Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
Nashkuru kwa waliotoa maoni na mapendekezo kuhusu Mohamed Said,nitamfikishia kwani nimewahi kumuona katika msikiti wa Ibadhi Br.12 anapendelea kuswali swala za Maghrib na Isha.

Nina azma ya kutaka kufanya mahojiano nae ili aweze kunieleza wapi tutapata vitabu kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya vizazi vijavyo hasa kitabu hiki "The life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968): The untold story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika". Nikipata nakala yake nitawaarifu juu ya upatikanaji wake.

Mbali ya hayo sikiliza mahojiano yake na radio presenter wa Radio Butiama iliyoko columbas Ohio na unaweza kufuata linki hii kwa ajili ya kwenda kudowload PodOmatic | Podcast - Radio Butiama - Mahojiano na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili - Voice of America. Nimejaribu kuiweka hapa ila file ni kubwa about 17.2MB
 
Kwani walikuwa wanatafuta uhuru wa waisalamu au wa Watanganyika?...mbona hiyo Tanganyika African Association (TAA) ya 1920 haikuitwa Tanganyika Moslem African Association (TMAA) ?
 
Kwani walikuwa wanatafuta uhuru wa waisalamu au wa Watanganyika?...mbona hiyo Tanganyika African Association (TAA) ya 1920 haikuitwa Tanganyika Moslem African Association (TMAA) ?

Sikiliza mahojiano ya Mohamed Said na Radio presenter wa Radio Butiama utapata jibu lako na hata kama una maswali mengine utapata majibu yake.
 
Sikiliza mahojiano ya Mohamed Said na Radio presenter wa Radio Butiama utapata jibu lako na hata kama una maswali mengine utapata majibu yake.

Sihitaji kusikiliza...hainisaidii chochote...na wala haikusaidii wewe zaidi ya kuku-confuse zaidi
 
Sihitaji kusikiliza...hainisaidii chochote...na wala haikusaidii wewe zaidi ya kuku-confuse zaidi

Don't be stubborn...................you will come to know something. Haija ni confuse ila nimeelewa kuwa kuna mambo muhimu sana yameachwa katika historia ya nchi yetu ambapo ni haki ya kila mtu kujua ukweli halisi.
 
Sikiliza mahojiano ya Mohamed Said na Radio presenter wa Radio Butiama utapata jibu lako na hata kama una maswali mengine utapata majibu yake.

Jibu swali mkuuu hapo nawe unapoteza manti nzima ya Uhuru kabisa ive nawe kwa hakili yako Uhuru wa nchi waujumlisha na dini kweli?? kwahiyo wewe una suggest udi uwepo katika serikali?Au

Wewe ni mzalendo kweli au ni mtanzania basi tu mtanzania tofautisha DINI na SIASA tafuadhali, mtu yeyote atakae ingiza Dini ndani ya SIASA ni maskini wa mawazo kabisa anataka kuupotosha UMMA. kweli MUNGU unamwingiza kwenye mambo ya siasa??

Kwani walikuwa wanatafuta uhuru wa waisalamu au wa Watanganyika?...mbona hiyo Tanganyika African Association (TAA) ya 1920 haikuitwa Tanganyika Moslem African Association (TMAA) ?

Mleta mada iabidi ajibu maswali haya kama mtu mwenye kichwa kinachofanya kazi.
Ukiweza kujibu maswali ya kimsingi kama hayabasi unaweza kuhesabika kama mtu mwenye akili timamu.
La sivyo mawazo ya huyo Mohammed Said ni ya kijinga na kuleta machafuko at best.
Tusiibadilishe historia kwa kudonoa vipendele vinavyo kupendelea.Harakati za ukombozi wa Tanzania hazikuanza na waislamu.Mkwawa alikuwa babu yenu?au Isike Meli na wengine?
Harakati kabla ya uhuru zilianza baada ya vita kuu ya pili.Mjomba wangu mimi alikwenda Burma na Misri na Beghazi.
WaTangayika wa wakati huo ndio waliorudi na kusimuliaweakness za mzungu na alivyokuwa akitoa uharo kutokana na kipigo cha mzungu mwenziwe.Hii iliwapa nguvu kuwa mzungu hana lolote zaidi ya mwafrika.Hii nimesumuliwa na mjomba wangu ambaye ana miaka karibu 90 na yuko hai hadi leo!
Mawazo ya kijinga kama ya huyu Mohammed Said yatashabikiwa na wajinga weziwe.
 
Jibu swali mkuuu hapo nawe unapoteza manti nzima ya Uhuru kabisa ive nawe kwa hakili yako Uhuru wa nchi waujumlisha na dini kweli?? kwahiyo wewe una suggest udi uwepo katika serikali?Au

Wewe ni mzalendo kweli au ni mtanzania basi tu mtanzania tofautisha DINI na SIASA tafuadhali, mtu yeyote atakae ingiza Dini ndani ya SIASA ni maskini wa mawazo kabisa anataka kuupotosha UMMA. kweli MUNGU unamwingiza kwenye mambo ya siasa??

Kwanza si swala la kuchanganya dini na siasa ila ni kufahamu ukweli juu ya Historia ya nchi hii.

Pili Mwalimu hasa ndio alichanganya dini na siasa,hii imeonekana wazi baada ya yeye kuingizwa TANU.

Tatu kwa itakadi za kiislamu huwezi kutenganisha dini na siasa,vyote vinakwenda pamoja.
 
Mleta mada iabidi ajibu maswali haya kama mtu mwenye kichwa kinachofanya kazi.
Ukiweza kujibu maswali ya kimsingi kama hayabasi unaweza kuhesabika kama mtu mwenye akili timamu.
La sivyo mawazo ya huyo Mohammed Said ni ya kijinga na kuleta machafuko at best.
Tusiibadilishe historia kwa kudonoa vipendele vinavyo kupendelea.Harakati za ukombozi wa Tanzania hazikuanza na waislamu.Mkwawa alikuwa babu yenu?au Isike Meli na wengine?
Harakati kabla ya uhuru zilianza baada ya vita kuu ya pili.Mjomba wangu mimi alikwenda Burma na Misri na Beghazi.
WaTangayika wa wakati huo ndio waliorudi na kusimuliaweakness za mzungu na alivyokuwa akitoa uharo kutokana na kipigo cha mzungu mwenziwe.Hii iliwapa nguvu kuwa mzungu hana lolote zaidi ya mwafrika.Hii nimesumuliwa na mjomba wangu ambaye ana miaka karibu 90 na yuko hai hadi leo!
Mawazo ya kijinga kama ya huyu Mohammed Said yatashabikiwa na wajinga weziwe.

It is very simple,sioni sababu ya watu kutosikiliza mahojiano ya Mohamed Said na Radio presenter wa Radio Butiama. Mahojiano yalikuwa mazuri na kulikuwa na maswali ya msingi sana ambayo yote yamejibiwa. Still mtu hataki kusikiliza ana demand apewe majibu what's is this????
Especially swali analoliuliza halina msingi zaidi ya maswali aliyouliza Radio presenter ambayo alipewa majibu yote.

Tuwe wastaarabu jamani..............
 
Utumbo mtupu uhuru wa Tanzania ulipiganiwa na wananchi wote wa wakati huo kwakuwa walikuwa na sababu za kupigania uhuru.Mtemi mirambo,mangi meli,Mkwawa na machifu wengine wengi hawakuwa waislamu kama mleta mada anavyotaka kutupotosha.
 
Ishu si kutafuta uhuru wa waislamu au wakristo ndio maana akina bibi Titi walimkubali Nyerere wengine walipokuwa na mashaka nae ishu ni kwa nini historia iliyoandikwa na wanayofundishwa watoto haisemi ukweli juu ya jambo hili? Maana tunajua mawakala moja ya mawakala wa ukolono ni dini na pia tuambiwe basi hata katika kupigania uhuru dini pia ilitumika na ielezwe mchango wake maana inavyoonekana kuna kama vile kuna kundi fulani lilikuwa la wajinga na walikaa pembeni hawajui la kufanya, hawakupata elimu ndio maana mpaka leo wako nyuma na kundi lingine wao ndio walikuwa msitari wa mbele na wao ndio walikuwa wengi serikalini wakafanya ufisadi na kujiimarisha mpka leo familia zao zipo katika werevu na wengina awle katika ujinga. Tuichukulie mada kwa kuangalia taswira iliyipo na si kuwa fanatics
 
Angalia kuna hoja hapa kuwa hiyo bakwata imeamriwa isogeze mbele siku za kufunga ili sikukuu iangukie jumamosi na jumapili kama itavyokuwa kwa x-mas. ONA SHEIKH WA BAKWATA ANAITWA TBC AKAELEZEE SULA HILO ANAANZA KUUOMBEA UCHAGUZI.
 
Domokaya ondoka kwenye box la dini akili zitakurejea
 
kaka

naomba niulize swali moja kama hao waislamu walikuwa mashujaa na werevu kama unavyotuimbia leo iweje tena CUF hawana mwelekeo wowote hapo Tanganyika. Hizi fikra zakutaka kujifanya kundi fulani 'machi-nowa' kuliko wengine sijui mnazitoa wapi?.
 
Mkuu umenena akili zao wanawaza zaidi maulidi na masufuria ya ubwabwa
 
Utumbo mtupu uhuru wa Tanzania ulipiganiwa na wananchi wote wa wakati huo kwakuwa walikuwa na sababu za kupigania uhuru.Mtemi mirambo,mangi meli,Mkwawa na machifu wengine wengi hawakuwa waislamu kama mleta mada anavyotaka kutupotosha.

Tatizo mtu anadandia hoja tu bila ya kupitia source zote zilizowekwa na aliyeweka mada.

Ni kwamba sio kweli kwamba kabila na dini nyingine hazikupigania uhuru wa Tanganyika ila kundi la waliopigania Uhuru wa Tanganyika kwa makusudi haikuandikwa ukweli kuhusu wao na mchango wao kama walivyotoa watu wengine kutoka dini mbalimbali na kabila mbalimbali.

Hii ndio kusudio kuu ya mada hii na si venginevyo.

Kinachotakiwa ni haki na sio upendeleo wa aina yoyote ile. Ila kwa kuwa watu wengine inawauma kuona ukweli ndio utaona analeta mambo yasiyo na maana katika mada hii.
 
History should be used to build a better future!!!!! but Sheikh Mohamed Said's motive is to destroy the national unit.

Mnasahau kuwa wakati huo uislam ulikuwa Pwani tu na miji michache sana ya bara km tabora na kigoma. Na mnasahau kuwa it is the same nyerere who crated unity among yourselves kwa kuwatengenezeaa BAKWATA ili mweze kupenya mpaka huku bara na kuendelea kuilea BAKWATA kwa kuipa ruzuku wakati hakutoa hata kipande cha fedha kuzilea taasisi za kikristo badala yake alizinyang'anya hata taasisi zake (za kikristo) kama hospitali ( muhimbili kwa mfano) shule kama minaki and pugu, all to fever you people. Shame on you!!! you should respect nyerere kuliko hata wakristo wanavyomheshimu.

Because kila kitu lazima mfanyiwe ndiyo maana hata court zenu za kidini (kushughulikia issues za ndoa) mnataka serikali ndiyo iwatengenezee ilhali internal courts za kikristo zinazosimamiwa na wachungaji, mapadre na maaskofu zinazoshughulikia issues za ndoa hazikuanzishwa na serikali.

Kwa hakika naelewa hamaki za wengi hasa wasiokuwa Waislam wanaposoma kitabu changu The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Utold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press 1998, London. Naelewa shida wapatayo halikadhalika wasomapo makala zangu tofauti ninazojitahidi kueleza yale ambayo kwa hakika yamekosewa aidha kwa makusudi au kwa kutokujua kuhusu historia ya TANU.

Naelewa simanzi wanayopata Waislam wanaponisikia katika mihadhara na mazungumzo ya kawaida ninapowaenzi mashujaa wa uhuru wengi wao wakiwa Waislam ambao kwa hila wamefutwa katika vitabu na kumbukumbu za taifa letu.

Ukiachia mbali hayo mjadala huu ungekuwa na maana sana endapo wanaoamua kuzungumza suala hili wangejikita katika mada badala ya kuchanganya mada. Katika kufanya hivyo wangeweza kuhoji yale ambayo wanadhani ni uongo. Hii ingenipa mie nafasi ya kujibu na kusema kile ninachokijua.

Ama kuhusu Mwalimu Nyerere hapana hata mahali ambapo nimemvunjia heshima na wala siwezi kukosa adabu kiasi hicho ila ninalosema ni kuwa kuhusu TANU chama hicho hakuanzisha yeye na nimeeleza kwa kirefu sana jinsi chama kilivyoanza, kuchipua kwake hadi kuwa chama chenye nguvu kabisa. Kama kuna mtu anaona vibaya kwa kuelezwa ukweli huu ni bahati mbaya sana.

Ama kuhusu mambo ya elimu, kuwapo kwa Waislam Tanganyika na wingi wao, Bakwata nk. majibu Alhamdulilah yapo na kama itabidi nitayaeleza Insha Allah.
 
Mbona sijawahi kusoma mahali kokote kuwa uhuru wa nchi hii uliletwa na wakristo? Ama mbona sijawahi kusoma kokote kuwa waislamu hawakua na mchango wowote katika uhuru wa nchi hii? Ama katika wote waliotajwa, mbona sijawahi kusoma maamndiko yeyote yakisema hawakuwa na mchango wowote? Mbona hatusemi labda uhuru wa nchi umepiganiwa na watu wengi ila Nyerere ndo anaonekana kinara peke yake na badala yake tunaingiza hoja ya waislamu na mchango wao kwa uhuru? Kuna ajenda gani ya siri hapa? Acheni hizo bwana!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom