Ukitongoza msichana wa siku hizi jipange

EMMYGUY

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
10,898
24,904
Wabari Wakuu!


Maisha yetu yanazidi kubadilika kila kukicha, kuna mambo hapo mwanzoni hayakuwepo na kuna mengine pia yalikuwa yanatokea. Uolewaji wa wanawake katika jamii zetu kwa kipindi cha nyuma ulikuwa ni wa kufuata maadili na misingi ya jamii.

Kadri ya ulimwengu unavyozidi kwenda ndio na mambo yanazidi kubadilika, mfano uchumba wa siku hizi sio dili tena kama zamani. Watu wamekuwa wakitumia neno uchumba kwa lengo la kupata kile wanachokitaka, maana inaaminika uchumba ni hatua kubwa inayofikiwa na wapenzi kabla ya ndoa.

Siku hizi ukimtongoza mwanamke anakuwa mwepesi sana wa kuhalalisha mahusiano yenu yawe wazi, hata kama mwanaume huna mpango wa kumuoa tayari wao wanakuwa wanaonyesha dalili zote za kutaka kuolewa.

Wanaume wengi hata humu JF wamekuwa wakilalamika kuhusu hichi kitu. Sijajua hasa tatizo ni nini mpaka wanafikia katika hatua hiyo, ukimtongoza binti leo kesho tayari hata ndugu wameshajua.

Hebu tujadili hili jambo kwa pamoja.
 
ha ha ha.. kama kweli.. kuna mtu analalamika kamzingua suster du kwenye harusi. kesho yake tu kawekwa profile picture watsup my huby.. kaka zake demu na dada zake demu wote wamemjua plus marafiki wa sister du nao wanawish happy relation kwa profile pic ya shemeji yao...

jamaa alijutaaa
 
wanahalalisha kihivyo ilikuoneshea jamii kuwa nayeye sendoff au harusi yake imeshakaribia.
 
Inategemea ume mtongozaje!!!

Lakini sikuna kiuzi nimekiona kuwa wa tz hawajui kutongoza , tukianzia pale nadhani tuna weza solve hii case
 
Vitu vinavyochangia.

1. Kuanza mapenzi katika Umri Mdogo. Hii ndio tunaweza sema ni kubwa kuliko zote sababu mabinti wengi wanlkifika 20 anakuwa ameshatembea na wanaume hata kumi. Tayari alishaumizwa vya kutosha kwahiyo we mwanaume ndo uko chuo au umemaliza chuo au ndo umeanza kutoka kimaisha ndo unawaza sasa nawe uanze kutafta mpenzi. Kwahiyo kabla we hujamconfirm tayari ye ashajiconfirm maana yuko desperate kuolewa ashachoka.

2. Chereko ya TBC na vipindi vingine kama hivyo.

Yaan hili ni jipu kwa wadada maana wakiangalia hivi vipindi akili inaruka wanawaza kuolewa tu na kufunga ndoa ya kifahari. Kwahiyo hiyo ukijilengesha tu sijui nakupenda tayari anakuita we mchumba na anataka mfunge ndoa ili na yeye aonekane chereko. Ukimuuliza baada ya hapo maisha yatakuwaje, hajui chochote.

So wazazi wanawajibu wa kukaa na watoto wao toka wakiwa darasa la tatu kuanza kumfundisha maisha. Mzazi unakuta anamfundisha mtoto kukatika ekotite unategemea hapo akikua kitatokea nini. Baadae oooo watoto wa siku hizi, kumbe mzazi hujijui. Pumbafu kabisa
 
Hahahah...i can guess!!..umejipanga tangu kitambo sana mfilipino!!

Hii "valentine" nahisi ni yako yaan ushindwe mwenyewe tu!
Hahah me kila siku kwangu ni valentine, si unajua wafilipino ni mahabati mwanzo mwisho. Ila lazima ntafanya kitu fulani hivi amazing sana
 
Back
Top Bottom