Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
asiyejua historia yake ni mtumwa, hii wala haina kubishana mtu aende pale E&D Vission Publishing, Afika sana nyuma ya corner bar au club ambiance akapata kitabu kinachoitwa Wanawake wa Tanu kilichoandikwa na bibi Titi Mohamed, Mambo yote hadharani.Kwa vile ilishasemwa ukitaka kumnyima mtanzania kitu kiweke katika kitabu wengi mnaishia kubishana, hii tunayoambiwa sio historia ya kweli ya tanganyika

Kwa hakika naelewa hamaki za wengi hasa wasiokuwa Waislam wanaposoma kitabu changu The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Utold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press 1998, London. Naelewa shida wapatayo halikadhalika wasomapo makala zangu tofauti ninazojitahidi kueleza yale ambayo kwa hakika yamekosewa aidha kwa makusudi au kwa kutokujua kuhusu historia ya TANU.

Naelewa simanzi wanayopata Waislam wanaponisikia katika mihadhara na mazungumzo ya kawaida ninapowaenzi mashujaa wa uhuru wengi wao wakiwa Waislam ambao kwa hila wamefutwa katika vitabu na kumbukumbu za taifa letu.

Ukiachia mbali hayo mjadala huu ungekuwa na maana sana endapo wanaoamua kuzungumza suala hili wangejikita katika mada badala ya kuchanganya mada. Katika kufanya hivyo wangeweza kuhoji yake ambayo wanadhani ni uongo. Hii ingenipa mie nafasi ya kujibu na kusema kile ninachokijua.

Ama kuhusu Mwalimu Nyerere hapana hata mahali ambapo nimemvunjia heshima na wala siwezi kukosa adabu kiasi hicho ila ninalosema ni kuwa kuhusu TANU chama hicho hakuanzisha yeye na nimeeleza kwa kirefu sana jinsi chama kilivyoanza, kuchipua kwake hadi kuwa chama chenye nguvu kabisa. Kama kuna mtu anaona vibaya kwa kuelezwa ukweli huu ni bahati mbaya sana.

Ama kuhusu mambo ya elimu, kuwapo kwa Waislam Tanganyika na wingi wao, Bakwata nk. majibu Alhamdulilah yapo na kama itabidi nitayaeleza Insha Allah.
 
Tatizo mtu anadandia hoja tu bila ya kupitia source zote zilizowekwa na aliyeweka mada.

Ni kwamba sio kweli kwamba kabila na dini nyingine hazikupigania uhuru wa Tanganyika ila kundi la waliopigania Uhuru wa Tanganyika kwa makusudi haikuandikwa ukweli kuhusu wao na mchango wao kama walivyotoa watu wengine kutoka dini mbalimbali na kabila mbalimbali.

Hii ndio kusudio kuu ya mada hii na si venginevyo.

Kinachotakiwa ni haki na sio upendeleo wa aina yoyote ile. Ila kwa kuwa watu wengine inawauma kuona ukweli ndio utaona analeta mambo yasiyo na maana katika mada hii.

Mkuu Maalim Al Saidy, mimi sitaki kukutukana lakini watu wanasema katika uerevu kuna watu aina mbili , mjinga na mpumbavu.
Mjinga ana chances za kuuelewa ukweli kwa kuelimishwa na kufikiri , huyu ana chances za kuendelea na kufanya mambo yanayoendeleza jamii.
Mpumbavu ni yule ambaye ataambiwa ukweli , atasoma ukweli, ataujua ukweli lakini bado atahadithia na kutema pumba.
Hii mada sitaki kuamini kuwa inaendeshwa na watu wa aina hii ya pili.
Al Saidy unapokuja na kuniambia uhuru wa nchi hii ulianza na waislamu you are insulting our intelligence and stature of the african and his historical background.
Uislamu na Ukristo wote ni wakuja, and both were resisted by our forefathers.
Kama unafikiri unaweza kuandika historia vizuri zaidi baada ya kula pilau na kupata hadith zilizopindishwa na wahubiri wenye nia ya kuleta mifarakano katika jamii basi your staure might be lower than I expected.
Sorry again I dont mean to insult but this type of islamisation of the peoples struggle for indepenence will definately backfire onto your selves.We hope we dont have to bear to see you guys wearing bombs on your waists just to make your point.
 
Kwa hakika naelewa hamaki za wengi hasa wasiokuwa Waislam wanaposoma kitabu changu The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Utold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press 1998, London. Naelewa shida wapatayo halikadhalika wasomapo makala zangu tofauti ninazojitahidi kueleza yale ambayo kwa hakika yamekosewa aidha kwa makusudi au kwa kutokujua kuhusu historia ya TANU.

Naelewa simanzi wanayopata Waislam wanaponisikia katika mihadhara na mazungumzo ya kawaida ninapowaenzi mashujaa wa uhuru wengi wao wakiwa Waislam ambao kwa hila wamefutwa katika vitabu na kumbukumbu za taifa letu.

Ukiachia mbali hayo mjadala huu ungekuwa na maana sana endapo wanaoamua kuzungumza suala hili wangejikita katika mada badala ya kuchanganya mada. Katika kufanya hivyo wangeweza kuhoji yake ambayo wanadhani ni uongo. Hii ingenipa mie nafasi ya kujibu na kusema kile ninachokijua.

Ama kuhusu Mwalimu Nyerere hapana hata mahali ambapo nimemvunjia heshima na wala siwezi kukosa adabu kiasi hicho ila ninalosema ni kuwa kuhusu TANU chama hicho hakuanzisha yeye na nimeeleza kwa kirefu sana jinsi chama kilivyoanza, kuchipua kwake hadi kuwa chama chenye nguvu kabisa. Kama kuna mtu anaona vibaya kwa kuelezwa ukweli huu ni bahati mbaya sana.

Ama kuhusu mambo ya elimu, kuwapo kwa Waislam Tanganyika na wingi wao, Bakwata nk. majibu Alhamdulilah yapo na kama itabidi nitayaeleza Insha Allah.
Mohammed,
Hakuna mahali popote katika historia ambapo Nyerere alidai kuwa ndiye aliyeanzisha TANU. Nakumbuka nikiwa mdogo baada ya uhuru tumesoma historia ya TANU wakati huo vitabu vingi vimeandikwa na wazungu, na wakizungumzia historia ya TAA mpaka ilipopelekea kuundwa kwa TANU. Nyerere hakudai hivyo, na kama kuna mtu aliyedai kuwa Nyerere pekee ndiye aliyeanzisha TANU, basi huyo anapotosha historia kwa sababu zake mwenyewe. Hali kadhalika, mbali ya kutambua mchango wa Waislamu katika harakati za TANU, hawa hawakuwa peke yao, kwa sababu ukiangalia historia ya TANU ilikuwepo michango ya watu wengi mbalimbali katika sehemu mbali mbali za Tanganyika. Ni kweli Waislamu walikuwa shina la harakati lakini harakati zilipanuka na kushirikisha watu mbalimbali katika kona zote za Tanganyika.
 
Mohammed,
Hakuna mahali popote katika historia ambapo Nyerere alidai kuwa ndiye aliyeanzisha TANU. Nakumbuka nikiwa mdogo baada ya uhuru tumesoma historia ya TANU wakati huo vitabu vingi vimeandikwa na wazungu, na wakizungumzia historia ya TAA mpaka ilipopelekea kuundwa kwa TANU. Nyerere hakudai hivyo, na kama kuna mtu aliyedai kuwa Nyerere pekee ndiye aliyeanzisha TANU, basi huyo anapotosha historia kwa sababu zake mwenyewe. Hali kadhalika, mbali ya kutambua mchango wa Waislamu katika harakati za TANU, hawa hawakuwa peke yao, kwa sababu ukiangalia historia ya TANU ilikuwepo michango ya watu wengi mbalimbali katika sehemu mbali mbali za Tanganyika. Ni kweli Waislamu walikuwa shina la harakati lakini harakati zilipanuka na kushirikisha watu mbalimbali katika kona zote za Tanganyika.
=====
Jasusi
Mimi naweza kuongeza kwa kusema, kilichowaleta wapigania uhuru pamoja wakati ule si uislamu wao bali utanganyika wao. Napata shida sana mtu anapoanza argument inayomaanisha kuwa mtu anakuwa Mwislamu kabla hajawa mtu, au anakuwa Mwislamu kabla hajawa Mtanzania. Niyasemapo haya namaanisha pia kwa dini nyingine zote zinazopenda kuvaa miwani ya dini katika kuangalia historia ya taifa letu.
 
Kwa hakika naelewa hamaki za wengi hasa wasiokuwa Waislam wanaposoma kitabu changu The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Utold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press 1998, London. Naelewa shida wapatayo halikadhalika wasomapo makala zangu tofauti ninazojitahidi kueleza yale ambayo kwa hakika yamekosewa aidha kwa makusudi au kwa kutokujua kuhusu historia ya TANU.

Naelewa simanzi wanayopata Waislam wanaponisikia katika mihadhara na mazungumzo ya kawaida ninapowaenzi mashujaa wa uhuru wengi wao wakiwa Waislam ambao kwa hila wamefutwa katika vitabu na kumbukumbu za taifa letu.

Ukiachia mbali hayo mjadala huu ungekuwa na maana sana endapo wanaoamua kuzungumza suala hili wangejikita katika mada badala ya kuchanganya mada. Katika kufanya hivyo wangeweza kuhoji yake ambayo wanadhani ni uongo. Hii ingenipa mie nafasi ya kujibu na kusema kile ninachokijua.

Ama kuhusu Mwalimu Nyerere hapana hata mahali ambapo nimemvunjia heshima na wala siwezi kukosa adabu kiasi hicho ila ninalosema ni kuwa kuhusu TANU chama hicho hakuanzisha yeye na nimeeleza kwa kirefu sana jinsi chama kilivyoanza, kuchipua kwake hadi kuwa chama chenye nguvu kabisa. Kama kuna mtu anaona vibaya kwa kuelezwa ukweli huu ni bahati mbaya sana.

Ama kuhusu mambo ya elimu, kuwapo kwa Waislam Tanganyika na wingi wao, Bakwata nk. majibu Alhamdulilah yapo na kama itabidi nitayaeleza Insha Allah.

Mkuu. Hapa si una-plug kitabu chako tu ili kiuzike ujipatie vijisenti?Hakuna kipya unachotueleza maana wote tunajua fika kuwa walikuwepo waislamu na wakristu na wasio na dini katika hayo mapambano. Na kadhalika walikuwepo waislamu vibaraka kama walivyokuwa wengine wa dini nyingine. Unachofanya ni kama mtu aje aandika kitabu kuzungumzia mchango wa WANAUME au WANAWAKE katika kugombea uhuru, ukizima kabisa mchango wa jinsia nyingine. Au unataka kutuambia kuwa waislamu waliongoza mapambano wakiwa na nia ya kutangaza taifa la kiislamu?

Amandla......
 
*Uislamu Tanganyika 4*
Mohd Said anatueleza kwamba gazeti la "African Events" lilizuiliwa kuuzwa Tanzania kwa sababu ya makala aliyoandika Mohamed Said kuhusu juhudi za Waislamu kupigania uhuru wa Tanganyika. Akafika kutishiwa. Zama za Nyerere Waislamu serekalini walifika kuficha majina yao ya Kislamu.




Hii peke yake inaku-discredit labda utuambie wakina Rashid Mfaume Kawawa, Bakari Mwapachu n.k.wote walislimu? Watu walibadili majina shuleni kutokana na kutaka kurudia mtihani ambao walifeli mara ya kwanza. Mara nyingi walifanya hivi kwa kuhamia sehemu nyingine ya nchi ambako wenyeji wake walikuwa hawajachangamkia elimu. Wachaga wakajiita majina ya kimasai au kizaramo n.k. Leo kutaka kuingiza dini humu kunaonyesha wazi kuwa ajenda yako ni kupotosha historia ambayo wengi tuliiishi. Na wengine ingawa tulikuwa wamisheni ndugu zetu nao walibadilisha majina, wakina John wakaitwa Jafari!

Amandla....
 
Ijue Historia ya Kweli ya Kuasisiwa kwa TANU

Mohamed Said

Nimesoma makala kuhusu Mzee Lameck Makaranga Bogohe (Nipashe Julai 7, 2010) iliyoandikwa na Denis Maringo ambae ametambilishwa kama Mwanahistoria na Mwanasheria kitaaluma na ni Mkurugenzi wa Kituo cha Haki na Demokrasia - Centre for Justice and Democracy (CJD).

Inaelekea nia ya makala hiyo ilikuwa kuwakumbusha wananchi historia ya kuasisiwa kwa TANU na waasisi wake hasa kwa kuwa tulikuwa katika sikukuu ya saba saba ambapo tunakumbuka siku TANU chama kilichopigania uhuru wa Tanganyika kilipoanzishwa tarehe 7 Julai 1954. Ajabu ni kuwa katika vitu vinavyostaajabisha sana ni kupuuzwa kwa historia hii iliyotukuka ya kudai uhuru wa Tanganyika pamoja na kupuuzwa kwa wazalendo walijitolea muhanga wakati ule kuhakikisha kuwa Tanganyika inajikwamua kutoka katika makucha ya ukoloni wa Waingereza. Mzee Bogohe analalamika kwa kusema kuwa "…katika vitabu kila Tanu iandikwapo ni Mwalimu Nyerere." Kwa hakika Mzee Bogohe si wa kwanza kuliona hili hata mie kuna wakati hili jambo lilikuwa likinistaajabisha sana hata nikafikia kuona kuwa labda CCM chama kilichokuja baada ya TANU hawajipendi na hawawapendi mashujaa wao lakini nikajagundua kuwa si kama hawajipendi ila hawapendi historia ya wazalendo wengine wanapenda historia ya Julius Nyerere peke yake na atajwe pweke bila ya kumuhusisha na yeyote yule.

Mzee Bogohe amesema mengi kuhusu udhaifu huu lakini mie sitanukuu moja baada ya jingine katika masikitiko yake ila nitazungumza kwa ujumla tu na kujaribu kusahihisha yale ambayo nimeona labda kwa uzee, siku kuwa nyingi kupita na kwa kukosa nyaraka halisi za rejea za historia ya kuanzishwa kwa TANU kuna mengi mzee wetu ameyasahau au ameyakosea kwa tarehe na maudhui yenyewe katika matokeo yaliyopelekea kuundwa kwa African Association mwaka 1929 na katika kuigeuza African Association kuwa Tanganyika African Association (TAA) mwaka 1948 na mwishowe kuundwa kwa TANU 1954. Katika maelezo hayo nitaelezea vilevile harakati zilizokuwapo pale New Street Makao Makuu ya TAA wakati wazalendo viongozi wa TAA kati ya 1950 – 1953 walipokuwa wanapanga mikakati ya kuunda TANU. Wakati huo ni ukweli usiopingika kuwa hakuna kati yao ukimtoa Hamza Mwapachu na Joseph Kasella Bantu aliyekuwa amemsikia Julius Nyerere.

Imethibitika hivi sasa kuwa Nyerere hakupendezewa na historia ya kweli ya kudai uhuru wa Tanganyika ambayo ilianza miaka mingi nyuma kabla yake kiasi cha takriban nusu karne. Historia ya African Association (baadae chama kikaja kujulikana kama Tanganyika African Association - TAA) chama kilichokuja kuunda TANU 1954 inaanza katikati ya miaka ya 1920 na kinara wa harakati hizo alikuwa Kleist Sykes (1894 - 1949) baba yao marehemu Abdulwahid (1924 – 1968), Ally na Abbas Sykes. Kumbukumbu za Kleist zinaonyesha kuwa alitiwa hamasa za kuanzisha African Association na Dr Dr James Kwegyir Aggrey kutoka Ghana aliyekuja kutembelea Tanganyika mwaka wa 1924. Kleist alikuwa Mwafrika msomi katika kiwango cha enzi zile akizungumza Kiingereza na Kijerumani. Dr Aggrey katika mazungumzo na viongozi wa Dar es Salaam Waafrika akiwamo Kleist Sykes aliwashauri viongozi wale kuwa ili kupata maendeleo haraka itakuwa busara kwa wao kama Waafrika kuwa na chama chao kitakachowajumuisha Waafrika wote. Ilimchukua Kleist na wenzake miaka mitano hadi kufikia kusajili African Association mwaka 1929 Kleist akiwa katibu mwanzilishi na Mzee Bin Sudi akiwa rais wake. Viongozi hawa baada ya kuasisi African Association wakaasisi chama kingine Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika mwaka 1933. Mingi ya mikutano ya kuanzisha African Association ikifanyika nyumba moja Mtaa wa Magila Mission Quarters, nyumba hii baadae ilikujanunuliwa na John Rupia. Hii nyumba bado ipo hadi leo. Wanahistoria bado wananafasi ya kwenda izuru nyumba hii kabla haijavunjwa na kujengwa ghorofa.

Historia ya TANU ukiitaka kwa undani inaanza miaka hii 1929 na mwanzoni mwa 1930. Sasa kupitia vyama hivi viwili viongozi wake wakajenga majengo mawili, moja ni hiyo nyumba ambayo hadi leo ipo ambayo yalikuwa makao makuu ya African Association Mtaa wa New Street. Jengo hili lipo na lilikuja kufunguliwa na Gavana Ronald Cameroon mwaka 1933. Bwana Ally Sykes ana picha ambayo inaonyesha sherehe za ufunguzi wa jengo hilo ikimwonyesha baba yake, Gavana Cameroon, Mwalimu Mdachi Shariffu, Machado Plantan na viongozi wengine wa African Association. Hii ndiyo nyumba iliyokuja kuasisiwa TANU mwaka 1954. Marehemu Abdulwahid Sykes katika kumbukumbu zake anasema yeye alikuwa akifuatana na baba yake kila siku za Jumapili pale New Street na akimuona baba yake na viongozi wenzake wakijenga nyumba ile kwa kujitolea. Jengo la pili ni hilo ambalo sasa ni shule ya Msingi ya Lumumba ambapo zamani ilikuwa makao makuu ya Al Jamiatuli Islamiyya na vilevile ilikuwa Al Jamiatul Islamiyya Muslim School. Viongozi wa mwanzao na wanachama wa awali wa TANU walitokana na vyama hivyo viwili. Taarifa hizo zote na kumbukumbu nyingine za harakati za siasa katika Tanganyika zipo mpaka leo katika hifadhi ya familia ya akina Sykes. Mwandishi wa makala hii zilimsaidia sana katika kuandika kitabu, The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 -1968 The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika kitabu kilichochapwa London mwaka 1998 na tafasiri yake ya Kiswahili kuchapwa na Phoenix Publishers, Nairobi mwaka wa 2002.

Historia hii ya TANU kama ilivyo hapo juu ilikuja kuandikwa na Abdulwahid Sykes na Dr Wilbert Kleruu mwanzoni mwa miaka ya 1960 kwa ushauri wa Mwalimu Nyerere, Mwalimu Kihere na Dossa Aziz. Inasemekana historia ile kama alivyokuwa akiandika marehemu Abdulwahid Sykes ikawa kama inamtia unyonge kidogo Nyerere. Inasemekana Nyerere hakuipenda historia ile. Kwa hakika historia hii ambayo yeye hayumo hakuipenda kabisa na ikabidi mradi huo wa kuandika historia hiyo ufe kabla ya kazi kukamilika. Abdulwahid Sykes akajitoa katika kazi hiyo akamuuacha Dr Kleruu yeye aendeleenayo. Kleruu alimaliza kazi hiyo kwa namna inavyosemekana alivyoelekezwa na Nyerere lakini mswada ukabaki pale Makao Makuu ya TANU bila kuchapwa kwa muda mrefu. Inasemekana mswada uliibiwa na ukajachapwa kitabu bila ya ridhaa ya TANU. Hata hivyo haijulikani nyaraka zile za mwanzo kama zilivyoandikwa na Abdulwahid Sykes ziko wapi kwa sasa kwani juhudi za mwandishi kuzipata katika maktaba ya CCM Dodoma ziligonga mwamba.

Baada ya wizi huo TANU ikaunda jopo la wataalamu wake ambalo lilikaa kitako na kuandika historia ya TANU na kitabu kikachapwa (Historia ya Chama Cha TANU 1954-1977, Dar es Salaam, Kivukoni Ideological College, 1981). Kitabu hiki kilipotoka wengi hasa sie wazaliwa wa Dar es Salaam kikatustaajabisha kwani kwa kweli kilikuwa kitu kingine, ile haikuwa historia ya TANU na haitakujakuwa. Kwa uchache unaweza kusema ilikuwa historia yake Nyerere kuanzia mwaka wa 1954 na hata hivyo ilikuwa ikichagua nini la kuandika jina gani la kutaja na lipi la kukwepa. Kwa nini nasema kukwepa? Kitabu kizima hakuna hata sehemu moja ambako waasisi wa siasa za Tanganyika - ukoo wa akina Sykes ulipotajwa. Huwezi kuandika historia ya Nyerere ukaacha kuwataja watu hawa na wazalendo wa Dar es Salaam waliomtia katika siasa za TAA na TANU watu kama Mwinjuma Mwinyikambi, Jumbe Tambaza, Mshume Kiyate, Iddi Tosiri na ndugu yake Iddi Faizi na kaka yao Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Dossa Aziz, Hamza Mwapachu, Clement Mtamila, Dr Michael Lugazia, John Rupia, Dr Vedasto Kyaruzi, Dr Luciano Tsere, Dome Budohi, Dennis Phombeah, Zuberi Mtemvu, Ali Mwinyi Tambwe, Tatu binti Mzee, Titi Mohamed, Asha Ngoma na majina kwa kweli ni mengi ukisema uyataje hutoweza kuyamaliza kwa ukamilifu wake. (Titi Mohamed amehutubia mkutano wa TANU miezi michache baada ya kuundwa kwa TANU pale Mnazi Mmoja hamjui Nyerere wala hajaona sura yake inafananaje). Ikawa sasa historia hii ya ukwepaji baadhi ya majina ya wazalendo Mwalimu akaipenda na ndiyo ikawa historia rasmi inayokubalika ya TANU na harakati za kudai uhuru hadi leo.

Katika hali kama hii ndipo ikawa watu kama Mzee Bogohe lau kama walikuwa na mchango wao katika siasa za kudai uhuru wa Tanganyika wakawa wamewekwa pembeni hawatajwi anatajwa Nyerere peke yake. Itoshe kumaliza kipengele hiki kwa kusema kuwa katika chaguzi za siasa za kusisimua katika historia ya Tanganyika ni ule uchaguzi wa TAA wa 1953 wakati Nyerere alipogombea nafasi ya urais wa TAA dhidi ya rais wake aliyekuwa anamaliza kipindi chake Abdulwahid Sykes pale katika ukumbi wa Arnatouglo tarehe 17 April 1953. Kukutana kwa Abdulwahid Sykes na Nyerere mwaka wa 1952 na siri za harakati alizozikuta Nyerere kwa Abdulwahid Sykes ni kisa cha kumsisimua mtafiti yeyote wa historia. Mama Maria Nyerere lazima atakuwa na kumbukumbu hizi za wao na akina Sykes pale mtaa wa Kipata nyumbani kwa Ally Sykes na Aggrey Street nyumbani kwa Abdulwahid Sykes na pilka pilika za hatari za kuwakwepa makachero wa Special Branch wakiongozwa na Amri Kweyamba na vijana wake. (Amri Kweyamba alidumu katika kazi hiyo hata baada ya uhuru lakini sasa akiitumikia serikali ya TANU na Nyerere siyo ile ya Gavana Edward Twining). Pale Kipata ndipo Ally Sykes alipokuwa ameficha mashine ya kudurufu ambayo alikuwa akichapa makala za siri (Waingereza wakiziita za uchochezi) kuhamasisha Waafrika dhidi ya ukoloni. Shajara za Abdulwahid Sykes za kipindi hiki (1950 - 1954) ameziandika kwa hati mkato na inasikitisha kuwa hadi leo akina Sykes hawajataka kuzitoa kwa watafiti zisomwe kwa faida ya historia ya nchi yetu na kizazi kijacho.

Wazee wengi wa Dar es Salaam na wengi wao weshatangulia mbele ya haki wanafahamu fika kuwa kama unataka kumpa sifa mtu mmoja kwa kuanzisha TANU basi hatakuwa Nyerere sifa hiyo ni ya marehemu Abdulwahid Sykes ambae katika uongozi wake kuanzia 1950 hadi 1953 ndipo aliposhughulikia katiba ya TANU na kuleta mbinu mpya ya kupambana na Waingereza kiasi cha kuwa baada ya majalada ya Kiingereza kule London kuwekwa wazi (baada ya kupita miaka 50) taarifa za siri za kikachero za Special Branch zinaonyesha kuwa Abdulwahid walimchukulia kama mtu "hatari." Alikuwa hatari kwa kuwa ndani ya TAA katika miaka ya mwanzo ya 1950 Abdulwahid akiwa ndiye rais TAA ilikuwa na uhusiano na harakati za Mau Mau chini ya akina Kenyatta na Bildad Kaggia huko Kenya na Kenneth Kaunda toka Northern Rhodesia. Itoshe tu kusema mwaka 1950 Abdulwahid Sykes alifanya mkutano wa siri na viongozi wa KAU Nairobi wakiwemo Kenyatta mwenyewe, Kaggia, Kungu Karumba na wengine nia ikiwa ni kuunganisha nguvu za Tanganyika na Kenya katika kuupiga vita ukoloni. Kisa cha Ally Sykes na Kenneth Kaunda ni kisa kingine cha kusisimua sana. Baada ya kuwasiliana na Kaunda mwaka 1953 na Kaunda kumwalika Ally Sykes na Dennis Phombeah katika mkutano wa wanaharakati wa ukombozi kusini ya Afrika uliokuwa ufanyike Lusaka Ally Sykes na Dennis Phombeah waliishia mbaroni mjini Salisbury Southern Rhodesia. Hizi ndizo zilikuwa harakati za TAA pale Makao Makuu na hawa ndiyo walikuwa viongozi walokuja iasisi TANU.

Niongeze kidogo kwa kusema kuwa na hili suala la katiba ya TANU wala si kitu cha kukipigia sana kelele kwani walichofanya viongozi wa TAA ilikuwa kunakili katiba ya Convention Peoples Party (CPP) chama alichokianzisha Kwame Nkrumah. Mahali palipoandikwa CPP viongozi wa TAA waliweka TANU. Kwa hakika kama kuna kitu cha kujivunia katika maandiko yaliowahi kuandikwa na TAA basi ni ile memorandum ya TAA Political Subcommittee iliyotayarishwa mwaka 1950 na uongozi wa TAA na kusainiwa na viongozi hawa wafuatao: Abdulwahid Sykes, Sheikh Hassan bin Amir kama Mufti wa Tanganyika na Zanzibar; Dr Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, Said Chaurembo, John Rupia na Stephen Mhando. Waraka huu ndiyo Nyerere alikwendanao Umoja wa Mataifa mwezi Machi mwaka wa 1955 na kuusoma mbele ya Baraza la Udhamini. Hiki ndicho kitu cha kuringia na kujivunia si hiyo katiba ya TANU waliyonyambua toka kwa Nkrumah. Inasemekana hatima iliyoikumba ile kazi ya historia iliyoandikwa na Abdulwahid Sykes kuibiwa pale Makao Makuu ya TANU imeikumba na nyaraka hii muhimu ya kihistoria iliyotayarishwa mwaka 1950 na viongozi wa TAA. Haishangazi leo ukisikia baadhi ya viongozi wakiikashifu TAA wakinadi kinywa kipana na bila ya soni ati TAA hakikuwa chama cha siasa bali kilikuwa chama cha starehe.

Mzee Bogohe anasema jina la TANU kalitoa yeye na anataka atambulike kwa hilo, sawa. Wangapi leo wanajua kuwa kadi za TANU za kwanza 1000 alizitengeneza Ally Sykes na akazilipia kutoka mfukoni kwake binafsi? Wangapi leo wanajua kuwa kadi ya Nyerere ya TANU ni namba 1 na imetiwa saini na Ally Sykes? Wangapi wanajua kadi namba 2 ya TANU ni ya Ally Sykes mwenyewe na namba 3 ni ya kaka yake Abdulwahid Sykes? Vipi kaka mtu apate kadi namba 3 na mdogo namba 2 ikiwa utamaduni wa Kiafirika na adabu zetu ni kumtanguliza mkubwa mbele? Majibu yapo na ndiyo yanayokoleza utamu wa historia ya kweli ya TANU. Kinyume cha hapo utapambana na historia ya kubuni na kitu cha kubuni au kisichokuwa na ithibati siku zote huwezi kukitegemea kujenga hoja thabiti.

Hapa si mahali pale kuyaeleza yote hayo. Bwana Ally Sykes yu hai na wanahistoria waende wakamhoji watapata faida kubwa. Sasa na tujiulize, lipi kubwa. Kutoa jina la TANU au kukianzisha chama chenyewe cha TANU? Historia imeshuhudia kuwa hadi anaingia kaburini marehemu Abdulwahid Sykes hakupata kukumbusha kuwa TANU chanzo chake ni baba yake au kuwa yeye ndiye aliyemweka Nyerere katika uongozi wa TAA na mwishowe TANU. Msisitizo ni kuwa hadi marehemu Abdulwahid Sykes anaingia kaburini 1968 hakupata kujinasibu kwa kuanzisha TANU wala kusema kuwa alikuwa yeye ndiye aliyempa Nyerere nafasi ya uongozi kwanza katika TAA 1953 na kisha 1954 katika TANU. Abdulwahid Sykes kwa waliomjua wanasena alikuwa mtu muungwana sana. Juu ya hayo yote alofanya ukiondoa kuwa alikuwa kati ya wafadhili wanne wa awali wa TANU wengineo wakiwa mdogo wake, Ally, John Rupia na Dossa Aziz hawa wote wametolewa katika kumbukumbu za historia ya TANU. Ukikisoma kitabu cha historia ya TANU kilichoandikwa na Kivukoni College hili utaliona dhahiri.

Tumalize kisa chetu. Yapo makosa kidogo katika simulizi ya Mzee Bogohe bila shaka ni kwa sababu ya miaka mingi kupita. Mzee Bogohe anasema kuwa Mhasibu Mkuu wa kwanza wa TANU alikuwa Julius Mwasanyangi. Ukweli ni kuwa mweka hazina wa kwanza wa TANU alikuwa Iddi Faizi Mafongo aliyekuwa mhasibu vilevile wa Al Jamiatul Islamiyya. Iddi Faizi Mafongo ndiye aliyekuwa na jukumu la kukusanya fedha za safari ya Nyerere kwenda Umoja wa Mataifa mwezi Machi 1955. Katika nafasi yake ya kuwa mweka hazina wa vyama hivyo viwili Iddi Faizi alitoa fedha katika hazina ya za Al Jamiatul Islamiyya na kuzitia katika mfuko wa TANU ili kufanikisha safari ile. Iddi Faizi ana historia nzuri sana na ni jukumu lao sasa wanahistoria kuzitafuta habari zake. Iddi Faizi, Sheikh Suleiman Takadir na Nyerere ndio waliotembea Jimbo la Mashariki mwaka 1958 kuwahamasisha wana -TANU wasisuse kuingia katika Uchaguzi wa Kura Tatu.

Iwe itakavyokuwa nyaraka za historia zinaonyesha kuwa alotoa jina la TANU alikuwa marehemu Abdulwahid Sykes na jina hilo alilitoa Kalieni Camp India mkesha wa Christmas mwaka 1945 akiwa askari wa 6 Batallion, Burma Infantry katika King's African Rifles (KAR) wakati wa Vita Kuu ya Pili. Kalieni Camp ndipo askari wa KAR walipokuwa wamekusanywa wakisubiri kurudishwa makwao baada ya kumalizika vita. Ukienda katika shajara yake ya mwaka huo taarifa hizi utazikuta. Juu haya hilo haliondoi ukweli kuwa huenda na Mzee Bogohe na yeye vilevile alikuwa na wazo la kuanzisha chama cha siasa hata kama si kile cha TANU. Ala kuli hali muhimu ni kwa wanahistoria kuwatafuta wazee hawa na kupokea hazina ambayo si muda mrefu itatoweka.Wangapi leo wanajua kuwa ni Hamza Mwapachu na Abdulwahid Sykes ndiyo waliomsukuma Nyerere katika ulingo wa siasa? Au wangapi wanajua historia ya madaktari watano – Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr Joseph Mutahangarwa, Dr Wlibard Mwanjisi, Dr Michael Lugazia na Dr Luciano Tsere na mchango wao katika kusukuma mbele harakati za TAA kati ya 1948 – 1950?

Kwa kumaliza napenda kumuuliza msomaji wangu kuwa je, haishangazi kuwa historia ya kutukuka kama hii ya wazalendo na mashujaa wetu leo imetupwa na haipewi thamani? Kama inashangaza je, haiwi vyema tukajiuliza kwa nini imekuwa hivi? Ni nini viongozi wetu wanachokiogopa katika kuwaenzi mashujaa wa uhuru wa Tanganyika? Je ndiyo tuchukulie kuwa Tanzania ni nchi isiyokuwa na mashujaa wake? Wasomaji hamkubaliani nami kuwa kuna haja kubwa sana ya kuandika upya historia ya uhuru wa Tanganyika na kuwaenzi wale wote waliotoa mchango katika vita vya uhuru? Kwa kumaliza makala haya namshukuru Mzee Lameck Bogohe kwa kufunua kinywa na kutueleza yale anayoyajua katika kuanzishwa kwa TANU na kuonyesha kidole kwa yale ambayo ameyaona yanapotosha historia hiyo. Nitafurahi sana Insha Allah kama watajitokeza wengine na kuandika wanayoyajua kuhusu mashujaa wetu wa uhuru ambazo habari zao hazijulikani na wengi. Je hapana haja ya kuiuliza CCM hivi hadi lini wataiacha historia yao inapotoshwa na kupotea?

Mohamed Said
8th Julai 2010
mohamedsaidsalum@yahoo.com
 
Huwezi kuandika historia ya Nyerere ukaacha kuwataja watu hawa na wazalendo wa Dar es Salaam waliomtia katika siasa za TAA na TANU watu kama Mwinjuma Mwinyikambi, Jumbe Tambaza, Mshume Kiyate, Iddi Tosiri na ndugu yake Iddi Faizi na kaka yao Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Dossa Aziz, Hamza Mwapachu, Clement Mtamila, Dr Michael Lugazia, John Rupia, Dr Vedasto Kyaruzi, Dr Luciano Tsere, Dome Budohi, Dennis Phombeah, Zuberi Mtemvu, Ali Mwinyi Tambwe, Tatu binti Mzee, Titi Mohamed, Asha Ngoma na majina kwa kweli ni mengi ukisema uyataje hutoweza kuyamaliza kwa ukamilifu wake. (Titi Mohamed amehutubia mkutano wa TANU miezi michache baada ya kuundwa kwa TANU pale Mnazi Mmoja hamjui Nyerere wala hajaona sura yake inafananaje). Ikawa sasa historia hii ya ukwepaji baadhi ya majina ya wazalendo Mwalimu akaipenda na ndiyo ikawa historia rasmi inayokubalika ya TANU na harakati za kudai uhuru hadi leo.

Hapa tuu panakushtaki. Hao wakina John, Clement, Michael, Luciano, Dennis .... wote walikuwa waislamu? Wakina Sykes walianzisha vyama viwili kimoja TAA na kingine cha waislamu. TAA na sio Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ndicho kilichozaa TANU. Hao waasisi walivitenganisha makusudi wakijua kuwa malengo yake yalikuwa tofauti. sasa leo unapokuja kutuambia kuwa TAA kilikuwa chama cha kiislamu unataka kutuambia nini? Si heri hao wakina Sykes waliachiwa wachume wapendavyo wakati wa Nyerere. Nani anawajua wakina Phombeah, Kyaruzi & Company? Bila shaka historia si ya TANU peke yake nbali ya nchi nzima imeegemea mno kwa Nyerere lakini si kwa sababu ati alikuwa mkristu bali ni kwa sababu yeye ndiye alikuwa kiongozi aliyeonekana wa mapambano hayo. George Washington hakupigana peke yake kuwaletea uhuru wamarekani lakini ni yeye ndiye anayeenziwa. Sawa sawa na wakina Kaunda, Nkrumah na wengine. Ungetusaidia wote kama ungeandika historia ambayo ingejaribu kutafuta ukweli wa watu waliosahauliwa bila kujali dini, kabila au jinsia yao. Kwa kufanya unachofanya unageuka mchochezi tu na si mwana historia. Uhuru nchi hii haukeletwa na wakristu peke yao, au waislamu peke yao au Nyerere paeke yake au Familia ya wakina Sykes peke yao. Wengi zaidi ya hawa walichangia, wengi wao ambao wamesahaulika. ndivyo historia ilivyo.

Amandla.....
 
CCM ya leo imejaa mafisadi sidhani wana hamu hata ya kuchambua historia yao. Wangefurahi zaidi kama jina la Nyerere lingesahaulika Tanzania.
 
Ndugu Mohammed Said,

Nimesoma kwa makini sana hiyo assertion yako lakini baada ya kumaliza kusoma nikagundua kuwa hicho kitabu kina nia ya kuinua uislamu badala ya uafrika kwanza, na cha kustajabisha ni kuwa kulikuwa na wakristo ndani yeka na umewataja kama mzee marehu Joseph kassela bantu, John Rupia marehemu, Clement Mtamila, Dr Michael Lugazia, Dr Vedasto Kyaruzi, Dr Luciano Tsere, Dome Budohi, Dennis Phombeah, je hawa si wote hawakutendewa haki kutokana naa assertion zako? kuwa jitihada za uislamu katika mapambano ya kung'oa mkoloni? hicho kitabu ni dhahili kabisa kiko bias! na kinatia shaka kubwa juu ya facts zote tunazolazimishwa watanzania kuamini, nadhani tukirejea nyuma tutakumbuka kuwa ancestors wetu kabla ya kuwasili kwa waarabu katika pwani ya afrika mashariki waliweza kupambana na bishara haramu ya utumwa ambao ulikuwa unadhalilisha utu wa mtu na hoa waliotuletea dini ya kiislamu ambao ni waarabu! sasa je na mimi nikiku challenge kutokana na imani yako ya uislamu ambayo imekusukuma kupotosha historia ya mapambano ya kujipatia uhuru haikuanzia wakati wa waingereza tu balii ilikuwapo toka enzii za waarabu kwenye pwani ya afrika mashariki ambapo babu zetu ambao walikuwa wapagani walipambana nao na kushindwa ndipo wakawa wanachukuliwa watumwa na hao hao waarabu waliokuja kuwapa dini hiyo ya kiislamu! sasa mbona hatujaona umeanzia kwenye shina la mapambano dhidi ya waarabu? lakini nanakuelewa nia yako ni kumwonesha kuwa nyerere alikuwa anafunika nguvu za waislamu na uislamu uliosaidia kuleta uhuru! kwa nini mantiki yako isiwe kwa watanganyika waliosaidia kpambana na kuunda vyama vilivyopigania uhuru? Nadhani mtu yeyyote ambaye anataka kupotosha uma kwa kutumia mlango wa udini, anapaswa kukemewa kwa nguvu zote, hichi kitabu hakina nia ya kuwaelimisha watanzania kuhusu wapambanaji na waasisi wa TANU bali kinajenga hoja ya kipuuzi ya udini, nadhani unasahau kuwa hao wote walikuwa wanaanzisha vuguvugu la kupata chama cha siasa kitakachoweza kuikomboa nchi yetu na hatimaye kupata uhuru, na sio jumuiya ya dini ya kislamu, na inawezekana kabisa hao wazee wote walimleta nyerere kuwaongoza ili kiweze kupatikana chama cha siasa na sio jumuiya za kidini kama mzee sykes na wenzake walivyoanzisha huko nyuma, usisahau kuwa nyerere alikuwa msomi wa kwanza wakati huo ndo maana walimuhitaji to put things together ili kuwa na chama cha siasa chenye malengo ya kupigania uhuru! wakati akina syskes na wenzake walikuwa hawajui waanzie wapi? na ndugu yangu hata katika kila taaasisi, familia, kampuni, nchi, jumuiya au chama jambo lolote zuri likitokea anaepata credit huo ni kiongozi wa jahazi hilo, hivyo acha wivu wa kijinga kuwa mpaka messenger unataka apewe credit! seriously tunatambua kuwa nyerere alikuwa ndio mtu aliweza to put things together mpaka TANU ikazaliwa na hatimaye tukapata uhuru lakini hakuwa peke yake kuna watu wengi aliokuwa nao ambao waliweza kufanikisha kuundwa kwa TANU na hatimaye kupata uhuru na wote hao walikuwa wanapambana na kujitoa kama watanganyika na sio waislamu. KUNA MACHIFU MBALIMBALI AMBAO WALIKUWA NA JITIHADA ZA KUPAMBANA NA WAJERUMANI, NCHINI KOTE sio DAR ES SALAAM pekee! hivyo basi uhodari wa mwalimu Julius Nyerere kuunganisha nguvu hiyo ndani na njee ya nchi ndio viliweza kuzaa matunda, ya uhuru.
Tuache masuala ya kuandika vitu ambavyo havina tija kwa Taifa letu kwa misingi ya kuinua dini flani, sio ukristo wala uislamu, mapambano yalikuwepo kabla ya ukristo wala uislamu! na waliokuwa kwenye harakati za awali sio wakristo wala waislamu pekee yao, hata wapagani walikuwemo lakini wote walikuwa watanganyika. sasa hizo historia za udini za kuchongwa zinatoka wapi? na kwa taarifa yako hiyo nyumba ya mtaa wa ndanda mission kota mimi nilikwisha wahi kuishi hapo! sasa hivi mama Rupia anaweka investment ndo maana inatakiwa kubomolewa! na suala la nauli ya nyerere kwenda UN kuhutubia umoja wa mataifa alitoa MAREHEMU JOHN RUPIA na sio jumuiya ya waislamu kama ulivyopotosha! na ndio maana mzee Rupia alinunua nyumba hiyo kwa sababu alikuwa tajiri mkubwa kipindi hicho kutoka usukumani maeneo ya magu! na vugu vugu lote hilo chimbuko la kuanzisha vyama vya kisiasa lilianzia Tabora school ambayo ilikuwa inaitwa ST. MARYS hapo awali ambao akina kassela bantu, nyerere, kawawa, kasanga tumbo, fundikira ndipo walipokutana kama wasomi na watoto wa machifu, mzee hicho kitabu chako ni hadithi tu za sungura mjanja umeacha facts nyingi ambazo zipo na watu wengi waliokuwapo na kushuhudia bado wapo lakini kwa sababu ulikuwa na lako jambo la udini then ukaamua kupuuzia facts zote na kuandika manyanga ambayo mtanzzania yoyote hawezi kuelewa swala la uislamu badala ya utanganyika uliokuwepo!
 
Hizi ni video za muhadhara wa Sheikh Mohamed Said alioutowa UDSM kwa MSAUDI. Natumai utafaidika nazo kwa kujuwa historia ya Waislamu Tanganyika.


*Uislamu Tanganyika 5*
Viongozi wa TANU walizungumza maandishi ya Mohamed Said na wakataka kuchukulia hatua kali. Lakini Nyerere alikataa ili asipewew Mohamed umuhimu na umaarufu.
Katika miaka ya 1950, jiji la Dar-es-Salaam lilikua na la Waislamu. Hata mabibi wa Kikristo walikua wakivaa mabuibui, kivazi cha Waislamu.

YouTube - ‪Waislamu Tanganyika 5.flv‬‎
Hapa ndio nasema mtu anaweza kusoma sana lakini kama akili yake imejazwa kutu ya udini , si rahisi mtu huyo kuwa ameelimika.Anatazama kila kitu katika miwani aliyovalishwa ya udini.Rahisi mtu huyo kuvalishwa mabomu na kuangamiza wengine huku akifiri anatenda mema kwa aliyemtuma.
Hivi kuna vazi la kiislamu?
Kuna vazi la mashariki yakati linalovaliwa na waarabu na wayahudi vilevile.
Kwa hili naona mtu aliyevalishwa akili ya kufikiri vile dini yake inavyo mtuma.
Huyu M Said asichangaye itikadi ya kiarabu an dini ya kiarabu.Kuna waarabu wengi tu wakristo wanaovaa kwa mila na desturi hiyo.
Hii inaonyesha jinsi mtu alivyo pakwa kiitikadi na kutoweza kupambaniua sawasawa argument yake na kuiweka bayana.Ni suala lile lile la mtu aliyesoma sana , anajua ukweli lakini akili imepindishwa kukidhi matakwa ya uongo.
 
Why do we want to use religion to separate us? Hawa watu wengine ni wanyonge kwa ndani na haya mafundisho ambayo wanayatoa kwa jumla jumla kwamba dini moja ndio ilikuwa kinara kuliko nyingine ni manifestation ya unyonge huo. Sasa kwa nini dini hiyo haikuchukua madaraka? Sababu iko wazi...suala la uhuru halikuwa ni suala la kidini...lilkuwa ni suala la watanganyika wote.
Maneno na hoja wanazozitoa leo zinafanana na hadithi ile ya jinsi dua za kuku zisivyoweza kumpata mwewe.
 
CCM ya leo imejaa mafisadi sidhani wana hamu hata ya kuchambua historia yao. Wangefurahi zaidi kama jina la Nyerere lingesahaulika Tanzania.

It clicks now in my mind...this could be the motive, Jasusi
 
Hayo ya Mohamed Said sio mapya tangu kitabu chake hicho kilipochapishwa!

Ni lazima huyo Mohamed atambue kuwa huwezi kuandika historia ya nchi kupitia “biographical methodology of an individual - simply put: a history of a country is more than an individual person’s biography!

Kwa nini akina Mohamed Said & Co hawakuyasema hayo wakati Nyerere na waasisi wengine wakingali hai?

Kwa nini wasimwulize Mzee Patrick Kunambi, ambaye alishawahi kukana madai ya Abdulwahid Sykes?

Mara, Oh, Nyerere alitekeleza Waislamu...mbona Nyerere huyo ndiye alitoa ubaguzi wa rangi mashuleni hata kabla ya uhuru?

Sisi wengine tuliwahi kwenda shule kama hizo za serikali wakati watoto wenzetu Waislamu wazazi wao waking’ang’ania kuwapeleka madarasa!

Hivi kwa nini tusi-transform our time into other constructive and productive ends rather than to continue dwelling on (or regurgitating) non-starter issues raised by Mohamed Said?
 
Ndo maana mimi ktk reply yangu ya mwanzo niliomba wataarishaji wa Lecture (mhadhara) pamoja na Dr. Mohamed Said, wangetoa mwaliko kwa 'umma' wote wa vijana wanafunzi hapo UDSM wahudhurie, maana penye mchanganyiko wa 'wengi' kama hapa JF hapakosi 'msisimko' kama aliokuwa anautoa Dr. Mohamed Said kwa maprofesa wake akiwa mwanafunzi miaka hiyo akiwakumbusha kuna zaidi ya Nyerere kama kina Sykes, Rupia, Mtamila, Tsere, Karimjee n.k.

Hakika JF imeleta msisimko kwa ku-challenge point of view ya 'mtoto wa mjini' al-waatan Dr. Mohamed Said mpaka majina ambayo siyo ya Kiislamu yakajitokeza ktk harakati za vuguvugu la kupanga mikakati ya kumngoa mkoloni iwe msikitini, vijiwe vya mtaani, jumuia za kisomi au ma-veterani wa vita kuu ya Kwanza na Pili za dunia.
 
WELL,going through all this,i feel like having been hit by a bolt of lightning-totally confused,future generations will demand answers. what left me astounded is "hata mabibi wa kikristo walikuwa wanavaa mabuibui"
 
I was under the impression that independence was brought about by like minded individuals who got together regardless of ther race, gender, religion or tribe. The struggle for independence of Tanganyika was just that....for Tanganyika and Tanganyikans. Starting to break down the demographics of who did what seems to be in contradiction to what was meant to be achieved.

I can not claim to be an expert of the history of the independence struggle. But if i remember correctly when learning the history of the struggle for independence I was taught the names of the people and what they did. I was never told their religion and with the mind of a child neither did I even consider trying to look at the religion of these people.

Now you can present history in any way you want ti. You can look at what role individuals of a certain religion, tribe or gender played or you can look at their collective efforts. Today writing something claiming the part Muslims played in the struggle for independence is asking for special recognition of the religion and it's role. And to be honest it's funny that thus far I'm seeing the history of Muslim players within the TANU movement. So if it's history we are seeking then why I'm I only hearing about TANU? What about the parts other parties and groups played? But you have decided to take the history of only the winning factions of the struggle for independence and micro scoped it to see who in your religion did what.

So I'm sorry but I don't believe that religion had any part to play in the independence struggle. I believe it is people who played a part and those people had their own religions, their own tribes and their own genders. People got together as was convenient. If Muslims or Christians got together it is because it was easier for them to form a primary group but religion did not dictate their thirst for independence.
 


Hizi ni video za muhadhara wa Sheikh Mohamed Said alioutowa UDSM kwa MSAUDI. Natumai utafaidika nazo kwa kujuwa historia ya Waislamu Tanganyika.
*Uislamu Tanganyika 5*
Viongozi wa TANU walizungumza maandishi ya Mohamed Said na wakataka kuchukulia hatua kali. Lakini Nyerere alikataa ili asipewew Mohamed umuhimu na umaarufu.
Katika miaka ya 1950, jiji la Dar-es-Salaam lilikua na(ni?) la Waislamu. Hata mabibi wa Kikristo walikua wakivaa mabuibui, kivazi cha Waislamu.

YouTube - ‪Waislamu Tanganyika 5.flv‬‎


Bado nalazimika kurudi katika kipengele hiki ambacho factually it is incorrect and is based on heresay or outright lies-UONGO!
UONGO ukirudiwa rudiwa sana hasa kwa watoto au vijana ambao wanapokea uongo huo na kuuamini, wanaweza kufikiri kuwa ni ukweli kumba sivyo.
Jiji la Dar es salaam pamoja na kupewa jina hilo na waarabu halijawahi kuwa jiji la kiislamu kama Mohammed Said anvyopenda kueleweka.
Yeye anasema miaka ya 1950's jiji lilikuwa la waislamu, sasa tujiulize , baada ya uhuru waislamu wote walikufa?
Au serikali mpya ya kiafrika baada ya uhuru ilipiga marufuku uislamu jijini Dar es salaam.
Ni dhahiri kuwa majibu ni hapana.

Mimi nimebahatika kufika Dar es salaam muda mrefu kidogo, toka miaka ya 60 baada ya uhuru.
Hayo anayoeleza, miaka hiyo sikuiona achilia mbali wale waliokuwa wakivaa baibui kama utamaduni wao unavyowaagiza.
Ningemuuliza basi swali la ziada Mohammed Said kama itikadi za "hata mabibi wa kikristo kuvaa baibui, kivazi cha waislamu" nacho kikapotea na ukoloni?
UONGO unapoanza kuwa dhahiri unakera kidogo.
Je? kutoka miaka ya 1950's hadi 1960's tabia za watu wa dar es salaam zikabadilika kabisa? kutoka za kiislamu kuwa za kitu kingine?
Mimi nilikaa mitaa ya waswahili kabisa huko TEMEKE.Mzee Mtemvu alikuwa jirani na watoto wake tumesoma pamoja.
Hayo Mohammed Said anayoongelea katika mada zake ni ya kudhania ili tu kuupa umaarufu udini wake.
Siwezi kujua, lakini mtu wa aina hii yuko programmed ili kuona kila kitu katika miwani ya yule aliyemprogramme.
Sasa kwa nini UONGO huu unarudiwa rudiwa ili uonekane ukweli?
Mwaka 1986 nilifika Uingereza kwa kozi ya mwaka mmoja.Kati ya marafiki zangu mmoja alikuwa mu Iran.Alinishangaza sana siku moja kwa kutamka hadharani kuwa Tanzania ni nchi ya Kiislamu.Nikamwuliza source na akatoa kitabu kilichoandikwa na taasisi moja ya kiislamu ikiwa imezionyesha kijani nchi zote za "kiislamu", Tanzania ikiwa moja wapo.
Nikamtolea official Goverment statistics nilizokuwa nazo pamoja na paphlets za TTC(Tanzania Tourists Corp) na kumpa ukweli kuwa Tanzania hatuna dini katika serikali wala siasa.Ikwa zamu ya rafiki yangu huyo mu Iran kushangaa kitabu chake kwa kusema UONGO.
Inaelekea Mohammed Said is part of a wider campaign ya kueneza na kupandikiza uongo ili tukujenga hisia za dini yake.
Lakini namshauri kuwa kueneza dini vyema misingi ya UKWELI lazima iheshimiwe.
 
Mwanafalsafa1,
Nimemsoma sana Mohammed Said kuhusu uasis wa TANU na juhudi za uhuru wa Tanzania ziliasisiwa na Waislamu. Kwa mujibu wake, Nyerere alipochukua madaraka aliwasahau na kuwatekeleza Waislamu waliomkaribisha Dar-es- Salaam na kwenye TANU. Anakubali kuwa Waislamu walikuwa nyuma kielimu kwa sababu ya sera za ukoloni, lakini hakiri kuwa Nyerere alijaribu kurekebisha kasoro hizo. Jinsi ninavyomsoma nadhani theme yake ni kwamba kwa sababu Waislamu "walianzisha" harakati za uhuru, walistahili kuwa na bigger share of the national cake kuliko ilivyo hivi sasa, na wakristo wamechukua nafasi zote za juu nchini wakati kulikuwa na hujuma za makusudi kuzuia Waislamu wasiendelee kielimu. i.e kufutwa kwa EAWMS mna Jamat Islamiya. So this is a call to Moslems to bring about a true liberation.
 
CCM ya leo imejaa mafisadi sidhani wana hamu hata ya kuchambua historia yao. Wangefurahi zaidi kama jina la Nyerere lingesahaulika Tanzania.

It clicks now in my mind...this could be the motive, Jasusi


Watu kama huyu Sheikh Mohamed Said ni watu wa hatari kweli kweli kwani kauvaa udini kama shati. Kila kitu kwake kinaangaliawa kwa macho ya Udini na yawezekana wanatumiwa bila kujua kwani mapungufu na machafu ndani ya Uongozi wa sasa hayawezi kufuliwa kwa kulichafua jina la Mwalimu Nyerere. Walivyokosa adabu kuna wengine wanaanza kuhoji hadi uamuzi wa Mwalimu Nyerere kumtoa Nduli Idi Amin ardhini kwetu kwa kumpa kipigo - kisa ? Udini. Sheikh Mohamed Said ametanguliza Udini mbele ya Utaifa - this is sad, really sad.
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom