Umeme wakatika bungeni, waziri aomba mshumaa (aibu)

hadi jana usiku waliokuwa wakichangia bungeni, walikuwa wakichangia gizani, huku vitaa vyekundu vya maic ndo vikionekana...haibu gani hii jamani na bunge hilo latazamwa na wengi..bado tunajivunia serikali sikivu
 
kuna baadhi ya mambo huwa yanatokea tanzania tu...........hutayaona popote duniani
 
Ndiyo tunajua tanzania yote iko kwenye tatizo la umeme lakini mahitaji na matumizi yake yanatofautiana huwezi kulinganisha madhara ya kukosa umeme hospitalini na kwenye bar kwa vile wote waliomo ni wananchi walewale. Jiulize kwanini waziri wa michezo aliomba radhi kukatika kwa umeme wakati wa mashindano ya Kagame na kwa nini wasiombe radhi kukatika kwa umeme jana Bunju au Kibaha kwa Mathias.

Kwa hiyo wewe unaona bunge na hospitali zipo level moja? Bunge na viwanda je? Bunge ndio linalohitaji umeme kupita kwingine kote hadi iwe aibu kukosekana kwake bungeni?
 
Bunge halina powerful standby generator? Ukute hata lile la Ikulu halina mafuta mpaka umeme ukatike ndio wakimbilie mafuta pale BP!!!!!!!!!!
 
Bunge halina powerful standby generator? Ukute hata lile la Ikulu halina mafuta mpaka umeme ukatike ndio wakimbilie mafuta pale BP!!!!!!!!!!
Mzee hiyo powerful generator lazima itakuwa mitambo ya Dowans.
 
Kwa kweli ni vema umeme uendelee kukatika bungeni, ili bajeti ya wizara ya Nishati itakapojadiliwa tena kuwe na umakini mkubwa.
 
Kwa hiyo wewe unaona bunge na hospitali zipo level moja? Bunge na viwanda je? Bunge ndio linalohitaji umeme kupita kwingine kote hadi iwe aibu kukosekana kwake bungeni?
Sasa ulitaka ataje mifano yote na wewee?
 
Aibu ya nini jamani? kwani mnataka umeme umkatikie nani! hao wabunge wapo kwenye casino hilo hawana shida ila sisi tunaotegemea tuonyoe ili tule, tuchomelee ili tule nk ndo tujihurumie. Shame on gvt!
 
Ndiyo tunajua tanzania yote iko kwenye tatizo la umeme lakini mahitaji na matumizi yake yanatofautiana huwezi kulinganisha madhara ya kukosa umeme hospitalini na kwenye bar kwa vile wote waliomo ni wananchi walewale. Jiulize kwanini waziri wa michezo aliomba radhi kukatika kwa umeme wakati wa mashindano ya Kagame na kwa nini wasiombe radhi kukatika kwa umeme jana Bunju au Kibaha kwa Mathias.

Ni unafiki tu. Yaani umeme kukatika U/Taifa si sawa ila ni sawa tu kukatika kiwalani, tunduma, buguruni na kwingineko. Hii nchi bwana! Wote twahitaji umeme, iwe ikulu, mahospitalini, jeshini, viwandani ama uraiani, wote twahitaji umeme.
 
Aibu si kwa wabunge kukosa umeme ila aibu ni kutumia mshumaa, sawa na aibu ya uwanja wa taifa kutumi taa ya gari la ambulance wakati wa kukabidhi kombe. Inakuwaje bunge lisiwe na standby generator au taa ya kandili basi walau tochi kuliko kutumia mshumaa ambao ni hatari.

Lakini kwa upande mwingine mimi naona sawa tu kwa vile bunge linaangaliwa na mataifa mbalimbali ujumbe umefika hadi kwa wafadhili wetu na investors ambao Kikwete amekwenda kuwadanganya ili waje wakijua mapema kuna tatizo la umeme.

that would make more sense. Utasikia mafuta ya generator yameliwa...
 
Hii ipo kwenye hansard? Ilitokea lini? Hivi aibu ni wabunge kukosa umeme au wananchi? Kwangu mimi aibu ni pale wananchi wanapokosa umeme kwa masaa 18 kila siku. Wabunge nao ni wananchi, na hivyo nchi ikiwa kwenye shida ya umeme, kwa nini wao wawe spared? Unapoweka hilo neno aibu hapo, unakuwa kama unasema wao ni special group ambalo halitakiwi kukosa umeme...
Naunga mkono hoja.
 
Walikuwa wanaomboleza juu ya boss wao Jairo kuumbuka! Wanaona sasa hakuna haja ya kuficha kwa kuwa uwezekano wa kuendelea kula bata ni mdogo!.
Kwa kweli jana hapa Dodoma umeme ulikuwa kama Indicators za taa za gari mara ukate mara urudi within 5 to 10 seconds!.
Sielewi tatizo lilikuwa nini japo nafikiri ni mjinga mmoja alikuwa anachezea ili kuwainjoy watumiaji!
Nadhani shirika husika litatoa uongo wao kua tatizo lilikuwa nini kama walivyodanganya juu ya kukatika umeme uwanja wa taifa!
 
WanaJF! Huo ukumbi wa bunge haunaga genereta automatic?
Mafuta yalikua yameisha! Si bajeti ilikataliwa kupita na million 50 wameshatoa sasa we unafikiri pesa itatoka wapi tena!!
Labda Jairo azirudishe zile pesa alizokua amekusanya kufanikisha kupitishwa kwa bajeti!
 
Back
Top Bottom