Ngoromiko
JF-Expert Member
- Sep 15, 2011
- 554
- 175
- Thread starter
- #21
Wazee wangu nchi hii tuna kila kitu isipokuwa tunachokosa ni kimoja tu uongozi bora na siasa safi.Tatizo hapa ni watawala ambao bila shaka ni ccm.Watawala hawa kwa miaka 50 wamekosa dira ya kuingoza nchi hii kuelekea kufaidi neema tuliyojaliwa na Mwenyezi Mungu.Wamekuwa ni wabinafsi, wamekosa uadilifu,sio wazalendo,wamekosa pia akili na uelewa wa masuala ya uchumi na hivyo kuachia raslimali za nchi hii kuchukuliwa na wageni bila huruma huku wao wakipewa kitu kidogo sana kwa ajili yao na famiilia zao.Tuache masihara ya kiitikadi ktk masuala nyeti kama haya.Ndugu zangu angalieni mfano wa vinchi vidogo kama Mauritius hawana rasilimali yeyote ni kisiwa kidogo ktk bahari ya Hindi,wanategemea utalii na kilimo cha miwa pekee,angalia walivyopiga hatua.Wana uchumi mzuri,ni mojawapo ya nchi pekee nne Africa zenye uchumi mzuri sana zingine ni Botswana,Gabon na Africa ya Kusini wana literacy rate 85% na ni moja ya nchi zenye utawala bora na democracy nzuri,wamewahi kupata nishani ya Ibrahim kuhusu utawala bora.Sasa sisi tuna tatizo gani hadi tuwe masikini kiasi hiki licha ya rasilimali lukuki na ardhi nzuri tuliyo nayo.
Tujiulize wananchi tunahitaji kuchukua hatua,na hatua nzuri kwa sasa ni kubadilisha uongozi wa nchi kabisa tuwaone na wengine watafanya nini badala ya kutegemea walewale ambao wametuangusha kwa muda wote huo.Mbona nchi za wenzetu hubadilisha utawala mara kwa mara na wanaendelea mbele,sisi tunaogopa nini?Ni wakati muafaka wa kubadilisha watawala kwani hata wengine wakifanya vibaya si tutawaondoa tu shaka ya nini?
Mabadiliko ya uongozi wa nchi yatafanywa na Watanzania kidemokrasia watakapoona kuna haja ya kufanya hivyo na muhimu zaidi watakapoona kuna chama kinachoweza kuaminika kukabidhiwa dola.
Kwa sasa hakuna chama makini cha upinzani kinachoweza kuaminika na kupewa ridhaa hiyo. Waliopo ni wanaharakati tu.