Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,513
113,643
Majaji1 final.png
Majaji 2final.png

Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila siku za Jumatatu, huwaletea makala za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambayo huchapishwa na gazeti la Nipashe la Jumapili, ambazo ziko kwa mtindo wa maswali, majibu ya maswali hayo, utayapata wewe mwenyewe, na kisha tutawatafuta wahusika, ku balance hii mada, hivyo kwa mada hizi za mhimili wa Mahakama, mtu wa kubalance tuhuma hizi ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma.

Baada ya makala kuhusu Ofisi ya DPP, wiki hii, naugeukia Mhimili wa Mahakama.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akiwaapisha Majaji wapya 28 wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani, Rais Samia alisema na hapa ninanukuu

“Tatizo la ucheleweshwaji wa kesi katika Mahakama zetu bado lipo, kama mnavyosema Wanasheria haki inayocheleweshwa ndio haki inayokataliwa, hivyo ni imani yangu kuwa baada ya upatikanaji wa Majaji hawa ucheleweshaji wa kesi Mahakamani utapungua na hatimaye haki kupatikana kwa wakati,” alisema Mhe. Rais Samia.

Rais Samia akaendelea kwa kuitaja Ibara ya (107) A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mamlaka ya utoaji haki ni Mahakama, “hivyo jukumu lililopo mbele yenu ni kubwa sana, basi ni vyema mkatekeleze majukumu yenu mliyopewa kwa uaminifu, mkaongoze vyema na mkaongozwe na utu na nafsi zenu katika kuwatumikia wananchi,” Mwisho wa kunukuu.

Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alimshukuru Mhe. Rais kwa uteuzi wa Majaji hao wapya huku akiwa na imani kuwa idadi hiyo italeta mabadiliko makubwa ambayo yataonekana mara moja.

Jaji Mkuu, Prof. Juma alisema “Mhe. Rais napenda nichukue fursa hii kukushukuru kwa kutupatia Majaji hawa, idadi hii itasaidia kupunguza mzigo wa mashauri kwa Majaji waliopo na hivyo kusaidia kuleta mabadiliko ambayo yataonekana mara moja,” alisema Mhe. Jaji Mkuu.

Prof. Juma, aliendelea “Mhe. Rais idadi ya Majaji inapanda na kupungua kulingana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kustaafu kwa Majaji pamoja na Majaji wengine kupangiwa majukumu mbalimbali, hivyo bado tunaomba kuendelea kupatiwa Majaji kadri nafasi zinapopatikana ili kuendelea kutoa huduma ya haki kwa kuwa wananchi wengi kwa sasa wanafahamu haki zao na hivyo kufungua kesi kwa wingi,” alieleza Jaji Mkuu.

Kwa vile hoja yangu ya makala hii ni kuangazia uwezo mdogo wa baadhi ya Majaji na Mahakimu wetu, kutokuwa na jicho la ndani, lenye uwezo wa kuona haki, kunakochangia ucheleweshaji wa kesi na ukosefu wa haki, naomba kutoa historia fupi ya maisha yangu na jicho la ndani.

Jicho la Ndani ni Nini?
Jicho la ndani ni uwezo wa kuona vitu visivyoonekanika kwa macho ya kawaida, kwa kizungu wanaita intuition, mtu akifanya kitu sirini, ukiwa na intuition utamjua tuu!. Hivyo mtu akibambikiwa kesi majaji wenye intuition wataona guilty conscience or innocence kwa mshtakiwa!.

Mimi Paskali Mayalla, zaidi ya kuwa mwandishi wa habari na mtangazaji, mimi pia mtu wa mastori, yaani stori teller, hivyo kwa wapenzi wa mastori, unaweza kufuatilia sehemu hii ya Mastori ya Pasco Mayalla, ila wewe kama sio mtu anayependa mastori, unaweza ku skip hii segment ya mastori
Mastori ya Pasco Mayalla
Mimi nimezaliwa katika familia ya watumishi wa serikali kwa baba na mama, Baba Mzee Andrew Mayalla (RIP), akihusishwa na ile Kesi ya Mauaji Mwanza ya 1976. Enzi za Nyerere, mtumishi wa umma ukistaafishwa kwa manufaa ya umma, breki ya pili ni kurejeshwa kijijini, hivyo tukarejeshwa kijijini usiku usiku kufuatia kesi hiyo. Baba yetu mdogo Mzee Mateo Kasanga, akatufata kijijini, mimi na dada yangu Maria, na kutuleta jijini Dar es Salaam kuishi na familia yake.

Mimi nikaanza kuifuatilia “Kesi ya Mauaji Mwanza” kwenye gazeti la Mzalendo kila Jumapili, Baba alikuwa anatetewa na Wakili Murtaza Lakha, kati ya washitakiwa wote, ni baba yangu pekee ndio alinasuka, kutokana na umahiri wa wakili Lakha, wengine wote walifungwa vifungo virefu. Toka wakati huo, nikaanza kudevelop interest ya kuwa kama Lakha ili nisaidie watu kupata haki mahakamani.

Familia ya Mzee Kassanga ilikuwa na watoto 6 ukijumlisha na watoto wawili, tunakuwa watoto 8, ni familia kubwa. Ukitokea wizi wowote, udokozi, automatically unajihisi unahisiwa ni wewe, maana kabla ya ujio wenu hakukuwa na wizi wala udokozi. Kuna siku usiku Mama K, alisahau fedha mezani, asubuhi akakuta zimepungua, kuna mtu amedokoa!. Wote hatujui ni nani, Baba alishika fimbo, na watoto wote tuliitwa, na kuambiwa tutachapwa wote hadi tumtaje aliedokoa. Kwa vile hakuna aliyemuona ni nani, wakubwa wote tulikula mboko!.

Baada ya kula mboko za kutosha, sisi wanaume tunaambiwa “msilielie kama wanawake”, hivyo unajikaza, lakini usiku ukikumbuka umekula mboko bila kosa, unajikuta machozi yanakutoka, kwa wote kupigwa bila kosa, kwa kosa la mmoja wenu!, nikaanza kujiuliza iweje akose mmoja, halafu tuadhibiwe wote bila hatia?, kiukweli nilianza kuwa mbishi.

Baadhi ya adhabu, nikaanza kunote huku wengine tunasosoneka kuonewa, kuna mwingine amelia kidogo tuu, akanyamaza na kuanza kutucheka. Nikamwambia Mama K, aliyefanya kitendo hicho ni fulani. Mama akaniuliza ulimuona?, umejuaje?, nikasema sikumuona, ila najua tuu atakuwa ni fulani!. Nikaulizwa umejuaje hadi kumtaja?, nikasema najua tuu!. Huko kujua tuu, bila ushahidi wowote, ndio jicho lenyewe la roho!. Nilyemtaja akaulizwa akakataa kata kata kuwa namzingizia!.

Tukiwa shule, mwenzetu kila saa anatafuta kitu, mara big G, mara mihogo ya mbilimbi, mara kashata, mara karanga, kila nikumuuliza anasema amenunuliwa na rafiki zake. Nikamuuliza mmoja wa marafiki zake, akasema ni fulani kaja na hela ya noti!, (enzi hizo noti ni hela nyingi), huyo rafiki akasema ananituma mimi ninunue na kugawia wengine. Hiyo ikapita.

Siku nyingine tena kukatokea udokozi mwingine, na wote tukaitwa, baba fimbo mkononi kama kawaida msiposema ni nani, wote tutakula mboko!. Baada ya kuwatazama wote usoni, wengine wote wanaogopa kuchapwa, mmoja wetu amekauka tuu, huku hana wasiwasi wala haogopi. Kwanza nilianza ubishi, kwasababu mimi najijua sijadokoa, hivyo leo sikubali kuchapwa bila kosa!. Kumgomea Dingi, kunahitaji ujasiri wa ajabu!, maana... Basi nikanyoosha kidole na kusema ni fulani!. Niliyemtaja akaruka kimanga, Mama K akaniuliza ulimuona, nikasema hapana, akasema si nilikukataza kumsingizia mtu kitu bila ushahidi?!.

Baba akaruhusu niseme ni kwanini, nimesema ni fulani, nikasema sisi wengine wote tunaogopa, mwenzetu hana wasiwasi, Nikaruhusiwa kuthibitisha, nikaomba kumsachi, huwezi amini, niliibua fedha ya noti imesundwa kati kati ya daftari!. Mhusika aliruka kuwa hajui imefikaje, nikageuziwa kibao ni mimi nimeichomekea!. Tangu hapo, hapo kwenye familia ya Kasangas, ikawa likitokea tukio lolote la sintofahamu ni nani, mimi ndio naitwa kuendesha uchunguzi na nikaanza kuitwa Inspecta Pasikali!.

Tukutane wiki ijayo, kuendelea na simulizi hii, ili kuuonyeshea huo uwezo mdogo wa baadhi ya Majaji na Mahakimu wetu umetokana na nini na athari za Majaji na Mahakimu wenye uwezo mdogo ni nini kwenye mustakali mzima wa utoaji haki nchini.

Part II
Kwa Maslahi ya Taifa: Kila Mtu Anaweza Kuwa Mwanasheria, ila Sio Kila Mwanasheria Anaweza Kuwa Jaji, Majaji wawe ni wale tuu wenye Uwezo wa Kutenda Haki.

Leo naendelea ile simulizi ya wiki iliyopita ili kuuonyeshea jinsi baadhi ya majaji na mahakimu wetu, walivyo na uwezo mdogo wa jicho la ndani la kubaini haki, au hatia na athari za hao Majaji na Mahakimu wenye uwezo mdogo huo, kwenye mustakabali mzima wa utoaji haki nchini.

Simulizi iliishia mimi kuwa na uwezo wa uchunguzi wa kubaini uhalifu mdodo mdogo wa nyumbani, nikadhamiria nikiwa mkubwa nitasomea sheria ili kuwa Wakili kama Murtaza Lakha. Nilijiunga Shule ya Sekondari ya Tambaza, kisha Ilboru ili kusoma sheria. Matokeo ya kidacho cha 6, nilikosa Division 1 kwa pointi moja tuu!, enzi hizo, shahada ya Sheria ikitolewa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pekee, ukikosa Divisheni 1, sahau sheria!, na hivyo ndivyo ndoto yangu kuwa mwanasheria, ilipogota na kuyeyuka kwa muda, nikaamua kusomea uandishi wa habari na kuwa mtangazaji. Ule uwezo wa jicho la ndani, ni tool muhimu kwa mwandishi yoyote wa habari za uchunguzi, hivyo wakati nikiendesha kipindi cha "Kiti Moto", kuna baadhi ya viongozi walikuwa wanakimbia!, maana kuna maswali mengine ya kihabari, yale maswali ya kipolisi yatasubiri!.

Baada ya kuhudumu kwenye utangazaji kwa miaka kadhaa, huku nikiendelea kutamani kuwa wakili, nilifanya mitihani ya mature age entry ya sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na kufaulu vizuri, hivyo nikajiunga na Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kusomea sheria, LL.B. Nikahitimu tena kwa kupata LL.B (Hons), ila kitu cha ajabu sana na huwezi amini, baada ya kuhitimu sheria, nikajikuta napenda zaidi kazi ya uandishi wa habari, ambayo ndio naendelea nayo hadi sasa, hivyo hata graduation sikuhudhuria, wala digree ya sheria sikuwahi kuihitaji, nikaiacha hapo hapo chuoni, ila sasa baada ya miaka zaidi ya 10 tangu kuhitimu, nikaamua kuifuata shahada yangu, nilipigwa butwa, kukuta shadada yangu, is nowhere to be seen!. Nikathibitisha kwa transcript ndio nikachapishiwa upya, hivyo kuonekana kama nimesoma LL.B kwa kipindi cha miaka 15!.

Ninimeamua kujikita kwenye uandishi wa kuangazia madhaifu ya kisheria katika mfumo wetu wa utoaji haki, yaani The Justice System, na makala hizi, zitafuatiwa na vipindi vya redio na Televisheni, vya “Kwa Maslahi ya Taifa”, kuwaelimisha Watanzania kujua haki zao, kutoa msaada wa kisheria kwa wasio na uwezo, kupitia vipindi maalum vya msaada wa kisheria, na wakati huo huo kuangazia mapungufu kwenye mfumo wetu wa sheria, The Justice System ili mapungufu hayo yarekebishwe, Watanzania wapate haki.
Lengo la simulizi hii ni kuwadurusu baadhi ya majaji na mahakimu wetu, jee wana uwezo wa kubaini hatia kwa kutumia jicho la ndani?, intuition, jee kwenye utoaji wa humuku zao, wanazingatia "utu na nafsi"?, na sio kutegemea tuu vifungu vya sheria na ushahidi pekee?. Ili jinai itendeke ni lazima kuwepo kwa mambo mawili, actus reus (kitendo cha jinai) na mens rea, (nia ya kutenda jinai). Jee mfumo wetu wa kupata majaji na mahakimu wetu, unahusisha amplitude test kubaini uwezo wa hao majaji na mahakimu kutumia jicho la ndani la utu na nafsi kubaini nia ovu ya kutenda jinai? yaani intuition?, Jibu ni hapana!.

Tanzania ili mtu kuwa hakimu, ni kwanza kuhitimu shahada ya sheria, na kuomba ajira ya uhakimu, kwenye kuajiriwa, kupitia Tume ya Kuajiri ya Mahakama iliyo chini ya Jaji Mkuu, ila kwenye hadidu za rejea, hakuna amplitude testi yoyote kupima uwezo wa waombaji kuwa na jicho la ndani la kubaini jinai, na matokeo yake ndio baadhi ya hawa mahakimu kwenye mahakama zetu wenye uwezo mdogo, na matokeo yake ni kwa baadhi yao, kutokuwa na uwezo wa kutoa hukumu za haki huku wengine wakituhumiwa kula rushwa!. Udhibitisho wa tuhuma hii ya uwezo mdogo wa mahakimu wetu kutoa hukumu za haki ni mlolongo wa rufaa, na matokeo ya rufaa nyingi kukubaliwa.

Ili kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani ni Tanzania, ni kwanza kuwa mwanasheria, kisha jina lako likapendekezwa na Tume ya ajira ya Mahakama, na kupelekwa kwa rais, mtu unateuliwa kuwa jaji, napendekeza, ili Tanzania tupate majaji kama Lord Denning, tuongeze vigezo vya mtu kuteuliwa Jaji. Kila mtu anaweza kuwa mwanasheria, lakini sio kila mwanasheria anaweza kuwa Jaji. Mfano mzuri ni mtu aliyekuwa DPP kinara wa ukandamizaji wa haki, halafu mtu huyo anateuliwa kuwa Jaji, unategemea nini?!. Kama akiwa DPP alifanya madudu yote yale ambayo sasa ndio yanafumuliwa, akiwa Jaji, atatenda haki?. Unless kama wakati akiwa DPP, baadhi ya maamuzi yake ilikuwa ni kufuata maelekezo, then sasa akiwa Jaji, atakuwa Jaji mzuri, lakini kama akiwa DPP alishindwa kutenda haki, haitegemewi akiwa Jaji atatendaje haki!.

Nchi za wenzetu hadi wana vifaa maalum vya kubaini kama mhusika anasema uongo, (lie detectors), Majaji wetu na Mahakimu lazima wawe na uwezo huo, ili kuepuka kuwatesa watu kwa kuwasweka ndani miaka mingi watu wasio na hatia. Yako mazingira mtu anakutwa na ushahidi wa kuhusika na jinai fulani, na wengine hadi kuhukumiwa kunyongwa, na akiisha nyongwa ndipo ushahidi unakuja kupatikana kuwa amehukumiwa kwa makosa. Majaji na Mahakimu wetu, wakiwa na jicho la rohoni, wataweza kuiona haki na kutoa hukumu ya haki hata kama ushahidi utaonyesha kuhusika.

Kwa maoni yangu, tatizo la msongamano wa kesi, sio idadi ya majaji na mahakimu, bali ni ubovu wa sheria zetu na uwezo mdogo wa baadhi ya majaji na mahakimu kukosa jicho la roho kubaini hatia, na udhaifu wa vyombo vyetu vya upelelezi. Mfano kwa tukio kama lile shambulio la Lissu, hata sisi tuu waandishi wa habari za uchunguzi, tungehitaji IJ ya siku moja tuu, kubaini chanzo cha wasiojulikana hao, na kukitumia kama lead kuwabaini, lakini kwa vyombo vyetu vya uchunguzi ni mpaka leo hakuna taarifa zozote!.

Kwa kesi kama ya kina Rugemalila, sisi waandishi wa habari za uchunguzi, tungehitaji siku 7 tuu, kuwawekea ushahidi wote mezani, lakini vyombo vyetu vya uchunguzi, ni zaidi ya miaka 4 sasa na bado kesi haijaanza kusikilizwa!, kwenye mazingira kama hayo, hata tungekuwa na majaji 100, wangefanya nini?.

Kwa bahati mzuri, mimi nimebahatika kuwa mwanafunzi wa Prof. Ibrahim Juma, hivyo namfahamu vizuri kwa kauli, uwezo na matendo, jicho hilo la rohoni analo, na kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Mahakama ndio mhimili rasmi wa utoaji haki Tanzania, hivyo nina imani kubwa na Mhimili wa Mahakama chini ya Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, licha ya changamoto za utoaji haki, inauwezo wa kuwapatia haki Watanzania.

Kufuatia mhimili wa mahakama kushiriki Maonyesho ya Saba Saba, makala ya wiki ijayo, nitawaletea ushiriki wa Mahakama kwenye Saba Saba.

Paskali
Update
Wanabodi kuanzia sasa, kwenye hoja zangu ninazoibua, zile ambazo zimepatiwa majibu nitakuwa natoa update ya hoja husika na jibu la hoja iliyopatiwa majibu.

Kwenye bandiko hili nilitoa hoja kuhusu uwezo wa majaji wetu kuwa na jicho la ndani la kubaini haki.

Hoja hii imeleta matokeo chanya ambayo nimeyaeleza hapa
Msikilize Rais Samia anesema nini kuhusu majaji
P
Update
Hatimaye kipindi cha kuzungumzia haya kiko tayari na kitatangazwa na Channel Ten, kila siku za Jumapili saa 3:00 usiku na marudio ni Jumatano saa 9:30 mchana.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=IXfA8sZkNPxpaeZn
P
 
Attachments

  • Majaji 1.pdf
    678.1 KB · Views: 19
  • Majaji 2.pdf
    610.2 KB · Views: 11
Kwa kesi kama ya kina Rugemalila, sisi waandishi wa habari za uchunguzi, tungehitaji siku 7 tuu, kuwawekea ushahidi wote mezani, lakini vyombo vyetu vya uchunguzi, ni zaidi ya miaka 4 sasa na bado kesi haijaanza kusikilizwa! Kwenye mazingira kama hayo, hata tungekuwa na majaji 100, wangefanya nini?
Yaani Pasco kuna vitu ukifikiria vinatisha sana Hawa ndio wamepewa mamlaka ya kutoa haki. Duniani kweli tunapita Haki tutaipata mbinguni
 
Kwa maoni yangu, tatizo la msongamano wa kesi, sio idadi ya majaji na mahakimu, bali ni ubovu wa sheria zetu na uwezo mdogo wa baadhi ya majaji na mahakimu kukosa jicho la roho kubaini hatia, na udhaifu wa vyombo vyetu vya upelelezi. Mfano kwa tukio kama lile shambulio la Lissu, hata sisi tuu waandishi wa habari za uchunguzi, tungehitaji IJ ya siku moja tuu, kubaini chanzo cha wasiojulikana hao, na kukitumia kama lead kuwabaini, lakini kwa vyombo vyetu vya uchunguzi ni mpaka leo hakuna taarifa zozote!
Wachunguzi wwnyewe akina Sirro?
 
Tatizo kubwa la hii nchi (serikali) wenye uwezo mdogo ndio watawala wenye uwezo mkubwa wa kupambanua mambo ndio watawaliwa

Wapo tayari kutengeneza sheria mbovu wawezavyo na zikawa implemented.
 
Mahakimu na Majaji wanauwezo mkubwa sana kutoa haki lakini wanaendeshwa na watawala! Magufuli aliwatumia vibaya sana kupotosha haki na hii ilisababishwa na njaa zao na kutaka kupandishwa vyeo.

Jaji Mkuu ndiyo alikuwa chawa kabisa wa Magufuli akasahau wajibu na nafasi yake katika jamii!
 
Niliona kesi ya Manji kipindi kile alivyoleta wanasheria wazungu, na jinsi alivyoshinda kesi huku maagizo kuwa afungwe.

Nikawaza kama majaji wetu walikuwa intimidated na kingerezw zaidi cha mawakili?
 
Judiciary competence has very little to do with the problem.

Kutokuwepo uhuru wa mahakama na rushwa ndizo sababu kuu. Jiulize hii torrent ya reversal of judgement ya kesi kadhaa iliyotokea hivi karibuni ni kiashiria tosha. Na hakuna mabadiliko katika judiciary.
 
Majaji/mahakimu wanaongozwa na mawazo ya kum-favour bosi wao/mamlaka ya uteuzi kwenye hukumu wanazotoa, hawako huru, ile rasimu ya Warioba ilikuwa muarobaini tosha wa hili tatizo, siamini kama tatizo lao kuu ni weledi, wengi wao wako vizuri, labda bahati mbaya itokee kiubinadamu.
 
View attachment 1841771View attachment 1841772
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila siku za Jumatatu, huwaletea makala za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambayo huchapishwa na gazeti la Nipashe la Jumapili, ambazo ziko kwa mtindo wa maswali, majibu ya maswali hayo, utayapata wewe mwenyewe, na kisha tutawatafuta wahusika, ku balance hii mada, hivyo kwa mada hizi za mhimili wa Mahakama, mtu wa kubalance tuhuma hizi ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma.

Baada ya makala kuhusu Ofisi ya DPP, wiki hii, naugeukia Mhimili wa Mahakama.
Bahati mbaya, haijaelezwa ni namna gani TUME ya mahakama huwa inapata majina ya watu inaowapendekeza kuwa majaji. Wakati wa hafla hiyo ya uapishaji wa majaji, Jaji Mkuu alielezea jinsi mchakato wa uteuzi wao ulivyokuwa lakini haikuelezwa ni vipi katika majaji 18 sijui 23 hajapatikana Jaji hata mmoja kutoka miongoni mwa mawakili wa kujitegemea (kutoka TLS - sio wa kutoka sekta za elimu - maana nao wanaonekana ni mawakili binafsi). Akaeleza mlolongo wa interviews na kadhalika lakini ikaonekana kama ni soga tu, maana kiuhalisia inaonekana uteuzi wa majaji ni maamuzi tu ya Rais na wala sio kuwa anafuata mapendekezo kutoka Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Februari 1, 2021, Rais Magufuli alimteua Zephrine Galeba kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa kwa kuwa tu aliandika hukumu kwa lugha ya Kiswahili. Hukumu yenyewe ilitoka tarehe 29 Januari 2021 kama sikosei, yaani sijui walishauriana saa ngapi na Jaji Mkuu na walishauriana kwa njia gani - simu au maandishi, mtu akala uteuzi; Je kuandika hukumu kwa Kiswahili kweli ilikuwa ndio kitu cha maana kumpa uteuzi wa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa?? Uwezo wa uchambuzi wa sheria wa huyu Jaji ulizingatiwa kweli?? Matokeo ndio haya ya kuwa na majaji wenye uwezo mdogo sana wa sheria pamoja na uchambuzi na kutafsiri sheria.
 
... unapogeuza nafasi zinazopaswa kuzingatia weledi na umahiri kuwa za kichama ndipo tatizo linapoanzia. "Teuzi ziko nyingi. Kama umekosa uteuzi kwenye ubunge tutateuana kwenye nafasi nyingine; ukuu wa wilaya, mikoa, na maeneo mengine"; aliwahi kusikika kiongozi mmoja mwenye madaraka akitamka hivyo hadharani. Unategemea nini?
 
Kwa vile hoja yangu ya makala hii ni kuangazia uwezo mdogo wa baadhi ya Majaji na Mahakimu wetu, kutokuwa na jicho la ndani, lenye uwezo wa kuona haki, kunakochangia ucheleweshaji wa kesi na ukosefu wa haki, naomba kutoa historia fupi ya maisha yangu na jicho la ndani.

Lengo la simulizi hii ni kuwadurusu baadhi ya majaji na mahakimu wetu, jee wana uwezo wa kubaini hatia kwa kutumia jicho la ndani?, jee kwenye utoaji wa humuku zao, wanazingatia "utu na nafsi"?, na sio kutegemea tuu vifungu vya sheria na ushahidi pekee?. Ili jinai itendeke ni lazima kuwepo kwa mambo mawili, actus reus (kitendo cha jinai) na mens rea, (nia ya kutenda jinai). Jee mfumo wetu wa kupata majaji na mahakimu wetu, unahusisha amplitude test kubaini uwezo wa hao majaji na mahakimu kutumia jicho la ndani la utu na nafsi kubaini nia ovu ya kutenda jinai?.
Paskali
Hili ni bandiko la swali, jibu lake ni leo pale, mahakama ya uhujumu, jee Jaji ataonyesha uwezo?.
Let's wait and see.
P
 
Kila mtu anaweza kuwa mwanasheria, lakini sio kila mwanasheria anaweza kuwa Jaji. Mfano mzuri ni mtu aliyekuwa DPP kinara wa ukandamizaji wa haki, halafu mtu huyo anateuliwa kuwa Jaji, unategemea nini?!. Kama akiwa DPP alifanya madudu yote yale ambayo sasa ndio yanafumuliwa, akiwa Jaji, atatenda haki?.
...Dah!...jiwe gizani...
 
View attachment 1841771View attachment 1841772

Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila siku za Jumatatu, huwaletea makala za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambayo huchapishwa na gazeti la Nipashe la Jumapili, ambazo ziko kwa mtindo wa maswali, majibu ya maswali hayo, utayapata wewe mwenyewe, na kisha tutawatafuta wahusika, ku balance hii mada, hivyo kwa mada hizi za mhimili wa Mahakama, mtu wa kubalance tuhuma hizi ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma.

Baada ya makala kuhusu Ofisi ya DPP, wiki hii, naugeukia Mhimili wa Mahakama.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akiwaapisha Majaji wapya 28 wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani, Rais Samia alisema na hapa ninanukuu

“Tatizo la ucheleweshwaji wa kesi katika Mahakama zetu bado lipo, kama mnavyosema Wanasheria haki inayocheleweshwa ndio haki inayokataliwa, hivyo ni imani yangu kuwa baada ya upatikanaji wa Majaji hawa ucheleweshaji wa kesi Mahakamani utapungua na hatimaye haki kupatikana kwa wakati,” alisema Mhe. Rais Samia.

Rais Samia akaendelea kwa kuitaja Ibara ya (107) A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mamlaka ya utoaji haki ni Mahakama, “hivyo jukumu lililopo mbele yenu ni kubwa sana, basi ni vyema mkatekeleze majukumu yenu mliyopewa kwa uaminifu, mkaongoze vyema na mkaongozwe na utu na nafsi zenu katika kuwatumikia wananchi,” Mwisho wa kunukuu.

Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alimshukuru Mhe. Rais kwa uteuzi wa Majaji hao wapya huku akiwa na imani kuwa idadi hiyo italeta mabadiliko makubwa ambayo yataonekana mara moja.

Jaji Mkuu, Prof. Juma alisema “Mhe. Rais napenda nichukue fursa hii kukushukuru kwa kutupatia Majaji hawa, idadi hii itasaidia kupunguza mzigo wa mashauri kwa Majaji waliopo na hivyo kusaidia kuleta mabadiliko ambayo yataonekana mara moja,” alisema Mhe. Jaji Mkuu.

Prof. Juma, aliendelea “Mhe. Rais idadi ya Majaji inapanda na kupungua kulingana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kustaafu kwa Majaji pamoja na Majaji wengine kupangiwa majukumu mbalimbali, hivyo bado tunaomba kuendelea kupatiwa Majaji kadri nafasi zinapopatikana ili kuendelea kutoa huduma ya haki kwa kuwa wananchi wengi kwa sasa wanafahamu haki zao na hivyo kufungua kesi kwa wingi,” alieleza Jaji Mkuu.

Kwa vile hoja yangu ya makala hii ni kuangazia uwezo mdogo wa baadhi ya Majaji na Mahakimu wetu, kutokuwa na jicho la ndani, lenye uwezo wa kuona haki, kunakochangia ucheleweshaji wa kesi na ukosefu wa haki, naomba kutoa historia fupi ya maisha yangu na jicho la ndani.

Mimi Paskali Mayalla, zaidi ya kuwa mwandishi wa habari na mtangazaji, mimi pia mtu wa mastori, yaani stori teller, hivyo kwa wapenzi wa mastori, unaweza kufuatilia sehemu hii ya Mastori ya Pasco Mayalla, ila wewe kama sio mtu anayependa mastori, unaweza ku skip hii segment ya mastori
Mastori ya Pasco Mayalla

Lengo la simulizi hii ni kuwadurusu baadhi ya majaji na mahakimu wetu, jee wana uwezo wa kubaini hatia kwa kutumia jicho la ndani?, jee kwenye utoaji wa humuku zao, wanazingatia "utu na nafsi"?, na sio kutegemea tuu vifungu vya sheria na ushahidi pekee?. Ili jinai itendeke ni lazima kuwepo kwa mambo mawili, actus reus (kitendo cha jinai) na mens rea, (nia ya kutenda jinai). Jee mfumo wetu wa kupata majaji na mahakimu wetu, unahusisha amplitude test kubaini uwezo wa hao majaji na mahakimu kutumia jicho la ndani la utu na nafsi kubaini nia ovu ya kutenda jinai?. Jibu ni hapana!.

Tanzania ili mtu kuwa hakimu, ni kwanza kuhitimu shahada ya sheria, na kuomba ajira ya uhakimu, kwenye kuajiriwa, kupitia Tume ya Kuajiri ya Mahakama iliyo chini ya Jaji Mkuu, ila kwenye hadidu za rejea, hakuna amplitude testi yoyote kupima uwezo wa waombaji kuwa na jicho la ndani la kubaini jinai, na matokeo yake ndio baadhi ya hawa mahakimu kwenye mahakama zetu wenye uwezo mdogo, na matokeo yake ni kwa baadhi yao, kutokuwa na uwezo wa kutoa hukumu za haki huku wengine wakituhumiwa kula rushwa!. Udhibitisho wa tuhuma hii ya uwezo mdogo wa mahakimu wetu kutoa hukumu za haki ni mlolongo wa rufaa, na matokeo ya rufaa nyingi kukubaliwa.

Ili kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani ni Tanzania, ni kwanza kuwa mwanasheria, kisha jina lako likapendekezwa na Tume ya ajira ya Mahakama, na kupelekwa kwa rais, mtu unateuliwa kuwa jaji, napendekeza, ili Tanzania tupate majaji kama Lord Denning, tuongeze vigezo vya mtu kuteuliwa Jaji. Kila mtu anaweza kuwa mwanasheria, lakini sio kila mwanasheria anaweza kuwa Jaji. Mfano mzuri ni mtu aliyekuwa DPP kinara wa ukandamizaji wa haki, halafu mtu huyo anateuliwa kuwa Jaji, unategemea nini?!. Kama akiwa DPP alifanya madudu yote yale ambayo sasa ndio yanafumuliwa, akiwa Jaji, atatenda haki?. Unless kama wakati akiwa DPP, baadhi ya maamuzi yake ilikuwa ni kufuata maelekezo, then sasa akiwa Jaji, atakuwa Jaji mzuri, lakini kama akiwa DPP alishindwa kutenda haki, haitegemewi akiwa Jaji atatendaje haki!.

Nchi za wenzetu hadi wana vifaa maalum vya kubaini kama mhusika anasema uongo, (lie detectors), Majaji wetu na Mahakimu lazima wawe na uwezo huo, ili kuepuka kuwatesa watu kwa kuwasweka ndani miaka mingi watu wasio na hatia. Yako mazingira mtu anakutwa na ushahidi wa kuhusika na jinai fulani, na wengine hadi kuhukumiwa kunyongwa, na akiisha nyongwa ndipo ushahidi unakuja kupatikana kuwa amehukumiwa kwa makosa. Majaji na Mahakimu wetu, wakiwa na jicho la rohoni, wataweza kuiona haki na kutoa hukumu ya haki hata kama ushahidi utaonyesha kuhusika.

Kwa maoni yangu, tatizo la msongamano wa kesi, sio idadi ya majaji na mahakimu, bali ni ubovu wa sheria zetu na uwezo mdogo wa baadhi ya majaji na mahakimu kukosa jicho la roho kubaini hatia, na udhaifu wa vyombo vyetu vya upelelezi. Mfano kwa tukio kama lile shambulio la Lissu, hata sisi tuu waandishi wa habari za uchunguzi, tungehitaji IJ ya siku moja tuu, kubaini chanzo cha wasiojulikana hao, na kukitumia kama lead kuwabaini, lakini kwa vyombo vyetu vya uchunguzi ni mpaka leo hakuna taarifa zozote!.

Kwa kesi kama ya kina Rugemalila, sisi waandishi wa habari za uchunguzi, tungehitaji siku 7 tuu, kuwawekea ushahidi wote mezani, lakini vyombo vyetu vya uchunguzi, ni zaidi ya miaka 4 sasa na bado kesi haijaanza kusikilizwa!, kwenye mazingira kama hayo, hata tungekuwa na majaji 100, wangefanya nini?.

Kwa bahati mzuri, mimi nimebahatika kuwa mwanafunzi wa Prof. Ibrahim Juma, hivyo namfahamu vizuri kwa kauli, uwezo na matendo, jicho hilo la rohoni analo, na kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Mahakama ndio mhimili rasmi wa utoaji haki Tanzania, hivyo nina imani kubwa na Mhimili wa Mahakama chini ya Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, licha ya changamoto za utoaji haki, inauwezo wa kuwapatia haki Watanzania.

Kufuatia mhimili wa mahakama kushiriki Maonyesho ya Saba Saba, makala ya wiki ijayo, nitawaletea ushiriki wa Mahakama kwenye Saba Saba.

Paskali
Naona watu wengi mitandaoni wanajadili namna majaji wanavyopatikana. Watu wanahoji
1. Jaji anapatikana Kwa kupanda vyeo serikalini?
2. Wanapatikana Kwa UMAHIRI?
3. Wanatokana na perminmance nzuri kwenye private sector?
4. Wanatoakana na ukubwa wa GPA?
5. Wanatokana na mahusiano Yao na wanasiasa au wanapatikana Kwa vigezo vipi?

Wengine wanasema walivyoona akina Samata na Wariaoba waliamini Majaji wote wanazaliwa kuwa majajaji lakini lakini wakiangalia majaji wa tume ya uchaguzi na wengine wa kariba hiyo wanaamini Jaji siyo upeo ni cheo kama vyeo vingine.

Thought ya tatu inajikita kwenye siasa, je majaji wanapatikana Kwa fadhili kutoka kwa anayetawala au mbinu Gani utumika. Thought hii inawaangalia akini Biswalo Mganga na kubaini kumbe Ukiaaribu somewhere unaweza kupelekwa Judicial akasugue bench!

Wewe unaamini Jaji kwa Tanzania ni mwenye qualities zipi na anapatikanaje?
Bitte, Beatrice Kamugisha, karibu pande hizi, kuna kitu niliraise kuhusu uwezo wa majaji wetu kubaini jinai na kutoa haki.
P
 
Kama tumewahi kuhoji utendaji wa rais na hakuna tatizo, why not majaji?. They are human beings hivyo they are capable of doing mistakes na ndio maana kuna rufaa.
P
Ikiwa una wasiwasi na utendaji wa mhimili unaosemekana upo huru (Uhuru wa bandia),wakati huo huo ukiutegemea ukupe haki, huoni ni hatari?...
 
Back
Top Bottom