Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
LG: Napenda uzingatie hili. Mimi humu ukumbini sihitaji ku-convince yeyote kuhusu nielezayo. Mimi hapa naeleza historia ya wazee wangu vipi walianzisha mapambano dhidi ya ukoloni na yote muhimu yaliyotokea wakati ule, mengi ambayo hayakuwa yakijulikana na wengi. Ni hivyo tu.

Sidhani kwa kufanya hivyo kutakuwa na kushinda au kushindwa. Hivi anetoa vipande nani hapa? Ni mimi niliekuwa na vitabu nilivyoandika na papers au wewe unaesoma kazi zangu?

Unapoandika usiache moyo ukatawala kichwa chako. Kama unataka kuwa msomi bingwa jitulize na jifunze adabu ya ilm. Utakuwa msomi makini, wakupendeza na kila mtu akiona jina lako atataka kukusoma kwa kuwa ana hakika atafaidika.

William Shakespeare anasema: "There is a tide in the affairs of men taken from the flood will lead on to fortune..." malizia ujumbe wako uko hapo mwisho la huwezi mtafute mjuzi akueleze au wanaukumbi wakusaidie.

Huku ndiko kusoma. Naona tuanze taratibu mimi na wewe kusomeshana. Nafanya haya yote kwa kuwa nakuona una juhudi lakini zinahitaji kuelekezwa na kuongozwa.
 
FM: Naogopa hata kukuambia maana ungekuwa umesoma kitabu hayo usingeyaleta hapa ukumbini. Ungesoma jinsi Salum Mpunga na Yusuf Chembera kutoka tawi la TANU Lindi walivyoivunja ngome ya Wamishionari Songea na pembezoni mwake mwaka 1956...................

Hili ni moja ya tatizo lako KUBWA ndugu yangu Mohamed Said.............ninaweza kuwa pamoja na wewe.....lakin nikiangalia nje ya box nakuona wewe ni Mbaguzi...........katika mahitimisho yako watu wana/tunakuangalia kwa mtizamo kama huo hapo juu............chuki yako dhidi ya wamisionari.............

............Hawa ni watu wa bara tena bara kubwa kabisa. Chembera alikuwa mwanafunzi wa Sheikh Yusuf Badi na sheikh ndiye aliyeandika hotuba ya kupokea uhuru Lindi na hotuba ile ilisomwa na mwanafunzi wake Yusuf Chembera mbele ya DC Mkoloni. .

Kumuandikia hotuba kiongozi mbona ni jambo la kawaida...........wengine wako wanafanya kazi nchi za watu na wanaandikia hotuba (kuhusu miradi ya maendeleo) viongozi wa nchi ambayo wao si raia..........hivyo ni vitu vya kawaida sana...............

..........Sema utakavyosema lakini kuitoa TANU mikononi mwa wazee wetu huo ni muhali mkubwa na wenyewe walitaka kabla hawajafa hilo tulijue........................
Hakuna aliyekatazwa kuandika/rekebisha historia kama ilivyoandika..............kuna mahali umesema............ilm sio static ni dynamic..........kwenye historia kila siku watu wanafanya utafiti wanaandika/rekebisha kulingana na facts.......na watu tumekupa KUDOS kwa hilo bila hiana................tatizo lako linakuja pale unapotaka kuonyesha Kikundi fulani pekee ndio kilichangia sana/kuanzisha ukombozi wa Tanganyika na hasa wazee wetu wa Kiislam..............tena uache kufuru kwa kuwaongelea wazee wetu maneno ya uongo..............kuwa walikupa barka ulete ubaguzi wa kidini.......wakati wao hayo mawazo si ya kwao.............japo kwa kuangalia juhudi zao za kulijenga/kulikomboa Taifa................

CCM ndiyo pata mpatae yaani ya wote jumla jamala. Katika kuasisiwa kwa CCM Nyerere anachukua alama mia kwa mia.

CCM ni yake khasa wala hana mpinzani. Tumsifie kwa hilo..

Kama anavyokuleza Fundi Mchundo UNARUDIA MAKOSA ya kuona kosa kwa mwenzako lakini unachoandika wewe hapo juu huoni kuwa ni kosa lile lile............ndio maana nikasema its funny..............hapa chini

Duuuhh sasa..............this is funny

Ogah: Ingekuwa bora laiti ungesema kitu. Au wewe waonaje? Au ungesema kwa Kiswahli hiki ni kichekesho ingekuwaje? Mimi si mjuzi wa Kiingereza nionee huruma.

Uzuri hapa JF ukitia neno tu watu watakujibu/kukupongeza/kutofautiana/kukanusha...............inategemea na ukweli wa jambo unalozungumzia na facts utazo-present.............kwa hiyo hapa JF watu hupeana DARSA.........its a two way traffic (nimekuonea huruma kidogo wee mjuzi wa Kimanyema)
 
Ogah: Hahahahaha! Wamanyema sisi kwa ubishi hautuwezi. Jamaa wawili wa Kimanyema wako Magomeni Mapipa wanashindana ile picha ya simba wa Agip ina miguu mingapi? Mmoja kasema kumi na mbili mwenzake kasema kumi na sita. Agip iko Swahili na Morogoro Road. Imebidi wachukue daladala hadi pale wakaenda kuhesabu miguu. Jamaa aliyeshindwa akasema kwa ile lafidhi yetu, "Eee bwana umesema kweli."
 
Ogah: Iko siku Mungu atatujaalia tukajuana Insha Allah. Utanijua kama mimi ni mbaguzi au la...kubagua ni mwiko katika mafunzo yetu.
 
Uislamu wao unaingiaje hapa katika jitihada yao ya kugombea uhuru? Walipigania uhuru kwa sababu walikuwa ni Waislamu au kwa sababu walikuwa ni wazalendo waliotaka kumwondoa mkoloni? Suala hili linahusu Wakristo pia waliokuwa mbele pamoja na Waislamu kugombea uhuru.

Ikiwa sababu ni kwamba walikuwa ni wazalendo, kuna haja gani ya kutaja dini badala ya kusema Watanganyika tu? Ikiwa kuna umuhimu wa kutaja dini zao, Ukristo na Uislamu, tajeni pia makabila yao.

Tutaishia wapi? Tunaweza pia kusema "Wachaga na Elimu Yao ya Juu Katika Ujenzi wa Taifa Kuliko Makabila Mengine."

Halafu watakuja Wahaya, Wanyakyusa na wengine na elimu yao.

Tusiwasahau Wakerewe kama Mkandara anavyotukumbusha kwamba ni kati ya makabila yaliyopata elimu ya juu kuliko makabila mengine.

Tusiwasahau pia Wanyasa. Wengi wao walipata elimu kabla ya makabila mengi nchini Tanganyika na walipata kazi mbali mbali kwa sababu ya elimu yao.

Tutaje makabila hayo tunapozungumzia maendeleo katika nchi yetu na tuseme ni Wachaga, Wahaya, Wanyakyusa, Wakerewe, na Wanyasa waliochangia kuliko makabila mengine kati ya makabila 126 nchini Tanzania, na kabla ya hapo nchini Tanganyika.

Tusisahau ulinzi wa taifa: "Wakuria Jeshini Wanavyo Ilinda Nchi Yetu Kuliko Makabila Mengine."

Tuwashukuru Wakuria kuliko watu wa makabila mengine jeshini.

Madaktari: "Jinsi Daktari Mnyakyusa Francis Mwaisela, Kati ya Madaktari wa Kwanza Nchini, Alivyowatibu Watu wa Makabila Mengine kule Nzega Miaka ya Mwanzoni 1940s."

Si kwa sababu alikuwa ni Mtanganyika na mzalendo, ni kwa sababu alikuwa ni Mnyakyusa.

Ukombozi wa taifa: "Mzanaki Julius Nyerere Kutoka Kabila Dogo Alivyoikomboa Tanganyika Kutoka kwa Wakoloni."

Na kadhalika. Badala ya kusema wazalendo wa Tanganyika, na baadaye, wa Tanzania.

Pia hao wote hawakuwa peke yao hata mwanzoni.

Ukiangalia jithada ya kugombea uhuru, hata kabla ya TANU na Tanganyika African Association kuanzishwa, kulikuwa na watu katika kila kabila, kila wilaya, na kila jimbo waliokuwa wanatetea na waliokuwa wanagombea haki za Mwafrika.

Wakumbukeni hata akina Mkwawa, Mirambo na wengineo. Kumbukeni pia Maji Maji.

Haikuwa ni kwa sababu ya dini zao au makabila yao. Walikuwa wanapambana na ukoloni. Hakukuwa na TANU au Tanganyika African Association miaka ile.

Acheni udini na kuwatenganisha wananchi kwa ubaguzi wa aina yoyote.
 
Nilisikia historia ndefu ya TAA Hadi TANU ikitolewa kwenye chombo kimoja Cha habari nchini na mmoja ya mtu aliejitambulisha ndie alimpokea baba wa Taifa TABORA na kumkabidhi Duka auze hUKO TABORA. na alisema mzee huyo kwamba baba nyerere alijiunga TAA mwaka 1952 miaka miwili kabala ya chama hicho kuunagana na TAA. jee kabala ya hapo nani waliokuwa viongozi wakuu wa TAA?
 
Mkuu
Tumewasahau majina yao na hakuna kumbukumbu yoyote inayoonesha kuwa kulikuwa na viongozi hao kabla. Kama umezikuta sehemu kumbukumbu hizo, tumwagie hapa na sisi tuwajue..... Au yeyote anayewajua...sisi tunajua ni Nyerere tu.Ndiye kiboko yetu watz.
 
Nilisikia historia ndefu ya TAA Hadi TANU ikitolewa kwenye chombo kimoja Cha habari nchini na mmoja ya mtu aliejitambulisha ndie alimpokea baba wa Taifa TABORA na kumkabidhi Duka auze hUKO TABORA. na alisema mzee huyo kwamba baba nyerere alijiunga TAA mwaka 1952 miaka miwili kabala ya chama hicho kuunagana na TAA. jee kabala ya hapo nani waliokuwa viongozi wakuu wa TAA?

Ndiyo Muhogomchungu, historia imepindishwa duniani kote, mfano mvumbuzi wa Amerika hakuwa Chris Columbus bali Omar bin janjaweed al marghrib, binadamu wa kwanza kukanyaga mwezini hakuwa mwamerika ni Mukhtar ibn twaeeb al shabab aliyezaliwa yemen, hata mtu wa kwanza kutamka kuwa dunia ni duara siyo Galileo bali alikuwa Muhammed al madina raia wa saudi arabia. Ukirudi hapa kwetu bongo utaambiwa kuwa raisi wa kwanza wa Tanganyika alikuwa Nyerere badala ya mheshimiwa mtukufu alhaj Ali Hassan Mwinyi. Kwa kweli upotoshaji huu wa historia wa maksudi hautendei haki sisi waungwana wapenda amani, ndo sababu tunalazimika kujitoa mhanga kwa kujiripua ili tupate haki yetu.

Wasalaam
 
Big up mkuu,ila mwenze2 umepata historia hizi kutoka ktk vtabu gani?tuambie nac tuwenavyo tumechoka kupwagwa....na Raisi wa kwanza wa Tanganyika kama alikuwa Alhaj A.H.Mwinyi,je? Nyerere alikuwa Raisi wa kwanza wa Nchi gani. Nitashukuru kwa majbu yako.
Ndiyo Muhogomchungu, historia imepindishwa duniani kote, mfano mvumbuzi wa Amerika hakuwa Chris Columbus bali Omar bin janjaweed al marghrib, binadamu wa kwanza kukanyaga mwezini hakuwa mwamerika ni Mukhtar ibn twaeeb al shabab aliyezaliwa yemen, hata mtu wa kwanza kutamka kuwa dunia ni duara siyo Galileo bali alikuwa Muhammed al madina raia wa saudi arabia. Ukirudi hapa kwetu bongo utaambiwa kuwa raisi wa kwanza wa Tanganyika alikuwa Nyerere badala ya mheshimiwa mtukufu alhaj Ali Hassan Mwinyi. Kwa kweli upotoshaji huu wa historia wa maksudi hautendei haki sisi waungwana wapenda amani, ndo sababu tunalazimika kujitoa mhanga kwa kujiripua ili tupate haki yetu.

Wasalaam
 
Ndiyo Muhogomchungu, historia imepindishwa duniani kote, mfano mvumbuzi wa Amerika hakuwa Chris Columbus bali Omar bin janjaweed al marghrib, binadamu wa kwanza kukanyaga mwezini hakuwa mwamerika ni Mukhtar ibn twaeeb al shabab aliyezaliwa yemen, hata mtu wa kwanza kutamka kuwa dunia ni duara siyo Galileo bali alikuwa Muhammed al madina raia wa saudi arabia. Ukirudi hapa kwetu bongo utaambiwa kuwa raisi wa kwanza wa Tanganyika alikuwa Nyerere badala ya mheshimiwa mtukufu alhaj Ali Hassan Mwinyi. Kwa kweli upotoshaji huu wa historia wa maksudi hautendei haki sisi waungwana wapenda amani, ndo sababu tunalazimika kujitoa mhanga kwa kujiripua ili tupate haki yetu.

Wasalaam
Mkuu,
Hii yako kali. ulikuwa na hasira na umetumia kejeli ulipoandika mchango wako. tafadhali ukijirudi edit kwa faida ya kuendeleza mjadala kwa faida yetu sote.Kuna wengi wanaotaka kufahamu mambo ya historia ya nchi yetu.
 
mwenyekiti wa TAA alikuwa ni Abdulwahid sykes....

Nyerere alijiunga na TAA akiwa TABORA SCHOOL NA Hamza mwapachu
 
Mwanzilishi ni Kawawa alikuwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi na ndiyo kikawa. Lakini walikuwa wanamtafuta mtu ambaye ni msomi na ataweza kuwawakilisha na ndiyo wakampata nyerere.
 
Abdulwahid Sykes alikuwa msomi hasaa,lakini baada ya nyerere kuunganishwa na wazee Mashekhe wa TAA wazee walimkubali kwa kigezo kimoja tu kuwa chama kionekane kinausawa wa kidini. Waliamua kumtuma UNO kwa michango wa Waislam misikitini hadi nauli ikatosha na yeye akaahidi kutokuwaangusha Waislam baada ya mafanikio ya kupata uhuru.Walimpa uongozi kwa kua walitaka umoja wa mataifa wajue kuwa wote Waislam na Wakristo wa Tanganyika wanataka Uhuru kwa pamoja,ila kumbuka safu yote ya wapigania uhuru ni Waislam.Baada ya Uhuru Nyerere aliwasaliti waislam na kukichukua kikundi kidogo cha vibaraka wapenda ubwabwa ili kuudidimiza Uislam na hapa Mashekhe wengi walitiwa kizuizini na wengine kufukuzwa nchini.Wapigania uhuru wengi wamekufa bila heshma zozote na wengine bado wapo ila ni wazee sana pamoja na yote hayo wazee wote hawatajwi na historia hata kidogo'huu ni wizi wa historia'.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom