Unaangalia vigezo gani kununua Laptop? Chagua Laptop inayoendana na matumizi yako

Alfatonics

Member
Mar 2, 2022
18
29
Kuna mambo kadhaa ya kuzingatia kabla ya kuchagua laptop ya kununua
Processor, Storage,RAM, Display, Graphics n.k

1.Processor
Hapa ndo kwenye performance nzima ya kompyuta yako Ni namna kompyuta inavyochakata taarifa au kila kitu unachofanya kwenye kompyuta yako kinapitia hapa kufanyiwa kazi
Processor ikiwa na uwezo mkubwa kompyuta yako itakua fasta zaidi kwenye utendaji kazi wake.
Hupimwa kwa clockspeed (GHz)

2. Storage
Hapa ni uwezo wa kompyuta kuhifadhi data zako.

Kwa Sasa ziko storage za aina mbili (SSD &HDD).

Hupimwa kwa bytes(MB,GB,TB?

3. RAM
Hii ni temporary storage inachukua taarifa kupeleka kwenye processor
Ukubwa wa RAM hufanya kubeba taarifa nyingi kwa sekunde.
Hupimwa kwa bytes

4. Display
Hapa ni size ya kioo chako unapendelea kikubwa, kidogo au size ya Kati Ni wewe tu
Hapa pia utachagua Kama kiwe touch screen au kawaida
Hupimwa kwa inch(diagonal)

5. Graphic Card(GPU)
Hapa tunaongeza uwezo wa kompyuta katika kuchakata taarifa zake, tunaiongezea uwezo processor kutokana na matumizi ambayo unakuwa nayo.

Kuna baadhi ya softwares haziwezi endeshwa na kompyuta zisizo kuwa na GPU ni vizuri kabla hujanunua kompyuta ujue Ni matumizi gani utakuwa nayo
Wanaotengeza hizi card wapo Nvidia,AMD n.k

Tuje hapa Sasa
a) Ram 2gb-4gb , storage 32gb-500gb, processor 1.0ghz-2.0ghz. Kusomea, kuangalia muvi,kufanya kazi ndogo ndogo kama typing,Excel, power point n.k

b) Ram 4gb-8gb , storage 320gb-500gb, processor 2.0ghz-2.5ghz. Software development (coding), graphics design(Photoshop, illustrator n.k), na hayo yote hapo juu kwenye (a)

c) Ram 8gb-16gb , storage 500gb-1TB, processor 2.0+,graphic card 2gb+. Hapa utaweza kufanya design kama za AutoCAD, solidworks, Animations n.k

NOTE
Processor Ni somo Pana sana Kuna ishu za generation,basic and logical processors, n.k Yani unaweza ona clockspeed(GHz) Ni 2.2ghz lakini no. of processors ziko 4 lakini nyingne ikawa na 1.8ghz af no.of processors zikawa 8.

Hapa usikariri kuwa processor lazima iwe kubwa, generations matters alot

Zingatia zaidi processor kwa mahitaji ya kompyuta yenye kazi nzito maana RAM, storage Ni rahisi kuongeza Ila processor hutaweza kuongeza
 
Kuna la kujifunza huwa naangalia Kampuni mfano Acer, Apple na Lenovo. Nikiona za Dell, Hp etc naona hazina ubora
 
Naona ni kampuni zinazotengenez laptop imara zaid
Anhaa naona pia Ni mapenzi zaidi ndo yanafanya mtu kuchagua kampuni dhidi ya nyingine,
Wapo wengine wanapendelea zaidi dell kuwa zinadumu zaidi kuliko hp

Wengine Apple japo zinapendwa Ila wengi Bei zinawashinda
 
Hivi mkuu brand gan ya laptop ni imara zaidi

Na je kuna laptop hazina gpu na kama zipo nitazijuaje
 
Uimara wa laptop hatutaangalia zaidi brand inategemea na model ipi umechukua mfano labda ukachukua hp ya 300k na ukachukua dell ya 500k then ukalinganisha ubora haitakua sawa
Ubora utalinganishwa na model za hizo laptop za kampuni moja na zaidi Ni kutokana na matumizi yako maana Hawa wafanyabiashara wanatengeneza kila mtu apate so ukitaka Bora zaidi Basi utalipa pesa zaidi
Kwa maana ya kudumu labda kuhimili mikiki mikiki sana labda mtu sio mtunzaji anahitaji kidogo yenye uimara kwa nje ningesema labda dell computer zao nyingi Zina roho flani ya paka kuliko computer nyingi za hp, MacBook nao wanajitahidi japo kwao unalipia zaidi
 
Kigezo changu kikuu kwenye kununua laptop ni 'battery life'. Kwa sababu mimi ni freelancer na ninafanya kazi zangu nyumbani hivyo Tanesco wakizima umeme ninahitaji kitu reliable na ndiyo sababu ninakubali sana MacBook zenye M1 au M2, yani zinakaa na chaji hadi raha.

Hayo ma Ram, sijui GPU na ma core - i10,000 kwa sisi hazina muhimu.
 
Hivi mkuu brand gan ya laptop ni imara zaidi

Na je kuna laptop hazina gpu na kama zipo nitazijuaje
Laptop zisizo na GPU zipo, na kawaida sana zenye GPU ndo zinaandikwa utaona sticker imebandikwa ya hiyo GPU yako hapo mbele ya laptop
Au unaweza ingia ndani sehemu ya search ukaandika system information ukapata taarifa zote za computer yako, au ukaandika task manager af chagua palipoandikwa performance utaona taarifa za GPU Kama ipo
 
Kigezo changu kikuu kwenye kununua laptop ni 'battery life'. Kwa sababu mimi ni freelancer na ninafanya kazi zangu nyumbani hivyo Tanesco wakizima umeme ninahitaji kitu reliable na ndiyo sababu ninakubali sana MacBook zenye M1 au M2, yani zinakaa na chaji hadi raha.

Hayo ma Ram, sijui GPU na ma core - i10,000 kwa sisi hazina muhimu.
Sure kwa freelancer chaji Ni muhimu sana Kama una matumizi ya kawaida tu unaweza chaji Mara moja tu kwa siku
 
Kigezo changu kikuu kwenye kununua laptop ni 'battery life'. Kwa sababu mimi ni freelancer na ninafanya kazi zangu nyumbani hivyo Tanesco wakizima umeme ninahitaji kitu reliable na ndiyo sababu ninakubali sana MacBook zenye M1 au M2, yani zinakaa na chaji hadi raha.

Hayo ma Ram, sijui GPU na ma core - i10,000 kwa sisi hazina muhimu.
Amd siku hizi laptop zake hazina utofauti sana na Apple, pia intel i5 1230U ni nzuri,

Amd 7xxx series ndo zimetoka nazo pengine battery life ikawa zaidi ya M1 na M2,
 
Laptop zisizo na GPU zipo, na kawaida sana zenye GPU ndo zinaandikwa utaona sticker imebandikwa ya hiyo GPU yako hapo mbele ya laptop
Au unaweza ingia ndani sehemu ya search ukaandika system information ukapata taarifa zote za computer yako, au ukaandika task manager af chagua palipoandikwa performance utaona taarifa za GPU Kama ipo

Mkuu labda wewe umeangalia tu High end GPU uhalisia kila laptop ina GPU.
Kwenye computer yoyote (desktop/laptop) huwezi pata picha kwenye screen bila GPU.

GPU ziko za aina mbili:
1. Integrated GPU
Hii inakuwa ndani ya CPU, kwenye kila laptop hii ipo, haina memory yake hivyo huchukua kiasi kidogo cha RAM na kufanya ndio memory yake ndio maana dedicated memory yake huwa ni ndogo sana. Ukiangalia vizuri specs kwenye computer yako yenye 8GB RAM utaona kwenye RAM kumeandikwa Installed memory 8.00 GB (7.88 GB usable) hichi kiasi kilichopungua 0.12 GB kinaitwa Hardware reserved ambacho hutumika na baadhi ya hardware za computer yako hasa integrated GPU.

Ukitaka kubadilisha kwenda iliyobora kwenye desktop utabadilisha tu CPU ni rahisi tu ila lazima socket ziendane,
Ila kwa laptop Hii haiwezekani kuibadilisha labda uwe umevuka level za wahindi unamkaribia mchina ndio utaweza, maana ni lazima ubadilishe kabisa CPU uweke nyingine kibaya ni kwamba watengenezaji wake hawauzi kwa individuals wanauziana manufacturers to manufacturers so ni lazima utoe kwenye laptop moja uweke kwenye nyingine.

2. Discrete GPU
Hii inakuwa chip na circuit yake ambayo ina memory yake hivyo dedicated memory yake inakuwa kubwa, ina performance kubwa ukilinganisha na integrated.
Ukitaka kubadilisha au upgrade kwa desktop ni simple zingatia power supply unachomeka kwenye Motherboard umemaliza ila kwa laptop process ni ile ile tu kama integrated ilivyo.

IMG_1193.jpg

Mfano hii mashine ina GPU 2
1. Integrated GPU => Intel HD 530
2. Discrete GPU => Nvidia GTX 750Ti

NOTE
kwenye destkop sio CPU zote zina GPU kwa ndani yake mfano core i series zote ambazo zina F mwishoni hazina integrated GPU
 
View attachment 2545647
Mfano hii mashine ina GPU 2
1. Integrated GPU => Intel HD 530
2. Discrete GPU => Nvidia GTX 750Ti

NOTE
kwenye destkop sio CPU zote zina GPU kwa ndani yake mfano core i series zote ambazo zina F mwishoni hazina integrated GPU
Uko sahihi Ila muuliza swali nadhani Kuna GPU aliyomaanisha na ndio maana nikamjibu vile pengine anahitaji mashine ya kufanyia rendering kumuambia tu PC yenye intel graphics kuwa Ina GPU anaweza kosa anachotaka
 
Bila graphic card hatuwezi ona picha kwenye screen
 
Back
Top Bottom