Kwa mtazamo wangu sikutegemea kabisa kama chama cha siasa kikongwe kama CCM kutumia muda wake mwingi kuelezea mambo ya umbea kwa kushirikisha viongozi wakubwa kabisa wa serikali katika umbea huo very sad. Haya yanatokea ikiwa kunaongezeko kubwa la changamoto za kimaisha ambazo hazina majibu na wananchi wameanza kutoelewana na kupigana wao kwa wao na wao na serikali yao. Huku chama tawala wakiwa Busy kupiga umbea hali inazidi kuwa mbaya mitaani kwetu kila siku. Ndipo ninapojiuliza
1. Maisha ya mtu binafsi katika jukwaa la siasa yanahusu nini?
2. Je ndugu zangu hawa wameuliza wananchi kuwa wanachokihitaji ni kusikia Slaa alifanya nini na wala si maji, elimu bora huduma za afya bora au hata barabara bora
3. Je Ndugu zangu hawa CCM wamejiuliza kuwa hivi sasa je bado wapo katika kusimamia ilani yao au hivi sasa wapo kwenye kujibu mapigo tu hata kwa umbea wa aina yoyote
Mimi ina nipa wasiwasi kwamba kuwa mwanasiasa ni moja ya njia ya kutengana na Mungu lakini pengi itategemeana na upo upande gani?