Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,925
- 30,273
asiyejua historia yake ni mtumwa, hii wala haina kubishana mtu aende pale E&D Vission Publishing, Afika sana nyuma ya corner bar au club ambiance akapata kitabu kinachoitwa Wanawake wa Tanu kilichoandikwa na bibi Titi Mohamed, Mambo yote hadharani.Kwa vile ilishasemwa ukitaka kumnyima mtanzania kitu kiweke katika kitabu wengi mnaishia kubishana, hii tunayoambiwa sio historia ya kweli ya tanganyika
Kwa hakika naelewa hamaki za wengi hasa wasiokuwa Waislam wanaposoma kitabu changu The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Utold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press 1998, London. Naelewa shida wapatayo halikadhalika wasomapo makala zangu tofauti ninazojitahidi kueleza yale ambayo kwa hakika yamekosewa aidha kwa makusudi au kwa kutokujua kuhusu historia ya TANU.
Naelewa simanzi wanayopata Waislam wanaponisikia katika mihadhara na mazungumzo ya kawaida ninapowaenzi mashujaa wa uhuru wengi wao wakiwa Waislam ambao kwa hila wamefutwa katika vitabu na kumbukumbu za taifa letu.
Ukiachia mbali hayo mjadala huu ungekuwa na maana sana endapo wanaoamua kuzungumza suala hili wangejikita katika mada badala ya kuchanganya mada. Katika kufanya hivyo wangeweza kuhoji yake ambayo wanadhani ni uongo. Hii ingenipa mie nafasi ya kujibu na kusema kile ninachokijua.
Ama kuhusu Mwalimu Nyerere hapana hata mahali ambapo nimemvunjia heshima na wala siwezi kukosa adabu kiasi hicho ila ninalosema ni kuwa kuhusu TANU chama hicho hakuanzisha yeye na nimeeleza kwa kirefu sana jinsi chama kilivyoanza, kuchipua kwake hadi kuwa chama chenye nguvu kabisa. Kama kuna mtu anaona vibaya kwa kuelezwa ukweli huu ni bahati mbaya sana.
Ama kuhusu mambo ya elimu, kuwapo kwa Waislam Tanganyika na wingi wao, Bakwata nk. majibu Alhamdulilah yapo na kama itabidi nitayaeleza Insha Allah.