Unahitaji Moyo wa Chuma kufikia maamuzi haya .....

Nadhan hapo hakuna suala la kuwa bwana 'hassan'ameweza kwakua yeye ni mjeda ila ni moyo ambao kila binadamu anatakiwa kua nao afterall he loved her without knowing what he knows now.rose still rose even after roating
 
Nadhan hapo hakuna suala la kuwa bwana 'hassan'ameweza kwakua yeye ni mjeda ila ni moyo ambao kila binadamu anatakiwa kua nao afterall he loved her without knowing what he knows now.rose still rose even after roating

Hili nalo neno!
 
Huo upendo umekaa KIYESU YESU!
Hongera zake ingawa ndo inavyotakiwa kuwa ie katika shida na raha kuanzia kwenye uchumba ndoa na mpaka maisha baada ya ndoa
 
Life is all about decisions, sometimes very tough decisions this is one of my favaurite quotes,

There is nothing beutifull in this world that true love feelings, hasa zikiingia kwa pande zote mbili, mnaweza kufanya kitu cha ajabu sana, kuna watu wanaoa hadi abnormal in the sake of love, kuna jamaa nilionaga dstv ni mtu mkubwa sana sony corpolation simkumbuki jina, alifosi kuoa mwanamke aliyepata matatizo ya ubongo kwenye ajali na akawa unsound mind, but jamaa aligoma kumuacha akampandisha church na akapata nae watoto wawili wazima japokuwa mke wake ni unsound mind... Dunian kuna watu wana feelings za ajabu


Huyo jamaa nimemkubali, loh!
 
Ningeomba msamaha kwa Mola kwani nisingeweza kabisaaa!!! Big up Mr Hassan. Ni wachache wanaweza kuwa na moyo kama wako.
 
Nimeshawahi kutibu couple ya aina hii (discordant couple), kwa kweli zipo nyingi...na mara nyingi ni mwanamke anakuwa HIV +ve na mwanaume ni -ve. Na mara nyingi pia wanaume huwa wanabaki na wanawake zao japo wengine huwa hawataki kushiriki nao tendo la ndoa.

Kuna couple moja niliwahi kuitibu nao walikuwa wachumba mwanamke akawa +ve na mwanaume -ve, wakaoana, lakini yule mwanaume hakuwa anasikiliza ushauri wetu wa jinsi ya kujikinga wakati wa kupata mtoto, baada ya miezi 6 ya ndoa mwanaume naye akawa +ve, alilia sana, lakini wakaendelea. Na sasa wana mtoto mmoja hasiye na maambukizi.

Alikosea sana. Mkuu riwa nina swali itabidi niku-pm kiongozi wangu.
 
dah! Unyanyapaa haukubaliki lakini unausikiliza na moyo pia,hakuna anayejua nin kitatokea kesho au baadaye siku ya leo but kwa hili la huyo jamaa ni zaidi ya upendo kama hakukuwa na fact nyingine,binafsi lisingewezekana na Mungu angenisamehe kwa kweli...
 
Binafsi nisingeweza kabisa ingawa ingeniuma sana! Hongera yake bwana hassan kwa ujasiri.
 
Jana kupitia ITV, nilisikia ushuhuda wa dada mmoja kwa jina la Zainabu kama sijakosea ambaye alikuwa anaishi na mchumba wake Mwanajeshi aitwa Hassan, huko Tanga na kuhamia Dar. Baada ya kusumbuliwa na matatizo ya kiafya kwa muda, walienda kupima na huyo dada kugundulika kuwa na Virusi vinavyosababisha UKIMWI wakati mumewe alikuwa safi.

Kwa upendo mwingi, kaka yule aliamua kufunga ndoa na mchumba wake huyo mwenye HIV, na Mungu aliwabariki mwaka jana wamepata mtoto asiye na maambukizi baada ya kufuata ushauri nasaha na kupima.

Swali langu: Ungekuwa wewe ni mume/mke na huna HIV unapata mchumba mwenye HIV, utakuwa tayari kufanya maamuzi ya kuoa/kuolewa kama alivyofanya mwanajeshi Hassan? Tafadhali nipe maoni yako!

Point to take: Tusiwanyanyapae wenye HIV na UKIMWI, kama jamii, tuna uwezo wa kuishi nao bila matatizo yoyote endapo tutawapa ushirikiano wa kutosha na kuondoa dhana ya ubaguzi na hofu ndani ya mioyo yetu.


Wenu,
HorsePower

Nikimpenda kama alivyopenda Hassan inawezekana lakini nikimpenda tofauti uamuzi wangu utakuwa tofauti pia!
 
Unaweza kumkwepa huyo kwa sababu ya status yake lakini muumba ana maajabu yake, ukapata huo Ukimwi kwa njia nyingine. Ukitaka kuoa na wewe ukataliwe, au kama una mke na yeye akukimbie...!!!! Tafakari kabla hujajibu hivi.
Kwani walioathirika wamefanya nini cha ajabu ambacho wewe mtakatifu hufanyi?

Mimi siowi hata siku moja, sababu ukifa unakuwa kama wale wapalestin wano jirupua...ni watu wa motoni tu.

Sitaki kujiua na ngojea Malaika mtoa roho siku yangu ikifika atoe roho yangu, sababu kapewa kazi na Mungu.

Ukichukua uamuzi wa kuowa mwanamke amabaye unajua ana HIV, ni kama vile una commit suicide...kitu ambacho Mungu hakipendi na anaye fanya hivyo akifa kwa aids, haendi peponi hata siku moja.
 
wanawake wanaweza. lakini kwa wanaume, nampa big up Hassan. nisingetegemea mwanamme awe na moyo wa ujasiri kiasi hiki, siiti wa chuma kama wengi mlivyosema. Ukimwi mtu yeyote anaweza kuupata kwa njia yoyote ile. ili mradi unahudhuria hospitali zetu hizi ambazo madaktari hawako makini. Ikiwa mgonjwa wa mguu anapasuliwa kichwa kwani wewe kuwekewa damu yenye virusi ni kitu kikubwa au kutolewa jino na vyombo ambavyo haviko sterilized.. ni rahisi sana hapa kwetu. tuwe makini tunapoongea jamani. hakuna aliyeomba hiyo hali, wala hakuna anayejipeleka kuambukizwa.
 
Back
Top Bottom