Ummy Mwalimu: Ruksa Madaktari kutumia hospitali za Serikali kama private clinic baada ya muda wa kazi

Ummy anafanya kazi kwa kuajiriwa na watanzania, hana mamlaka ya kugeuza hospitali zetu tunazoziendesha kwa kodi zetu ziwe za binafsi baada ya saa za kazi!! Ajenge hospitali zake na kuwapa hao madaktari!!
Anakiri kabisa kuwa huduma za umma siyo nzuri, kwa nini asiziboreshe? kwani kazi yake ni nini?
 
Maamuzi ya Ummy kuhusu hospitali zetu nikiunganisha na maamuzi ya mama kuhusu bandari zetu itapelekea jamii kuwa na mashaka na uwezo wa jinsia hii kwenye kusimamia maslahi ya umma!! Wenye jinsia hii simameni kuwaambia hawa kuwa wanawaharibia!! 2025 tutaiogopa jinsia hii kama mambo menyewe ni kama haya!!
 
Wanajeshi nao ikifika muda wa kuisha hiyo saa 9.30 jeshi linabadilika kuwa jeshi binafsi kama Wagner group!! Watatumia silaha kufanya ulinzi binafsi kwa wenye fedha zao!!
 
Wewe unafurahia kupanga foleni?
Kero ya kupanga foleni huwezi kuitatua kwa staili hiyo!! Ongeza madaktari na hospitali!! Halafu hospitali za private si zipo?? Anayetaka huduma ya private aende huko!! Ummy ametukosea pakubwa sana!! Tunamlipa kwa kodi zetu halafu anatukosea staha kiasi hicho? Mamlaka ya kubinafisisha hospitali zetu kayapata wapi??
 
Vipi kwa sisi tulioko Wilayani ambako hakuna hospital za Private? Kwanini tupange foleni kimasikini?
 
Siasa unaziletea wewe sasa aliyekwambia serikali haifanyi biashara nani? kuna huduma za bure? 24Hrs ni kupokea watu wa dharura tu. Wewe una hiyari ya kuchagua kama unataka huduma za bei nafuu nenda muda wa kazi unataka special treatment nenda kwa muda wako shida iko wapi. Labda nimesema hujui haya Hosp zote zinafanya biashara hutaki kukaa foleni unalipa fast track hata sehemu za kupumzika ziko tofauti ni juu yako unataka nini. Kuna watu wana pesa zao wanataka special treatment ila mtu wa kawaida anapata huduma pia ila anaenda kwa muda wa kazi, huwezi kwenda jioni kumpata Dr labda iwe emergency na utapata Dr wa zamu tu sio bingwa kukupa kama huduma ya kwanza sio zaidi ya hapo.
Chief kama hujui unacholipia hospitali ni kwaajili ya nini bora utulie sawa. Pale hulipi mtu, ile sio biashara. Nani kakwambia pesa unayoitoa ukifika hospitali inalipa mishahara ya watumishi wa afya, hivi nyie kweli mnajua kweli sekta ya afya inavyoendeshwa au kukariri. Fast tracking na special treatment ni nani aliyekwambia ni legally approved isipokuwa kwa makundi maalumu. Au ulivyoona kuna bima zina fast track basi ukajua ni kitu cha kawaida. Nchi ya ajabu kweli. Special treatment ni kwaajili ya nani haswa au hospitali ilijengwa kwa kodi za watu fulani maalumu na sio watanzania wote. Haha! Eti special treatment kwakuwa uliona kuna private ward ukafikiri ni serikari ikasema kuwe na private wards😂😂😂. Siunajua kuwa hospitali pia inapanga jinsi ya kujiendesha na kamwe haitakiwi kuingiliana na mpango kazi wa serikari. Wewe hizo fast tracking sijui special treatment usifikiri ni serikari bali ni board ya hospitali wanafanya mipango ambayo kamwe haitakiwi kuingiliana na serikari. Wewe ulichoona hapo ndicho kinachofanyika hapo au mnakariri. Yaani kadri mnavyoigeuza afya kuwa biashara ndio mzigo unavyoongezeka kwa wananchi siunajua. Yaani wananchi wengine vichwa moja wanawafanya wengine wateseke kinoma. Hujui hata hospitali inavyoongozwa unakariri tu kuwa serikari ndio inayopanga kila kitu. Huku ukikariri kuwa ile pesa unayoitoa kumuona daktari basi ni biashara, kwahiyo faida anakula daktari au watumishi wa afya. Acheni siasa hii ni afya ni uhai wa watu.
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa ruhusa rasmi kwa Madaktari nchini walioajiriwa na serikali kufanya kazi Binafsi kwenye Hospitali za serikali baada ya muda wa kazi kuisha.

Waziri Ummy ametangaza uamuzi huo leo Mkoani Simiyu, wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Simiyu katika ziara yake Mkoani humo.

Waziri Ummy amesema

"Tusiweke urasimu Daktari huyu baada ya saa kumi mruhusu afanye shughuli zake za Private hapa, atawaona mnakubaliana percentage, Ocean Road nilifanya hivyo. Turuhusu hapa ni kuweka utaratibu tu, kuna Mgonjwa anataka aje wakati hakuna fujo.

Hata mimi kuna watu hawapendi kwenda hospitali za Serikali, mchukulie kama RC yupo busy aanze kupanga mafoleni, anataka akienda sehemu nimekuta chumba maalumu kimetengwa, kina makochi, kuna maji, kuna chai, kuna kahawa, kuna soda.

Daktari atamuita Muuguzi, Daktari atanisikiliza, Muuguzi atanichukua sampuli zangu kama nimeondoka ni kufanyiwa radiology tu lakini vitu vingine nitafanyiwa hapohapo."

Wataalamu wa Afya waonywa kupunguza Semina

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu Ummy Mwalimu amewataka Wataalamu wa Afya nchini kupunguza semina ili kuwa na muda zaidi wa kutoa huduma bora za matibabu kwa Wananchi.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Julai 10, 2023 katika ziara yake Mkoani Simiyu wakati akiogea na Viongozi wa Mkoa huo chini ya Mkuu wa Mkoa Dkt. Yahaya Nawanda.

“Wataalamu wa Afya punguzeni semina maana mmekuwa na semina nyingi hadi kupelekea Wagonjwa kukosa huduma kwa wakati na kumekuwa na msomgamano mkubwa katika vituo vya kutolea huduma za afya sababu ya semina”

Waziri Ummy pia amesema katika utolewaji wa huduma za afya nchini hakuna kilichosimama kwakuwa Serikali imejenga majengo ya Hospitali, imetoa dawa na vifaa tiba, hivyo ni jukumu la Wataalamu wa Afya ni kutoa huduma bora patika vituo hivyo.

“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia kila kitu katika Sekta ya Afya ikiwemo majengo, vifaa tiba, kuajiri Wataalamu na sasa ni jukumu letu Wataalau kutoa huduma bora kwa Wananchi kwani ndio dhamira ya Serikali”

Eti huo ndio utetezi wake
 
Wewe usijifanye kuandika gazeti hapa ukadhani ndio akili sana. Nani asiyejuwa kuna bodi sasa wewe akili yako bodi inaamua mambo ikiwa Serikali au tuseme Tamisemi hawalijui hili? Sijakwambia fast track ina cover cost au mishahara na ndio maana siku zote huduma zimekuwa poor kwa sababu ya kutaka vya rahisi wakati serikali haina uwezo. Ndio maana kuna watu wanaenda private hosp kwa huduma bora na malipo ya juu, hii ndio mifumo yetu wala sio Hosp tu hata mashule unataka ya bei rahisi ya serikali yapo unataka private zipo hakuna wa kukuchagulia. Nenda Muhimbili au Benjamin Mkapa kalazwe halafu uje uweke bill hapa.

Sasa wewe shida yako nini? kwani uliambiwa Hosp zinafungwa? waziri kasema baada ya muda wa kazi huduma ziendelee kama private nini unapoteza katika hili? nani wakukuhudumia bure baada ya muda wa kazi. ondoa mawazo ya kijamaa na umaskini hapa, grow up.
 
Unajuwa gharama za kitengo cha moyo Kikwete? si Hosp ya serikali ile, sasa nenda pale kalazwe ujue shughuli yake, unajuwa private room Ben Mkapa ngapi kwa siku? halafu unasema Hosp za maskini nenda kaone gharama zake, kuna vipimo mpaka laki 6 pale kama huna bima utaenda kuchangishiwa kama harusi. Hakuna huduma za bure
 
Apitie hiyo ‘patient safety’ policy framework ya WHO, imekuwepo toka 2004. Above ni latest update.

Halafu waingie google waone watakuta kila nchi iliyoondelea na zisizo zime adapt hiyo policy kama sehemu ya usimamizi wao wa huduma za afya.

Baadhi ya mambo yaliyo humo ndani 👇

0B710C46-1050-4955-9E33-DDE992489534.jpeg

Kila taasisi inatakiwa kuweka mfumo imara wa usimamizi kulinda usalama wa mgonjwa anapopewa huduma; huyo dokta hizo ‘after hours’ services anasimamiwa na nani.

Taasisi ina jukumu la kusimamia clinical services zote zinazotolewa kwenye kituo chake.

Hospitali inajukumu la kuwasiliana na wateja na familia zao kwenye kujadili huduma.

Hospitali inajukumu la kutengeneza na kusimamia mifumo in multi-disciplinary working.

Amongst other things zilizotajwa hapo; mtu mmoja anaweza toa huduma ya afya yeye mwenyewe kweli? Bila ya kuwa under supervision ya taasisi na team work ya kituo.

762D38D6-2487-4C94-A500-E2F92A3F764F.jpeg

Majukumu ya kutekeleza na kusimamia hizo sera yanaanzia juu kabisa wizarani na wanatakiwa kutengeneza sheria au regulations kuhakikisha patient safety inakuwa sehemu ya everyday operational ya afya.

Taasisi zinatakiwa kutengeneza policy za usimamizi wa hayo mambo; siyo mtu ajifanyie kazi bila ya kusimamiwa na taasisi.

Among other things mentioned above.

FDF574C6-1114-48FC-B88B-544C36F84E61.jpeg

Above ni action plan, ukienda kila nchi inayojitambua na ipo serious kwenye kwenye quality ya huduma zao. Utakuta washatengeneza policy ya ‘safe guarding’ on patient safety inayofanania na hiyo ya WHO kama sehemu ya usimamizi wa lazima kwenye utoaji huduma za afya.

Sasa uje kukaguliwa na external auditor wa health services wa nchi zilizoendelea halafu wakute hakuna hizo mechanism za kusimamia usalama wa wateja uone headlines itakazo chukua hiko kituo kwa ku risk usalama wa wateja na waziri kushindwa kusimamia sector.

Huyu wetu ndio kwanza ana bariki madokta kujiendeshea clinic zao ndani ya hospitali.

Afya ni very regulated sector, huko hakunaga ubunifu wa mtu binafsi namna ya kutoa huduma na usimamizi wake. Ni jukumu la taasisi (management yake) muda wote.

Binafsi nilishaamua kumu ignore waziri wa afya afanye anavyotaka, ila anaweza kuja na jambo la ovyo mpaka ukashtuka kama hili ambalo ni hatari sana na linaweza vuruga ufanisi wa taasisi nzima; kwa sababu ya upeo wake mdogo mno kwenye hiyo sector.

Afya ni sector pekee duniani ambayo usimamizi wake ni central hakuna ubunifu ni regulations na policies tu kutoka juu tu utafuata sio vinginevyo.
 
Wewe usijifanye kuandika gazeti hapa ukadhani ndio akili sana. Nani asiyejuwa kuna bodi sasa wewe akili yako bodi inaamua mambo ikiwa Serikali au tuseme Tamisemi hawalijui hili? Sijakwambia fast track ina cover cost au mishahara na ndio maana siku zote huduma zimekuwa poor kwa sababu ya kutaka vya rahisi wakati serikali haina uwezo. Ndio maana kuna watu wanaenda private hosp kwa huduma bora na malipo ya juu, hii ndio mifumo yetu wala sio Hosp tu hata mashule unataka ya bei rahisi ya serikali yapo unataka private zipo hakuna wa kukuchagulia. Nenda Muhimbili au Benjamin Mkapa kalazwe halafu uje uweke bill hapa.

Sasa wewe shida yako nini? kwani uliambiwa Hosp zinafungwa? waziri kasema baada ya muda wa kazi huduma ziendelee kama private nini unapoteza katika hili? nani wakukuhudumia bure baada ya muda wa kazi. ondoa mawazo ya kijamaa na umaskini hapa, grow up.
Mjomba embu acha kuzungumza vitu kutoka kichwani na kudhani that’s how things work.

Hiyo idea mbovu na hatari.
 
Weka hatari yake ni nini? waziri kasema Muhimbili mwaka wa 20 huu wanafanya hayo na Kikwete 15 years alichofanya kuongeza wigo na hosp za rufaa mikoa yote lakini hakuna jipya yanafanyika sana Dar na Dodoma kwa miaka sasa sio leo. Wewe sema hatari zake nini nitakuelewa
 
Kama inafanyaka embu elezea inavyosimamiwa na maeneo gani.

Kwa sababu mtu mmoja na nurse wake awezi toa huduma ya afya.
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa ruhusa rasmi kwa Madaktari nchini walioajiriwa na serikali kufanya kazi Binafsi kwenye Hospitali za serikali baada ya muda wa kazi kuisha.

Waziri Ummy ametangaza uamuzi huo leo Mkoani Simiyu, wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Simiyu katika ziara yake Mkoani humo.

Waziri Ummy amesema

"Tusiweke urasimu Daktari huyu baada ya saa kumi mruhusu afanye shughuli zake za Private hapa, atawaona mnakubaliana percentage, Ocean Road nilifanya hivyo. Turuhusu hapa ni kuweka utaratibu tu, kuna Mgonjwa anataka aje wakati hakuna fujo.

Hata mimi kuna watu hawapendi kwenda hospitali za Serikali, mchukulie kama RC yupo busy aanze kupanga mafoleni, anataka akienda sehemu nimekuta chumba maalumu kimetengwa, kina makochi, kuna maji, kuna chai, kuna kahawa, kuna soda.

Daktari atamuita Muuguzi, Daktari atanisikiliza, Muuguzi atanichukua sampuli zangu kama nimeondoka ni kufanyiwa radiology tu lakini vitu vingine nitafanyiwa hapohapo."

Wataalamu wa Afya waonywa kupunguza Semina

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu Ummy Mwalimu amewataka Wataalamu wa Afya nchini kupunguza semina ili kuwa na muda zaidi wa kutoa huduma bora za matibabu kwa Wananchi.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Julai 10, 2023 katika ziara yake Mkoani Simiyu wakati akiogea na Viongozi wa Mkoa huo chini ya Mkuu wa Mkoa Dkt. Yahaya Nawanda.

“Wataalamu wa Afya punguzeni semina maana mmekuwa na semina nyingi hadi kupelekea Wagonjwa kukosa huduma kwa wakati na kumekuwa na msomgamano mkubwa katika vituo vya kutolea huduma za afya sababu ya semina”

Waziri Ummy pia amesema katika utolewaji wa huduma za afya nchini hakuna kilichosimama kwakuwa Serikali imejenga majengo ya Hospitali, imetoa dawa na vifaa tiba, hivyo ni jukumu la Wataalamu wa Afya ni kutoa huduma bora patika vituo hivyo.

“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia kila kitu katika Sekta ya Afya ikiwemo majengo, vifaa tiba, kuajiri Wataalamu na sasa ni jukumu letu Wataalau kutoa huduma bora kwa Wananchi kwani ndio dhamira ya Serikali”

Pia soma:
Hapa tunahamishwa. Nia ni kututoa kwenye mjadala wa bandari tu..!!
 
Unajuwa gharama za kitengo cha moyo Kikwete? si Hosp ya serikali ile, sasa nenda pale kalazwe ujue shughuli yake, unajuwa private room Ben Mkapa ngapi kwa siku? halafu unasema Hosp za maskini nenda kaone gharama zake, kuna vipimo mpaka laki 6 pale kama huna bima utaenda kuchangishiwa kama harusi. Hakuna huduma za bure
Gharama za kulipwa Muhimbili kila part naijua kwanzia MNH yenyewe, MOI, JKCI na Mloganzila. Pia jkci sio kitengo cha Muhimbili ni taasisi inayojitegemea. Halafu BMH ushasema unataka private room, hayo ni matakwa yako na starehe zako sio utaratibu wa umma. Hospitali za kanda na hospitali ya taifa za serikari ni taasisi zinazojitegemea, siunajua taasisi zinajiendesha zenyewe ila sio hospitali za rufaa kushuka chini. Tumia akili, usilete biashara kwenye afya za watu. Kama mshahara haukutoshi acha kazi kafanye nyingine ila sio kuleta madili hospitali. Mkiona mshahara hautoshi daini kuongezewa mshahara na kama rasilimali watu hawatoshi daini serikari kuongeza rasilimali watu. Ila sio kudanganywa na serikari huku wakiwaachia watu wapige pesa wakati bajeti ilitengwa nyingi. Kama kila mtu akiamua kufanya hivyo kwenye sekta yake kwenye ofisi za serikari mtakuwa wa kwanza kulalamika hapa.
 
Wewe usijifanye kuandika gazeti hapa ukadhani ndio akili sana. Nani asiyejuwa kuna bodi sasa wewe akili yako bodi inaamua mambo ikiwa Serikali au tuseme Tamisemi hawalijui hili? Sijakwambia fast track ina cover cost au mishahara na ndio maana siku zote huduma zimekuwa poor kwa sababu ya kutaka vya rahisi wakati serikali haina uwezo. Ndio maana kuna watu wanaenda private hosp kwa huduma bora na malipo ya juu, hii ndio mifumo yetu wala sio Hosp tu hata mashule unataka ya bei rahisi ya serikali yapo unataka private zipo hakuna wa kukuchagulia. Nenda Muhimbili au Benjamin Mkapa kalazwe halafu uje uweke bill hapa.

Sasa wewe shida yako nini? kwani uliambiwa Hosp zinafungwa? waziri kasema baada ya muda wa kazi huduma ziendelee kama private nini unapoteza katika hili? nani wakukuhudumia bure baada ya muda wa kazi. ondoa mawazo ya kijamaa na umaskini hapa, grow up.
Wewe kama gazeti huwezi kusoma acha. Huduma za afya hazisimami baada ya muda wa kazi maana ukitoka shift yako ataingia mwingine. Ufanye private clinic wakati daktari na wauguzi wengine wapo. Unafanya private clinic kwenye majengo na vifaa tiba walivyonunua wananchi kwapesa zao na ukasomeshwa kwa pesa zao maana madaktari before 2020 walikuwa wanapewa grant na wachache loans na hawarudishagi hizo pesa. Acheni kualika fraud kwenye mambo ya afya huku mkiwa mmeubariki kwasababu ya siasa zenu. Strict policy ifuatwe, kama ni mali ya umma iwe ya umma uache kuleta ulafi wenu kwenye mali za umma. Watanzania tunafikiri hatujuani😂😂😂😂, mkipewa tu upenyo mnajua mmeachiwa kujiachia. Kafanye private clinics huko unapopewa faida wewe ila sio kwenye mali ya umma. Kama private bora, basi nendeni hujakatazwa ila chakushangaza foleni haziishi huku serikarikini. Ndio ujue kuwa watanzania wanapotumia social construct kutengeneza mali za umma ili ziwafaishe wote ni kwasababu uchumi wa mtu mmoja mmoja ni mbovu sana. Wewe unatuletea selfishness na more capitalism hadi kwenye afya, yaani seriously afya, hama nchi kama unataka special treatment.
 
Back
Top Bottom