Jaji Mkuu: Jamii inawanyanyapaa na Kuwatenga Majaji na Mahakimu Kutokana na Hukumu zao

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,775
Jaji Mkuu Prof.Ibrahim Juma amesema Majaji na Mahakimu wamekuwa wakinyanyapaliwa na kutengwa na jamii Kwa sababu ya kazi Yao ya kutoa Hukumu hivyo kuwa kwenye kundi kubwa la msongo wa mawazo hasa Wanawake.
---
MAJAJI na mahakimu wananyanyapaliwa na jamii kutokana na hukumu wanazotoa mahakamani, Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahimu Juma, amesema.

Akiwa na angalizo mahususi kwa watendaji wenzake wa mahakama, Jaji Mkuu Juma ameanika vitendo vya unyanyapaa kwa kundi hilo, akiwataka majaji na mahakimu wanawake kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi kwa kuwa wao ndiyo kundi linaloathiriwa zaidi na unyanyapaa huo.

Akirejelea katika utafiti uliofanyika Marekani kuhusu msongo wa mawazo na ustahimilivu kwa majaji wa Marekani, Prof. Juma amewataka watendaji wenzake wa mahakama kupambana na kikwazo hicho ili kufanya kazi zao vizuri.

Nipashe

My Take

Kwani wewe Jaji hukusikia Kauli ya Makonda? Mahakama imejaa dhuluma.

Sasa kama watu wanapindisha sheria Ili kuwapendelea wenye pesa na Vyeo na kunyima Haki maskini Kwa nini wasinyanyapaliwe na jamii?

Sio tuu Majaji Bali hata mapolisi ni wa kunyangapaliwa na kufukizwa kwenye jamii Kwa sababu ya matendo Yao ya uonevu.
 
katika mambo yoote, fanya kila kitu kwa haki. Neno la Mungu lilipojadili kazi ya mapolisi, linasema TOSHEKENI NA MISHAHARA YENU, hiyo ni alart tu kwamba rushwa acheni, sio hao tu hata mahakama.

Neno la Mungu pia limesisitiza sana KUTOTOA USHAHIDI WA UONGO. kutoa ushahidi wa kweli hata kama mtu anafungwa sio kosa, ila kutunga ushahidi ni dhambi kabisa.

Majaji na mahakimu wakifanya kila kitu kwa haki, bila kupendelea mwenye pesa au asiye na pesa, mwenye cheo au asiye na cheo, mwanasiasa au asiye mwanasiasa, Mungu atawabariki. ila wakila rushwa, itawatafuna hakika.
 
Kwahiyo anataka hata ndugu zake billionaire msuya wasiwanyanyapae majaji?
Yule mama wa vipande 12 vya nyama awapende watu wa mahakama?
 
Back
Top Bottom