Unaishi vipi na mwanaume asiyepokea ushauri wa mwenza/ watu wengine?

Usifosi ushauri wako utumike kwenye pesa ya mtu mwingine, we kama umeolewa base kwenye duties zako zinazokuhusu kama kufua, kupika na usafi hayo mengine ni juu ya mme wako akiamua akushirikishe ni sawa asipo amua kukushirikisha ni sawa pia kwasababu Yeye ndio Bosi kwenye familia yenu anajua nini atafanya chakula kipatikane na wewe kama mke wake upendeze.
😁😁😁imebidi nicheke,sasa kama
Sipendezi niendelee tuu kukaa kimya?
 
Wewe ulipoanza kufanya Plan zako yeye mbona hakupinga??? Wanawake huwa mna changamotoo sanaa unataka ununue kiwanja kimyakimyaa au ufanye ujenzi kiwanja cha urithi bila kiomba ushaurii ila mwenzio akianza kufanya jambo lake unaona hayupo sahihiii..
Plan gani tena mkuu?mimi hapana jengaa kwenye kiwanja cha urithi
 
Kuna watu hawashauriki hata waangukie pua mara 100 hawakubali ushauri kabisa. Ni toxic behaviour kuibadili sio rahisi inahitaji muda na matukio mengi tena kwa anaekubali kujifunza kutokana na makosa.
 
Inabidi nianze kukubaliana na hili tu.
Fanya kinachowezekana maana madhara yake yanagharimu adi ustawi wa familia. Nakwambia haya kwa sababu nimekulia familia ya aina hii mpaka kesho mzee wangu hashauriki licha ya kuwa anaangukia pua mara nyingi ila hakomi.
 
Back
Top Bottom