki licha ya kuwa anaangukia pua mara nyingi ila hakomi.
Please naomba unisaidie point mbili tatu kwenye hapo pa kufanya kinachowezekana….nifanye vitu gani??
 
Please naomba unisaidie point mbili tatu kwenye hapo pa kufanya kinachowezekana….nifanye vitu gani??
Ukishamjua mtu utajua namna ya kuishi nae, kuna baadhi ya mambo unaweza kufanya mwenyewe ila kuna yale ambayo huwezi kufanya bila yeye na hapo ndio shida inakuwepo.

Kwa experience yangu mama alikuwa anamshauri asipoufuata na matokeo yakawa mabaya mzee baba anakata tamaa na kuanza kusua sua na hapo mama anachukua jukumu la kufanya kama alivyoshauri mwanzo.

Kwa unachoweza kufanya be ready for it kwa sababu kuna mambo unajua fika yasipofanyika kwa namna fulani ni lazima yatafeli tu.
 
Huyo sio kwamba hapokei ushauri kabisa kutoka kwa watu. Anapokea ushauri vizurii tu ila ushauri usio sahihi. Kitendo cha kuachana na Project A na kukimbilia kuanzisha nyingine hapo ni ushahidi kwamba kuna watu walimshauri ila huo ushauri haukuwa sahihi kwake.
AISEE
 
Wanawake wengi hawajui kuwashauri wenza wao vizuri, mwanamke anaweza kukushauri jambo la ajabu na anataka ulifanye utake usitake na usipolifnya ni kununiana, na wakati mwingine mwanamke anakupa ushauri wakati Hana input yeyote ila maneno tu, wanaume tumepewa kipawa Cha kufanya maamuzi , unaamua halafu utajilaumu au kujishushukuru baadae, after all sio Kila ushauri lazima ufuatwe ushauri mwingine ni kama nguvu za giza!
 
Okaay umenifumbua macho,asante.!sasa naomba ushauri namna ya kudeal na hii tabia yake.
Its very simple mathematics hapo. Mwenye njaa mpe chakula kinyume chake usimpe, mwenye shida msaidie kinyume chake usimsaidie. Ambaye hataki kushauriwa usimshauri sababu ameshakuonyesha hataki kufuata unachomwambia.

Jitihada zako elekeza kwenye eneo la kupambana na ujenzi wa mambo mengine ambayo yeye haingii muache atengeneze hasara zake.
 
Back
Top Bottom