Ukweli kuhusu kwanini unaamini dini unayoiamini

Mayu

JF-Expert Member
May 11, 2010
6,637
10,722
Swali la MSINGI;

IN THE FIRST PLACE, KWANINI UNAAMINI KATIKA DINI UNAYOIAMINI?

Kabla hujaendelea kusoma be honest with yourself na ujijibušŸ™

Ok tuendelee.
Kila mtu kwa mujibu wa imani yake amekua akijenga HOJA NZITO kueleza ā€œUKWELIā€ na u HALALI wa Mungu wake huku akinukuu maandiko ya dini yake kwa ufundi mkubwa sana na kukosoa imani zingine.

UKWELI ni kwamba SIO KWELI kwamba dini unayo iamini ULIICHAGUA kwa hiyari yako baada ya kujiridhisha ni SAHIHI na ya KWELI

UKWELI ni kwamba 95% ya watu wote Duniani wanaamini dini wanazo ziamini ikiwa ni MATOKEO ya MALEZI/MAKUZI, GEOGRAPHY/HISTORY, nasio machaguo yao

MALEZI YA MZAZI.
Wazazi wanachangia pakubwa sana kupitia ile TRUST dhidi ya watoto...... kuna trust kubwa sana ya mtoto kwa mzazi. Mtoto toka mchanga anamuamini mzazi 100% na anaanza kuaminishwa na kujengewa hofu kuhusu Mungu husika hadi anapokua kijana.

Teenagers are suspicious, lakini hadi kufikia hapo inakua too late, brainwashed damage ya mzazi inakua beyond repair

MAKUZI YA JAMII
Namna jamii inavyoishi kwa kumkuza Mungu

Mitaani watu wataapa kwa jina la Mungu, kila kitu kikitokea watu watesema namshukuru Mungu au namuachia Mungu, jamii inatoa nafasi kubwa kwa viongozi wa dini kama kwenye misiba harusi nk

Majanga makubwa yakitokea viongozi wataingoza maombi ya kitaifa nk nk

Mtaani huko ukisema hadharani hakuna Mungu kila mtu atakuona unalaana au umechanganyikiwa, nchi nyingine una uwawa kabisa

GEOGRAPHY/HISTORY
Je wewe mkristo wa Iringa au muislam wa Tanga vipi kama ungezaliwa na wazazi wa kihindu India kwenye viunga vya Punjab ambapo 99% ni Budha?

Vipi ungezaliwa kule milimani China ambapo 100% ya wakaazi ni Budha?

Kwa mfano Tz watu zaidi ya 80% wanajua dini mbili tu ukristo na usilam, hawana kabisa access ya kujua dini zingine, hii ipo kwa nchi nyingi sana duniani kote. Nchi kama North korea hali ndio mbaya kabisa.

Huko China kuna majimbo ukiwauliza kuhusu Yesu au Mudi hawajui kabisa kama vile wewe ukiulizwa kuhusu dini kuu ya wachina na Mungu wao hujui chochote labda u googlešŸ˜‚

JE, WEWE UPO KWENYE IMANI YAKO KWA SABABU GANI?

Kisha tafakari dhana nzima ya uwepo wa Mungu mmoja kama inawezekana kwa kuzingatia malezi makuzi jiografia na historia šŸ™

JE NI NINI ROLE YA MUNGU WA KWELI KUHAKIKISHA WATU WOTE WANAMJUA?
 
Ukweli nikwamba dini au imani ya dini fulani imekua kama milki ya familia na jamii husika.

Leo mtu akitaka kubadili dini anawaza familia itamchukuliaje. Bora kuacha mke kuliko kubadili dini. Maswali nimengi mno.

Hapa ukitaka kufunga ndoa( kwa walio wengi) na mtu swali lakwanza ni dini kisha mengine yatafuata
Habari za dini ni nzito kidogo sio rahisi kama tunavyozijadili hapa
 
Kuna asimilia fulani ya imani ya kweli katika kila dini -- hata zile ambazo zinaeneza uongo wa wazi.

Ukweli unaweza kuchanganywa na uongo ilimradi tu uvutie akilini mwa watu wanaopenda kudanganyika na kudanganywa.

Aidha, ukweli halisi wa Mungu haujifichi na wala hauna sababu ya kujificha.

Kanuni ya ukweli ni kudhihirika kama nuru ya adhuhuri, isiyohitaji wala umahiri kuing'amua.

Kanuni ya uongo ni kujificha kama giza la usiku wa manane, linalohitaji kutia maanani ili kupata utambuzi wa ziada ili kubaini kinachoendelea duniani.

Tatizo la wengi sana si kwamba hawaujui ukweli.

Shida ipo kwenye maslahi binafsi wanayohofu yatavurugika iwapo wakiufuata ukweli.

Maslahi (mali, kipato, fedha, familia, marafiki, mazingira, mfumo, mipango fulani fulani, nk)

Shida ipo kwenye utaratibu mpya wa maisha watakaolazimika kuufuata iwapo wakiukubali ukweli huo.

Shida ipo kwenye raha na starehe potofu watakazolazimika kuzivua kwa vile zinakinza ukweli mpya ambao hawana budi kuupokea.

Shida ipo akilini mwao kwamba jamii iliyowazoea wakiwa hivi itawaonaje ghafla tu wakiwa vile.

Shida ipo kwenye utashi wao ambao haujafanya maamuzi ya kina, wakidhani kwamba wana muda wa ziada kesho, ambayo kimsingi haitafika kamwe.
 
Chakushangza kila mmoja anaamini dini yake ni ya kweli.

Waislam wanasema Allah anajibu maombi yao lkn nao wakristo wanasema Yesu anajibu maombi yao. Mungu wa kweli wapo wangapi?

Na kama ni mmoja, mbona watu wanaabudu Miungu tofauti lakini wanapata matokeo sawa? Anayeabudu Mungu wa uongo anapata matokeo sawa na anayeabudu Mungu wa kweli,hii imekaaje?

Au maombi ni dhana tu lkn hakuna kitu kama hicho?
 
Dini ni njia ya kukupeleka kwa MUNGU Ila sio lazima uwe na dini ndo uwe Karibu na MUNGU.
Unaongelea jambo usilolijua, na wengi wanafanya kosa hili. Haiwezekani kabisa kutengenisha dini, Mungu, Shetani na mwanadamu.

Dini ni mfumo wa imani. Imani ni ama iko kwa Mungu au Shetani.

Kila tunalowaza na kutenda hutegemea ni kanuni ya nani kati ya Mungu na Shetani imetawala mawazoni.

Hivyo kutengenisha dini na Mungu (au hata na Shetani) ni kufanya kosa lilelile apendalo Ibilisi baba wa uongo.

Dini ni ama ya uongo au ukweli. Dini ni maisha ya kila siku. Dini ni mawazo, maneno na mwenendo wa mtu. Dini kamwe katu haiepukiki; hakuna awezaye kuikwepa.

^Ni rahisi zaidi kwa Juma Nkamia kupenya katika utando wa siasa, kuliko mtu mahiri kuingia katika maficho asimofikiwa na dini.^ ~ Maamrisho 10:25.
 
1708707134379.jpg
 
Imani unazaliwa nayo ila dini unaikuta duniani ukimzaa mtoto anakuwa na Imani na mungu ila Hana dini hivo dini zote tunazikuta tu duniani ila Imani tunazaliwa nazo Nirahisi Mimi kuamini nitapata au kufanikiwa jambo fulan hata kama Sina dini
 
Umejuaje mtoto akizaliwa anakuwa na imani? Any way tuachane na hayo najua hauna jibu tuendelee kujifarijii ziku zetu ziishe kwa amani tuwe udongo , kwisha
 
Swali la MSINGI;

IN THE FIRST PLACE, KWANINI UNAAMINI KATIKA DINI UNAYOIAMINI?

Kabla hujaendelea kusoma be honest with yourself na ujijibušŸ™

Ok tuendelee.
Kila mtu kwa mujibu wa imani yake amekua akijenga HOJA NZITO kueleza ā€œUKWELIā€ na u HALALI wa Mungu wake huku akinukuu maandiko ya dini yake kwa ufundi mkubwa sana na kukosoa imani zingine.

UKWELI ni kwamba SIO KWELI kwamba dini unayo iamini ULIICHAGUA kwa hiyari yako baada ya kujiridhisha ni SAHIHI na ya KWELI

UKWELI ni kwamba 95% ya watu wote Duniani wanaamini dini wanazo ziamini ikiwa ni MATOKEO ya MALEZI/MAKUZI, GEOGRAPHY/HISTORY, nasio machaguo yao

MALEZI YA MZAZI.
Wazazi wanachangia pakubwa sana kupitia ile TRUST dhidi ya watoto...... kuna trust kubwa sana ya mtoto kwa mzazi. Mtoto toka mchanga anamuamini mzazi 100% na anaanza kuaminishwa na kujengewa hofu kuhusu Mungu husika hadi anapokua kijana.

Teenagers are suspicious, lakini hadi kufikia hapo inakua too late, brainwashed damage ya mzazi inakua beyond repair

MAKUZI YA JAMII
Namna jamii inavyoishi kwa kumkuza Mungu

Mitaani watu wataapa kwa jina la Mungu, kila kitu kikitokea watu watesema namshukuru Mungu au namuachia Mungu, jamii inatoa nafasi kubwa kwa viongozi wa dini kama kwenye misiba harusi nk

Majanga makubwa yakitokea viongozi wataingoza maombi ya kitaifa nk nk

Mtaani huko ukisema hadharani hakuna Mungu kila mtu atakuona unalaana au umechanganyikiwa, nchi nyingine una uwawa kabisa

GEOGRAPHY/HISTORY
Je wewe mkristo wa Iringa au muislam wa Tanga vipi kama ungezaliwa na wazazi wa kihindu India kwenye viunga vya Punjab ambapo 99% ni Budha?

Vipi ungezaliwa kule milimani China ambapo 100% ya wakaazi ni Budha?

Kwa mfano Tz watu zaidi ya 80% wanajua dini mbili tu ukristo na usilam, hawana kabisa access ya kujua dini zingine, hii ipo kwa nchi nyingi sana duniani kote. Nchi kama North korea hali ndio mbaya kabisa.

Huko China kuna majimbo ukiwauliza kuhusu Yesu au Mudi hawajui kabisa kama vile wewe ukiulizwa kuhusu dini kuu ya wachina na Mungu wao hujui chochote labda u googlešŸ˜‚

JE, WEWE UPO KWENYE IMANI YAKO KWA SABABU GANI?

Kisha tafakari dhana nzima ya uwepo wa Mungu mmoja kama inawezekana kwa kuzingatia malezi makuzi jiografia na historia šŸ™
Hizi dini za kigeni uislam na ukristo na zingine zilizotoka ughaibuni, ni utumwa na utapeli mtupu. Zote zina agenda mbaya iliyojificha.

Hizi dini zimewasaidia sana wageni kuiba raslimali zetu na kupenyeza agenda zao mbaya katika jamii zetu.

Huwezi tenganisha hizo dini na ukoloni pia na serikali. Maana msingi wa hizo dini ni unyonyaji, udanganyi, unyang'anyi pia na kueneza hofu na ujinga kwa watu.

Na kibaya zaidi hizi dini zinatumia, wazazi, walezi.na jamii kuwa recruiter wa watoto wadogo wasio na uelewa wa agenda zao.

Ebu tujitafakari, hivi miaka yote ya hizi dini kuwa hapa africa zimetusaidia nini? Tofauti na wao kunufaika maana makanisa na misikiti ni kama maduka yao kwani kuna % ya mapato ya sadaka inaenda kwao.

Mtu mweusi anakazana kwenda kanisani na kumtolea Mungu sadaka wakati jirani yake hana pesa ya chakula na mtoto wa jirani kafukuzwa ada.

Tunakazana kuchanga na kujenga makanisa na misikiti ili tuende kumuomba Mungu ajira na pesa badala ya kuchanga na kuanzisha miradi ya maendeleo na kutengeneza ajira kwa vijana na kuongeza uchumi wa nchi.

Jamii imekuwa ya kijinga sana kwa kuendekeza hizo imani za dini. Zimejaa unafiki mkubwa sana na zinaendelea kutudidimiza.

Wachina wanakazana kutengeneza na kugundua microchips za computer ila sisi tunakazana kwenda kanisani na misikitini kumuomba Mungu.

Dini za kigeni ni scam. Ila yatupasa kuboresha social activities na belief system ya kwetu.
 
Chakushangza kila mmoja anaamini dini yake ni ya kweli.

Waislam wanasema Allah anajibu maombi yao lkn nao wakristo wanasema Yesu anajibu maombi yao. Mungu wa kweli wapo wangapi?

Na kama ni mmoja, mbona watu wanaabudu Miungu tofauti lakini wanapata matokeo sawa? Anayeabudu Mungu wa uongo anapata matokeo sawa na anayeabudu Mungu wa kweli,hii imekaaje?

Au maombi ni dhana tu lkn hakuna kitu kama hicho?
Mungu hayupo.

Allah, Yesu ni dhana za kutungwa na kufikirika tu...
 
Umejuaje mtoto akizaliwa anakuwa na imani? Any way tuachane na hayo najua hauna jibu tuendelee kujifarijii ziku zetu ziishe kwa amani tuwe udongo , kwisha
Ukitaka kujua hilo mchukue mtoto huyo huyo aliyezaliwa Tanzania aende aishi china atakuwa na iman ya kichina Buddha ,akienda roma atakuwa na iman ya Kiroma hivo hivo akienda uarabun atakuwa na iman ya kiarabu hata mababu zetu hawakuzaliwa na dini ila walizaliwa na Imani ndio maana waliomba miti,misitu, mawe,vinyago na walifanikiwa Kwa kuwa wana imani hata hao wanao amini shetani wanaimani ndio maana wanafanikiwa na wanaomini mungu nao wanafanikiwa hivo amini tuna zaliwa na Imani ndio dini zetu

Na ili ungie kwenye dini zote kubwa lazima uwe na imani ukiwa huna Imani hawakuitaji maana huwezi fanikiwa
 
Ukweli nikwamba dini au imani ya dini fulani imekua kama milki ya familia na jamii husika.
Leo mtu akitaka kubadili dini anawaza familia itamchukuliaje. Bora kuacha mke kuliko kubadili dini. Maswali nimengi mnooooo.
Hapa ukitaka kufunga ndoa( kwa walio wengi) na mtu swali lakwanza ni dini kisha mengine yatafuata
Habari za dini ni nzito kidogo sio rahisi kama tunavyozijadili hapa
Upo sahihi kabisa mkuu
Mtoto wa dada yangu alipata mume wa kiislam....... familia nzima waligoma kasoro mimi na baba yake tu
Yaani ilionekana ni laana kubwa
Na cha ajabu wanaoingoza kupinga wengine hata habari ya dini hawana muda nayo ila wanajua tu wao wakristo basiii
 
Kuna asimilia fulani ya imani ya kweli katika kila dini -- hata zile ambazo zinaeneza uongo wa wazi.

Ukweli unaweza kuchanganywa na uongo ilimradi tu uvutie akilini mwa watu wanaopenda kudanganyika na kudanganywa.

Aidha, ukweli halisi wa Mungu haujifichi na wala hauna sababu ya kujificha.

Kanuni ya ukweli ni kudhihirika kama nuru ya adhuhuri, isiyohitaji wala umahiri kuing'amua.

Kanuni ya uongo ni kujificha kama giza la usiku wa manane, linalohitaji kutia maanani ili kupata utambuzi wa ziada ili kubaini kinachoendelea duniani.

Tatizo la wengi sana si kwamba hawaujui ukweli.

Shida ipo kwenye maslahi binafsi wanayohofu yatavurugika iwapo wakiufuata ukweli.

Maslahi (mali, kipato, fedha, familia, marafiki, mazingira, mfumo, mipango fulani fulani, nk)

Shida ipo kwenye utaratibu mpya wa maisha watakaolazimika kuufuata iwapo wakiukubali ukweli huo.

Shida ipo kwenye raha na starehe potofu watakazolazimika kuzivua kwa vile zinakinza ukweli mpya ambao hawana budi kuupokea.

Shida ipo akilini mwao kwamba jamii iliyowazoea wakiwa hivi itawaonaje ghafla tu wakiwa vile.

Shida ipo kwenye utashi wao ambao haujafanya maamuzi ya kina, wakidhani kwamba wana muda wa ziada kesho, ambayo kimsingi haitafika kamwe.
Letā€™s assume Mungu wa kweli Zeus
Je mtoto wako ana nafasi ya kumjua achilia mbali wewe?
Huyu Mungu wa ā€œkweliā€ Zeus anampango gani na mtu aliyezaliwa Afaghanistan au Uswatini? Ambaye hana access ya kumjua kabisa

Hoja kubwa hapa ni nini ROLE ya Mungu wa kweli ili watu kumjua?
Kwanini kumuamini Mungu ni matokeo ya historia jiografia na malezi na sio based na FACT?

Sijui umenielewa?
 
Back
Top Bottom