Alikuja kama mvua, siku moja tu ambayo haitakaa ikasahaulika- Ainekshah

Neo_Trapper

Member
Sep 21, 2021
27
39
Vingi vizuri zaidi huja ukiwa huna shida navyo, huja wakati imani yako ikiamini kuna vizuri kumbe unapishana gari la mshahara...😁

Yaani kwa lugha rahisi ni kusema kuwa, "Vizuri huja muda wako ukiwa unaamini uwepo wa vizuri feki vilivyotengeneza ukungu machoni mwako." πŸ˜‚

Legends mpo wapi?
πŸ˜‚

Enzi zilee mapenzi nayaita ni ujinga nilikuwa napendwa sana na wadada wazuri, wakaniita mume πŸ™„ wakaninunulia mazaga, nguo kunifulia wengine wakanibaka kabisa ...🀣🀣 wengi kuzidi wote wakamuahidi mama lazima niwaoe πŸ˜†

Nilipokuwa sasa 😁
Yeeeeh!! sijui walienda wapi ...🀣🀣🀣🀣

Ukiachana na hiyo kuna kile kipindi nasoma sasa,

Kipindi hicho niko mdogo sana nilikuwa naliliwa na wasichana shuleni hii ilikuwa ni darasa la pili mwaka 2013 ...πŸ˜‚

Wasichana walikuwa wanalia seriously huku wakilitaja jina langu na kudai kuwa walikuwa wananipenda sana ...πŸ˜‚

Namkumbuka mdada mmoja alikuwa anaitwa Aineksha, huyu mdada alikuwa na drama sio poa alikuwa na balaa lake kumshinda yule Roshin Patel wa kwenye Jamai Raja...πŸ˜€

Alikuwa mdada mzuri ambaye aliwindwa sana na wavulana wengi pale shuleni, alikuwa mpole ...sauti yake sijawahi kusikia mfano wake popote pale tangu nimfahamu Aineksha mpaka leo ...πŸ™†β€β™‚οΈ

Alikuwa mweupee, mwenye sura ya kuvutia sana alikuwa na umbo ambalo lilimpagawisha kila mwanaume aliyeyafahamu mapenzi ...πŸ™„

Wanafunzi walipagawa wakarusha nyavu zao lakini wapi mtoto kawachomolea ...πŸ˜€ walimu wa kiume nao hawakucheza mbali walijaribu bahati zao lakini Aineksha alikaza kamba ...🀣


Sasa bwana siku moja nipo zangu nimepoa darasani nikapewa ki~memo na mshikaji wangu anaitwa Allen...😳

Kwanza nilishangaa sana nikaishia kujiuliza ni nani huyu anatafuta balaa la makofi ...🀣 wengi walikuwa wananifahamu sana pale darasani yaani ukinipa ki~memo hakikisha umeandika content la sivyo makwenzi na makofi mbele ya darasa zima...πŸ˜‚

Nikakifungua chaap ...😳

Allen: Mzee, siku hizi unatongoza wadada na hausemi ...☻️ kuna wakati ukipitia hali kama hiyo nishirikishe nikupe voko zangu au kama unajiweza basi isitokee bahati mbaya nikapita na shemeji ...unakosea Danny!

Mimi: Acha ufala Allen, nakuheshimu sana ujue, ulisikia lini mimi namtaka msichana yeyote humu darasani? Lini? Wapi? Nani kasema? Au uliona wapi au gazeti gani liliandika?

Allen: Broo mimi sijawahi kuvaa miwani ujue nimeona mwandiko wako sehemu flani...😳 umeshuka mashairi kaka mpaka nimekubari...😁 kuna sehemu umeandika, "Nikupendae ni wewe darling, kamwe sitabadili chaguo langu ...😘 kushinda kwa rafiki yako ni vizuri pia ila kuna muda acha vyote njoo uuchambue moyo wangu."
Wewe noma! Aliyekuita Sharukh Khan hakukosea kabisa.

Ulikuwa ni mfulizo wa meseji za nguvu kati yangu mimi na Allen...mshikaji wangu wa pale darasani, kumbe Allen ndiye aliniandikia kibarua kile ambacho nilihisi kuna mtoto wa mtu alikuwa anataka makofi ...🀣

Mimi: Mbona sikuelewi Allen unazungumza nini?

Allen: Aineksha babaa... Aineksha!!!

Mimi: Amefanya nini?

Allen: Aineksha kananiii....aubasiii 😳

Mimi: Aisee 😑 hakuna kitu ambacho sipendi kama kupewa taarifa nusunusu.

Nilipomaliza kumtumia kibarua kile nikamfuata, mimi nilikuwa ninakaa mbele halafu Allen alikuwa anakaa nyuma kabisa ila kwenye msitari uleule niliokuwa nimekaa mimi, wakati naenda nikampita Aineksha ambaye alionekana kuingiwa na hofuu sana sikujali mimi huyoo, nikaenda mpaka kwa Allen.

Mimi: Kuna nini?

Allen: Kuna nini? Kwani wewe hujui nini?

Mimi: Allen kiukweli mimi sijakuelewa kabisa, umesema mimi nimemtongoza Aineksha? Lini?

Allen hakunijibu chochote, alinyoosha kidole kwenye dawati la mbele kupitia kwenye bega langu..moyo wangu ukapiga paah..!!

Nikageuka haraka kuangalia kile ambacho Allen alikuwa akinionyesha, nikamuona Aineksha ameshika karatasi kubwa iliyojaa maandishi na michoro mingi ya kopa ❀❀

Nikaenda nikaimnyakua na kisha nikazipiga hatua kuelekea kwenye dawati ambalo nilikuwa ninakaa ili niisome vizuri barua ile, kabla ya kuisoma ilivutia sana tu hata kwa kuitazama...😊

Mtu mzima nikapumua na kuanza kuisoma...

Maajabu sana aisee ...😊

Kumbe barua ile ilikuwa imeandikwa na Aineksha mwenyewe na lengo lake inifikie mimi ila alikuwa anaogopa kunipatia kutokana na tabia ya kumpiga kila mtu aliyekuwa ananichatisha vitu vya hovyo hasa wasichana (hii niliambiwa na Mariam, rafiki yake Aineksha)...🀣

Alooh! mtoto alishuka mashairi mpaka moyo ukaanza kulainika wenyewe ...😁

Unajua ngoja nikwambie kitu msomaji, kuna wakati mapigo ya moyo yanazidi mpaka huhitaji msaada wa kushika kifuani ndipo uyasikie yaani unayasikia tu bila kushika kifua tena kwa masikio yako hayo...πŸ˜πŸ˜† hicho ndicho kilichonitokea siku hiyo

Ile barua alikuwa hajaimaliza kwani kuna sehemu nilifika alianza kulitaja jina langu,

"Danny"

Nilipolisoma tu likajirudia akilini nikahisi kama ameniita hivii...😳 sijakaa sawa nikabamizwa kofi la usoni nikashituka kutoka ndotoni nikiwa natoka jasho jingi mbele yupo mama ameshikilia fimbo 🀣

Looh! Ilikuwa jumatatu na jua tayari lilishachomoza nikageuka kuangalia saa ya ukutani ilikuwa saa nne asubuhi...πŸ™„πŸ€£πŸ€£

Nikaruka kitandani ile nipo hewani nikasindikizwa na kofi la mgongo mpaka chinii....

HII SIKU NILIANZA KUIKOSOA BORA NINGEOTA NAENDA HAJA.

MWISHO...✍️
 
20240115_233655.jpg


KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Kwa hiyo mkuu sasa hivi ulisha feli form four. badala usome urudie mtihani upate credit za kwenda veta kusomea diploma unakuja hapa kutusumbua na ujinga wako?
 
Ulokole una lostisha sana mkuu!!

Unaacha totoz za maana unakuja kuangukia Kwa vitu vya ajabu!

So sad!
Kuna mtu alinisanua sikumsikiliza"IPO siku utajilaumu sana we jamaa,Hawa madem wanaokufeel watie tu hata kwa reference baadae usitose!sikusikia so sad!
I can feel the heat now!
 
Back
Top Bottom