Uliza chochote kuhusu kujiunga Chuo Kikuu Huria Tanzania

Mkuu nashukuru sana nimefanikiwa na nimepata intake ya mwezi April Bach 3 bila maelezo yoyote
Naomba niulize baada ya hapa nini kinafuatia ili niangalie namna ya kupambana na yajayo.
nenda katika OUT centre ya eneo ulipo ukiwa na admission letter yako(kama umeshatumiwa na kama bado subiri),kisha ukifika hapo watakufungulia akaunti ya SARIS na utajisajili katika masomo unayotakiwa kusoma kwa Semister husika na baada ya hapo utapata kuona kiasi cha ada ambacho utatikiwa kulipa,na utaenda katika ofisi za uhasibu kuchukua Control number na kufanya malipo ya kiasi unachohitaji alafu utarudisha Deposit Slip chuoni na utapewa Risiti ya Chuo yenye kuonyesha kiwango ulicholipa ,na baada ya hapo utakuwa umeshapatiwa mawasiliano na Coordinator wako na utaanza kupata uatartibu wa masomo kulingana na Level yako ya Masomo(Undergraduate au Postgraduate)
 
Back
Top Bottom