Mwanaitelejensi
Senior Member
- Jan 30, 2011
- 104
- 2
Inasikitisha sana kuona Brig Gen akiwa anababaika kujibu maswali ya waandishi wa habari matokeo yake anajibu kwa mkato na ujeuri bila ya kujali Wananchi kuwa wanaangalia na wanataka kujua au kusikia kilichotokea ni nini hasa huko G'Mboto. Hii ndio naashiria ni jinsi gani Jeshi letu lilivyokuwa na vilaza wasiokuwa na Elimu ya upambanuaji wa maelezo au kujua kujibu maswali, anaulizwa swali anajibu tofauti na swali lenyewe. Umefika sasa wa kuajiri watu wenye umri wa kuanzia 18-24 kama nchi nyingine wanavyofanya na kuwapa Elimu ya kutosha. Kwani Jeshi sikuhizi linaendana na Elimu sio kujuana na kupachikana kama anavyofanya Kikwete kuwapa kazi washikaji wake. Kikwete ndio muharibifu wa hii nchi yetu