Hakuna uchawi wa chuma ulete, ni visingizio vya watu wazembe

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
Anaandika, Robert Heriel

Ni Watu wajinga pekee watakaoamini mambo ya Pesa kupotea kimazingara, ati kupotea kichawi! Chuma Ulete!

Yaani ati unaweka Pesa kwenye kibubu labda laki tatu za Kitanzania alafu Baada ya muda ukija kuangalia unakuta elfu hamsini. Huo ni Uongo Mkubwa utakaoaminiwa na watu wajingawajinga. Ni kama Ile Michezo ya mazingaombwe ndio kiini macho.

Mwaka 2018 nilifanikiwa kuanzisha Duka la vipodozi nililochanganya na Nguo zilizokuwa kwenye midoli pamoja na uwakala wa M-PESA na Airtelmoney pamoja na Tigo-pesa. Kwa nje nilikuwa nimeweka Mitungi ya Gesi mikubwa na midogo. Haikuwa biashara kubwa Sana. Ilikuwa ni mtaji wa milioni tano kasoro.
Hii ilimaanisha kuwa nilikuwa ninabiashara nne ndani ya Fremu moja.

Biashara ya nje ilikuwa ni Bodaboda ambayo nilimkabidhi mtu awe ananipa hesabu kila Siku anirushie elfu 8.

Haya tunakuja kwenye hesabu za mapato ya faida,

1. Upande wa miamala;
M-PESA. Faida ilirange 4500- 6000 Kwa Siku.
Airtelmoney 3000 - 4500 Kwa Siku.
Tigo-pesa. 3500 - 5000 Kwa Siku.
Hivyo faida ya Jumla ilikuwa 15,000/= Kwa upande wa miamala.

2. Vipodozi na Nguo
Hii biashara sio ya Wateja wa kila Siku. Hii inategemea Wateja wakudumu hivyo hesabu yake nilikuwa naipigia Kwa mwezi ambayo faida yake ilikuwa sio zaidi ya laki moja (100,000/=).

3. Mitungi ya Gesi
Hii biashara inafaida kama utakuwa unajua Kula na bodaboda pamoja na Migahawa ya wachoma chipsi.
Kwenye mtungi mkubwa ambao faida yake ni 5000 -6000 unaamua kugawana na bodaboda pamoja na wachoma nyama na chipsi, hivyo utawapunguzia bei utapata faida ya elfu nne.

Mtungi mdogo huo Kwa vile faida yake ni ndogo isiyozidi elfu nne hiyo utampatia bodaboda miatano. Akijumlisha na aliyemtuma anapata elfu moja miatano. Kwa siku faida ilikuwa inarange 10,000. - 15,000/= Kwa habari ya biashara ya mitungi.

4. Biashara ya bodaboda
Nishaeleza Kwa Siku ni elfu nane ( 8,000/=).

Jumla ya mwisho Kwa biashara zote ilikuwa inarange Tsh 30,000/= mpaka Tsh 50,000/= kama faida kwa Siku. Siku ya Jumamosi haikuwa siku ya kazi hivyo sikuwa naingiza chochote. Hivyo kwa mwezi faida ilikuwa inarange laki tisa mpaka milioni moja na laki mbili.

MATUMIZI
1. Chakula
i) breakfast Tsh 1,000/=
ii) Lunch. 3,000/=
iii) Dinner. 2,500/=
Jumla Kwa Siku 6,000/= mpaka 7,000/=

2. Usafiri
Bodaboda 2,000/= kwenda kurudi. Ingawaje nilikuwa ninabodaboda yangu Ila sikutaka kuitumia Bure.

3. Vocha
Tsh 1000/= kipindi hicho unapàta GB 1 na Midakika kibao.
Jumla ya matumizi ya muhimu Kwa Siku Tsh 10,000/=.
Kwa mwezi Tsh 300,000/=.

Bado Sabuni, Dawa ya meno, mafuta nk, ingawaje nilikuwa nafua kwa wiki mara moja, na mche wa 2500 nilikuwa nautumia mwezi mzima. Dawa ya meno ya elfu tano nilikuwa natumia mwezi mzima, mafuta ya kupaka ya Vaseline for men elfu tano, mwezi mzima.

Pesa za Serikali za mitaa
Takataka Tsh 3,000/=.
Ulinzi Tsh 3,000/=.
Hivyo matumizi ya Jumla yanarange Tsh 300K - 400k.

Hapo hakuna Mademu, Kwa kweli katika wanaume bahili Kwa upande wa kuhonga Wanawake ninaweza kuwa kwenye Listi.

Faida ya kutokuhonga;
1. Hautudumu na Wanawake muda mrefu hivyo utakuwa na muda wa kufanya mambo yako ya uwekezaji.

2. Hautakubaliwa na Wanawake kirahisi. Hii itakuepusha na magonjwa ya zinaa.

3. Hautakuwa na kusumbuliwa sumbuliwa kisa mapenzi na utaepuka maumivu ya kijingajinga ya mapenzi.

4. Hautakuwa mtu wa kujilaumu na kujiona mjinga Kwani haiwezekani ufanye kazi kwa jasho na kupoteza muda wako mwingi kazini alafu mwanamke aje achukue Pesa yako kirahisi kisa tuu akupe mapenzi,
Hiyo Kwa kijana mdogo kama mimi niliona kama kujidharau na kutojithamini.

Kadiri Pesa inavyoongezeka ni lazima akili na ubunifu viongezeke, kuza biashara na fungua uwekezaji mwingine.

Fungamana na wafanyabiashara wengine kuweka mitandao yako vizuri. Ni muhimu kuwa na connection nzuri ya Wafanyabiashara WA biashara yako, wasafirishaji wa mizigo na parcel n.k.

Epuka kuwa na mazoea na watu wa serikali (TRA, Fire kama unauza mitungi ya Gesi, Watu wa TFDA n.k) Watakufanya kama kituo cha kukuchuma Pesa. Jitahidi kuonyesha hali yako ni ngumu ya biashara hata kama unapata faida inayokuridhisha.

Kwani Taikon mbona umetoka nje ya Mada? Alafu hujaeleza mtaji ulipata Wapi? Yaani umeanzia juu kwa juu!

Ni kweli nimeanzia juu Kwa juu lakini pia nimetoka nje ya Mada Makusudi, Ila nitarejea;

Biashara ni maamuzi tuu, biashara ni kuipenda na kuiheshimu. Ukishapenda kufanya biashara kinachofuata ni uamuzi wa dhati, kujitoa Kwa dhati yote. Huo ndio mtaji namba moja wa biashara. "Ooh! Taikon usituletee mambo ya Motivation Speaker hapa."

Nimemaliza chuo, na nataka kufanya biashara. Biashara gani, wapi, Kwa mtaji gani, itawezekanaje? Maswali yasiwe mengi kuliko majibu. Kila swali hujibiwa Kwa muda wake.

Nilianza biashara kidogokidogo Kwa kununua mitungi used Kwa Watu tangu nikiwa Chuo. Kila nilipoona mtandaoni wauza mitungi used nilinunua nilipokuwa na Pesa.

Nilibahatika kuona mtandaoni Shelfu za aluminium na Kioo zikiuzwa mtandaoni Kwa bei ya kutupa kama milion moja hivi, Nikanunua. Hiyo milioni moja ilikuwa Akiba ya Pesa za Boom niliyokuwa naipata chuoni.

"Taikon acha kutupiga kamba, hata sisi tumesoma chuo. Ile pesa ni ndogo na haitoshi," ni kweli haitoshi kwa mtu mwenye matumizi ya ujana, ila kwangu ilitosha, kutokana na sababu mbili kuu;

1. Mimi ni bahili wa kiwango cha juu

Hivyo suruali tatu, tisheti tano, kiatu kimoja, na Sendo moja vilitosha kuvaa Mwaka mzima. Kulakula pasipo hesabu hilo kwangu huwezi kuliona. Simu niliyoinunua Mwaka wa kwanza 2014 niliitumia mpaka 2019 bila kubadilisha.

Kipindi nasoma sikuwa MTU wa kudhurura hovyohovyo kwani nilijua ili nifanye movement yoyote lazima Pesa itumike. Route yangu ilikuwa Sinza(mahali ninapoishi) kwenda Chuo(Udsm) mara mojamoja nilienda Mabibo Hostel tena hiyo ni mara moja kila Baada ya semister moja.

2. Nilikuwa napika nyumbani, hivyo chakula ilikuwa gharama nafuu

Niliitumia fursa ya kuishi nje ya hostel kujinufaisha kiuchumi na kiuzoefu Kwa Maisha ya mtaani. Hapo nilianza kujidhatiti Kwa kununua vitu vidogodogo kama kitanda, Godoro, mapazia, Sofa la Watu Wawili, kiti cha kiofisi cha kuzunguka cha kusomea, Feni n.k.

Hapo pia utaniuliza nilikuwa napata Pesa wapi? Kwa sababu kitanda na Godoro tuu bei yake haipungu laki tatu, sofa jipya 250,000/=. Jibu; lipo kwenye hoja ya Chini👇👇

3. Nilifanya kazi ya kushona nguo

Niliunga urafiki na fundi mmoja pale mtaani, Kwa bahati tunatoka mkoa mmoja hvyo alinichukulia kama Ndugu na mdogoake. Nikamuomba anifundishe kushona na ikiwezekana awe ananitumatuma vikazi vya hapa na pale. Mpango ulifanikiwa.

Nikaanza kufundishwa kushona na ndani ya miezi sita nikajua kushona. Hivyo sikuwa na sababu ya kushinda Vimbwetani Huko chuoni kwani nilikuwa ninakazi huku mtaani. Kupitia kushona nilipata Pesa ndogondogo za Kula, Hii ilifanya Pesa ya boom niliyokuwa napewa na serikali isitumike.

Fikiria kiraka kimoja cha nguo unashona Kwa elfu mbili na Kwa wale Wateja wenye kulialia unafanya Bukubuku. Kwa Siku kuondoka na elfu tano au elfu tatu ilikuwa kawaida. Hiyo Pesa kwangu ni nyingi Kwa sababu ninajipikia. Ni pesa inayoingia isiyo na matumizi zaidi ya nauli ya chuoni iliyokuwa 800 na vocha ya Buku tuu.

Hivyo boom kila likitoka ni Tsh 510,000/=, laki mbili lazima ninunue kitu kimoja kikubwa ndani ya chumba, kisha laki na nusu akiba, alafu inayobaki ndio inakuwa ya matumizi. Achilia mbali zile laki Saba za mwanzo ukiingia na zile za Field.

Mwaka wa pili kwenda watatu, ndio nikaanza Mpango WA kufanya biashara, Nikanunua mitungi ya Gesi pamoja na shelves za aluminium za vioo kwaajili ya kuwekea bidhaa za vipodozi.

Biashara kwa sisi vijana maskini huanza kidogo kidogo, ni ngumu kuanza biashara kwa mtaji mkubwa wakati umetoka familia Maskini. Kwanza hauna mtaji lakini la pili ambalo ni kubwa zaidi ni kuwa hauna uzoefu.

Mpaka ninamaliza chuo nilikuwa nimeshaandaa mazingira ya Biashara kasoro bidhaa;
a) Nilinunua Mitungi Mitano mikubwa ya Gesi na midogo ya Gesi ikiwa mitupu, hivyo ikibaki tuu kuijaza.
b) Nikanunua Shelvu za aluminium za vioo kwaajili ya kuwekea vipodozi.
c) Nikanunua Midoli ya nguo Ile ya kusimamia. Nilinunua minne, miwili ya mwanzo nilinunua Kwa Tsh. 80,000/= Kwa kila Mdoli. Raundi ya pili, Nikanunua Midoli miwili tena Kwa Tsh 100,000/= Kwa kila mmoja. Hapa nilibakiza kununua tuu nguo.

Kufikia hapo nilikuwa nimefikia Nusu ya malengo na Kwa mbali niliona uwezekano.

Nikamaliza chuo bado nikiwa nashona, sasa hapa hesabu zilitakiwa ziwe za haraka Kwa sababu chanzo kimoja cha mapato yangu ambayo ni Boom kimeisha, hivyo kiakiba changu kama sitafanya uwekezaji wa haraka kinaweza kuisha alafu nikajikuta nauza vitu vyote nilivyohangaika kuvipata Kwa kujibana mno.

Kwa bahati ikatokea kazi ya Customer Care Executive Pale Vodacom kupitia Kampuni ya ISON. Nikaomba, nikaitwa Usahili nikapita. Walikuwa wakilila laki Nne na ushee hivi Kwa masaa 8, tuu Kwa siku.
Nikasema sio Mbaya.

Kutoka Sinza mpaka Kituo cha kazi Mlimani city sio mbali, unatembea tuu Kwa mguu. Hiyo ilinisaidia. Nikapiga Ile kazi huku nikiwa naweka mazingira ya kufungua Biashara ya vipodozi. Nikapata connection ya vipodozi pale Kariakoo. Nikachukua mzigo kama WA milioni moja hivi. Kisha nikaanza kutafuta Fremu.
Hapa ndio mziki ulipo.

Sikutaka kuwa vichochoroni na wala sikutaka kuwa pembeni MWA Barabara kuu Kutokana na ughali wa Fremu. Nikapata Fremu maeneo ya Goba, tatizo likawa connectivity ya Sinza na Goba. Yaani ilinipasa nitumie gari mbili, lakini nikasema nisijipe visingizio, nijaribu.

Nikafungua hiyo biashara, Kodi ilikuwa elfu 80 Kwa mwezi na unalipa Kwa miezi minne. Hivyo 320,000/= kama Kodi, kupeleka fundi akuwekee Zile Shelvu na kudizaini na kusafirisha mizigo ikawa imemalizika 400,000/=.

Baada ya kukamilisha kila kitu, sikufungua kwa wiki moja hivi nikitegeshea Mshahara ili ninunue lakini ya uwakala ya M-pesa bahati nzuri nilikuwa nafanya kazi Huko hivyo hiyo haikunisumbua.

Sasa changamoto iliyobaki ni namna ya kugawanya muda wa kazi ya kuajiriwa Vs kujiajiri. Kazi ya Customer Care ilikuwa niya shift kuna Wakati mnaingia kuanzia Asubuhi mpaka Mchana, kuna wakati mnaingia mchana mpaka saa nne, na kuna wakati mnaingia Usiku saa nne mpaka Asubuhi.

Nikafanya hiyo kazi Kwa miezi sita huku nikifanya kibiashara changu, hapo Nikanunua Bodaboda. Niliponunua bodaboda nikasema pesa ya bodaboda ndio itafidia Mshahara niliokuwa naupata huku ISON.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa, wazo la kufungua Biashara ya Dagaa likamea mwishoni mwa Mwaka 2018. Kikawaida Taikon ni MTU wa ideas, na kila ideas lazima iwe documented, niiandike, na applicability yake. Nikaona wazo hili linaweza kuwa wazo zuri Kwa Muktadha wa Maisha ya watanzania.

Ukishaliandika wazo lako na kuliwekea applicability yake unaanza kulifuatilia Kwa Makini Kupata taarifa sahihi. Hata hivyo sio rahisi Kupata taarifa sahihi bila kuingia kwenye hiyo biashara moja Kwa moja. Zingatia biashara zote zinahitaji Mfumo na usimamizi.

Changamoto nilizokumbana nazo ni pamoja na;
1. Kutokuwa na uzoefu wa biashara.

2. Sikuwa nimesajili biashara na hivyo sikuwa nalipa Kodi. Hivyo nilikuwa napata usumbufu kutoka kwa waserikali. Mara kufunga ukisikia wanakuja mara wamekukamata mnaanza kujadiliana. Hii Njia ya kuwaepuka ni kusajili biashara na kulipa Kodi ili ufanye Kwa Amani.

3. Wafanyakazi wasio waaminifu hasa bodaboda. Mara kakamatwa kituo cha polisi na kuitoa pikipiki lazima utoe Pesa.

4. Kila biashara inausajili na Leseni yake. Hivyo kumbuka nilikuwa ninabiashara mbili zinazosimamiwa na mamlaka mbili tofauti mathalani, biashara ya Mitungi ya Gesi inasimamiwa na Mamlaka sijui ya zimamoto na unatakiwa upewe Leseni. Na biashara nyingine ya vipodozi ambayo inasimamiwa na TFDA sijui kama sijakosea spelling.

Changamoto za mahesabu ya Mapato na matumizi katika biashara ndio huzaa kitu kinaitwa chuma ulete.

1. Wanasema Mali bila Daftari huisha bila habari.
Taikon kila tumizi nitakalotumia hata kama nimenunua BIG G lazima lionekane kwenye kitabu cha kumbukumbu ya matumizi ya siku, mwezi na Mwaka.

2. Ni vizuri Kila biashara iwe na Pesa yake na kama biashara moja itamkopa mwenzake ni vizuri kuandika.
Mfano, Biashara ya Uwakala wa Pesa, endapo Pesa Cash imeisha alafu ukataka kuchukua Pesa za biashara ya vipodozi au mtungi wa Gesi ni muhimu kuandika ili kutojichanganya baadaye.

3. Kila biashara lazima iwe na uwezo wa kujiendesha, mfano usichukue Pesa ya biashara ya vipodozi kufanya matengenezo ya bodaboda, hiyo iweke kama mkopo. Hizo ni biashara mbili tofauti. Bodaboda ijiendeshe yenyewe, halikadhalika na hizo biashara nyingine.

4. Matumizi ya msingi na muhimu ya Familia(Yako,) itenge Pesa yake kabisa na ijulikane Kwa Siku unatumia kiasi gani.

5. Usitembee na Pesa nyingi ambazo hauna matumizi nazo.
Kwa mfano hauna Sababu ya kutembea na laki tano mfukoni ikiwa unafanya matembezi ya kawaida.
Kama ni pesa ya dharura iwe kwenye hesabu na ndio utembee nayo.

6. Usinunue vitu bila mipango. Yaani umeona kitu Fulani kinapitishwa na wamachinga wewe unanunua hata kama haukupanga.

7. Usinunue vitu hovyohovyo kama hauna matumizi navyo Kwa wakati husika. Mbali na kumaliza Pesa kijinga lakini pia vinajaza nyumba yako pasipo sababu ya msingi.

8. Usihonge wala kutoa Pesa kijinga ikiwa kweli wewe ni mfanyabiashara ambaye bado biashara yako ni ndogo na haijakomaa.

9. Sehemu unayowekea Pesa ijulikane na wewe tuu. Na kuwe na kiwango cha kawaida kuitunza Pesa ndani Kwa usalama.

Wengi wanaosema hawaoni Pesa zao na wanahofia chuma ulete wanatatizo la kimatumizi, hawana kumbukumbu ya matumizi katika kitabu, kingine ni wanaibiwa na mtu anayejua wanapoweka Pesa zao. Alafu wanasingizia chuma ulete.

Taikon acha nipumzike sasa.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
Mkuu upo sahihi kwa asilimia 75 hivi, vingine sio juhudi tu na Mungu ausike husda ni nyingi sana.. unaweza fanya kila kitu kwa usahihi lakini watu wakikunja nafsi tu kwisha habari yako,. Ahsante umetuongezea kitu sisi life seekers..

Ni kweli Kabisa.
Kuishi na watu vizuri inaweza kusaidia, Ila huwezi kuepuka Watu wenye hasidi, husda na wafitini
 
Anaandika, Robert Heriel

Ni Watu wajinga pekee watakaoamini mambo ya Pesa kupotea kimazingara, ati kupotea kichawi! Chuma Ulete!

Yaani ati unaweka Pesa kwenye kibubu labda laki tatu za Kitanzania alafu Baada ya muda ukija kuangalia unakuta elfu hamsini. Huo ni Uongo Mkubwa utakaoaminiwa na watu wajingawajinga. Ni kama Ile Michezo ya mazingaombwe ndio kiini macho.

Mwaka 2018 nilifanikiwa kuanzisha Duka la vipodozi nililochanganya na Nguo zilizokuwa kwenye midoli pamoja na uwakala wa M-PESA na Airtelmoney pamoja na Tigo-pesa. Kwa nje nilikuwa nimeweka Mitungi ya Gesi mikubwa na midogo. Haikuwa biashara kubwa Sana. Ilikuwa ni mtaji wa milioni tano kasoro.
Hii ilimaanisha kuwa nilikuwa ninabiashara nne ndani ya Fremu moja.

Biashara ya nje ilikuwa ni Bodaboda ambayo nilimkabidhi mtu awe ananipa hesabu kila Siku anirushie elfu 8.

Haya tunakuja kwenye hesabu za mapato ya faida,
1. Upande wa miamala;
M-PESA. Faida ilirange 4500- 6000 Kwa Siku.
Airtelmoney 3000 - 4500 Kwa Siku.
Tigo-pesa. 3500 - 5000 Kwa Siku.
Hivyo faida ya Jumla ilikuwa 15,000/= Kwa upande wa miamala.

2. Vipodozi na Nguo
Hii biashara sio ya Wateja wa kila Siku. Hii inategemea Wateja wakudumu hivyo hesabu yake nilikuwa naipigia Kwa mwezi ambayo faida yake ilikuwa sio zaidi ya laki moja (100,000/=).

3. Mitungi ya Gesi
Hii biashara inafaida kama utakuwa unajua Kula na bodaboda pamoja na Migahawa ya wachoma chipsi.
Kwenye mtungi mkubwa ambao faida yake ni 5000 -6000 unaamua kugawana na bodaboda pamoja na wachoma nyama na chipsi, hivyo utawapunguzia bei utapata faida ya elfu nne.

Mtungi mdogo huo Kwa vile faida yake ni ndogo isiyozidi elfu nne hiyo utampatia bodaboda miatano. Akijumlisha na aliyemtuma anapata elfu moja miatano. Kwa siku faida ilikuwa inarange 10,000. - 15,000/= Kwa habari ya biashara ya mitungi.

4. Biashara ya bodaboda
Nishaeleza Kwa Siku ni elfu nane ( 8,000/=).

Jumla ya mwisho Kwa biashara zote ilikuwa inarange Tsh 30,000/= mpaka Tsh 50,000/= kama faida kwa Siku. Siku ya Jumamosi haikuwa siku ya kazi hivyo sikuwa naingiza chochote. Hivyo kwa mwezi faida ilikuwa inarange laki tisa mpaka milioni moja na laki mbili.

MATUMIZI

1. Chakula
i) breakfast Tsh 1,000/=
ii) Lunch. 3,000/=
iii) Dinner. 2,500/=
Jumla Kwa Siku 6,000/= mpaka 7,000/=

2. Usafiri
Bodaboda 2,000/= kwenda kurudi. Ingawaje nilikuwa ninabodaboda yangu Ila sikutaka kuitumia Bure.

3. Vocha.
Tsh 1000/= kipindi hicho unapàta GB 1 na Midakika kibao.
Jumla ya matumizi ya muhimu Kwa Siku Tsh 10,000/=.
Kwa mwezi Tsh 300,000/=.

Bado Sabuni, Dawa ya meno, mafuta nk, ingawaje nilikuwa nafua kwa wiki mara moja, na mche wa 2500 nilikuwa nautumia mwezi mzima. Dawa ya meno ya elfu tano nilikuwa natumia mwezi mzima, mafuta ya kupaka ya Vaseline for men elfu tano, mwezi mzima.

Pesa za Serikali za mitaa
Takataka Tsh 3,000/=.
Ulinzi Tsh 3,000/=.
Hivyo matumizi ya Jumla yanarange Tsh 300K - 400k.

Hapo hakuna Mademu, Kwa kweli katika wanaume bahili Kwa upande wa kuhonga Wanawake ninaweza kuwa kwenye Listi.

Faida ya kutokuhonga;
1. Hautudumu na Wanawake muda mrefu hivyo utakuwa na muda wa kufanya mambo yako ya uwekezaji.

2. Hautakubaliwa na Wanawake kirahisi. Hii itakuepusha na magonjwa ya zinaa.

3. Hautakuwa na kusumbuliwa sumbuliwa kisa mapenzi na utaepuka maumivu ya kijingajinga ya mapenzi.

4. Hautakuwa mtu wa kujilaumu na kujiona mjinga Kwani haiwezekani ufanye kazi kwa jasho na kupoteza muda wako mwingi kazini alafu mwanamke aje achukue Pesa yako kirahisi kisa tuu akupe mapenzi,
Hiyo Kwa kijana mdogo kama mimi niliona kama kujidharau na kutojithamini.

Kadiri Pesa inavyoongezeka ni lazima akili na ubunifu viongezeke, kuza biashara na fungua uwekezaji mwingine.

Fungamana na wafanyabiashara wengine kuweka mitandao yako vizuri. Ni muhimu kuwa na connection nzuri ya Wafanyabiashara WA biashara yako, wasafirishaji wa mizigo na parcel n.k.

Epuka kuwa na mazoea na watu wa serikali (TRA, Fire kama unauza mitungi ya Gesi, Watu wa TFDA n.k) Watakufanya kama kituo cha kukuchuma Pesa. Jitahidi kuonyesha hali yako ni ngumu ya biashara hata kama unapata faida inayokuridhisha.

Kwani Taikon mbona umetoka nje ya Mada? Alafu hujaeleza mtaji ulipata Wapi? Yaani umeanzia juu kwa juu!

Ni kweli nimeanzia juu Kwa juu lakini pia nimetoka nje ya Mada Makusudi, Ila nitarejea;

Biashara ni maamuzi tuu, biashara ni kuipenda na kuiheshimu. Ukishapenda kufanya biashara kinachofuata ni uamuzi wa dhati, kujitoa Kwa dhati yote. Huo ndio mtaji namba moja wa biashara. "Ooh! Taikon usituletee mambo ya Motivation Speaker hapa."

Nimemaliza chuo, na nataka kufanya biashara. Biashara gani, wapi, Kwa mtaji gani, itawezekanaje? Maswali yasiwe mengi kuliko majibu. Kila swali hujibiwa Kwa muda wake.

Nilianza biashara kidogokidogo Kwa kununua mitungi used Kwa Watu tangu nikiwa Chuo. Kila nilipoona mtandaoni wauza mitungi used nilinunua nilipokuwa na Pesa.

Nilibahatika kuona mtandaoni Shelfu za aluminium na Kioo zikiuzwa mtandaoni Kwa bei ya kutupa kama milion moja hivi, Nikanunua. Hiyo milioni moja ilikuwa Akiba ya Pesa za Boom niliyokuwa naipata chuoni.

"Taikon acha kutupiga kamba, hata sisi tumesoma chuo. Ile pesa ni ndogo na haitoshi," ni kweli haitoshi kwa mtu mwenye matumizi ya ujana, ila kwangu ilitosha, kutokana na sababu mbili kuu;

1. Mimi ni bahili wa kiwango cha juu.
Hivyo suruali tatu, tisheti tano, kiatu kimoja, na Sendo moja vilitosha kuvaa Mwaka mzima. Kulakula pasipo hesabu hilo kwangu huwezi kuliona. Simu niliyoinunua Mwaka wa kwanza 2014 niliitumia mpaka 2019 bila kubadilisha.

Kipindi nasoma sikuwa MTU wa kudhurura hovyohovyo kwani nilijua ili nifanye movement yoyote lazima Pesa itumike. Route yangu ilikuwa Sinza(mahali ninapoishi) kwenda Chuo(Udsm) mara mojamoja nilienda Mabibo Hostel tena hiyo ni mara moja kila Baada ya semister moja.

2. Nilikuwa napika nyumbani, hivyo chakula ilikuwa gharama nafuu.
Niliitumia fursa ya kuishi nje ya hostel kujinufaisha kiuchumi na kiuzoefu Kwa Maisha ya mtaani. Hapo nilianza kujidhatiti Kwa kununua vitu vidogodogo kama kitanda, Godoro, mapazia, Sofa la Watu Wawili, kiti cha kiofisi cha kuzunguka cha kusomea, Feni n.k.

Hapo pia utaniuliza nilikuwa napata Pesa wapi? Kwa sababu kitanda na Godoro tuu bei yake haipungu laki tatu, sofa jipya 250,000/=. Jibu; lipo kwenye hoja ya Chini👇👇

3. Nilifanya kazi ya kushona nguo.

Big up..
Ni bandiko mujarab kabisa, ukiondoa kichwa cha Uzi
 
Ila bloangu kwenye miamala ya kipesa hasa hyo sijui ya mpesa,tigopesa and the likes sometimes chuma ulete ipo,mi nilishapigwa 2.4M,nilipasuka mwenyewe wala sio utani.

Ilikuwa hivi,Mteja kaja kuweka elf60,ilikuwa jioni jioni hivi mishale ya saa 11.Kwenye droo la hela kulikuwa na 2,400,000/=,nikaenda kuichanganya ile pesa ya mwisho ya yule mteja kwenye hyo droo,kukawa na 2460,000/=.

Hakukuwa mteja mwingine yeyote aliyekuja kufanya muamala wowote hadi nafunga duka saa 12 jioni.

Mziki unaanzia hapa sasa,kwa kawaida nikifungaga biashara lazima nihesabu tena fedha ili niingize hesabu vitabuni,kuja kuhesabu sasa,DROO halina hata senti tano na hakuna aliyeingia dukani labda kuvunja mlango wala nini,Maji niliita MMAAAAAAA,nuliyumba mnooooooooo.

Haya na wewe niambie ulikuwa unafanyaje fanyaje kuwaepuka WALOZI kama hao?
 
Maana halisi ya genius na mchungu wa mafanikio.. hili somo ni zaidi ya degree.
 
Back
Top Bottom