Kama jina langu lilivyo ndivo ninavyotaka, kudakia mambo ya kijiweni tunapojadili mambo mazito yatokeayo katika jamii ni hatari ya kufunikafunika ukweli ulijificha nyuma ya pazia, na kumbuka wasanii wanaoongoza nchi hii hutumia mwanya wa hoja dhaifu kujenga mambo yao, lakini huwa sipendi mambo ya vijiweni kuyaweka ndiyo msingi wa majadiliano, kwa sababu hakuna mwanafamilia hata mmoja kutoka katika hawa wawili kamanda na mama aliyemsindikiza kulalamikia wanayotunishiana misuli hapa JF. Bara tujadili mazingira na makandokando ya kifo hicho tukihusianisha na matukio kadhaa ya mfululizo tangu Dr. Ulimboka na hadi tulipo sasa.
Tusipoangalia tutachelewa akili kutusahaulisha mambo muhimu na kuhangaika kujadili mambo ya ngoni yasiyohakikiwa. Mengi wanayojadili hapa ni ya kufikirika ambayo hayaja hakikiwa.
Kuna uwezakano marehemu alikuwa na ndugu yake wa kike na siyo kama story inavyoeleza hapa.