Maalim Seif Shariff na Vijana wa Tanzania Bara Uchaguzi Mkuu 1995 Sehemu ya Pili

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,264
MAALIM SEIF SHARIFF NA VIJANA WA TANZANIA BARA UCHAGUZI MKUU 1995 SEHEMU YA PILI

Katika mazungumzo yetu Starlight Hotel, Maalim Seif ni kama vile hakuweza kujiaminisha kuwa kweli Tanzania Bara kuna mtandao ambao ungeweza kuwa msingi wa chama cha CUF kukua na kustawi. Huwezi kumlaumu kwa kuwa mtandao huu ulikuwa huwezi kuuona kwa macho lakini ulikuwapo.

Mtandao ulikuwapo hata kabla mtandao wenyewe wa watu maarufu ndani ya CCM kuwepo na kusikika. Naamini Maalim hakujuta kwa kuletewa vijana badala ya wazee wetu kwani kila alipopita mikoani na vijijini alipokelewa na vijana hawa.

Baadae zilitufikia taarifa kuwa wapinzani wetu walishangazwa ni lini tulijenga mtandao ule wa nchi nzima na bila shaka swali hili pia lilikuwa kichwani kwa Maalim. Mtandao huu wetu sisi ulikuwa wa watu wa kawaida kabisa wengi wao vijana. Watu masikini wasio na chochote.

Haukuwa mtandao kama mtandao ulivyofahamika wa watu mashuhuri ndani ya CCM wenye kutajika na wenye madaraka katika jamii. Mtandao huu ulikuwa na maajabu yake. Uliweza kumkusanyia Prof. Lipumba saini 200 Morogoro za kumdhamini kama mgombea urais kwa tiketi ya CUF kwa usiku mmoja.

Kulikuwa na msemo, ''Kitanda kwa kitanda.'' Huu ulikuwa ni mtandao wa watu masikini ya Mungu hawakuwa na fedha kilichokuwa kikiwasukuma ni mapenzi ya nchi yao na ari ya kupigania usawa na haki kwa kila mwananchi bila ya ubaguzi. Mtandao huu haukumtupa Maalim mkono na walikuwa na yeye hadi mwisho wa maisha yake.


View: https://youtu.be/z0glaDrYNVU

Sehemu ya kwanza soma Maalim Seif Shariff na Vijana wa Tanzania Bara Uchaguzi Mkuu 1995 Sehemu ya Kwanza
 
MAALIM SEIF SHARIFF NA VIJANA WA TANZANIA BARA UCHAGUZI MKUU 1995 SEHEMU YA PILI

Katika mazungumzo yetu Starlight Hotel Maalim Seif ni kama vile hakuweza kujiaminisha kuwa kweli Tanzania Bara kuna mtandao ambao ungeweza kuwa msingi wa chama cha CUF kukua na kustawi.

Huwezi kumlaumu kwa kuwa mtandao huu ulikuwa huwezi kuuona kwa macho lakini ulikuwapo.

Mtandao ulikuwapo hata kabla mtandao wenyewe wa watu maarufu ndani ya CCM kuwepo na kusikika.

Naamini Maalim hakujuta kwa kuletewa vijana badala ya wazee wetu kwani kila alipopita mikoani na vijijini alipokelewa na vijana hawa.

Baadae zilitufikia taarifa kuwa wapinzani wetu walishangazwa ni lini tulijenga mtandao ule wa nchi nzima na bila shaka swali hili pia lilikuwa kichwani kwa Maalim.

Mtandao huu wetu sisi ulikuwa wa watu wa kawaida kabisa wengi wao vijana.

Watu masikini wasio na chochote.

Haukuwa mtandao kama mtandao ulivyofahamika wa watu mashuhuri ndani ya CCM wenye kutajika na wenye madaraka katika jamii.

Mtandao huu ulikuwa na maajabu yake.

Uliweza kumkusanyia Prof. Lipumba saini 200 Morogoro za kumdhamini kama mgombea urais kwa tiketi ya CUF kwa usiku mmoja.

Kulikuwa na msemo, ''Kitanda kwa kitanda.''

Huu ulikuwa ni mtandao wa watu masikini ya Mungu hawakuwa na fedha kilichokuwa kikiwasukuma ni mapenzi ya nchi yao na ari ya kupigania usawa na haki kwa kila mwananchi bila ya ubaguzi.

Mtandao huu haukumtupa Maalim mkono na walikuwa na yeye hadi mwisho wa maisha yake.


View: https://youtu.be/z0glaDrYNVU

Mtandao uliotegemea zaidi misikiti ya vijana wenye siasa kali aka wavaa vipedo.
 
Back
Top Bottom