Ukweli kUhusu Mgogoro wa Seif na Hamad Rashid CUF

ASKOFU MSAIDIZI

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
209
23
Nimefuatilia makoa mkuu ya CUF nikagundua kuwa hali ni tete kwani kuna makundi Moja ni la Hamadi Rashid na Jingine ni la Maalim Seif Na kwamba makosa aliyofanya Seifu yamewagusa wengi na hapana Shaka kwamba ameanza kuyarekebisha!!!

Moja ya Mambo ambayo yamekuwa kero kubwa ni suala la pesa ambapo Mgao wa pesa za operations za Makao makuu zilikuwa hazipo Wakati kule Pemba wanatanua kwa kutumia fedha za serikali.

Julius Mtatilo aliwahi kuongea na gazeti la Sema Usikike akaelezea ukata wa fedha ambapo analazimika kutumia fedha zake Mwenyewe kwa ajili ya shughuri za Chama !!!

Mtatilo aliwahi kulalamika kwamba Ruzuku imechelewa lakini ukweli ni kwamba hata Ruzuku hiyo ilipotolewa ilikuwa haipelekwi Wilayani kama sheria inavyotaka!!

Mtu wa karibu na ofisi ya Uhasibu anasema Juzi tu baada ya Hamadi Rashidi kuelezea nia ya kugombea nafasi ya Katibu Mkuu ndipo Maalimu Seif akaamuru pesa zipelekwe kwenye Wilaya 1oo na kila Wilaya imepelekewa 300,000/= katika awamu ya kwanza na Fungu lililotengwa ni Tshs 180m kwa miezi 6.

Baadhi ya maofisa wa makao Makuu CUF wanalalamika kuwa ni kwa nini fedha zote hizo zilikuwa hazipelekwi mpaka watu walalamike??

Mjumbe Mmoja wa Baraza kuu kutoka Pemba anasema Maalimu Seif anatafuta njia za kumufukuza Hamad Rashid na jana aliitisha kikao cha siri Pemba na kufanya njama za kuandaa kashifa za Hamad Rashid lakini Watu waliokinyume na sef Pemba wakafichua uovu huo!!!

Mpaka sasa Cuf kimekuwa chama cha kuwindana!!!
Maalimu hataki Uchaguzi ufanyike na sasa anataka atoe urithi jambo ambalo halikubaliki!!!
 
eeehhh basi mambo ni magumu kama ni kweli. Je, haya ndo matokeo ya ndoa yao na ccm? Mbona tunajua ndoa ni kuvumiliana????
 
Eh makubwa madaraka ni ulevi sio?maskini akipata ****** hulia mbwata yaani m2 anasahau haraka alikotoka,embu watulizane watz tuna shda za kutosha,
 
Hakuna asie elewa kuwa hamad rashid ni pandikizi anatumiliwa ili kuja kuharibu maridhiano zanzibar kw muangusha kiongozi wa maridhiano kw upande wa cuf
 
Ndoa imewaponza, magamba namba mbili. Laana waliyonayo chama cha magamba imeshawatia mimba.
Hamad Rashid ni pandikizi la chama gani??
Je, ni CCM au CHADEMA???

Mimi nimeshindwa kukuelewa , Kwani muafaka wa CCM na CUF ulikuwa ni CUF na CCM au ni Maalimu Seif na Karume???
Kwani katika muafaka hakuna demokrasia ya Uchaguzi???

Hivi kuitisha Uchaguzi ni kuvuruga CUF???

Kwani siku zote Uchaguzi ukifanyika CUF watu walikuwa hawagombei??

Kwa nini unataka kuendekeza mambo ya Ubabe???
Kumbuka Vyama vyote vinakaribia kufanya Uchaguzi Taifa. CCM watafanya Mwaka 2012, CHADEMA mwaka 2012, CUF nao wanapanga 2012/2013 sasa demokrasia ni watu kugombea na sio kuleta Utume kwenye CUF!!!

WEWE huoni Wana CCM wanataka kumutoa Kikwete kwenye nafasi ya Uenyekiti Taifa???
Usibweteke Panua Mawazo!!!
 
Nimefuatilia makoa mkuu ya CUF nikagundua kuwa hali ni tete kwani kuna makundi Moja ni la Hamadi Rashid na Jingine ni la Maalim Seif Na kwamba makosa aliyofanya Seifu yamewagusa wengi na hapana Shaka kwamba ameanza kuyarekebisha!!!

Moja ya Mambo ambayo yamekuwa kero kubwa ni suala la pesa ambapo Mgao wa pesa za operations za Makao makuu zilikuwa hazipo Wakati kule Pemba wanatanua kwa kutumia fedha za serikali.

Julius Mtatilo aliwahi kuongea na gazeti la Sema Usikike akaelezea ukata wa fedha ambapo analazimika kutumia fedha zake Mwenyewe kwa ajili ya shughuri za Chama !!!

Mtatilo aliwahi kulalamika kwamba Ruzuku imechelewa lakini ukweli ni kwamba hata Ruzuku hiyo ilipotolewa ilikuwa haipelekwi Wilayani kama sheria inavyotaka!!

Mtu wa karibu na ofisi ya Uhasibu anasema Juzi tu baada ya Hamadi Rashidi kuelezea nia ya kugombea nafasi ya Katibu Mkuu ndipo Maalimu Seif akaamuru pesa zipelekwe kwenye Wilaya 1oo na kila Wilaya imepelekewa 300,000/= katika awamu ya kwanza na Fungu lililotengwa ni Tshs 180m kwa miezi 6.

Baadhi ya maofisa wa makao Makuu CUF wanalalamika kuwa ni kwa nini fedha zote hizo zilikuwa hazipelekwi mpaka watu walalamike??

Mjumbe Mmoja wa Baraza kuu kutoka Pemba anasema Maalimu Seif anatafuta njia za kumufukuza Hamad Rashid na jana aliitisha kikao cha siri Pemba na kufanya njama za kuandaa kashifa za Hamad Rashid lakini Watu waliokinyume na sef Pemba wakafichua uovu huo!!!

Mpaka sasa Cuf kimekuwa chama cha kuwindana!!!
Maalimu hataki Uchaguzi ufanyike na sasa anataka atoe urithi jambo ambalo halikubaliki!!!
Uchaguzi ni lazima HAKI SAWA KWA WOTE!!!
Mandevu lazima aachie ngazi!!! Hakuna mungu mtu hapa!!!
 
Seif:Kuna njama za kuhujumu maridhiano
Send to a friend
Monday, 11 October 2010 08:06


Geofrey Nyang'oro, Pemba na
Bernard Lugongo, Zanzibar

MGOMBEA urais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia (CUF), Seif Sharif Hamad ameituhumu CCM kuwa inafanya njama za kuhujumu maridhiano mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Hamad akishirikiana na Rais Amani Abeid Karume ndio waliokuwa vinara wa maridhiano hayo baina ya CUF na CCM, ambayo yalilenga kumaliza siasa za chuki na uhasama visiwani Zanzibar na kusababisha mabadiliko ya katiba ambayo yanaruhusu Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Lakini katibu huyo mkuu wa CUF ameanza kuwa na shaka juu ya utekelezaji wa maridhiano hayo wakati rais mpya wa Zanzibar akikaribia kupatikana.
Hamad, ambaye alikuwa waziri kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, alisema njama za kuhujumu maridhiano hayo zinafanywa na baaadhi ya vigogo ndani ya CCM wasioitakia mema amani iliyofikiwa hivi karuni visiwani humo.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika juzi kwenye Uwanja wa Pujini, Jimbo la Chonga Hamad alisema tayari vigogo hao wa CCM wamekutana kufanya vikao usiku na mchana ili kufanikisha azma hiyo.

"Lipo kundi la wana-CCM wanaotaka kuhujuma maridhiano ili waturudishe tulikotoka. Vigogo hao wanafanya vikao usiku na mchana na wanasema ndani ya miaka miwili watarudisha hoja ya kukataa maridhiano ili kupinga uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, kitendo hiki ni kitairudisha Zanzibar kwenye vurugu," alisema Seif.

Seif alitaja mikakati ambayo CCM wamefikia kuwa ni kuhakiksha wanapata majimbo mengi ya uwakilishi ili hata kama yeye atashinda serikali itakayoundwa isiwe na nguvu ili waweze kumuondoa kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.
Alisema baada ya kufanikiwa kwa mbinu hiyo, CCM watapitisha hoja ya kuwataka wananchi kupiga kura juu ya aina gani ya serikali wanayoitaka kwa lengo la kuvuruga maridhiano na kuondoa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

"CCM wanafanya juu chini ili kupata majimbo mengi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu lengo wawe na wajumbe wengi kwenye baraza la wawakilishi na wakifanikiwa wataleta hoja ya kutokuwa na imani na rais kama mimi nitashinda, na kuniondoa pia watarudisha hoja ya kwa wananchi ya kupiga kura kupinga maridhiano,"alisema Seif.
Seif aliwataka wakazi wa visiwa hivyo kuunganisha nguvu zao kwa kuichagua CUF ambayo ina nia thabiti ya kulinda mardhiano yaliyofikiwa nakuund aserikali ya umoja ili visiwa hivyo viweza kudumisha amani na kufanya shughuli za maendeleo.

Alisema Mzanzibari yeyote anayekataa CUF kwa sasa anayakataa maridhiano na anayekataa maridhiano anakataa amani na maendeleo ya visiwa hivyo.
"Anayepinga CUF anakataa mardhiano amani na utulivu na maendeleo. Kama hatutaki kuchinjana, tulinde mardhiano na rais anayeweza kulinda maridhiano hayo ni mimi," alisema Seif.

"Mnaiona hali ilivyo kwa sasa mnataka turudi tulikotoka? ninyi wenyewe ni mashahidi... mahali popote penye vurugu hakuna shughuli za maendeleo, hivyo anayekataa CUF anakataa amani na utulivu, anakataa maendeleo."
Katika mkutano huo ambao pia alipokea wananchama wapya 640, Seif alivishukia vyama vingine vya upinzani vilivyosimamisha wagombea katika majimbo ya Pemba akisema ni vibaraka wa CCM ambao wameletwa kwa kazi moja ya kuwagawa wanachama wa CUF.

Alisema vyama hivyo vimetumwa na CCM na vimepewa fedha ili kuja kuwamega wanachama wa CUF ili kutoa nafasi ya ushindi kwa chama hicho ambacho alisema kinachaha kutafuta kuungwaji mkono na wakazi wa Zanzibar.
"Kuna vyama vingine ni vidogo hata havifahamiki na vinajua hata vikisimamisha wagombea hapa Pemba haviwezi kupata hata kiti cha udiwani hapa, lakini vimesimamisha wagombea. Naomba mnielewe hivi vimetumwa na CCM, vimepewa fedha na lengo lake ni kuwagawa wanachama wa CUF ili CCM iweze kupata ushindi," alisema Seif.
Katika hatua nyingine mgombea huyo alitembelea eneo la Tundaua, mahali kilipo kisima cha mafuta kilichofanyiwa utafiti na kampuni ya BP ya Uingereza na kuwahakikisha wananchi hao kuwa akiingia Ikulu atahakikisha mafuta hayo yanachimbwa.

Alisema atahikisha kampuni za uwekezaji zinafanya kazi hiyo ili rasilimali hiyo iweze kuwanufaisha wananchi wa Zanzibar.
Hata hivyo, mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Ali Mohammed Shein alisema akiingia madarakani atalinda maridhiano yaliyofanywa kati ya chama chake na chama cha CUF na kutekeleza Serikali ya Umoja wa kitaifa.

Akihutubia mamia ya wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Garagara mjini Unguja juzi, Dk Shein alisema: "Nitahakikisha nalinda maridhiano yetu na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kufuatana na katiba yetu mpya."

Alisema kuwa ni muhimu kutunza maridhiano hayo na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ili kuhakikisha kuwa umoja na amani inakuwepo visiwani humo.
"Nia yetu ni kuiendeleza nchi yetu, na hivyo suala hili ni lazima tulitilie mkazo," alisisitiza.

Mwishoni mwa mwaka jana Rais Karume na Maalim Seif walikutana na kukubaliana kumaliza siasa za kihasama na baadaye kukukubaliana kuwa njia ya kumaliza siasa hizo ni kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Uamuzi huo uliungwa mkono na wananchi wa Zanzibar katika kura ya maoni baada ya asilimia 66.4 kukubaliana na muundo huo dhidi ya asilimia 33.6 waliokataa.



 
[h=2]Ukweli kUhusu Mgogoro wa Seif na Hamad Rashid CUF[/h]
Maalim Seif Anaaminika?
MAALIMU SEIF ANAUA CUF BARA!!!!!
Thursday, 18 November 2010 19:53 newsroom





Na Esther Mvungi,Dodoma
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Seif Sharif Hamad, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, amesema haina maana kwa chama cha siasa kupinga kila jambo. Amesema CUF kwa upande wa Tanzania Bara kinafanya kazi ya upinzani kwa ustaarabu na kuongeza: ìTutapinga kwa hoja na si kwa malumbano. Seif alisema hayo jana baada ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, katika sherehe zilizofanyika Ikulu Ndogo ya Chamwino. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hoja inayotolewa na baadhi ya wananchi na vyama vya siasa kuwa, CUF si chama cha upinzani kwa kuwa kimo ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Haina maana kama Zanzibar kuna maeleweno na upande wa pili wa Muungano iwe tofauti, tutafanya kazi zetu kistaarabu,î alisema Seif.
Alisema lengo la wote ni kuleta amani, hivyo CUF inataka yaliyotokea Zanzibar yahamie Bara.Seif alisema ni kweli kwa upande wa Zanzibar CUF si chama cha upinzani kwa kuwa kimo ndani ya serikali. CHADEMA imevitenga vyama vingine vya upinzani vya CUF, NCCR-Mageuzi na TLP katika kuunda kambi ya upinzani.Utengano kati ya vyama hivyo umekuwa ukijionyesha wazi bungeni, ambapo katika uchaguzi wa wajumbe wa Bunge la SADC-PF uliofanyika Jumanne wiki hii, wabunge wa CHADEMA walimdhihaki mgombea wa CUF.

Baada ya Injinia Mohammed Habib Mnyaa wa CUF kutangazwa mshindi katika kundi la vyama vya upinzani, wabunge wa CHADEMA walipiga kofi wakisema CCM, CCM.​
 
Back
Top Bottom