Ngoromiko
JF-Expert Member
- Sep 15, 2011
- 554
- 175
Wana-JF, napenda kuwashirikisha alichosema Mzee Peter Kisumo kuhusu CHADEMA:
Tatizo kubwa kwenye Chadema kuna wanaharakati na si wanasiasa, na haiwezekani kuongoza serikali kwa kuwa na viongozi wanaharakati.
Hawa Chadema wanachokifanya ni kuvizia makosa madogo madogo ya serikali na kisha kuwashawishi wananchi wawe upande wao,.
Wapo viongozi wa Chadema na waasisi, kama Mzee Edwin Mtei na watu wengine makini ninaowafahamu ndani ya chama hicho, sijawahi kuwasikia wakiropoka hovyo kama wanavyofanya baadhi ya viongozi wa chama hicho.
'Ikiwa hulka hiyo itandelea, kuna hatari ya kukosa sifa ya kushika dola vinginevyo watapata shida, kwani hakuna serikali inayoweza kwenda kwa kuendeshwa na wanaharakati'.
'Inatakiwa chama ambacho kitashinda kiwe na uwezo wa kuongoza katika hali ya amani na utulivu na si kuingia kwenye machafuko mara baada ya uchaguzi'.
'Ili Chadema ishike dola, ni lazima wajitahidi kujenga safu ya uongozi wa kutawala na si kuwa na viongozi ambao kila wakati wanahamasisha watu kuandamana, kugoma na kuvizia makosa ya serikali iliyopo madarakani'.
'Wanachokifanya Chadema ni sawa na wawindaji wanaokoka moto kwa ajili ya kuchoma nyama ili hali nyama yenyewe hawajaipata, ..... kazi ya kuingoa CCM si rahisi kama inavyofikirika'.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI