Anfaal
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 1,154
- 113
Mara baada ya uchaguzi mkuu, Chama cha Demokrasia na maendeleo kimeibuka kuwa ndio chama kikuu cha upinzani nchini. Juhudi za viongozi wa CHAMA hicho si za kubezwa. Kiuhalisia viongozi hawa wamewekeza muda na rasimili zao, za wanachama na hata wananchi wa kawaida na kukifanya CHAMA hicho kifike hapo kilipofika leo hii. Lakini pia kwa namna ya pekee, nguvu ya mtandao imekifanya CHAMA hicho kuimarika zaidi.
CHANGAMOTO kuu iliyopo mbele yake ni kukisuma chama hiki kwenda mbele. Ukweli ni kwamba organizeshen zozote zikikuwa mara nyingi ndio matatizo huongezeka. Na mikikimikiki ya ukuaji mara nyingi hupunguzwa na uwepo wa uwazi, uwajibikaji, haki na usawa. Kama haya yatakosekana basi ni rahisi kwa taasisi husika kuyumba. Mfano, sasa hivi CHADEMA imepata wabunge wapya wengi tu na ushawishi wao kabla ya chaguzi ulikuwa haufahamiki lakini huenda uchaguzi utawafanya wengi wawe maarufu kuliko hata wale waliopo CHADEMA. Uchaguzi huu huenda umewaleta watu waadilifu, wachapakazi na wanaosimamia haki kuliko hata wale waliokuwepo. Watu hawa ni muhimu kwa Taifa letu, tusiwabeze, tuwape uzoefu na nafasi ya kukitumia CHAMA.
Tukiachana na hayo, CHADEMA wamechagua viongozi viongozi wa upinzani bungeni. Safu yao ni nzuri na imeweza kuondoa hisia za makundi ambazo wengi huamini yapo. Lakini sasa; ipo haja kuu ya kushirikiana na wapinzani wenzao. Wapo viongozi wengi wa vyama vya upinzani ni wazuri saana na hawa wakitumika ipasavyo lengo kuu la upinzani, huenda likafikiwa; Maendeleo ya Taifa.