Ni jambo la kheri kuwa wanaharakati na wanasiasa hatimaye wametengana na kila mmoja anapambana na hali yake. Kuvunjika kwa koleo sI mwisho wa uhunzi.
Kwani hata nini cha mno kilipatikana tokea miaka 90 hadi leo kwenye muunganiko wa makundi haya? Hadithi zile zile za kuibiwa chaguzi na kutendewa ndivyo sivyo kulikopitiliza.
Japo umoja ni nguvu, bado yawezekana utengano huu ukawa ni mbaraka uliojificha (a blessing in disguise).
Uzi huu wenye kumtambua "kila mdau" kwenye siasa unahusika:
Tuzitambue tofauti za vyama vya upinzani (ACT, CHADEMA, CUF, nk) na Wanaharakati
Ikumbukwe vyamani kuliko sheheni wanasiasa waliotamalaki, wanaharakati pia wapo. La msingi ni kuwa, kuwa mwanaharakati hakumsimamishi mtu kuwa mwanasiasa. Hii ikizingatiwa kuwa vyama vyenyewe vya upinzani ni vyama vya harakati.
Tangu lini wasioamini kwenye demokrasia wakawa waumini au washirika kwenye kupambania demokrasia?
Vipi mpigania demokrasia kutomwona Mrusi ni mvamizi Ukraine, akakaa kimya asimwunge mkono Ukraine kwa hali na mali au hadharani?
Au vipi mpigania demokrasia kutomwona Israel kuwa ni mvamizi Palestina, akakaa kimya asimwunge mkono Palestina au HAMAS wenye kupambana na mwizi wao?
Undumila kuwili wa wamaagharibi mgogoro Gaza, Putin Dume!
Mpigania ukombozi au demokrasia hawezi kuwa mandumila kuwili.
"Vipi kuilaumu TCRA na Serikali kuzuia matumizi ya VPN wakati chamani na hata mitandaoni hamko tayari kukosolewa?"
Hatuwachukii CCM Kwa sababu ya jina lao, rangi wanazotumia au mwonekano wao. Tunawachukia kwa sababu ya vitendo vyao vya kutoheshimu demokrasia.
Kwamba hauheshimu demokrasia popote? Wewe pia hatuwezi kukuthamini. Wewe pia ni kama li CCM jingine tu katika rangi zako na mwonekano wako.
"Kwa hakika kupigana vita na wewe upande mmoja ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu."