Vyama vya upinzani na wanaharakati ni makundi mawili tofauti yenye mwonekano wa kufanana lakini kiuhalisia ni yenye kutofautiana sana. Yote mawili hujinasibu kumtumikia mwananchi kwenye agenda za ukombozi, ila yakiwa na malengo tofauti.
Kwenye muktadha wa siasa za hapa kwetu, agenda kuu ni ukombozi, yaani mabadiliko. Kwa muktadha huo vyama vyote vya upinzani ni wanaharakati. Uanaharakati wa chama hukoma kikiingia madarakani japo baadhi ya wanachama wake wanaweza kuendelea kuwa Wanaharakati..
Vyama vinaundwa na wanasiasa wenye malengo yao likiwamo la kushika dola. Wanaharakati (usu) malengo yao ni mabadiliko. Mabadiliko hayana mwisho.
Kwenye vyama kuna wanasiasa. Si kila mwanaharati ni mwanasiasa. Pia si kila mwanasiasa ni mwanaharakati. Uanaharakati wa mtu haukomi, bali uanaharakati wa vyama hukoma.
Wanasiasa wa upinzani na Wanaharakati hujinasibu kwa wananchi kuwa wanawakilisha matakwa yao, yaani agenda zao. Wawili hawa wanapata uhalali wa uwepo wao (relevance) kutokea kwa wananchi.
Kwa sababu wanasiasa na wanaharakati huwa na malengo tofauti, si nadra makundi haya kusigana.
"Tuzitambue tofauti zao:"
1. Mwanaharakati wa kudumu:
a) Kwenye katiba mpya na bandari: Atataka katiba mpya sasa. Biashara ya bandari haipo, sasa na hata milele.
b). Atasimama na wananchi siku zote.
c). Huyu si kigeugeu. Agenda za wananchi kwake ni za kudumu.
d). Akiitisha maandamano atakuwapo mstari wa mbele. Yuko tayari kufa au hata kufungwa badala au kwa niaba ya wananchi wake.
e) Siyo mnafki, ni muwazi na anachosema au ukimwangalia, (usoni) ana maanisha.
f) Ni kipenzi cha watu.
g) Hushawishi kwa nguvu za hoja si kwa hoja za nguvu.
h) Huyu huwa na wafuasi wa dhati, siyo wafuasi wa kulipwa (chawa). Hoja zake zajiuza. Hahitaji kukingiwa kifua.
I) Amedhamiria. Lugha yake, adui huielewa Kwa ukamilifu wake.
2. Mwanasiasa (asiyekuwa mwanaharakati wa kudumu)
a) Atasimama na suala la katiba au bandari au lolote la wananchi kama ana maslahi nalo binafsi tu. Humo yakiwemo maslahi kiuchumi na ki madaraka.
b) Husimama na wananchi anapoona kuna maslahi yake binafsi yaliyo wazi kwa wakati huo au yaliyo fiche.
c) Huyu gia kubadlika angani ni kawaida.
d) Agenda kipaumbele huwa ni maslahi binafsi. Za wananchi huwa ni kisingizio tu ambazo nazo hutumika kama daraja.
e) Huyu anachosema si lazima kuwa ana maanisha.
f) Hayuko tayari kuwa sehemu ya gharama za ukombozi ikiwamo kufa au kufungwa, yeye au jamaa zake. Huhamasisha wengine kuwa tayari kulipa gharama hizo.
g) Demokrasia kwake mtihani. Yaani alichoona yeye ndiyo masimamo. Haambiliki.
h) Huyu si nadra kuwa na wafuasi wa kulipwa, kumkingia kifua hata bila ya kuwa na hoja.
I) Anampenda mwanaharakati asiyejitambua Ili kumtumia Ili kuyafikia malengo yake.
Zingatia:
"Ni kwa usahihi kabisa anaposema Samia kuwa hata huko vyamani hali si shwari. Kwamba ukiwapa nafasi ya kuunda serikali, wengine humo watageuka na kuanza kuwapinga wenzao."
Bila shaka akimaanisha, pia kina Mpina, Polepole, Bashiru, nk huko kwao, CCM.
Mwanaharakati kamili ni wa kudumu kama Almasi.
Diamonds are forever!
Nyuzi mbili hIzi zinahusika:
1. "Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu"
2. "Upinzani - walio waoga (cowards) si Wafuasi"